Anko Michu Shkamoo,
Mie ni mdau wako hapa mtaa wa Mkunguni, Kariakoo. Zamani ulikuwa unapitaga, siku hizi sijui vipi. Anewei, mie nna dukuduku langu ambalo naomba nishee na wadau ili lipungue kama si kuondoka kabisa.
Dukuduku lenyewe ni kuhusu hii mambo ya DNA hasa katika upande wa mtu kuamua kwenda kupima ili kuhakikisha kama mtoto ama watoto ni wake ama la. Maswali...
1. Kupima DNA ni kubaya ama kuzuri?
2. Endapo kama itakutwa mtoto si wako nani wa kulaaumiwa; mama au baba?
3. Kama utakuta mwana si wako hatua gani bora ya kuchukua
Ni hayo to anko Michu, naomba usinibanie. maana nawee naweeee kha!
Mdau Yasmin
Kariakoo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 41 mpaka sasa

  1. Upimaji wa DNA utakuwa na maana pale tu ambapo kuna ugomvi usiosuluhika, kwa njia yoyote nyengine, kati ya wazee wawili kuhusu mtoto. Sura ziko mbili. Ama baba anakataa kuhusika na mtoto - hivyo kukataa jukumu la kumkimu mtoto huyo- au mama anambambakizia mtu mtoto akidai kuwa ndiye baba. Katika sura zote hizo mbili, mwanamke, mara nyingi, ndiye ajuwae baba mhusika wa mtoto. Katika sura zote hizo mbili, wa kulaumiwa namba wani ni yule anayekana jukumu lake la kisheria.

    Kama itatokea kuwa mwana si wako, na wewe ukawa ndiye unaedai kuwa ni wako, basi wa kulaumiwa ni wewe mwenyewe. Kuhusu hatua ya kuchukua hapo itategemea upande wa pili unataka kufanya nini. Wewe huna la kufanya, maana mtoto si wako! Sasa ufanye nini?!!!

    ReplyDelete
  2. hakuna haja ya kupima DNA,ni kutomwamini mwenzio,kwanza mi ukijifanya unaenda kumpima mwanangu DNA tunaachana hapohapo.

    Umuhimu wa DNA ubaki tu kwenye kesi za jinai kama ubakaji na uuaji ila si kumjua baba wa mtoto.

    ReplyDelete
  3. Hili ni swali la kipumbavu ambalo sijawai kukutana nalo katika maisha yangu.

    Na nadhani alioandika anayo majibu ila sijui nini anakitaka.

    Mjusi

    ReplyDelete
  4. Kupima DNA kama ni swala zuri au baya inategemea na mtu binafsi, na sababu zinazokufanya kutaka kupima. Mtoto anaweza akawa si wako lakini ukawa naye na mahusiano mazuri tuu kama baba na mwana, na pia anaweza akawa wako lakini akikuwa akakupiga ngeta kama hakujui. Ingawa, mimi binafsi kama ningekuwa na mtoto ningeangalia DNA ili kujua ukweli kwa sababu utamaduni wa uaminifu kwetu sisi wabantu ni kitu kigeni.

    ReplyDelete
  5. Nataka nimjibu Mdau Yasmin maswali yake matatu kama ifuatavyo;
    1. Kupima DNA ni kuzuri wala hakuna ubaya wowote. Kama una wasiwasi mtoto au watoto wanaweza kuwa si wako, ni bora kuondoa wasiwasi na kupima ili kujua ukweli ili uweze kuishi nao vizuri.

    2. Kama utakuta mtoto si wako,inategemea, siwezi kusema wa kulaumiwa awe nani kwa sababu hujatoa maelezo yanayojitosheleza ili kuweza kulichambua suala hili kujua wa kulaumiwa ni nani. Hata hivyo, kwa mawazo yangu, ishu kama hii ikitokea nafikiri sio vizuri kumtafuta wa kumlaumu, kwa sababu hiyo itakuwa sio suluhisho bali ni kuongeza matatizo zaidi. Nafikiri cha msingi ni kujaribu kujifiria wewe mwenyewe na kuongea na mwenzi wako kulizungumzia ili na kukubaliana jinsi ya kuendelea nalo huko mbele ya maisha yenu.

