POLE NA KAZI KAKA, 
WAPE WADAU HILI LIBENEKE MAANA HATA NASHINDWA
KULIKATEGORAIZI SIJUI LA TASWIRA OR.....HEHEEE NILIKUTANA NALO NIKIWA
VEKESHENI YA PANDE ZA IRINGA PASAKA HII.....
KWELI BONGO TUPO JUUU BRODAA..!!!!

Eddymak,
Mdau wa libeneke!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Wabongo wabunifu ila basi tu. Toyota wenyewe hawajashtukia uwezekano wa kutengeneza dabopanya wakati sisi tumeliona. Hapa ndio kutafuta ufumbuzi wa ndani kwa matatizo yetu ya ndani.
    Nyumbu, mpo?

    ReplyDelete
  2. Nakubaliana na mdau hapo juu hii kweli kiboko maana oo double coaster kumbe kuna double hiace aaa hii kiboko
    yaani ntajaribu kuwaonyesha hii picha hawa jamaa hapa ughaibuni zinakotoka hizo hiace naona watachoka wenyewe.
    Panya kuwekewa teriaz hii kiboko!!!
    mdau JP

    ReplyDelete
  3. Wazee,
    Sio Hiace tu hata FUSO zenyewe zikija hapa Bongo break ya kwanza Iringa. Huko inafumuliwa body lote na kusukwa upya. Wao wanaita kuweka double chasis. Ndio maana Fuso zinazidisha mzigo na Mjapan anabaki kushangaa.

    ReplyDelete
  4. tufanye mambo 3,
    1, tulifanyie uchunguzi wa kitaalamu ili kuepusha madhara

    2, tuliwekee 'TBS'

    3, Tulifanye liwe rasmi na hao mafundi wapewe mtaji wa kufanya makubwa zaidi

    Bila hivyo inaweza kuwa madhara kwa mtumiaji kwani brake nk zilitengezwa kwa uzito fulani nk nk

    ReplyDelete
  5. Mjep akishtukia hao jamaa anawashtaki. wamuulize Rajinder wa moshi rsaafrica.com

    ReplyDelete
  6. MDAU12:50PM,TIBIESI YA TANZANIA WANASUBIRI MATOKEO UKIUMWA TUMBO NDIO WANAFANYA UCHUNGUZI WANINI UMEKULA,LABDA TUSUBIRI T.B.S YA JAPAN.


    NAWAKILISHA

    ReplyDelete
  7. Mdau umenikumbusha mbali,hiyo hiace niliiona iringa miaka kama 4 iliyopita,ilinifurahisha sana,hapo ilipo panaitwa Mwanyingo au njia panda ya mkimbizi kwa Shayo,Wadau wa Tumaini university nadhani wananipata vizuri.Watanzania wabunifu sana.

    ReplyDelete
  8. Mdau umenikumbusha mbali,hiyo hiace niliiona iringa miaka kama 4 iliyopita,ilinifurahisha sana,hapo ilipo panaitwa Mwanyingo au njia panda ya mkimbizi kwa Shayo,Wadau wa Tumaini university nadhani wananipata vizuri.Watanzania wabunifu sana.

    ReplyDelete
  9. Bado ipo Iringa hiyo, mie niliiona This Jan.

    Hapo ilipo panaitwa MWANG`INGO sio Mwanyingo.

    MWANG`INGO ni jina la ukoo fulani wa kabila la WAHEHE waishio IRINGA. Originated TANANGOZI nje kidogo ya mji wa Iringa.

    Ni hayo tu wadau.

    ReplyDelete
  10. nyela bela kiki ichooo??
    swelaga tutafika tu wanyalu wa kuboma

    mmenibariki saaaaaaaaaaaNAAAAAA safi sana mko juu.

    wanyalu tuna akili saaaana tu sema tu hatujikwezi na maringi km makabila fulani ivi!!

    aluta kontinua

    ReplyDelete
  11. ......Double hiace vipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...