Mkuu wa udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza(katikati)akiongea na waandishi wa habari kuhusu Tuzo droo kubwa ya mwaka mwezi mei ambapo mshindi atajinyakulia shilingi Milioni 100. Kushoto ni Meneja bidhaa Boniface Emmanuel na kulia ni Meneja wa huduma na bidhaa Elihuruma Ngowi.
Vodacom Tanzania itachezesha Droo ya mshindi wa Tuzo droo kubwa ya mwaka mwezi Mei ambapo mshindi atajinyakulia shilingi milioni 100.
Hadi sasa Vodacom Tanzania imeshatoa zawadi ya zaidi ya shilingi milioni 797 fedha taslim kwa wateja wake kwa kipindi cha miezi 11 iliyopita.
Akizungumza Jijini, Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza alisema kwamba mbali na fedha taslim kampuni yake imewazawadia wateja wake 5,100 jumla ya shilingi milioni 255 ambao wameshinda muda wa maongezi wa shilingi 50,000 kila mmoja.
Alifafanua kwamba wateja 357 walizawadiwa fedha taslim kwa upande wa shilingi milioni moja moja ambazo hutolewa kwa wateja saba kila wiki sanjari na wale wa shilingi milioni 40 ambazo hutolewa kwa mshindi mmoja wa kila mwezi.
“Kwa kuwa tunaelekea mwisho wa programu hii na droo kubwa kuchezeshwa mwezi Mei, natoa wito kwa wateja wa Vodacom waendelee kufuatilia programu zetu hizo za Tuzo Droo na Tuzo Pointi,”
Alisema katika Droo kubwa ya mwisho mshindi mmoja atajishindia fedha taslim shilingi milioni 100.
Rwehumbiza alisema Vodacom Tanzania mapema mwezi Machi mwaka jana ilianzisha programu ya uaminifu ya tuzo pointi/Droo lengo likiwa ni kuwashukuru wateja wa Vodacom Tanzania kwa kuufanya mtandao wa Vodacom Tanzania kuongoza hapa Tanzania.
Alisema hadi sasa Watanzania wengi wameboresha maisha yao kupitia programu hii ya uaminifu, huku wengine wakijenga nyumba za kisasa na kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
“Kwakweli Programu hii imesaidia kuboresha maisha ya Watanzania walio wengi, waliobahatika kushinda ndani ya familia yetu kubwa ya Vodacom Tanzania wameboresha maisha yao,” alisema.
Rwehumbiza anaongeza “Bila Watanzania walio wengi kutuunga mkono tusingefika hapa ndiyo maana tuliamua kutenga zaidi ya shilingi bilioni moja kama zawadi kwa wateja wetu,”
Aliwaomba wateja wa Vodacom Tanzania kuendelea kuifuatilia kwa karibu programu hii kwani miongoni mwao wataendelea kuwa mamilionea.
Alizitaja baadhi ya njia kuu tatu za kujipatia pointi za Tuzo kuwa ni pamoja na mteja wa Vodacom kuendelea kuwa mteja wa Vodacom kwa wiki moja na kuvuna pointi moja.
Nyingine ni za kupokea, kupiga simu pamoja na kutuma ujumbe mfupi (SMS).
hivi voda kila mtu meneja?
ReplyDeletesio voda tu bali makampuni yote ya simu kila mfanyakazi ni meneja!
ReplyDeletelingine ninalojiuliza, hivi kazi za hao mamaneja ni kutangaza promosheni, udhamini, nk tu?