Rais wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Duniani na Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Samuel Sitta akifanya mazungumzo mafupi na Waziri Mkuu wa visiwa vya Bermuda, Mhe. Dr. Ewart Brown wakati Mhe. Sitta alipomtembelea Mhe. Brown ofisini kwake.
 Kiongozi wa Upinzani wa Bermuda, Mhe. Hubert Kim Swan akitoa zawadi kwa Mhe. Spika Samuel Sitta wakati viongozi hao walipokutana nchini Bermuda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Sisi nasi, yaani wee acha tu. Yaani kila Bunge viongozi ni sisi Watanzania. Spika wa Bunge la Afrika ni Mtanzania Muheshimiwa Mama Getrude Mongela. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mabunge ya Jumuiya ya Madola pia ni Mtanzania Muheshimiwa William Shija. Spika wetu Muheshimiwa Samwel Sitta ndiyo Rais wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Duniani ( Kwa msemo wa Blaza Michuzi). Spika wa Bunge la Afrika Mashariki pia alikuwa Mtanzania Muheshimiwa Kanali Abdulrahman Kinana.

    Wabunge wa Tanzania Oyeeee!!!!

    ReplyDelete
  2. Bermuda ni kisiwa kama kile cha New jersey aliko weka vijisenti vyake Chenge! Nadadisi tu jamani Bermuda biashara offshore ndio nyumbani kwao!!Spika ameenda kuchungulia vijisenti vyake?

    ReplyDelete
  3. Spika ndani ya Tax Heaven, Wafichako hela Mafisadi sijui anatusaidia vipi hapo au nae anachungulia usalama wa za kwake???!!

    ReplyDelete
  4. Kaswali kadogo.Je, kiashirio-jina 'Mheshimiwa' kinaweza kutumika tunapomtaja 'mheshimiwa' ye yote nje ya Bongo au kinatumika tu kwa 'waheshimiwa' wa Bongo tu. Na kama kinatumiwa kwa hao wa nje ya bongo ni vigezo vipi vinavyotumika wengine kuashiriwa 'mheshimiwa' na wengine kutoashiriwa hivyo? Ninauliza hivyo kwa sababu sijawahi kusikia kwa mfano Rais wa Marekani au seneta tikimwashiria "mheshimiwa Bush"!!!

    ReplyDelete
  5. OFISI YA MBUNGE AU KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI, NADHANI KAMA ZETU TU,TEHE TEHE

    ReplyDelete
  6. bermuda ndo nini??iko wapi?

    jamani????????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...