
Mabalozi, Wawakilishi, Wanajumuiya za Watanzania na baadhi ya Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba iliyotolewa na Mheshimiwa Balozi wa Tanzania, kwenye hafla ya Muungano.

Mheshimiwa Balozi, Mama Mwanaidi S. Maajar pamoja na Baba Balozi, wakimkaribisha Balozi wa Botswana na vilevile ni Mkubwa wa Mabalozi wa Nchi za Afrika hapa Uingereza, Mh. Roy Blackbeard.

Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mama Mwanaidi Senare Maajar,pamoja na Baba Balozi, Bwana Sherif Maajar, waliwakaribisha Mh. Dr Lindiwe Mabuza, Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Uingereza, akifuatiwa na Balozi wa Msumbiji, Mh. Antonio Gumede.

Mheshimiwa Balozi, Mama Mwanaidi S. Maajar {Pili Kushoto}, akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania kwenye Sherehe za kuadhimisha Miaka 45 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Toka kulia mwa picha ni Bwana Abubakar Faraj, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania hapa Uingereza, Bwana Katega-Muwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Birmingham, Bwana Maina- Mwenyekiti wa CCM Reading, Bwana Jackson- Mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania Birmingham, na Bwana Fredy {nyuma ya picha}- Mtanzania na Mtangazaji kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC-London

Mheshimiwa Balozi, akiwa na Maofisa wengine wa Ubalozi, baada ya kumalizika kwa Ibada ya kuiombea Nchi yetu Tanzania. Ibada hiyo uandaliwa kila Mwaka na Kanisa la Westminister Abbey inapofika siku ya Muungano. Kanisa la Westminister Abbey huandaa Ibada kwa Kila Nchi Mwanachama wa Commonwealth zinapofika siku za nchi zao Mataifa yao. Kulia mwa picha ni Bwana David Nginilla, Bwana Amos Msanjila, Mh. Balozi, Mama Mwanaidi. S. Maajar, Dada Caroline Chipeta, na Bwana Clement Kiondo.
Baadhi ya mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali jijini London nchini Uingereza, Ijumaa (24 Aprili 2009) walijumuika na Ubalozi wa Tanzania na Watanzania wote kusherehekea sikukuu ya Muungano iliyoadhimishwa Ubalozini hapo siku mbili kabla kutokana na kuangukia siku ya Jumapili.
Picha zinawaonyesha baadhi ya wageni waalikwa wakipokewa na Mheshimiwa Balozi Mwanaidi Sinare Maajar na Baba Balozi, Bwana Sharif Maajar na baadae wakisikiliza hotuba fupi iliyotolewa na Mheshimiwa Balozi
Baada ya tafrija hiyo fupi, Maafisa wa Ubalozi, na baadhi ya watanzania waishio Uingereza na Marafiki wa Tanzania walijumuika kwenye Ibada maalum ya kuiombea nchi inayoandaliwa kila mwaka na Kanisa la Westminster Abbey.
Kanisa hilo limekuwa likiandaa Ibada kwa kila nchi ambazo ni Wanajumuiya ya Commonwealth, Mheshimiwa Balozi alipewa fursa ya kusoma Somo la Pili katika ibada hiyo.
Hotuba kamili ya Mheshimiwa Balozi inapatikana:-
I can c my aunty Caro right there. Looking classic as always.
ReplyDeleteHongera Balozi Maajar! Hapa STATES tangu aondoke balozi Nyanganyi basi ndiyo hata muungano wala uhuru hatujui kinachoendelea! This is very sad. Yaani ubalozi wetu hapa Washington hata cook-out inawashinda? Na hawa viuongozi wa jumuiya yetu wakiisha pata kura na kushinda ndiyo basi tena hamna kinachoendelea. Maana nilikuwa natafuta habari kwenye mtandao huu kujua nini kinaendelea lakini hakuna kitu. Ubalozi nao umenyamaza kimya, jamani huu ni muungano its an historic event which few countries experienced. LONDON OOOOYYEEEEHHHHH! Mama maajar fanya kazi yako sisi kina mama tunakuunga mkono. Nadhani sasa tunahitaji mabalozi wa kina mama zaidi kuliko kina baba najua waosha kinywa mtaanza BUT THIS IS THE FACT ANGALIA MAMA WA LONDON ANAVYOSHIRIKIANA NA WATANZANIA WENZAKE. SISI HUKU HATA HIYO NYUMBA YETU (BALOZI RESIDENCE) HUKU TUMEISHAISAHAU INA RANGI GANI!!!!!!
