HABARI MR. MICHUZI.
 
MIMI NI MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 35 NINAISHI NA MWANAMUME NA TUNAWATOTO WAWILI.
 
KUNAJAMBO MMOJA LINANITATIZA, HUYU MWANAUME ALISHAISHI NA WANAWAKE WAWILI NA KILA MMOJA ALISHAZAA NAO MTOTO MMOJA MMOJA.

KINACHO NISHANGAZA HUYU MWANAMUME HUWA ANAENDA KULALA KWA HAO WANAWAKE BILA HATA TAARIFA. KATIKA HAO WANAWAKE PAMOJA NA MIMI HAKUNA HATA MMOJA AMEFUNGA NDOA NAYE.

 SASA NIMEMWAMBIA KWANINI ASIFUNGE NDOA NA MMOJA WETU AU WOTE BASI  KWA SABABU YEYE NI MWISILAMU HATAKI.
 
JAMANI WADAU NINAOMBENI MSAADA MAANA MWANAMUME MWENYEWE AJATULIA.  HATIMA YANGU ITAKUWA WAPI.
 
NINAOMBA MAJIBU YA KUJENGA NA SIO YA KUBOMOA .
 
AHSANTENI..
 
MASHA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. ACHANA NAE HUYO MLAFI. ATAWAPA UKIMWI WOTE WATATU. NENDA KAPIME!!!!!

    ReplyDelete
  2. Sasa dada kama umekufa na kuoza kwa jamaa na jamaa ulikuta ana wanawake tayari kawazalisha kwa nini usiendelee kuvumilia lakini ujue wewe umewapola wenzio kwa hiyo vumilia machungu tu,
    Mdau fidel80

    ReplyDelete
  3. Wewe ni sawa na Alan Shearer kwenda kubeba kaa la moto huku ukiliona. Ulimfuatia nini huyo bwana na kisha kwa nini ukae naye bila kufunga ndoa. Mtu kama huyo ogopa kama ukoma (ukimwi)...

    ReplyDelete
  4. MIE HUWA NASHINDWA KUELEWA INAKUWA NI KISWAHILI KIGUMU AU NINI? USHASEMA HUJAOLEWA SASA NENO LA WAKE WENZA AU MKE LINATOKEA WAPI TENA JINA WAKE AU MKE JINA KUBWA JAMANI> KUMBE UNAJUWA MNAYOFANYA NI UZINZI EH KAA PEMBENI MUOMBE MOLA WACHA MNACHOFANYA MPAKA AKUFATE KWA PENZI LA NDOA LA SIVYO UNAZIDI KUJIWEKEA ZAMBI WEWE NA YEYE PIA. PAZI. INSHALLAH MTAFUNGUKA AKILI NA UJINGA MTAUWEKA PEMBENI. Michuzi hizi mada siku hizi zinakuja kwa mafunzo au za kweli?.

    ReplyDelete
  5. ulishaambiwa mda tu kny vitabu.
    dawa ni kuacha zinaa. Nyie wote mnazini.

    ReplyDelete
  6. mpaka upate ukimwi ndio utatia akili wewe
    unajiita uke wenza kwani amewaoa huyo acha ufuska wako huo wewe
    endelea tu upate ukimwi ndio itakuwa vizuri mpumbavu wewe
    shame on you

    ReplyDelete
  7. mafunzo na kupunguza stress baada ya box za kufa mtu

    asante

    ReplyDelete
  8. SULUHISHO KWAKO NI RAHISI SANA.....MIDHALI "HULI" WALA "HULALI".....BASI WIKI MOJA LINAKUTOSHA KUJIENDEA "KUSTAREHE KWA AMANI" NA UACHANE NA HIZI KARAHA ZA DUNIANI.

    ReplyDelete
  9. wewe umeshawachokoza waosha vinywa maana hawajachonga siku nyingi leo umewapa uwanja haya mi yangu macho subiri upewe ushauri,maana hapo jibu unalo bila hata kuomba ushauri,kuna misemo ya kiswahili inasema kabla hujamua kujitupa ama kujirusha angalia chini kwanza kunaendeka kwani kuna uwezekano kuna mawe kuna michongoma mashimo everything na vyote hivyo vitakuumiza, sasa jiulize kabla ya kujirusha ulifikiria hayo au uliona kuna sponji litakupokea hutaumia, kazi kwakwo kama unaijuia maana yake .

