TAFADHALI SANA NDUGU MICHUZI,

 NAOMBA KWA HISANI YAKO UNIRUHUSU NIWEKE  OMBI LANGU HILI KWENYE BLOG YAKO HII PENDWA. NAOMBA WADAU WANISAIDIE MAMBO YAFUATAYO.

MIE BWANA, NATARAJI KWENDA UGHAIBUNI HIVI KARIBUNI.  SAFARI YANGU SI RASMI KAMA AMBAVYO WENGI WAMEKUA WAKISAFIRI KWA MAANA YA KWENDA KUSOMA NA  KUFADHILIWA NA SERIKALI, NDUGU, JAMAA AU TAASISI FULANI.  HAPANA.  SAFARI  YANGU NINAIANDAA MWENYEWE KAMA WAHANGAIKAJI WENGINE WANAVYOFANYA AU  WALIVYOFANYA.

MSAADA  NINAOWAOMBA WADAU WANISAIDIE NI KWAUZOEFU WAO WA  KUISHI HUKO UGHAIBUNI KWA MUDA MREFU JE NAWEZA NIKAFANIKIWA KWA KUJA    KUPIGA BOX?. NA KWA UZOWEFU NI NCHI GANI KWA SASA BOX LINALIPA?  NA LINALIPA KWA KIWANGO GANI KWA MAANA YA MCHANGANUO KWAMBA NCHI FULANI  SEHEMU FULANI BOX KWA SAA NI KIASI FULANI.

 NA BOX LENYEWENI    KUOSHAVYOO, KUOSHAVYOMBO, KUFAGIA BARABARA, KUMWAGILIA MAUA, KUOSHA MBWA, KUOSHA MAGARI, ULINZI KWENYE MADUKA, NA KWAMBA KWA SAA NI KIASI FULANI NK.

SUALA LA NITAFIKAJE HUKO SIPENDI LIJADILIWE NAOMBA NIJIBIWE KADIRI YA      NILIVYOULIZA.  HALAFU WALAVUMBI TAFADHALINI NAOMBA MSIHUSIKE NA JAMBO HILI, KWA KUWA KWA SASA SIUHITAJI MCHANGO WENU. 

WATAKAOPENDA KUWASILIANA NA 
                            MIMI WATUMIE
                       rajabumajuto@gmail.com
                          MDAU MAJUTO RAJABU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 51 mpaka sasa

  1. Majuto take care, Ulaya sasa hivi kugumu kazi hamna! Labda kama una ufahamu wa kazi za hospitalini na una vyeti vya huku huku sio bongo! Vinginevyo jina lako litamaanisha unakavyojisikia pindi ujapo huku.NB Pesa ipo Africa si Ulaya! Kama huamini soea Arusha pande za Mererani ucheki watu wanavyokula Bata!

    ReplyDelete
  2. rajabu majuto! lengo la safari umesema ni kupiga kitabu au buku?
    sasa mbona uhulizii ada ya masomo?malipo ya chumba cha mwanamfunzi?bima ya afya?viza ya aina gani unahitaji kama ya utalii? au student Viza?vyuo gani? na nchi gani?kuna masharti nafuu ya mwanafunzi? hapa ulichokiongelea ni kubeba box?watakuona kuwa unawafanyia dhiaka au mdhaa.
    Any way subiri wenyewe waosha vinywa wakirudi kubeba BOX watakujibu na kukushibisha kwa hoja zao.

    ReplyDelete
  3. Wadau wala msidanganyike huyu jamaa yuko kiwanja sema anatafuta sehemu ya kuhamia.
    Design box halilipi anakokaa, kachoka kuganga njaa kwahiyo anataka aweke nguo zake kwenye foronya apige mguu kutafuta sehemu nyingine.
    Au pale anapopiga box, miguu inawasha sana moto anatafuta ni wapi ataweza ni wapi ataweka matako chini hata kwa saa moja.
    Ubalozini ulienda mwenyewe...

    ReplyDelete
  4. mdau tottenham HaleApril 14, 2009

    nani alimwambia huyu jamaa kuwa kila anayekuja ughaibuni anafanya kazi ya kupiga box?? mimi namshauri huyu jamaa kuwa hatakiwi kuja ughaibuni kama hana professiona yoyote ya kumwezesha kufanya kazi nzuri. haya mambo ya box au siyo box si ya muhimu kwake kuyajua. yaani wabongo bado tunafikiria kusafiri kuja majuu kubeba boxes. this is 2009... we vipi bwana??? mdau London-Tottenham Hale

    ReplyDelete
  5. NJOO NETHERLANDS, HUKU KAZI ZOTE JAMAA WAMELEGALIZE, UKITAKA HATA YA KUUZA BANGI NA NYENGINE AMBAZO KWETU NI MARUFUKU. KWA SAA NI KATI YA EURO 6.5 HADI 8.

