Kamati ya muda ya kuundwa kwa Jumuiya ya Watanzania Northampton inapenda kuwataarifa Watanzania wote waishio Northampton na vitongoji vyake ( Wellingborough, kettering na corby), kuwa tarehe 3 Mei, siku ya jumapili kuanzia saa nane mchana  kutakuwa na mkutano wa kuundwa Jumuiya ya Watanzania waishio Northampton.

Mkutano utafanyika 4TH FLOOR 7-8 THE PARADE 
MARKET SQUARE 
NORTHAMPTON 
NN1 2EA

Watanzania wote mnaombwa kufika kwa wingi ili kufanikisha jambo hili muhimu na kuweza kujadili yale yote muhimu yanayohusu Watanzania waishio Northampton.

Kutakuwa na uchaguzi wa nafasi zote za uongozi, hivyo kufika kwako ndio kufanikisha suala hili muhimu.

-----------------------------------------------

UFUNGUZI WA TAWI LA CCM NORTHAMPTON - UK

Kamati ya muda ya Uongozi wa Shina la CCM Northampton inapenda kuwataarifu wanachama na wakereketwa wote wa CCM kuwa kutakuwa na ufunguzi wa Tawi la CCM Northampton siku ya tarehe 3 Mei kuanzia saa saba mchana na kuendelea.

Mkutano utafanyika 4TH FLOOR 7-8 THE PARADE 
MARKET SQUARE 
NORTHAMPTON 
NN1 2EA

Kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Tawi katika nyadhifa zote za uongzozi, ambao wataliwakilisha Tawi katika mikutano ya Chama katika ngazi ya Kitaifa yaani makao makuu ya CCM UK, Tawi la London.

Ufunguzi  huo utafanywa na kuhudhuriwa na Viongozi wa CCM Tawi la London, wanachama wapya pia mnakaribishwa kuhudhuria uzinduzi huu ambao ni muhimu kwa kila mkereketwa wa CCM.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na kamati ya muda kwa namba hizi;

Don Kay – 07534156334

Hassan (Zenj) -07747785357

Leybab Mdegela – 079545213515

Seleman (kinyozi) -07983977356

WOTE MNAKARIBISHWA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

    ReplyDelete
  2. kumbe northampton kuna watanzania? mimi nilifikiri wote huko ni wasomali na warwanda baada ya kuukana utanzania

    ReplyDelete
  3. Kidumu Chama cha Mapinduzi !
    Hongereni kamati yote kwa wazo hili. Umoja huu ni muhimu kwetu sote hapa Northampton na familia zetu changa najua kaka Jose pia atakuwepo.
    Shime tuhudhurie bila kukosa Meya Kassongo
    Tuhudhurie bila kukosa

    ReplyDelete
  4. Brilliant idea, long overdue !
    Keep on going guys , we are rooted for you !
    John

    ReplyDelete
  5. nyinyi naona sasa mnajitafutia matatizo, takriban asilimia 90 ya mlioko hapo n'hampton tunajua kuwa mumedai ni wakimbizi toka somali na burundi, sasa leo mnaanzisha umoja wa watanzania, wakijatokea watu wa home office mkatanoni mtasemaje? au mshasahau yule jamaa aloshikwa hivi karibuni baada ya kuikwepa interpol kwa miaka 15 imejinasisha mwenyewe pale aliposahu kama anatumia jina bandia na kutowa jina lake halisi alipokwenda job centre?

    ReplyDelete
  6. NINA IMANI KTK AGENDA ZA MKUTANO, MENGINEYO ITAKUWA NI:
    NAMNA YA KUONDOA UFISADI NDANI YA CCM.
    NAWASILISHA

    ReplyDelete
  7. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
    TUNAWAPONGEZA SANA NORTHAMPTON KWA JITIHADA ZENU, TUKO PAMOJA NANYI KUDUMISHA UMOJA WENU, TUTAKUJA KUJUMUYIKA NA NYINYI KATIKA UZINDUZI WA TAWI LA CCM NORTHAMPTON KATIKA TAREHE HIYO ILIYOPANGWA, JE KADI ZA UANACHAMA "CCM" ZITAKUWEPO?
    "CCM HOYEE" MDAU - NORTHAMPTON/UK

    ReplyDelete
  8. Kwa nini muunganishe MKutano wa WATANZANIA na Mkutano wa CCM ? Mimi ni Mtanzania tena halisi sio mwanariadha na vilevile sio mwana CCM sasa nitakujaje kwenye HUO MKUTANO ????????????

    ReplyDelete
  9. ccm juuuuu!!! kuna huyo jamaa anaitwa mr mdegella kati ya hao walioweka namba zao za simu hapo juu. mimi nataka kujua kujua kama ana undugu na kina mdegella wale wa ilula,iringa.kwani mie namjua exaud mdegella yuko dar,je ni jamaa zake? naomba pls rekebisha namba yako ya simu kwani ina 12 digits instead of 11. hamna namba kama hiyo UK. rekebisha namba nikutafute unaweza ukawa na watu wa karibu hapahapa london ila hatujuani. take care. c u in the meeting!!!!

    ReplyDelete
  10. Michuzi naona unapost watu wanavyo sifia tu. Me naona sio kitu kizuri kabisa kuingiza mambo ya siasa kwenye nchi za watu. Hiyo inawafanya watanzania wengine ambao sio ccm washindwe kuja. Mbona watanzania US,Japan na kwingine hawafanyi hayo mambo. Kama mnataka kuanzisha jumuia kwanini msianzishe jumuia ya watanzania badala ya kuingiza vya vya siasi nchi za watu.

    ReplyDelete
  11. Rahim (a.k.a. Dan/Dogo) atakuepo?? maana alifanikisha kweli mkutano wa wabongo akiwa Glasgow-Scotland pamoja na derm wake wa kichagga.

    ReplyDelete
  12. JAMANI MBONA TUNAJICHANGANYA!!! MNAWABAGUWA WANA CCM KWANI WAO SIO WATANZANIA?? KUMBE UBAGUZI HATA SISI TUNAO. MIMI NIKO KATIKA CHAMA CHA WALEMAVU NA NI MTANZANIA, JE MTANIBAGUWA KWENYE UMOJA WENU HUO WA WATANZANIA?? ACHENI ULIMBUKENI, NAOMBA TAFSIRI YA "UMOJA WA WATANZANIA"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...