Kamati ya muda ya kuundwa kwa Jumuiya ya Watanzania Northampton inapenda kuwataarifa Watanzania wote waishio Northampton na vitongoji vyake ( Wellingborough, kettering na corby), kuwa tarehe 3 Mei, siku ya jumapili kuanzia saa nane mchana kutakuwa na mkutano wa kuundwa Jumuiya ya Watanzania waishio Northampton.
Mkutano utafanyika 4TH FLOOR 7-8 THE PARADE
MARKET SQUARE
NORTHAMPTON
NN1 2EA
Watanzania wote mnaombwa kufika kwa wingi ili kufanikisha jambo hili muhimu na kuweza kujadili yale yote muhimu yanayohusu Watanzania waishio Northampton.
Kutakuwa na uchaguzi wa nafasi zote za uongozi, hivyo kufika kwako ndio kufanikisha suala hili muhimu.
-----------------------------------------------
UFUNGUZI WA TAWI LA CCM NORTHAMPTON - UK
Kamati ya muda ya Uongozi wa Shina la CCM Northampton inapenda kuwataarifu wanachama na wakereketwa wote wa CCM kuwa kutakuwa na ufunguzi wa Tawi la CCM Northampton siku ya tarehe 3 Mei kuanzia saa saba mchana na kuendelea. Mkutano utafanyika 4TH FLOOR 7-8 THE PARADE Kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Tawi katika nyadhifa zote za uongzozi, ambao wataliwakilisha Tawi katika mikutano ya Chama katika ngazi ya Kitaifa yaani makao makuu ya CCM UK, Tawi la London. Ufunguzi huo utafanywa na kuhudhuriwa na Viongozi wa CCM Tawi la London, wanachama wapya pia mnakaribishwa kuhudhuria uzinduzi huu ambao ni muhimu kwa kila mkereketwa wa CCM. Kwa taarifa zaidi wasiliana na kamati ya muda kwa namba hizi; Don Kay – 07534156334 Hassan (Zenj) -07747785357 Leybab Mdegela – 079545213515 Seleman (kinyozi) -07983977356 WOTE MNAKARIBISHWA
MARKET SQUARE
NORTHAMPTON
NN1 2EA


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
ReplyDeletekumbe northampton kuna watanzania? mimi nilifikiri wote huko ni wasomali na warwanda baada ya kuukana utanzania
ReplyDeleteKidumu Chama cha Mapinduzi !
ReplyDeleteHongereni kamati yote kwa wazo hili. Umoja huu ni muhimu kwetu sote hapa Northampton na familia zetu changa najua kaka Jose pia atakuwepo.
Shime tuhudhurie bila kukosa Meya Kassongo
Tuhudhurie bila kukosa
Brilliant idea, long overdue !
ReplyDeleteKeep on going guys , we are rooted for you !
John
nyinyi naona sasa mnajitafutia matatizo, takriban asilimia 90 ya mlioko hapo n'hampton tunajua kuwa mumedai ni wakimbizi toka somali na burundi, sasa leo mnaanzisha umoja wa watanzania, wakijatokea watu wa home office mkatanoni mtasemaje? au mshasahau yule jamaa aloshikwa hivi karibuni baada ya kuikwepa interpol kwa miaka 15 imejinasisha mwenyewe pale aliposahu kama anatumia jina bandia na kutowa jina lake halisi alipokwenda job centre?
ReplyDeleteNINA IMANI KTK AGENDA ZA MKUTANO, MENGINEYO ITAKUWA NI:
ReplyDeleteNAMNA YA KUONDOA UFISADI NDANI YA CCM.
NAWASILISHA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
ReplyDeleteTUNAWAPONGEZA SANA NORTHAMPTON KWA JITIHADA ZENU, TUKO PAMOJA NANYI KUDUMISHA UMOJA WENU, TUTAKUJA KUJUMUYIKA NA NYINYI KATIKA UZINDUZI WA TAWI LA CCM NORTHAMPTON KATIKA TAREHE HIYO ILIYOPANGWA, JE KADI ZA UANACHAMA "CCM" ZITAKUWEPO?
"CCM HOYEE" MDAU - NORTHAMPTON/UK
Kwa nini muunganishe MKutano wa WATANZANIA na Mkutano wa CCM ? Mimi ni Mtanzania tena halisi sio mwanariadha na vilevile sio mwana CCM sasa nitakujaje kwenye HUO MKUTANO ????????????
ReplyDeleteccm juuuuu!!! kuna huyo jamaa anaitwa mr mdegella kati ya hao walioweka namba zao za simu hapo juu. mimi nataka kujua kujua kama ana undugu na kina mdegella wale wa ilula,iringa.kwani mie namjua exaud mdegella yuko dar,je ni jamaa zake? naomba pls rekebisha namba yako ya simu kwani ina 12 digits instead of 11. hamna namba kama hiyo UK. rekebisha namba nikutafute unaweza ukawa na watu wa karibu hapahapa london ila hatujuani. take care. c u in the meeting!!!!
ReplyDeleteMichuzi naona unapost watu wanavyo sifia tu. Me naona sio kitu kizuri kabisa kuingiza mambo ya siasa kwenye nchi za watu. Hiyo inawafanya watanzania wengine ambao sio ccm washindwe kuja. Mbona watanzania US,Japan na kwingine hawafanyi hayo mambo. Kama mnataka kuanzisha jumuia kwanini msianzishe jumuia ya watanzania badala ya kuingiza vya vya siasi nchi za watu.
ReplyDeleteRahim (a.k.a. Dan/Dogo) atakuepo?? maana alifanikisha kweli mkutano wa wabongo akiwa Glasgow-Scotland pamoja na derm wake wa kichagga.
ReplyDeleteJAMANI MBONA TUNAJICHANGANYA!!! MNAWABAGUWA WANA CCM KWANI WAO SIO WATANZANIA?? KUMBE UBAGUZI HATA SISI TUNAO. MIMI NIKO KATIKA CHAMA CHA WALEMAVU NA NI MTANZANIA, JE MTANIBAGUWA KWENYE UMOJA WENU HUO WA WATANZANIA?? ACHENI ULIMBUKENI, NAOMBA TAFSIRI YA "UMOJA WA WATANZANIA"
ReplyDelete