Yesterday on the way back to work after our daily lunch break around 2.30pm, on the Itihad road, I spotted this man in his mid-fiftees 
Taking a walk in the busy road...
Luckily I had my camera, I took some shots of this strange event.... It took ten minutes for the police to arrive at the site and invite him nicely 
To their car...
Seems that he lost all his money like many here... To be stripped of all your belongings could probably push you to strip off your clothes!
Any other reason you think of why a man should walk naked IN DUBAI!
Cheers
Mdau wa Dubai
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Holy shiiit !! I think that is the outcome of ongoing Global financial crisis, here in states every now and then you hear murder suicide and it’s very sad to see people venting their financial difficulties by wiping out their entire families.

    ReplyDelete
  2. Mimi nafikiri huyo mjamaa yuko kwenye summer time kwa hiyo alikuwa anapunga hewa baada ya joto kali la udosini/jangwani

    ReplyDelete
  3. Mchungaji wa Deci azua balaa Dar

    2009-04-23 14:55:10
    Na Romana Mallya na Sharon Sauwa


    Mwenyekiti wa Kamati ya Dharura ya kampuni ya Development Entrepreneurship Community Initiative (Deci), Mchungaji Isaac Kalenge, jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kutimuliwa kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) kutokana na kumkashifu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

    Mchungaji Kalenge ambaye alilipia ukumbi huo kwa nia ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya Deci, alijikuta akitolewa nje kutokana na kitendo chake cha kusema kuwa Waziri Mkuu Pinda ``aliropoka`` na kupotosha kiasi cha fedha kinachomilikiwa na kampuni hiyo.

    Baada ya kusema hivyo, Ofisa Habari wa Maelezo aliyekuwa akisimamia mkutano huo, alimtaka afute kauli hiyo na azungumzie masuala ya kampuni yake na siyo kumdhihaki kiongozi wa serikali.

    Baada ya kauli hiyo, yalitokea mabishano kati ya waandishi wa habari, Maofisa wa maelezo walikuwa kwenye mkutano huo na Mchungaji Kalenge ambapo hata hivyo hayakufua dafu na badala yake taa za ukumbi zilizimwa na mkutano kuvunjika.

    Mkutano huo ambao ulitakiwa kufanyika kwa saa moja, ulifanyika kwa takribani dakika 15 na waandishi kutakiwa kutoka nje ya ukumbi ambao ulifungwa, lakini baadaye mchungaji huyo aliamua kuufanya chini ya mti uliopo nje ya jengo la Maelezo.

    Awali, Mchungaji Kalenge alianza mkutano huo kwa kumtaka Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuacha vitisho dhidi ya wanachama wa Deci.

    Alisema anashangazwa na hatua ya Kova kuwakataza wanachama wa Deci kukutana, ilihali Jeshi la Polisi linakutana na vigogo wa kampuni hiyo kwa siri wakati wao (Kalenge) ndio wenye fedha na vigogo wanaokutana na polisi wamepewa dhamana ya kutunza fedha hizo.

    Alisema kitendo cha Kamanda Kova kukataza wanachama wa Deci kukutana ni kinyume cha elimu ya polisi jamii inayosaidia kukamata wahalifu.

    ``Kova anapaswa kufahamu kuwa wanachama wa Deci wameshatambua kwamba fedha zao zimetapeliwa na kampuni hiyo na ndio maana wanahitaji kukutana ili waweze kutoa taarifa kamili za uhalifu huo kwa vyombo vya usalama, vinginevyo wasipopewa nafasi ya kutoa mawazo katika mikusanyiko ni hatari kwa viongozi wa Deci ambao wanaweza kuvamiwa na ikawa aibu kwa Jeshi la Polisi,`` alisema.

    Aliongeza kuwa wanayo taarifa kwamba viongozi wa Deci wameanza kurejesha fedha (mbegu) kwa wateja waliopanda hivi karibuni ambao hawajawahi kuvuna na pia maaskofu, wachungaji na vigogo wa serikali waliopanda zaidi ya Sh. milioni 10 wamerejeshewa mbegu zao na mavuno kinyemela.