    3. Kama utakuta mwana si wako,hatua ya kuchukua itategemea sana wewe mwenyewe na mazingira yako. Itategemea wewe unataka nini maishani na unataka kuendesha vipi maisha katika mambo kama haya. Suala kama hili halina jibu la ''yes'' an ''no'' na wala halifanani na swali kama la 1+2=3. Hili ni suala la binadamu na kwa kuwa binadamu si sawa kwa mitazamo kuhusu maisha, basi itakuwa ngumu kwa mtu mweingine kukueleza wewe kwamba ukikuta mtoto si waki basi fanya hivi au vile. Na hakuna jibu moja kwenye ambalo litawafaa watu zaidi ya mmoja. Itabidi tu wewe mwenyewe ujitazame na uone ni nini hasa unataka. Nafikiri hatari ya kutafuta jibu kwa watu kwenye ishu kama hii ni kwamba unaweza ukajikuta unafanya maamuzi kwa kutumia akili ya mtu mwingine na sio ya kwako. Kwa hiyo nafikiti jitambue kwanza wewe,uwe na jibu lako na ujue ni kwanini una hilo jibu, then unaweza ukajaribu kutafuta ushauri kwa watu unaowaamini lakini huku tayari ukiwa na jibu lako la mwanzo.

    Nafikiri kwa kiasi fulani, unaweza kupata mawaili matatu kutokana na mchango wangu huu.

    Ahsante.

    Mdau from London

    ReplyDelete
  6. Mdau Yasmin

    Swali zuri. Majibu ni kama ifuatavyo:

    1. Kupima DNA ni kuzuri
    2. Endapo kama itakutwa mtoto si wako wa kulaumiwa ni MAMA
    3. Kama utakuta mwana si wako hatua bora ya kuchukua ni kumrudisha kwa mwenyewe

    Natumai dukuduku lako sasa limekwisha. Kama bado usisite kuuliza zaidi kupitia comments hapo chini.

    ReplyDelete
  7. Kama una mtoto na anafanana na jirani yako kuliko mnavyofanana na wewe, wala usichelewe!

    ReplyDelete
  8. Huyu dada topic aliyo ileta ni mzuri, inaweza kutusaidia sana wengine. Mimi nina tatizo moja, nina watoto wawili wote weupe, lakini mimi na mke wangu ni weusi.
    Ingawa kitaalamu, inaweza lakini mimi nina wasiwasi, na nime mweleza mke wangu kuhusu hilo na yuko tayari kwa DNA, tunasubiri tupate fedha za kwenda kufanya test.
    Kwahiyo mchango wenu wa mawazo kujibu swali la huyu dada litanipa mwanga zaidi.

    ReplyDelete
  9. Mimi nikikuta mtoto si wangu, nasema Mungu atukuzwe. Japo, sitapima mwanangu NDA. Kama amezaliwa zizini mwangu, huyo ni wangu tu. Kama kuna mtu alinisaidia kumpata, mbona kupewa msaada ni jambo jema tu. Hata mimi natoa msaada mtu akiwa na shida.

    ReplyDelete
  10. ALIYESEMA SWALI HILI LA KIPUMBAVU SIDHANI KAMA NI KWELI KWASABABU MIMI SIJUI KAMA KWELI MTU UNATAKA KUHAKIKISHA KAMA KITU SI CHA KWAKO UNASHINDWA KWENDA KUANGALIA KWELI JAMANI? TUACHE HABARI ZA KIZAMANI MTOTO HUYU KAFANANA NA BABU YAKE ALIYEKUFA KAMUONA WAPI YEYE? LAZIMA TUWE WA SASA ZAIDI VIJANA SIKU HIZI HAWAELEWEKI KABISAA UMEMUACHA MKEO NYUMBANI UTAKUTA VIJANA KIBAO KILA KUKICHA HAYAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA...


    MADA MEZANI MDAU ABDALLAH NGATUNGA TEMEKE....

    ReplyDelete
  11. Jibu la swali unalo mwenyewe kusuka ama kunyoa

    ReplyDelete
  12. wakulaumiwa ni yule aliyebeba mimba kwa miezi 9 halafu hajui mwenye mtoto!

    ReplyDelete
  13. Vuteni Subra mambo mengine anahukumu muumba mwenyezimungu aliyefanya zambi ajaribu kutubu tu na aliyefanyiwa ana stahili mawili kusamehe au kutosamehe mengine anahukumu mwenyezimungu huku unajaribu usirudie kosa. Uzinzi jamani ni mbaya ndio unaleta WASIWASI kama huo katika mawazo yenu. Pazi.