    MDAU WA KAZI ZOTE UHOLANZI

    ReplyDelete
  6. Mabox dollar 13 kwa saa na kwa mwaka dollar 30000.kwa kwwli wageni wakija ndio wanafanyaga hizo kazi. Ukishaujua mji unatafuta kazi unayotakam marekano wanaoosha vyombo wamexicano. Kusafisha barabara ni kazi ta jiji. Na huwezi kufanya kana wewe sio rahis inalipa dollar1z kwa saa.

    ReplyDelete
  7. Mabox dollar 13 kwa saa na kwa mwaka dollar 30000.kwa kwwli wageni wakija ndio wanafanyaga hizo kazi. Ukishaujua mji unatafuta kazi unayotakam marekano wanaoosha vyombo wamexicano. Kusafisha barabara ni kazi ta jiji. Na huwezi kufanya kana wewe sio rahis inalipa dollar1z kwa saa.

    ReplyDelete
  8. check how pipo set themselves watu wana hasira shauri yako, ngoja watoke kwenye mabox yao!lol

    ReplyDelete
  9. Hebu kuwa serious! Kama unataka msaada, toa cv yako mfano elimu yako, unafanya nini kama uko tz nk. Watu watakushauri kama uko better-off Tz au utapata unafuu ukistolowey, wapi!

    ReplyDelete
  10. kweli unasafari lakini hujuwi unataka uende nchi gani je una visa ya nchi gani?
    au unatumia pass gani itakayokufanya uende popote ugaibuni??
    MIMI NIKO UGAIBUNI ILA HUKU HAKUNA MTU ANAYEOSHA VYOMBO ILA MASHINE,HAKUNA MTU ANAEOSHA GARI ISPOKUWA MASHINE, BARABARA PIA MPAKA UENDE KOZI NA NI GARI NDIYO LINAFAGIA NI MPAKA UWE NA LESENI NDIYO UPATE HIYO KAZI PAMOJA NA UJUZI AMBAYO NDIYO KOZI NA MWISHO
    PIA HUFANYI KAZI KIHOLELA MPAKA UPEWE NAMBA YA KUFANYIA KAZI YAANI SERIKARI IKUTAMBUE.

    NA MSHAHARA UTALIPWA KUTOKANA NA NAMBA ULIYO NAYO. MAMBO YOTE YAPO KI UTARATIBU SIO KIHOLELA UNAWEZA KUWA UGAIBUNI UKASHINDWA KUPIGA BOX KWA SABABU YA VISA YAKO KWA MFANO MTALII HARUHUSIWI KUFANYA KAZI.
    PILI WAZUNGU SIO LEZI MBWA WAO WANAWAOSHA WENYEWE LABDA HUKO USA NASIKIA WA AMERICA WEUSI NI WAVIVU HUENDA UKAPATA KAZI

    MWISHO NAKUTAKIA KILA LA KHERI NA SAFARI YAKO.

    ReplyDelete
  11. HEHEHEHEHEH
    HUYO HATA VISA HAPATI HUYO
    AISHIE KUSIKIA TU BOX BOX BOX KWENDA MBELE
    MDAU
    MATUKIO YUKEEIIIIIIII CLUB AFRIQUE

    ReplyDelete
  12. HUYU VISA HAPATI KWANZA KWA MAELEZO TU HAJUI ANATAKA NINI
    NA AKIPATA ATAISHIA AIRPORT MAANA MDAU NDIO VILE TENA HUYU
    BOX HUTALIJUA WALA KULISIKIA WEWE
    UTAISHIA HUKO HUKO NYAU WEWE
    MDAU
    MATUKIO YUKEIIII CLUB AFRIQUE
    A.K.A KUGISSIIIIIIIIIIIIII

    ReplyDelete
  13. ILA UNAHAKILI SANA MAJUTO NJOO TU UTAJUWA MBELE KWA MBELE KULA VUMBI NA KUJA KUOSHA MBWA SI BORA UJE UOSHE HAO MBWA KWANI WAKO FURU MATIBABU WANAWAZIDI HATA BINADAMU WA AFRIKA MIMI NIMEYAPENDA MAWAZO YAKO ILA UNGETUWEKEA PICHA YAKO HAPA NINGEONA KAMA SURA YAKO UNAWEZA KUTUSUA NA SAFARI YENYEWE KWANI WENGI HUISHIA AIRPORT YA BONGO NA KURUDISHWA.

    ReplyDelete
  14. Baba UbayaApril 14, 2009

    huyo Majuto atakuwa yupo huko huko Ughaibuni na sasa baada ya nyundo nyingi sana majuu na hali ya maisha aliyonayo kila mwaka mpya unapofika anaona "afadhali ya last year" hivyo anaanza kupoteza imani yake. Majuto wala "usijute" kwa muda ulopoteza huko.wee endelea kukata majani na kupalilia bustani kwani iko cku waweza kuokota "vijisenti".kaza buti King Majuto.

