Habari yako bwana Michuzi. Tunakawakaribisha wadau kutembelea libeneke la Varsity College Tanzania. Hapa wasomi wanakutana na kuzungumzia maswala mbalimbali muhimu kwa maendeleo ya Tanzania
Ahsante

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. MICHUZI, niko nje ya mada. Lakini hii story imeifanya Tanzania kusubiri kwa hamu.

    Habari za kuaminika ni kwamba Mrisho Ngassa hakubahatika kuingia hatua ya pili ya majaribio katika timu ya West Ham.Na tayari ameagizwa kupanda ndege kurejea Tanzania.

    Sababu zinazotajwa ni kushindwa kwake kumudu mchakato wa majaribio - fitness na awareness.

    Lakini pia kulikuwa na utata wa nyaraka zake. Mengi mtasikia zaidi BBC leo jioni.

    ReplyDelete
  2. Kama ni yawasomi unatutangazia umu kwa nini? si ukatangaze kwa wasomi wenzako

    ReplyDelete
  3. Anon wa kwanza sikuamini mpaka nione ktk news.Jamaa alitakiwa kuwa ktk training kwa wiki moja. Sasa hata wiki haijaisha wameshaona hafai? Kuna walakini hapa.

    ReplyDelete
  4. Anony wa pili, acha gadhba. Kama hutaki kwenda kutembelea libeneke yao, usiende. Kuna watu wa kila aina hapa, sio wote tunafuata starehe tu.

    ReplyDelete
  5. Anonymous wa pili kama ulikmbia umande sio sisi tuliokutuma, kama haikuhusu si unakaa kimya...mbona kwenye Tv huwa kuna matangazo ya pedi za kina mama na Tv zinatazamwa na watu wa jinsia zote? Au matangazo ya pombe kwani ni watazamaji wote wanaokunywa bia? Hii kama blog ya jamii basi kuna watu wa kategoria mbalimbali. Kuwa muungwana, huna cha kusema kaa kimya sio suala la andika uonekane=sema usikike.
    #@$Ebo$€
    acha uzumbukuku wako hapa, hii website inatusaidia graduates kukutana na marafiki zetu wa zaani waliopo sehemu mbalimbali duniani sasa wewe na mbekule zako...umeniboaaaaaa

    ReplyDelete
  6. AFANDE MIDAKOApril 19, 2009

    POLE SANA ANON WA2..ACHA ROHO YA KOROSHO!
    Hiyo site ni nzuri sana kwa vijana waliopo tz na nje wanaobweteka na vidiploma,advance diploma na degree eti wanajiona wamesoma.! vijana tembeleeni site hiyo muone maprofile ya vijana wadogo wakiTz na wazee waonaojua maana elimu ninini, usije kwenda kuomba kazi na mbwembwe ukajikuta peke yako kwenye interview una bachelor.

    ReplyDelete
  7. AFANDE MIDAKOApril 19, 2009

    KAKA MICHUZI NAOMBA UWEKE TAARIFA HII MUHIMU KWA WATANZANIA, NIMEIPATA GAZETI LA MWANANCHI Date::4/18/2009
    Na Gedius Rwiza

    http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=11423

    ”Jamii inatakiwa kuwa makini wakati mwanafunzi anapotaka kujiunga na chuo chochote kilichopo chini ya NACTE, ahakikishe kama kina usajili na kiwe kimekidhi mahitaji yote muhimu, vinginevyo hatutahusika kwa njia yoyote kwa kuwa mfumo wetu uko wazi na tumeelezea kila kitu,”alisema Mbilinyi.


    Aliongeza kuwa kwa sasa kuna baadhi ya vyuo ambavyo bado vinaendelea kutoa kozi ya Astashahada ya juu, wakati katika mfumo wa baraza hilo hakuna kipengele kinachoruhusu chuo chochote kilichopo chini yao kutoa kozi hiyo na kwamba yote hayo yanatokana na baadhi ya watu kushindwa kufuatilia mfumo wa NACTE.


    Aliwataka wanafunzi wote wanaotaka kujiunga na vyuo vilivyopo chini ya NACTE, kuonana na uongozi wa baraza hilo ili wapewe maelekezo pale watakapokuwa hawajaelewa juu ya mfumo wa baraza hilo na kwamba kama kila mtu ataelewa mfumo huo hakuna migogoro itakayojitokeza tena kati ya uongozi wa vyuo na wanafunzi.

    ReplyDelete
  8. AFANDE MIDAKO,,,hahahahaaa
    umeniacha hoi na iyo sentence nanukuu;

    "usije kwenda kuomba kazi na mwembwe zako ukajikuta peke yako kwenye interview una BACHELOR"

    kwakweli

    ReplyDelete
  9. astashahada ni certificate,diploma au advance diploma

    tafadhali nieleweshwe kidogo apa

    km huna jibu usitukane apa

    asanteni

    ReplyDelete
  10. NGASSA KATOLEWA JAMANI IMENIUMA SANA

    ni habari za kweli BBC ijumaa/jumamosi nimesikia mwenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...