    ReplyDelete
  14. kuna walakini kwa kila mtu anataka kujua ukweli wa jambo na ndio maana ikawa ni vyema kukumbuka kwa kutumia DNA na kwa kweli jambo hili wala tusifiche wanawake ndio wengi sana wanaangalia kuwa mshikaji au huyu mtu ana uwezi wa kulea mtoto basi wanalazimishia kuwa mtoto ni wako wakati sio na kwa upande mkubwa kwa kuwa wao ndio wanasababaisha basi kwa kweli hao ndio walaumiwe kwa kuwa wao ndio chanzo kikubwa cha mambo yote haya kwa kuwa mwanamke ndio anajua mtoto ni wa nani na amempata toka tarehe na hata siku kuna wengine huwa wanajua kwa kweli mdau nakushauri kwa kuwa kwa kuangalia tu inaonyesha una tatizo kama hilo basi kama umekuta si wako kwa kweli jitoe na ukina mambo yanakuwa magumu zaidi weka tangazo hata kwa picha ili tusaidiane kwa maoni ili tukutoe katika shida kama hii

    ReplyDelete
  15. HUYU MDAU ALIYEULIZA HILI SWALI YAMEISHA MKUTA AU ANA UGOMVI NA MWENZIE KUHUSIANA NA MTOTO? LAKINI MIMI NAONA NI UPUMBAVU, KWA MFANO MTU AMEOA LAKINI ANAHISI MTOTO ALIYEZAA NA MKEWE SIYO WAKE LAKINI WATU WANAJUA FULANI ANA MTOTO HALAFU ANAENDA KUPIMA INAGUNDULIKA MTOTO SI WAKO HIYO AIBU UTAIWEKA WAPI?

    ReplyDelete
  16. Kuna uhakika gani kuwa hicho kipimo kitatoa majibu 100% sawa, na ukizingatia nchi kama bongo, vitu vingi vinavyonunuliwa vinaletwa vimeshapitwa na wakati au vibovu.
    Nawaomba watakaopima wasichukulie jaziba, wavute subira wapime tena, na tena.

    ReplyDelete
  17. Annon April 21, 2009 3:00 PM,umenifurahisha kinoma. Yule mjusi aliyesema swali la kipumbavu nadhani watoto alio nao wote sio wa mumewe ndo maana ana hofu.
    Kama unahofu na uwezo upo just go for it.

    ReplyDelete
  18. NYIYE WANAUME CHEZEENI HAO HAO TEGEMEZI - MIMI UKITAKA KUWAPIMA WANANGU - UKITOKA HUKO OUT - UTAKUWA UMEULA WA CHUYA.

    ReplyDelete
  19. HUYU ALIYESEMA SWALI NI LA KIPUMBAVU NADHANI YEYE NDO ANAUPUMBAVU KICHWANI MWAKE.

    NI VEMA KUJUA UKWELI NA UHALISIA WA KILA JAMBO.SO KUPIMA DNA NI JAMBO SAHIHI KABISA.

    KUNA WANA MAMA WENGINE NI WAHUNI HADI HAWAJUI NA WANAKOSA UHAKIKA WA MTOTO NI WA NANI.UNAKUTA ANA MUME NA MABWANA WAWILI.NA WOTE HATUMII NAO KINGU NA ANATOA URODA MFULULIZO.HII HATA MUNGU HAPENDI.SO SIKU MIMBA IMEINGIA HANA UHAKIKA KAMILI NI YA MUME AU KATI YA WALE WAWILI.

    IKIGUNDULIKA MTOTO SI WAKO NI VEMA NA NI BUSARA MKE ATAJE BABAKE ILI MTOTO AENDE AKAPATE MALEZI YA BABA YAKE WA UKWELI.NA MTAJADILI KAMA BADO MNAPENDANA NA MKAHAKIKISHIANA HAKUNA KUTOKA NJE YA NDO TENA.MKAENDELE UPYA KUISHI KAMA MKE NA MUME.JAPO MAHAWARA NI NGUMU KUACHANA.PIA TUKUMBUKE KUNA GONJWA LA UKIMWII

    ReplyDelete
  20. jibu lake tumia kondom tuu, hautasingiziwa mtoto kamwe!

    ReplyDelete
  21. Kwa Tanzania nashauri upime DNA hata kama huna wasiwasi.