    ReplyDelete
  15. kama kweli unataka kuja ugaibuni pata kwanza visa kisha uombe ushauri ILA MIMI NAONA UNAWASHWA HUTO TUHELA TWAKO TUTAPOTEA BULE UGAIBUNI SIO PA KUNYERA

    ReplyDelete
  16. WE Michuzi usituyayushewe unajua viwanja wote.

    ReplyDelete
  17. Kwa haraka haraka msaada ulioomba na msaada inaoelekea unauhitaji haviendani. Una ujuzi na uzoefu gani? Tunaokutakia mema tusingependa uibukie ughaibuni na kuwa mwizi au tapeli maana kwanza lazima utafungwa na pili utaitilia aibu nchi yako. Nigeria sasa hivi inafahamika kama nchi ya matapeli, kitu kinachoweza kuleta ugumu kwa wapiga maboksi wanaokuja kuaminiwa katika baadhi ya majukumu.
    JE NAWEZA NIKAFANIKIWA KWA KUJA KUPIGA BOX? Unaweza ukafanikiwa, unaweza usifanikiwe. Inategemeana na mchanganyiko wa juhudi na bahati yako.
    NA KWA UZOWEFU NI NCHI GANI KWA SASA BOX LINALIPA? Baada ya kranchi makampuni mengi yanapunguza wafanyakazi sasa hivi na wafanyakazi wanaoathirika zaidi ni wapiga box. Vilevile kuna suala la ugumu wa kupata baraka za kufanya kazi. Kuna njia zisizo halali za kupiga boksi kwa makaratasi ya ki-EPA. Nakushauri usizifuate. Ukizifuata ujue badala ya kupiga boksi utaenda haja kwenye ndoo.

    NA LINALIPA KWA KIWANGO GANI KWA MAANA YA MCHANGANUO KWAMBA NCHI FULANI SEHEMU FULANI BOX KWA SAA NI KIASI FULANI. Utapewa majibu mengi sahihi yanayotegemeana na sehemu. Lakini nikutahadharishe kwamba ukisikia mtu analipwa dola 10 kwa saa huko New York na mwingine analipwa dola 8 kwa saa Atlanta basi usikurupukie kwenda New York. Pato la boksi ni kiashiria cha gharama za maisha za eneo husika. Utaambiwa pato lako la mwaka litakuwa $30,000 kwa mwaka lakini kuna makato ya kodi na kodi ya pango inabidi uyafikirie. Usisahau pia gharama za kula na usafiri. Chumba kiduchu cha kupanga Boston ni dola buku. Dola kumi na mbili elfu kwa mwaka zinaenda kwa mwenye nyumba kutoka kwenye $30,000. Wamexico huwa wanapanga uswazi na kukaa kinyemela utitiri wa watu katika chumba. Isitoshe kila kazi ina mafunzo yake. Tofauti na bongo yetu ambako kama ulirithi ujuzi wa kunyoa nywele kwa kutumia kitana na wembe basi unakamata mashine ya kisasa na kufanya kweli, ughaibuni lazima usomee fani ya urembo. Hakuna kazi isiyohitaji mafunzo ughaibuni.
    NImekuwa nikisikia kwamba maeneo ya arabuni yana neema. Kuna ujenzi mwingi unaendelea na kampuni za ujenzi zinahitaji madereva na watu wa kupiga kazi za mtulinga. Wadau wa Arabuni tupeni habari.

    ReplyDelete
  18. Majuto,
    Watu wengi wanadhani wabongo walioko US bado wanafanya kazi za kuosha vyombo, assembly line na kubeba box kama ilivyokuwa zamani. SI KWELI. Wabongo wameshajanjaluka kipindi...Vijana wengi siku hizi wanasoma kozi fupi fupi ambazo zinalipa sana hapa US. Kama EMS, sio EMS ya kusambaza barua, NO! kutoa huduma ya kwanza katika emmergence (Ambulance) vijana wanatengeneza kati ya dola 20 hadi 28 kwa saa, Madada wengi wamesoma na kupata vyeti vya Registered Nurse, wanatengeneza kati ya dola 30 hadi 42 kwa saa. Hizi ni kozi fupi za miezi mitatu na RN miaka miwili. Waliojitahidi kumalita degree zao wanatengeneza kati ya dola 75 hadi 90 kwa saa. Wabongo wengi wameacha kupanga(Rent) wamenunua nyumba. Huo ndio ukweli, acha kudanganywa na vijana waliokimbia US kwa kuogopa kwenda shule, au kwa kuiba vijisenti na kutoroka.Aidha vijana siku hizi wanafuata sheria wana papers, hivyo hawishi underground, Kwa wanaojua maisha US bado inalipa kama Mwadui. Mpe hi Michuzi. Mzee wa Shoka, Houston.