ReplyDeletesasa jamani mbona hapa hata Mzanzibar Mmoja hayupo angalu kudanganya ulimwengukwa kuwepo na wawakilishi wa pande zote za Huo mungani.
ReplyDeletekizuri kisifie jamani mama mwanaidi unajitahidi sana jamani...they should keep you there kwa miaka mingine kumi...!!!
ReplyDeletemdau birmingham
Tanzania tutabakia kupart wakati Mtwara Hospital,hakuna hata machela ya kubebea maiti.
ReplyDeletehuu muungano unatambulika na serikali tuu wazanzibari hatuutambuwi wala hatuutaki.
ReplyDeleteUncle Kiondoooooooo....tunakumiss United States but lukn gud
ReplyDeleteHey Kiondo, (Mzee wa Dali Kimoko) naona mambo yako sio mabaya, namuona Caro nae hajachacha, Nginila ndo usiseme, Nawe Msanjila yaani timu imekamilika. Tunawamiso sana jamani. Hongereni sana kwa maadhimisho, sie huku imepita kavu.
ReplyDeleteDua za kanisa za kuombea nini? hazisaidii ikiwa zanzibar hawautaki.
ReplyDeleteJamani nimefurahi kuona jinsi Balozi Majaar anavyowawakilisha na kuwa karibu na Watanzania wote huko UK. Kwa nini Balozi wa TZ hapa Marekani hususani DC na New York hamuwezi kuandaa sherehe za Kitaifa za Kitanzania kama mwenzenu Balozi Majaar anavyofanya. Kweli Rais Kikwete amepata mwakilishi huko UK na Wa-TZ wanajidai naye. Wa huku DC na New York kazi yao kulala tu na hata hawana muda wa kujua kama kuna WATZ. Ukienda Ubalozini kuanzia Reception ni Mhindi na Maafisa Ubalozi kuonana nao ni kazi labda mtu ambaye anajitahidi ni Afisa Ubalozi J. Sokoine lakini hawezi kufanya kitu kwa sababu hana final say. Watanzania kibao ukiwauliza Jina la Balozi hawalijui wengi utasikia wakisema tulimuona siku ya sherehe za Uhuru wa Tanzania pale ukumbi wa Langleypark.
ReplyDeleteJamani mwenzenu nina arllergy ya ajabu....yani wazungu siwapendi sijui kwa nini. Hasahasa WAINGEREZA.....hebu litazame hilo hapo kwenye picha ya pili lilivyosimama......halafu nilipokuwa uingereza nilikuwa carer....kumbe mwaya wazungu huwa hawatahiriwi.....mweh......HII MICHUZI USIPOITOA ITAKUWA IMEKULA KWAKO......kafie mbele huko....
ReplyDeleteIVI WEE MICHUZI MBONA UNABANA SANA?
ReplyDeleteKWANI NIMETUKANA??
aaaagh acha wewee
mi nmeuliza ivi ILO KISS LA BALOZI NA BALOZI MWEZIE WA KIKE picha #1 ina maana gani?katika dhifa kubwa la kitaifa??
pili,annon apo kasema vizuri hospital za bongo chokest nothing at all watu wala good-time tu,yan isingekua wafadhili??sijui ingekuaje kwa baadhi
balozi wa tanzania DC aendelee kuuchuna tu. watanzania wa DC watu wa ajabu sana. mzee nyang'anyi alifanya pati nyumbani kwake watanzania wakaiba simu na kuanza kupiga long distance nyumbani. watanzania wengine wakaiba vitu vidogo vidogo vya ndani na kwenye magari.