    Usiendekeze uaminifu ambao huvunjwa bila habari.

    Bora ulinzi kuliko uamininfu hoi kwa sababu watu woote walioambukizwa ukimwi, au kuibiwa unyumba (cheated), au kubambikiwa watoto, wamefanyiwa haya na watu wawapendao na kuwaamini.

    Hivyo tujali maisha ya woote kwa kuchungana. Dharau ushauri utakuta kimwi li ndani na kuambiwa umelileta wewe.

    Ama kama watoto si wako:
    1. wapeleke kwa baba yao
    2. mke achague kukaa na wewe au aende kwa awapendao zaidi.

    ReplyDelete
  22. Wake zetu si waaminifu ndio maana vipimo hivyo inabidi vituke ili kuweka mambo sawa pale kwenye utata,Unakuta mke wa mtu yuko na mtu mwingine ukiimuuliza anakwambia simpendi nililazimishwa tu kuolewa nae ndio maana niko na wewe.
    tena unapoanza mahusiano nae anakwambia sijaolewa {Binafsi nilishakutana na mke wa mtu na kuwa na mahusiano nae kwa muda mrefu bila kujua akidai hajaolewa kumbe mume wake ni mtu wa biashara za kusafiri}
    Kwa wewe uliyetaka msaada ukikuta mtoto si wako basi mama akueleze mwenyewe na utaamua ufanye nini maana siku zote mama ana uhakika na mtoto kuwa ni wake lakini Baba ni mashaka.

    ReplyDelete
  23. Inabidi kuwa makini tunapoamua kwenda kupima DNA. Nenda kapime DNA kama kweli "NI MUHIMU SANA".

    Kwa wale ambao tunafanya/tumeshafanya kazi maabara huwa inatokea wakati mwingine sampuli zinakuwa "CONTAMINATED" au "MIXED UP", au "MISHANDLED". Na ndiyo sababu katika kesi kubwa mahakamani, lazima aliyepima sampuli ataitwa mahakamani aelezee namna alivyochukua/alivyopokea sampuli, alivyoihifadhi, alivyoipima, na alivyothibitisha majibu ya sampuli husika. Wale wanaofahamu/wanaokumbuka kesi ya OJ Simpson Marekani, vielelezo vya DNA vilitupiliwa mbali mahakamani kwa kuwa havikuwa vimechukuliwa na kuhifadhiwa kwa umakini. Endapo mahali kama Marekani ambapo kuna umakini mkubwa vipimo vya DNA vinaweza kuwa na kasoro ndiyo sembuse Tanzania?

    Kama sampuli yako na mtoto hazikushughulikiwa kwa umakini na vitu hivi vikajitokeza, mnaweza kupata matokeo ambayo mkiyaamini na kuyafuata yatakuwa ni majuto maishani.

    Pia nadhani kwa kweli cha muhimu ni mahusiano mazuri kati yako na "MWANAO". As long as mtoto anakutambua na kukupenda kama BABA inatosha sana. Kama mkeo aliiba nje, hayo mwachie mwenyewe kwa kuwa nafsi itakuwa inamhukumu siku zote za maisha yake. Hiyo peke yake ni adhabu kubwa kupita kiasi.

    Inawezekana pia mpima DNA akawa ni jamaa/jirani mliyekuwa mnagombania DEMU siku za nyuma, akaamua kukushughulikia/kukukomoa kwa kukupa majibu mabovu.

    CHUNGA SANA!!!!

    ReplyDelete
  24. kupima ni vizuri mno lakini kama ukikuta mwana si wako kabla hujaamua kitu fikiria nyuma mawifi,mashemeji na wazazi wako walikuwa wanatoa kashfa kwa mkeo anajaza choo bila kujua siri ya mtungi au wewe baba ulikuwa unatimiza wajibu wako. then chukua uamuzi