    ReplyDelete
  19. kama una mtaji wa kutosha baki bongo tu,tuliza kichwa,ulaya siku hizi hailipi,na hii credit crisis ndio kabisa bora uwe mpole huko huko utalia bure,wenzako walioko huku walishazoea

    ReplyDelete
  20. mdau ulioomba ushauri ningependa uelewe kuwa,kama umeamua kuja kusoma basi ilibidi ujitayarishe tena sana kwani elimu Ulaya ni ghali especially Uk.kama huna saving yoyote huwezi kusoma huku kwani sheria za wanafunzi ni ngumu sana unaruhusiwa kufanya kazi part time.ukiwa likizo full time.sasa kama unakuja huku SIO RASMI kama ulivyosema mwenyewe kazi utapata lakini huto save akiba yoyote ya kukusaidia kusoma.nakama unakuja ili ufanye kazi, basi kwa taarifa yako tuu kazi hizo unazozitaja za box mpaka wazungu wenyewe hivi sasa wanazitafuta hawazipati.ila kama unataka tuu kuja ulaya kung'aza macho poteza hizo millions za shillings zako ni kama unatupa kwenye choo cha shimo maana ulaya unaisikia sio hii utakayoiona naongelea nikiwa ulaya kwa miaka 9.

    ReplyDelete
  21. daa huyu jamaa ananitia machungu tu,nimerudi sasa hivi toka kwenye box,(kitchen porter0wadau wa ugaibuni u know what i am talking about.anyway back to the topic.unajua wala maharage bongo wasenge sana nahisi tatizo hawaambiwi ukweli wakisikia watu wanakula kuku wanajua mambo safi maana kula kuku bongo ni issue mpaka sikuku,sio siri kuku ulaya ni kama maharage bongo ila hao kuku wanapatikanaje?siri ni yangu na wanaoishi ughaibuni.msidanganyike jamani ulaya siku hizi ni kama kariakoo tu hakuna tofauti yeyote,nahisi tatizo hatuwaambii ukweli,ukija huku utaona mwenyewe majuto,hakuna cha marekani wala uk,kote huko watu wamepita bora ya jana kuliko ya leo.kitu ninachoweza kusema unaweza kusoma kama unataka kusoma ila unyayo ni lazima uguse kisogo kwa kujipinda sio rahisi vile unavyodhani,kama una kamtaji kako hapo bongo bnora uendelee tu kufanya mambo yako hapo bongo na kula maharage kuliko kuja kula kuku huku.asante

    ReplyDelete
  22. Majuto, nenda Finland kazi hizo zote unazozitaka " NA BOX LENYEWENI KUOSHAVYOO, KUOSHAVYOMBO, KUFAGIA BARABARA, KUMWAGILIA MAUA, KUOSHA MBWA, KUOSHA MAGARI, ULINZI KWENYE MADUKA, NA KWAMBA KWA SAA NI KIASI FULANI NK." zinapatikana bwelele. Nenda Ukonga kakamate pipa iage minazi ya Yombo kata anga kupitia Amsterdam ukifika Helsinki utavikuta vyoo, vyombo, barabara, maua, magari, maduka nk vinakusubiri kwa saa Euro 6 mpaka 12. Utapewa nyumba bure, chakula bure, maji bure, nguo bure, kila kitu bure na mshahara juu na nauli ukitaka unaweza kupewa bure.

    ReplyDelete
  23. WE CHIZI MAARIFA HAPO JUU UNAYESEMA AENDE FINLAND, ACHA KUONGEA MAMBO USIYOYAJUA..KWA TAARIFA YAKO WATU WANAKIMBILIA HUKU ILI WAPATE ELIMU BILA YA KULIPIA FEES, WAKIMALIZA NDIO UAMUZI MTU ANAENDA MAHALI PENGINE AU ANABAKIA KUTAFUTA MAISHA, OFCOURSE KAZI ZA MAANA SIO RAHISI KUPATA LABDA UWE UMESOMA UNURSE, WATU WA INFO.TECHN KIASI FLANI WANAPATA KAZI.
    NIKO FINLAND MWAKA WA KUMI SASA,NIMESOMA DIPLOMA YA UNURSE NA KAZI NINAFANYA..HIZO KAZI ULIZOTAJA FINLAND SIJAWAHI KUZISIKIA MIAKA YOTE HII, HAKUNA KUOSHA MBWA, WALA MAGARI,ZAIDI YA HIYO YA KUOSHA VYOO NAYO UNAKUWA UMEAJIRIWA LABDA KUSAFISHA OFISI FLANI AMA RESTAURANT...ACHA KUROPOKA USIYOYAJUA, MWANA HARAMU WEWE,MAISHA NI POPOTE, MAISHA NI KUHANGAIKA,,,UNAFIKIRI WATU WOTE WAKIBAKIA BONGO NDO TUTAFANIKIWA KAMA KINA REGINAND MENGI AU WAKINA RAY C???
    MUOMBA USHAURI, INABIDI UWAELEZE WATU VIZURI, UMESOMA? UNA MTAJI GANI? ILI WAKUPE USHAURI MZURI, ILA HUYO MWENDAWAZIMU KIJANA ALIYEKUTISHA KUHUSU FINLAND, ACHANA NAYE, KAMA MTU UMELOST BONGO, HUJASOMA, LIFE HAINA MUELEKEO,,,AAAH WELCOME TO FINLAND, BEACH HILI BADO KABISA WALALAHOI LINATUTULIZA ROHO ZETU...