    ``Tunasema huu ni ubaguzi na dhambi kwani ni kinyume cha maadili ya kanisa, tunaliomba Jeshi la Polisi lishirikiane na sisi wanachama tuliotapeliwa ili tuwafikishe vigogo hawa mahakamani ili Jeshi liweze kujenga imani kwa wananchi,`` alifafanua.

    Kwa mujibu wa Kalenge, zaidi ya wanachama 500,000 wenye kipato kidogo wametapeliwa alisema ni kundi kubwa la wapigakura hivyo ni hatari kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiusalama.

    Kadhalika, alisema wanachama wa Deci hawana imani na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kutokana na kile alichodai kuwa amekuwa akitoa kauli zenye utata.

    Alisema pamoja na kwamba serikali inaikataa kampuni hiyo, yenyewe pia ni mwanachama na imekuwa ikichukua Sh. milioni 120 kila mwezi zinazolipwa na Deci kama kodi.

    ``Tunachotaka kukieleza ni kwamba sisi tuna mkataba na Deci, lakini tunashangaa kusikia eti serikali inachunguza majina ya wana-Deci bila kushirikisha wanachama,`` alisema.

    Katika hatua nyingine, uongozi wa Deci umetangaza muda wa zaidi ya wiki sita kwa ajili ya wateja wake kujiorodhesha katika ofisi zake ili waweze kurejeshewa mbegu walizopanda.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Timoth Ole Loiting`ye, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa zoezi hilo lilianza juzi ambapo wanachama walianza kujiorodhesha katika ofisi hizo wakianzia na wateja waliopanda Aprili mwaka huu.

    Hata hivyo, alisema baadhi ya wafanyakazi wao katika ofisi za Kisarawe mkoani Pwani walikamatwa na polisi wakati wakiendesha zoezi hilo kwa madai kuwa walikwenda katika ofisi hizo kwa lengo la kuiba.

    Mkurugenzi huyo alisema baada ya kupata taarifa hiyo, walichukua hatua ya kuwasiliana na polisi ambapo waliachiwa na kuendelea na zoezi hilo ambalo litawahusu wateja ambao hawajawahi kuvuna tangu kupanda kwa mbegu.

    ``Si sahihi kuwakamata kwa sababu kinachofanyika sasa ni makubaliano ya pamoja kati ya tume iliyoundwa kwa ajili ya kushughulikia jambo hili ambayo inaongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba,`` alisema wakati akihojiwa na kituo kimoja cha redio jijini jana.

    Alisema kinachofanyika katika ofisi zote ni kuorodhesha majina ya wateja ambao walipanda mbegu zao na hawajawahi kuvuna, tayari kwa kuanza zoezi la kuwalipa fedha zao katika utaratibu utakaotangazwa baadaye.

    Hata hivyo, hatua ya kuanza kulipa watu waliopanda Aprili mwaka huu kurudi nyuma, imelalamikiwa na wateja hao kwa madai kuwa waliopaswa kuorodheshwa kwanza ni wale waliopanda kuanzia mwaka jana.

    Anna Abdallah alitaka kurekebishiwa kwa utaratibu wa kulipwa mbegu zetu kwa kuanza na watu ambao wamepanda mbegu zao zamani na kisha kufuatiwa na wale wa Aprili.

    ``Tulikuwa tunaomba tuanze kulipwa sisi tuliopanda mwaka jana na kufuatiwa na wale ambao wamepanda hivi karibuni yaani Aprili mwaka huu,`` alisema.

    Akijibu malalamiko ya wateja hao, Loiting`ye, alisema walitumia utaratibu wa kuanza na wale waliopanda mbegu Aprili mwaka huu na kumalizia wale waliopanda mwaka jana, ili kurahisisha zoezi hilo.

    Hata hivyo, alisema wateja hao hawana haja ya kuhofia kwani wote waliopanda mbegu zao watalipwa kama walivyopanda.

    Wakati sakata la Deci likiendelea kufukuta, viongozi wawili wa kampuni nyingine ya upatu inayojulikana kwa jina la Masebe wamekamatwa jijini Dar es Salaam.

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema jana kuwa, jeshi lake limefanikiwa kuwatia nguvuni viongozi hao aliowataja kuwa ni Beno Thadei (32) mkazi wa Makumbusho na Samwel Tupa (35) mkazi wa Temeke.