    ReplyDelete
  25. Baba UbayaApril 21, 2009

    huyo aliyesema swali kuhusu DNA ni la kipumbavu nadhani yeye ndo mpumbavu mkubwa.
    kama una mashaka makubwa juu ya mtoto/watoto kama ni wako au la ni vyema kwanza kuongea na mkeo/mpenzi wako juu ya wasiwasi wako.kama maelezo ya mwandani wako hayajitoshelezi basi si vibaya mkakubaliana kwenda kupima hiyo DNA.
    kama mtoto ni wako ama si wako hayo mengine itakuwa ni juu yako muhusika.ktk suala la mahusiano ya ndani kama hayo ni vigumu kusikiliza watu wakueleze cha kufanya.kama kusuka ama kunyoa hiyo itakuwa juu yako.
    lakini kumbuka pia kama mtoto atakuwa ni wako basi huenda huyo mkeo/mpenzi wako naye akaanza kukuelewa vibaya zaidi kwa kumwona si mwaminifu.hivyo basi ushauri baada ya matokeo ya DNA hiyo itakuwa juu yenu wahusika.lakini tu fanyeni kile chenye manufaa kwa pande zote tatu(baba,mama na huyo mtoto/watoto).

    ReplyDelete
  26. ee bwana ee kapimeni. acheni unafiki. una wasiwasi halafu unamwogopa mkeo. atakuletea wengine hadi ukimwi.

    wewe dada unasema kuwa akienda kupima harudi. mtaishije wakati unajua kabisa kwamba atajua ukweli.

    nadhani tukipima sana itapunguza ukimwi kwani watatumia kondomu.

    ReplyDelete
  27. KITANDA HAKIZAI HARAMU

    ReplyDelete
  28. Kupima DNA ni jambo la busara sana na kila mtu anapaswa kufanya. Watu wengi wanadanganywa na wanawake kuwa watoto ni wao ilihali kweli. Iwapo ukikuta mtoto si wako wa kulaumiwa ni mwanamke, hilo halina ubishi na wala halitakiwi kuulizwa. Mtu yeyote anayekataa ukweli usijulikane ni muongo (cheater). Mimi kama ni mumeo au baba watoto wako wa kweli na wewe unania ya kuishi nami na umenizalia watoto kwa nini ukatae kupima DNA? Utakataa tu kwa kuwa unajua kuwa mtoto si wangu au huna uhakika ni wa nani kwa kuwa kipindi ulichopata ujauzito ulikuwa ukitembea na watu wengi bila kutumia kinga. Mwanamke anayesema kuwa ukienda kuwapima watoto DNA huniamini na nitaondoka, muache aende hakufai hata kidogo, kwa nini akatae ukweli kujulikana. Hii inamaanisha kuwa anakudanganya mambo mengi zaidi ya huyo mtoto. PIMA DNA ujue ukweli, upumbavu wa watu wachache usikufanye kujua ukweli. Na ukijua kuwa watoto si wako achana na huyo mwanamke, ni mshenzi na hakufai, huna sababu yeyote ya kuhangaika kulea watoto wa wenzako wakati unao uwezo wa kuzalisha wa kwako. Kubali ukweli kuwa mwanamke hakupendi na kakuchagua kukuumiza tu na kukutia mzigo ambao hukupaswa kuubeba. Haya mambo ya malipo ni kwa mungu ni ushenzi mtupu. Usijitie kwenye kitanzi kwa kutegemea kulipwa kwa mungu kwa kuwa hata mungu mwenyewe anasema anataka uishi maisha yenye raha si karaha. Hakuna sababu ya kushirikiana na mtu mwongo kwa kuwa ndimi zake ni sumu kama ulivyo moyo wake. Achana na mshenzi huyo, tafuta mwanamke atakayetaka kukuzalia watoto na kuona fahari na kukubali kupima. WATU TUAMKENI

    ReplyDelete
  29. KITANDA HAKIZAI HARAMU? Ni kweli lakini kwa baba halisi wa mtoto si kwa kusingizia asiyehusika. Yaani kwa ufafanuzi zaidi, si haramu kwa yule walolala pamoja na kutiana mimba ya huyo mtoto, kumsingizia mtu mimba ni haramu kubwa sana.

    ReplyDelete
  30. Wabongo si mchezo, ni elimu hatuna au ni unafiki unatujaa? Mtu anauliza, ukigundua kuwa watoto si wako hiyo aibu utaiweka wapi? Siamini macho na masikio yangu. Kwa mkeo kuzaa nje tu ni aibu tosha na hasa kama hujui na watu wote nje wanafahamu kuwa mtoto wenu na mkeo ni wa masawe muuza duka. Watu wanakucheka kila siku ukipita mbele yao wewe hufahamu. Pima DNA na ukijua kuwa mtoto si wako, huna sababu yeyote ya kuona aibu achana na huyo mshenzi mwanamke tafuta demu mwingine mzuri zaidi yake na akuzalie mtoto. Huna sababu yeyote ile ya kuogopa kumueleza mkeo au mpenzi wako kwenda kupima DNA na hasa kama kasema kuwa mtoto ni wako, anachokataa kwenda kujua ukweli ni nini kama siyo kakucheat na kuzaa na mtu mwingine? Acha ujinga, nenda kapime na akiondaka achana naye kabisa usimfuate kamwe.