    ReplyDelete
  24. Mimi ushauri wangu bora uende italy ndipo unaweza kupata kazi kwani kule napoli wanatafuta makontena sasa kama wewe ubavu wa kubeba maswala unao utaitoa mara moja.
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  25. Jaribu Sweden nasikia huko mambo safi.

    ReplyDelete
  26. kama unaweza kwemda nchi za scandinavia nadhani ni bora. shule ni bure, maisha mazuri, rahisi kupata kazi na population ni ndogo.

    mdau aliyekwambia uholanzi nadhani kasahau kukwambia lugha. hupati kazi bila lugha ambayo itakugharimu miezi kama sita kama unakamata haraka.

    ReplyDelete
  27. Nenda Congo DRC, kama unataka kufaidi maisha!

    ReplyDelete
  28. rose mlekwaApril 15, 2009

    wewe majuto njoo huku Houston mambo mwaaa kujiachia tu huna haja ya kufikiria box, totoz tupo na kuma unapenda bier na pambaz kama kawa mambo iko Houston kaka njoo achana na kelele ya box hapa ni kukomaa tu mwanangu nipe email nitakupa story zote kaka angu.

    ReplyDelete
  29. MAJUTO NAOMBA UNISAIDIE KITU KIMOJA, WEWE USIKATE TAMAA FIGT MPAKA MWISHO UJE HUKU UGHAIBUNI MIMI NIPO TEXAS, NAHUDUMIA KIBIBI CHA KAMA MIAKA86 HIVI NAKULA VIDOLA VYANGU KAMA 3300 KWA MWEZI. ILA NAOMBA UNITUMIE PICHA YAKO NIJUE KAMA UNALIPA MAANA UTAFIKIA KWANGU UKIFIKA KWANGU UTA ENJOY ILIMRADI UFAHAMU WAJIBU WAKO KWANGU ASILI YANGU MIMI NI PEMBA NA NIMEKAA SANA MOMBASA NADHANI UNAJUA NATAKA NINI NDUGU YANGU WEWE NI MTU MZIMA.

    ReplyDelete
  30. we kaka maisha yako bongo.......Mtu kwao......ulaya , amerika huko ni kwa kupiga book tu na kutafuta mtaji.......mzee kama huku huko safi baki bongo....

    ReplyDelete
  31. Majuto pole kwa maoni ya wa TZ wote hatupendani.Ingekuwa umezaliwa China au Mexio ungeona watu wanakupa namba za simu na email. Hapa mimi huwa nachuma straw berry na cucumber wakati wa summer na kupiga deki kwenye viwanda vinavyofanyiwa matengenezo wakati wa Summer.Huwa nalipwa dola 90 kwa siku kwa kuchuma strawberry na kiwandani nalipwa kama dola 120 kwa siku,tukifanya kazi usiku inaongezeka mara 2.Huitaji elimu zaidi ya kiingereza kidogo. Nio mji wa Malmo hizo kazi zinaanza mwezi wa 5 mpaka November,njoo ndugu yangu kama unaona inalipa- email kttz@yahoo.com,gharama kwa mwezi ni kama dola 100,maana tunalala kwenye ma container na viazi vikianza basi tunakula viazi na butter. kufikia mwezi wa 11 utakuwa na dola zako za kutosha kwenda kuanza kuosha vyombo Stockholm nayo haitaki Elimu unaweza kupata kama dola 1200 kwa mwezi,kibali cha kazi tunatumia majina ya wenzetu tunawalipa kama dola 50 kwa mwezi,magonjwa huku hamna. Labda ukifa. Karibu.

    ReplyDelete
  32. dah! kumbe wa piga box mmestarabika kiasi hicho.

    ReplyDelete
  33. UNAKULA KILO NGAPI YA SEMBE!!!!!!!!

    ReplyDelete
  34. hebu acha kuchafua watu roho zao kwani kubebe box mpaka ulaya tuu? siuende hata ipp wanakazi za viwanda,au kwa barkresa.unaonekana unataka kujakuzamia ulaya wewe sema ukweli wako,kama umeshindwa kuishi bongo nenda hata kenya pia kuna mabox.au hiyo pesa yako uliyopanga nauli,fanyia biashara.hata wewe unaweza kujiajili mwenyewe kubeba mabox.usichengue watu na ulaya yao.

