ZA kazi kaka Michuzi
Hii Naomba uipost kwenye website yako. Na hii ni kwa Vijana ambao hawajaoa tu.
Mie ni Msichana wa umri wa miaka 27 Ninae ishi na virus vya Ukimwi toka mwaka 2007. Najipenda na kujidhamini. sina maisha ya kubahatisha Nina ishi hapa Dar Nimepanga.na nimeajiriwa nafanya Dar katika ofisi flani sintoitaja kwa kujilinda kunyanyapaliwa.
Nina tafuta Mchumba ambae atakuja kuwa mme hapo badae na awe na elimu ya kutosha juu ya VVU.na awe mkristo.kabila sichagui.Awe na kazi ya kueleweka na uwezo wa kuendesha maisha ya kila siku asiwe mbambaishaji.
Maana inaniwia vigumu kupata Mchumba na Kumumweleza khari ya afya.Kama ufahamuvyo Watanzania wengi bado tuna usiri kwenye hili swala la HIV kwa ujumla.Atakae penda tuwasiliana kwa mail hii
Asante sana
Mbano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Dada wewe ni jasiri. Tanzania tungekuwa wazi na huu ugonjwa kama wewe ulivyo maambukizi yasingekuwepo. Usijali utapata mume kwani kuwa na virusi si kwamba ndio unakufa, Mungu atakujalia na watoto utapata muombe sana

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru dada kwa ujasiri huo wa kueleza hali yako kiafya. Lakini mimi ningependa kufahamu huyo mchumba wako unapenda awe pia anaishi na VVU au ana UKIMWI wenyewe au hana maambukizo yoyote ya VVU?

    ReplyDelete
  3. POLE DADA KWA AFYA YAKO LAKINI DADA ANGU SAMAHANI, SASA KAMA KAJITOKEZA MUISLAMU INAKUWAJE?AU ITAKUWAJE.

    MDAU ABDALLAH...............EN

    ReplyDelete
  4. Duh!...Enway sasa huyo mchumba unayemtafuta na yeye awe ameathirika au unahitaji awe mzima wa afya?

    Potz.

    ReplyDelete
  5. Watu waige mfano jamani. Kuwa hiv + sio mwisho wa maisha. Good luck, na mungu atakusaidia. Bless you

    ReplyDelete
  6. EEhhh!! NO COMMENT!

    ReplyDelete
  7. WATU WANGEKUA WOTE KAMA WEWE DUNIA INGEKUA SEHEMU NZURI SANA.MCHUMBA UTAPATA KWANI UKWELI WAKO UTAMUWEKA MUNGU KARIBU YAKO.PIA WATU HAMUHITAJI KUMPA POLE MAANA MNAMFANYA AJISIKIE VICTIM WAKATI ANAJIAMINI KABISA NA AMESEMA HANA TATIZO LOLOTE HIVYO POLE YA NINI?WALA KUA NA VVU SI KWAMBA ULIKUA MUOVO ZIKO SBB NYINGI ZIPELEKEAZO MAAMBUKIZI NAZANI HILO UNALIJUA NDO MANA HUOGOPI.ILA KUA MAKINI NA HAO WATAKAOKUANDIKIA UTUMIE BUSARA KUBWA KTK HILI

    ReplyDelete
  8. Weka picha basi kama uko sirias na suala zima la uwazi.

    ReplyDelete
  9. Dada hongera kwa uwazi na ukweli. Mungu atakujalia Mchumba umpendaye na tunakutakia kila la kheri. You are my hero!!
    Good Luck!!

    Mdau, Boston, US.

    ReplyDelete
  10. Unaweza ukampata lakini kuwa makini utakapo tumiwa sms kwani wengine watakuwa sio wakweli. kama hutajali tuambie ilikuwaje ukawa victim ili tujifunze kwani unaonekana `innocent` yaani umeonewa, lakini kwa sababu mazingira ya kupata ni mengi naomba kujua yako.na kwanini uliamua kupima? Nimesikia majuzi mdada na mkaka wenye ukimwi wamepata mtoto hana vijidudu kwenye damu???????. Mimi nimepima kwa sababu nina mahusiano na mtu wa mtu. sasa huyu wa upande wa pili anabana hataki kupima, hivyo ninampango wa kuacha biashara kabisa na mtu wa hivi kabisa.

    ReplyDelete
  11. annon apo juu
    unaweza na inawezekana kabisa mtoto akazaliwa puwa negative hana virus vya ukimwi kabisa,unaijua neverapine??

    ata km wazazi wote ni positive au mmoja ni positive,upo apo??
    so wajamen MKAPIME MJUE AFYA ZENU MUISHI MAISHA MAREFU

    dada congrats utapata mume na utazaa swaaaafi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...