    ReplyDelete
  31. MBONA MNAWASAKAMA WANAWAKE??? WABABA WANGAPI WAMEOA NA WANAWATOTO NJE YA NDOA?? MBONA WAKE ZAO HAWAWAFUKUZI NA KWENDA KUOLEWA NA MUME MWINGINE???? WATANZANIA STOP UJINGA MUANGALIE VITU IN A BROAD PICTURE THEN UJAJI!! SIYO MNASEMA TU WANAWAKE WALIOOLEWA SIO WAAMINIFU WAKATI KUNA WANAUME WENGI TU AMBAO WAMEOWA NA SIO WAAMINIFU!! AU KWASABABU HAMBEBI MIMBA???KWANI HAO WANAWAKE WANACHEAT NANANI KAMA SIYO NYIE WAPUMBAVU???

    HILI GAME LIKO FAIR WEWE LEA MTOTO TU AWE WAKO AU LA COZ HATA WEWE KUNA MTU ANAKULELEA MTOTO WAKO!!! GROW UP WANAUME WAKIBONGO!!!

    ReplyDelete
  32. kwakweli na muunga mkono anon.april22,2009 7:50 mimi naona haina haja ya kupima dna kamahakuna sababu maalum,mimi banafsi nilishafanya ushenzi huo na binti yuko kidato chapili,kwahiyo ikinitokea mimi nitasamehe kwasababu na mimi nilisha mfanyia mwenzangu.maana sijui nahasa wanaume na wanawake wa kiTanzania kwa kutongozeana ni hatari wengine wanajitongozesha.

    ReplyDelete
  33. waliojibu izi jazba utajua tu WANAUME,,,
    annon apo juu safi sana uliesema ivi ao wanawake wanazaa na kina nani???nyani au??

    hakuna wazinzi kama wanaume ndo mnaotongoza ao wake za watu mwawalala na kuwapa mimba,so tit for tat,,,mtabeba tu ao watoto.
    afu,tunawazibia AIBU zenu nyie waume kwani weeengi tu hamzai,mbegu zimebomoka so kuwafichia aibu zenu.
    pia,mbona sie tunawakubali watoto wenu wa NJE ya ndoa???tena wamficha mkeo adi siku labumbuluka mke akubali yote kwa masononeko.
    ivi,tukisema nani anaesambaza UKIMWI ktk ndoa mtasemaje???????nani jicho humtoka kwa mwezie/kumtamani????
    mbona wee MUME WA MTU UNAKULA WA NJE/MKE WA MTU??

    life s like tht bongo,wachache sana wenye uwezo wa kuhimili majaribu ya ngono,kila mtu hujaribiwa ktk hili!!!

    kwa ufupi "UKITAKA KULA SHURTI NAWE ULIWE KIDOGO"

    ReplyDelete
  34. Naona kuna watu wanataka toka nje ya topic, kama anon wa april 22 7:50 na 9:40.
    Inamaana kama wewe umeiba(mwizi) ukasamehewa na mimi si mwizi na naona naibiwa nikae kimya eti kwa kuwa kuna watu wengine wezi? kwahiyo kama mtu unawasiwasi ni bora kupima hata kama wanaume wengine wanacheat na wewe haucheat basi ubebeshwe matatizo kwa kuwa wanaume wengine si waaminifu?
    Hiyo topic ya wanaume wanazaa watoto nje ya ndoa nazani ni tofauti na DNA. Tafute muda na nyinyi muweke hiyo topic watu waijadili

    ReplyDelete
  35. Kama mwanaume ana wasiwasi na mtoto then na afanye DNA as long as analipa mwenyewe. The father of my child aliambiwa na watu kua mtoto si wa kwake mi nikamwambia kama huamini go for DNA he never did cos is a bit expensive hapa Ukerewe. Bongo inacost kiasi gani?