    ReplyDelete
  35. MALAYSIA,mdau njoo malaysia hizo kazi ulizozitaja ni chache sana,zipo nyingi sana zaidi ya hizo, bangi ndo inalipa sana huku tena yakutoka bongo inaaminika na inapendwa kuliko kwasababu ni kali unaujua kali mwana? kg 1 ya bangi huku ni RM 6000/= AU TSh 4 milion,sasa hivi airport inaruhusiwa unkilipa kodi

    ReplyDelete
  36. JAMANI MIMI SITANII NA WALA SIFANYI MZAHA KAMA BAADHI YENU MDHANIVYO NIPO SERIOUS,KWANINI NITANIE HALI YA KUWA KUKAA KWENYE INTERNET HUKO BONGO NUSU SAA NI TSH 1000 KWAHIZI CAFFE TUNAZOITA ZIKO FASTER. HIYO FEDHA.UKWELI NIKWAMBA SITANII.NAWASHUKURUNI NYOTE MNAOENDELEA KUNISHAURI NAWASHUKURU HATA WALE AMBAO KWAMAKUSUDI KABISA WANANITUKANA NA SIJAWAKOSEA LOLOTE,NASHANGAA HATA WEWE MLA VUMBI MWENZANGU WA KISIJU NAWE UNANITUSI,SIKUTARAJI KAMA BADALA YA KUNISHAURI MWENZENU MNANITUSI.MBARIKIWE NYOTE.. KWA WALE WANAOPENDA KUNIANDIKIA BARUA PEPE ANUANI YANGU NI rajabumajuto@gmail.com. MDAU MAJUTO

    ReplyDelete
  37. mimi nakushuri njoo uk kazi zipo mbona inategemea wewe unataka kazi gani wala uitaji vyeti walanini ni nguvu yakoukarimu najinsi unavyotaka wewe kuishi, kwa maana hiyo mimi niko reading mwaka wa 11 sasa nina fanya kazi za hotel nilianzia kuosha vyombo wakati ni ko college,hotel hiyo hiyo,nikaambiwa sasa utafuta na meza nikakubari, nkaambiwa sasa itabidi tukufundishe kuwa waiter maana umekwisha jua lugha kidogo, nikafanya haya sasa itabidi ufanye na bar,kwenye bar mambo mazuri maana kuna till hapo unachukua na vijisenti hapo nakakubali basi mambo yangu kidogo yakaanza kuwa afueni sasa basi bosi akaniomba niamie hapohapo hotelini sababu bar wanafunga late na transport nilikuwa sina basi na college nayo ni kamaliza,kwa maana hiyo vza ikayoyoma ,mimi nikahamia hotelini breakfast bure lunch bure dinner bure, kulala bure na tip napata,na vijisent kwenye bar napata, yani mambo siyo mabaya kabisa hizo credit crunch minazisikia tu sasa sasa hivi nakaribia kuwa supervisor kwa mshahara wa £9 kwa saa wakati nilianza na £4 kwa saa na bila kukatwa tax hiyo ni cash yako kila friday na chumba bure chakura bure ni mimi na tv yangu tu chumbani wala sitaki makuu na simuoneshi mbongo yoyote hapo maana wa kishajua tu nuksi, sasa haweawezi ni uliza tena mambo ya papers sababu wameshanijua vya kutosha na immigration hawaendi hata sikumoja hotelini na kazi kama hizi za kura na kulala hapohapo nyingi sana nawala hawa kuulizi kibali nikupata connect inalipa kuliko care na nurse na unaweza hata kwenda college hotelini kazi zipo wakati wote te wakati wa x-mas mashift kibao sasa hivi ni meshapata ujuzi wakotosha wa kuweza fungua hoteli yangu mwenyewe ya kisasa mara tu nikirudi bongo hivyo basi kuwa majuu sio kubeba mabox tu au kuwa nurse ndio kulipwa vizuri ni kujiweka vizuri katika maeneo ya kazi samahani sitataja jina la hoteli.uk

    ReplyDelete
  38. pole sana ila ukweli wewe uko ughaibuni unataka kushift place nyngine huko umeshaleta noma, eti wala vumbi!!!! huna lolote wewe mchovu tu mla vumbi mwenyewe kwani ukifa unawekwa wapi??? si kwenye hilo vumbi, kwa taarifa yako umeula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua, kaa huko huko uliko uolewe.