ReplyDeletehata wanapoalikwa basi inakuwa vurugu tu kwa mfano hawataki kabisa kusikiliza hotuba za wageni rasmi na mwenyeji wao. wanataka kutumia makazi ya ubalozi na sherehe hizo kulewa na kuzungumzia majungu yao.
balozi sefue endelea kuchapa kazi hujatumwa na raisi kwenda DC kuwafanyia watanzania pati.
Duh hata mimi hilo kiss la mdomoni sijalielewa. ndo kusema tumeendelea kiasi hicho??
ReplyDeleteWewe mtu wa hapo juu umetumwa nini na? Rejea definition ya balozi na kazi aliyotumwa na nchi then you can write your pumba. Mbona hatukusikia hizo tuhuma? Issue siyo kwenda nyumbani kwake issue ni kutoshirikiana na Watanzania. Wote ubalozi na uongozi wa DC METRO! Kila nchi angalau wanafanya something kwenye siku muhumi za sherehe. Kama hakuna pesa watanzania watajiorganize na kufanya something, inatakiwa nia na ushirikiano. Mbona Nyerere day ilikuwa nzuri? Watu walijitolea kupika vyakula bila mfuko wa serikali.
ReplyDeleteHapa D.C. There is no unity, bali ni majungu tuu. Tuna madaktari, manesi, wahadnisi, ma-acccountants na kila profession lakini nchi yetu haifaidiki na chochote kila sababu hakuna anayetaka kumake a difference back home. Kama tungekuwa na unity na strong association ikiongozwa na balozi wetu hapa DC, tungeweza kufanya mambo mengi. THIS IS THE MAIN POINT! UMOJA NA USHIRIKIANO KAMA WATANZANIA. PARTY IS SOMETHNG ELSE WHICH IS PART OF ANY NORMAL HUMAN LIFE!
Hongereni! Maskini Carol ungejua yule mkenya advocate alieko pale anavyokutenda huku bongo ungelia lakini ndio hivyo michuzi atabana comment ila usijali uko juu sana tu yule si mwajiriwa tu.
ReplyDeleteKISS NI MAENDELEO,,,
ReplyDeleteasa ukifika nchi za wenyewe live as they do!!
ni hayo
Anon wa D.C mie muuguzi ningependa kufanya mambo nchini kwetu lakini sijui jinsi ya kuanza. Naomba nielimishe nianzie wapi ?
ReplyDeleteSIDHANI KILA KITU LAZIMA KIFANYIWE SHMRA SHAMRA KUBWA KAMA HIZI.
ReplyDeleteKWA KIFUPI HUYU MAMA TANGU AMETEULIWA KUWA BALOZI HUKO UK, AMETUMIA HELA KIBAO KULIKO BALOZI NYINGINE ZOTE ZA TZ NJE.
WIZARA YA MAMBO YA NJE INAPASWA KUANGALI HILI. SIKU HIZI KUNA UWAZI KWA HIYO TUNAOMBA WENYE MAGAZTI WATUTAFUTIE MATUMIZI YA BALOZI ZETU, WABUNGE NA VIONGOZI WA SERIKALI ILI TUJUE FEDHA ZA WALIPA KODI ZINATUMIKAJE? NUKTA.
balozi wa dc hana wajibu wa kuorganize waswahili kusaidia nyumbani kwao. wataalamu wa kitanzania walioko DC mmoja mmoja wanaweza kusaidia ndugu zao, vijiji walivyotoka,shule au vyuo walivyosoma, bila kusimamiwa na balozi.
ReplyDeletepia kuna chama cha watanzania DC. hivi nao wanasubiri wasimamiwe na balozi ile kuorganize shughuli yoyote. kila kitu balozi awashikie kiboko?
watanzania walioko DC ni wezi na namshauri balozi asiwakaribishe nyumbani kwake.