    ReplyDelete
  36. hapa jibu ni rahisi tu!!
    1.chanzo cha kutaka kupima ni kuondoa mashaka uliyonayo au utata uliopo, hivyo KUPIMA DNA NI KUZURI)))).
    2.Kama mashaka yako yamethibitika kuwa ulidanganywa-ALAUMIWE MDANGANYAJI.
    3.Uamuzi wa kuchukuwa kama utakuta ulidanganywa utategemea na mtizamo wako na halihalisi ya swala lenyewe:-
    a). baba wa damu wa huyo mtoto yukohai au kafa?
    b)mtoto ni mdogo au mtu anaye jitegemea ktk maamuzi?
    c}.uhusiano kati yako na mtoto ukoje mzuri au mbaya.
    d).unakubali kwa hiari kumchukua na kumlea kama sehemu ya familia yako au moyo wako hauridhii kufanya hivyo.
    e). unaamua kumwadhibu mdanganyaji au kumsamehe na kusahau!!))))))))))))

    ReplyDelete
  37. lakini kunawanawake wengine anafanya makusudi ili apate mbegu ya mwanaume furani.halafu kunahistory fulani huko mikoa ya bara kuna baba mmoja alimkataa mtoto ila mamayake alimsamehe,matokeo yake yule mtoto akalelewa na wajomba zake wakamsomesha lakini ndiye alikuja kuwasidia wale ambao walionekana ndio wa huyo baba,kwavile yeye alikuwa mweusi kakazake walikuwa weupe basi akawa pailot wa ndege,akawasaidia wadogozake muda mwingine inasaidia maana unachanganya damu nzuri mtoto akiwa jambazi ndio majuto.Lakini zaidi ni kusamehe hakuna asiyeenda nje ya ndoa ila mtenda akitendewa hujisikia vibaya.Kwahapa tz watoto wataachwa wengi watu wakitaka kufanya hizo dna zao

    ReplyDelete
  38. NA IKIJULIKANA MTOTO NI WAKO BAADA YA DNA,,,utajuta maishani mwako mwote why ulim-doubt mkeo na ndio kifo cha pendo/penzi la dhati kati yenu wawili,yan mkeo hatakuamini milele,na je na wewe ukabambika mke wa mtu na analetwa mtoto kwa mkeo home itakuwaje???

    nani anahitaji msamaha/haki zaidi ya mwezie,,,think yu people

    kwa mazingira ya laboratory zetu bongo sijui majibu yanatokaje,mtajaza wenyewe,,,

    JIBU UNALO WEE MWENYEWE NA MKEO UMO NDANI

    ReplyDelete
  39. TATIZO SIKU ZOTE LINAAZIA KUSIKILIZA MANENO YA "WATU/NDUGU"

    ilhali nyie wawili wala hamkuona hilo toka mtoto azaliwa adi kakua.ndo mana ndoa hazidumu.wee kama ulimla mke wangu/mume sii nyamaza kivyako na relations zenu uko nyuma??

    kimpango wako kivyako

    shenzy

    ReplyDelete
  40. usiogope kupima dna kwa kuhofia utaonekana humwamini mkeo. Kimsingi sisi ni watu na hatuko kamili. Kama penzi likiisha taanzisha jingine.

    Tusiendekeze uaminifu zembe.

    ReplyDelete
  41. kwa mtu yeyote anaye jiamini haogopi kuwa edited(kukaguliwa)! watu wanaohofia eti mkeo atakuelewaje nadhani wana matatizo!! sisi ni binadamu,huwezi kunilazimisha kuamini kuwa kila anachofanya mwenzangu anafanya kwa usahihi!! nina haki ya kuwa na mashaka,nina haki ya kuuliza,na pia nina haki ya kuondoa mashaka yangu kama inawezekana kufanya hivyo! na yeye pia ana haki hizohizo anapokuwa na mashaka juu yangu.
    wala hiyo haipunguzi upendo,nadhani inauongeza zaidi pale unapo juwa kuwa mwenzio yuko wazi kwako 100%))))))))
    mimi DNA nipima kila mtoto wangu,tena sio kwa siri bali kwa uwazi na kwa kumshirikisha wife,tena wakiwa bado wangali wadogo kabisaaaa!)))))))))
    na yeye akitaka uwanja uko wazi any time any where!anahaki ya kuhoji na kujiridhisha kuwa hakuna utata ktk ndoa yetu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...