    ReplyDelete
  39. majuto maisha ukitaka kuyatafuta huwa hawaulizi hata wazazi wako kwani wanaweza kukukatisha tamaa hivyo wewe fanya vile hakili yako inavyokutuma,cha msingi sali na kumuomba mola wako akutangulie na kukufungulia njia na si kutangazia watu unataka kwenda kubeba box

    MIMI HIVI SASA NIKO UGAIBUNI SIKU NATOKA NYUMBANI NILITOROKA KWANI NILIJARIBU KUWADOKEZA KUWA NITASAFIRI KWENDA KUTAFUTA MAISHA WALIRUKA KAMA NIMEWAAMBIA NATAKA KUUWA.
    NADHANI UNANIELEWANA HIVI SASA NINAMAISHA MAZURI SANA NAMSHUKURU SANA MOLA WANGU NILIMUWEKA MBELE NA AKANIONA MIMI BONGO NILIKUWA NAUZA MACHUGWA BARABARANI NA KUTEMBEZA MITUMBA ILA KILIO CHANGU MWENYEZI MUNGU KAKISIKIA SIKUDANGANYI NINAMAISHA MAZURI SANA MWENYEZI MUNGU SHAHIDI NA NINAMSHUKURU MCHANA NA USIKU. UBARIKIWE SANA USIFE MOYO SISI WOTE NI VIUMBE WA MWENYEZI MUNGU

    ReplyDelete
  40. we pimbi kwel kwel halafu utaitwa majuto mpk kufa badala ya angalau kufight japo ubatizwe uitwe bahati kama akili zako mbovu namna hiyo,kwanza umeonekana huitaji ushauri ila unakashfu kazi za watu,pili ushauri wa bure kama unataka kuja kujaribu karibu stockholm,kanuni unafika unajilipua we msomali kisha utapelekwa huko kiruna au sundsvall ukaishi na dubwi,halafu utalazimisha kurudi stock na hicho kisent unacholipwa na social kwa mwezi kinatosha kwenda kulipia kulala kwenye korido kwa babu awale pale tensta,msosi usijali tembelea kwa wabongo piga story sanaa halafu wasifie sana hata km sifa za kijinga angalau watakutoa na vibawa na managryn,kwa babu pale napo lazima upakatwe utawauliza wenzio watakufahamisha vizuri,halafu kuhusu kazi mmmh,hiyo we njoo tu utajua ukifika kwani hizo zote ulizotaja ndo waswed wanazililia na watu wanaachishwa kila siku wanapewa wenye nchi lakini karibu ndo maisha yanaendelea,yakikushinda usipate tabu nenda ubalozini unalia kwa kiswahili km unataka kurudi bongo au kwa kabila ya kwenu kisha watakufanyia mpango ugeuke ukaione kipawa tena,nadhani mpk hapo kanauli katakua kameisha na kimbelembele cha kubeba box kitakua kimeisha kisha usisahau kusimulia wenzio uliyoyaona,valkommen kompis

    ReplyDelete
  41. Yaani hata wewe mlavumbi wa kisiju unamkebehi mwenzako!!!!?? ama kweli. tambola na mokili omoni makambo...Weeewe nina imani kweda dar hadi msimu wa embe hata hivyo mpaka upate dill mjomba wako akutume upeleke embe kariakoo. sasa huo ujanja wa kusema majuto umeutoa wapi? wadau tafadhali tumsaidieni mwenzetu kumpa tada zitakazo kuwa msaada kwake tuacheni dharau kwani nani hajui hali halisi ya bongo.acheni unyaanyapaa.
    MDAU IRAQ

    ReplyDelete
  42. ZIMBABWE KUNALIPA

    ReplyDelete
  43. NDUGU YANGU USITHUBUTU KUJA HUKU HAKUNA CHA MAANA WOTE TUNAKAZI ZA KUBABAISHA ILA HUA TUONA AIBU KUWAAMBIA NDUGU ZETU KAZI GANI TUNAFANYA.

    KAMA UMESOMA NI BORA UBAKI BONGO HIKO UTAPATA KAZI INAYOENDANA NA ELIMU YAKO.
    HUKU KITENDO CHA WEWE KUA MGENI HATA KAMA UMESOMA UTABAKI KUPATA KAZI AMBAYO HAISTAHILI NA ELIMU ULIYO NAYO
    HUA TUNAONA AIBU KUSEMA YANAYO TUSIBU

    ReplyDelete
  44. asalam mimi naona kaka majuto nikushauri uje hapa sweden katika mji unaitwa kiruna au boden yani mkwa kweli huku maisha ni mswano kabisa huna hata haja ya kufanya kazi manake pesa serikali inakupa ya matumizi nauli na chakula na wanawake wamejaa kibao nawau wote kwa kweli wanapenda waafrika kwa sana,yani hapa kuna mzee mmoja alikuja hapa sweden anitwa awale amekuja tangu mwaka 1972 hadi leo hajawahi kufanya wala nini yeye anakula social tu lakini alhamdulihi amejenga nyumba zake kiruna moja na boden mbili na bado amehama stockholm naye amejenga nyumba zake pale rinkeby na tensta basi anakula pesa za wapangaji tu,kwa hiyo huo mfano niliokupa inaonyesha jinsi maisha yalivyokuwa matamu na maraisi hapa sverige,au kama unataka kazi basi wewe fanya chapchap ukifika hapa stckholm mtafute ndugu ndizi kwa email ndizitensta@hotmail.com au makambakungsangen@vasagatan.se nadhani hapo utapata msaada unaotaka,asante

    mdau wa sweden

    rashid decco,mjanja from kigoma

    ReplyDelete
  45. mimi kwa ushauri wangu. hujasema una unri gani, elimu gani, na unafanya kazi gani bongo. na pia kwa vile hujasema unataka kwenda nchi gani basi najua hela za masafa marefu pia unazo. lakini mbona unaulizia tu box linalipa $ ngapi lakini hujaulizia gharama ya maisha nayo ni vipi? hivyo ushauri wangu ni huu kama mkazi wa USA niliyeanzia from the bottom.