    Alisema watu hao walikamatwa juzi katika ofisi za kampuni hiyo ambayo inajishughulisha na biashara ya kupanda na kuvuna fedha, zilizopo Buguruni.

    ``Baada ya kupata taarifa, polisi walifika eneo hilo na kuweka mitego yake ambayo ilifanikisha kuwanasa baada ya upekuzi ndani ya ofisi hizo, polisi walikuta vitabu vya risiti na mihuri vitu ambavyo tunavishikilia kwa ajili ya upelelezi zaidi,`` alifafanua.

    Aliongeza kuwa kwa sasa jeshi lake linaendelea kuwahoji watu hao ili kubaini uhalali wa kampuni hiyo, idadi ya wanachama na masuala mengine yanayohusu biashara hiyo.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  4. Mdau wa Dubai, Dubai ni nchi ama sehemu ya nchi?

    Kuna nabii mmoja hapa aliwahi kutangaza Dubai ni nchi na waumini wake wakaamini.

    ReplyDelete
  5. Its so sad to read and hear about whats going on in Dubai. Most people, espeacially expatriates are losing their jobs and end up living in the streets. Apparently, being bankrupt is not an option. Not being able to pay your bills can get you a jail sentence. We should really be aware of the laws of countries we go to and be prepared just in case anything were to happen. Poor guy.

    ReplyDelete
  6. Ooooh!You never know,pengine jamaa mbegu alizopanda deci zimekufa!!

    ReplyDelete
  7. Kredit Kranch hiyo kaka!

    ReplyDelete
  8. Global warming

    ReplyDelete
  9. Itakuwa sababu kubwa ni joto ndani ya Dubai kwa hiyo ameamuwa kuvuwa nguo zake ili apate hewa pia inawezekana alikuwa anhitaji apate ile rangi ya Brown kama wanvyo fanya wazungu wengi kule ulaya siku za juwa kali

    ReplyDelete
  10. mdau wa April 24, 2009 5:54 AM mbona hufahamiki? nabii/ ni nabii gani ni wakati gani na unaposema hapa unamaanisha nchi gani?

    ReplyDelete
  11. Huyu ni Phiri mwenda uchi au nani vileeeeee?

    ReplyDelete
  12. Huyo jamaa ana matatizo ya kiafya yaani mental illness.Si jambo la utani na kuzua balaa,bali wote tuombe dua ili Mwenyezi Mungu atupe neema ya kiafya na kimali...ameen,na Mola amsaidie huyo jamaa!

    ReplyDelete
  13. BIASHARA MATANGAZO; ASIJE KUWA ANATANGAZA BIASHARA
    AHSANTE BWANA MICHUZI

    ReplyDelete
  14. Where is our faith? Money or God? That is what can happen when money becomes our God.

    ReplyDelete
  15. Huyu lazima atakuwa yule Mwingereza anayesifika kwa ku-crash football games or events kwa kukimbia uchi.Nudists noma kweli.

    ReplyDelete
  16. I think before you post out a nasty comment inabidi mfikirie.

    Si mambo ya kucheka au kukebehi, ukiona mwenzio ananyolewa we anza kutia maji.

    Hii crisis haina mjanja wala mwenye akili it has touched even the most brilliant, wisest and intelligent people. Iliyobaki tumuombe Mungu atuepushe na janga hili na amuondeshee mwenzetu. Ameen

    ReplyDelete
  17. kama hii imetokea jana au juzi huyu atakuwa mtu wa pili kufanya hivi, weeks ago kuna jamaa alikutwa karibu na city center hapa dubai akiwa kama alivyozaliwa.

    ReplyDelete
  18. Its so sad to see a human being walking nude in the streets. What I can say is, life is like a cycle, whatever happens to your fellow today, will come to you tomorrow. This is applicable when the thing called economic crunch takes place. Lets pray for him/ those and ourselves too..

    ReplyDelete
  19. Read more:

    http://news.bbc.co.uk/panorama/hi/front_page/newsid_7986000/7986756.stm

    http://www.independent.co.uk/opinion/commentators/johann-hari/the-dark-side-of-dubai-1664368.html

    I hope Michuzi you will publish this!

    ReplyDelete
  20. The guy seems to enjoy the weather, as far as I know it is too hot in dubai around summer time

    What you all think ???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...