    1. kama umeshafikisha miaka 25 and up, huku hamna faida ya kuja kabisa siku hizi.mpaka uje usettle utakuwa umeshazeeka unafikiria kurudi home tu bila chochote.

    2. kama una mke na watoto don't ever dare to come here. ni taabu sana kupata kazi sasa hivi mpaka uweze kuwatumia hela nyumbani uliowaacha sio leo wala kesho.

    3. kama huji kusoma USA bora ukae tu bongo.

    4. USA sasa hivi social security hazitoki tu hivi hivi kama zamani. Na bila social yako za kuazima zitakutesa sana.

    5. kama unauwezo wa kukusanya nauli yote hiyo peke yako na hela ya kuanzia maisha peke yako huko....bora 2 stay there ...you are doing good. huku kuja ni kwa watu wadogo na watu wanaotaka kuanzia kwenye elimu. kama una elimu ya maana na kazi ya maana bongo ni kuzuri.

    sio nakukatisha tamaa au nakuzibia riski yako ila ukweli ni huo. tuliokuja zamani, system ilikua poa kweli to melt into their pot na bado ilituchukua miaka kuanza kuenjoy matunda ya kuishi huku.

    kazi za rejareja unaweza kupata lakini pia na maisha ya huku ni ya ngali sana basi hela yote unayopata utaishia kulipa bills tu.

    ukweli ni kuwa bongo ni easy sana kuishi kama unakazi nzuri.
    my 2 cents I hope these help

    ReplyDelete
  46. Baki zako bongo mabox hayana mpango zaidi ya kuugua mgongo baadaye na kudharirishwa kwa wingi na wazungu

    ReplyDelete
  47. Ndugu yangu Majuto, kama umesoma na una kazi ya maana hapo Bongo, mi nakushauri utulie zako Bongo uendelee na mambo mengine kama biashara, n.k na huku Ulaya njoo utembee baadae urudi zako Bongo kama anavyofanya kaka yetu Michuzi na ze Fulanazzz! Kama Bongo huna chochote cha maana, basi subiri subiri mpaka baadae manake uchumi huku umeanguka itakuchukua muda mrefu kupata kazi, manake sasa hivi hata wazungu wanatafuta hata hiyo kazi ya box. Kuhusu Sweden, kiukweli sio nchi rahisi, ni nchi ngumu na ghali, kuhusu kupewa social na serikali ni mpaka upate uraia kama umeoa Mswede na hiyo inachukua miaka 3 na zaidi, sio kwamba ukifika unaanza kupata social. Huo ni ushauri ambao ni wa ukweli kabisa. Nakutakia kila la kheri kwenye mipango yako ya baadae.

    ReplyDelete
  48. WADAU MLIONIPA E-MAIL MBONA MBONA WOTE MNENIPA E-MAIL ZA BANDIA, TAFADHALINI KAMA MMEAMUA KWA HIARI YENU KUNIPA ADDRESS ZETU, TAFADHALINI BASI,JARIBUNI ZIWE ZA UKWELI, KINYUME NA HIVI MFANYAVYO MNANIONGEZEA GHARAMA SISIZO ZA LAZIMA.KUHUSU KUTUKANWA NILITAMBUA ITAKUWA HIVYO WALA SISHANGAI,WATZ WENGI TUPO HIVYO. NITUMIE E-MAIL rajabumajuto@gmail.com

    ReplyDelete
  49. wadau wa ARABUNI mbona kimya hukonasikia udereva ni dili msaidieni majuto

    ReplyDelete
  50. Njoo Dubai.Dubai ni mji wa biashara na hakuna kodi unachotakiwa uende kuomba kibali cha kuuza bangi kwanza pale osterbay police wanatoa siku hizi au hata hivyo unaeza ukaenda nabangi yako yote sema kilo kumi mpaka pale airport dar es salaam ukifika ulizia customs wape huo mzogo wanaupima unalipia shilingi elfu arobaini kisha wanakupa kibali ukifika tu Dubai huangaiki unauzia huo mzigo airport,karibu

    ReplyDelete
  51. aiseee!!

    JK unaona wanao??UFISADI NCHI HII UNATESA SANA WATU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...