    ReplyDelete
  10. Simama kidete. Amua: Dump the bum! Kesi kwisha!

    ReplyDelete
  11. MIMI SIAMINI KAMA UMEKUFA UKAOZA KWA MWANAUME MWENYE WANAWAKE WAWILI,ILA UNGESEMA SHIDA ZAKO NDIYO ZINAKUFANYA UMG'ANG'ANIE MWANAMME MALAYA. UJUWE SHIDA MBAYA SANA ZINAWAFANYA WANAWAKE WATEMBEE NA VIBABU,MWANAUME MALAYA KAMA HUYO WAKO

    ILA WEWE DADA UNGEKUWA NA UWEZO USINGEKUBALI SHITI HIYO KULETEWA NA MTU UNGEMKIMBIZA KAMA PAKA

    MIMI BINAFSI SICHUKUWI SHITI BOLA NIJIKUNE NA NDIZI AU HATA NGUZI LA MHINDI

    ReplyDelete
  12. SAWA NA MTOTO KUAMBIWA USISHIKE PALE USIPOMWAMBIA SABABU ATAENDELEA KUSHIKA TU, JAMANI 1. UKIMWI 2.UZINZI MBAYA SIPENDI KUMPONDA JAMAA KAPIMENI MPO HATARINI. TIZAMENI MBELE HASA HAO WATOTO JAMANI. UKIMWI UKIMWI UKIMWI MBAYA MWENYEZIMUNGU ATUEPUSHE NA HILO GONJWA NA MAGONJWA MENGINE. TUWE WAAMINIFU KATIKA NDOA ZETU.

    ReplyDelete
  13. Shefii - ChinaApril 22, 2009

    Kama ni mkweli huyo sista, umri wa miaka 35 bado yuko fit na anahitaji apatiwe haki yake. Sasa inaonekana huyo dada japokuwa alifurahia kuwapora wenzie sasa anaumizwa na wivu pindi huyo BWANA wao anapokwenda kwa wale wa mwanzo na yeye kuachwa mpweke. Hii ni njia ya yeye kujiexpress kuwa anatafuta substitute ya kukava space pindi jamaa anapokuwa out ili kupunguza maumivu na pia kumkomoa jamaa. Jamani wanawake msishindane naye. Niliwahi kusikia kwenye taarabu moja kuwa "..mwanamume unapotoka na mwanamke pia hutoka, bali yeye anakuwa wa kwanza kurudi ili usishtuke.."
    Pole mama nanihii, just kadhana tu na kazi, ili ulishe wanao na kuwapa mapenzi bora yenye familia. Najua wao hawawezi kujifunza mazuri toka kwa baba yao, sasa wewe simama imara, kwani ulitafuta Bwana ukampata, kisha ukatafuta watoto ukapewa. Naomba sana acha kutafuta bwana myingine. Usikae ukafikiria sana ndoa, kwani hata walio katika ndoa nao kuna baadhi yanawakuta haya haya mpaka wengine wame-give up. JUST MIND LIFE. Nakushangaa sana kufagilia uke wenza (eti atuoe wote), hamna mwenye taimu hiyo siku hizi.. JUST MID YOUR LIFE, na nadhani unaonyesha dalili kuwa kuna siku utamwambia NAOMBA USIRUDI, NIMECHOKA SASA...

    Chaoooo

    ReplyDelete
  14. wajinga wakubwa nyie wanawake ndio mnaotufanya tudhalilike hivi hivi yaani kinyaa,anawaabuse nyie mnafurahia,i hate whe men do this kwa kisingizio eti ni mwislamu

    ReplyDelete
  15. Your story is nothing new in this world.If you've chosen to stick on him,baby mama drama will continue to hunt you for the rest of your life,sister.If you recall the way he approached you with all nice words,beautiful flowers,outings and all other stuff despite the fact that he had the other two,believe me this player will jump to number 4 when he becomes tired of you.Dont get fulled with this dude sister.You are still young not even the age of umarried Condolezza Rice.Why dont you break up and move foward,you never know someone may be interested on the road.Your body is so prestigious you dont wonna die and leave behind an innocent child suffer.

    ReplyDelete
  16. Samahani kwa kusema hivi" wewe ni mjinga" mapenzi mapenzi nini, unajua kabiisa kwamba anafanya anavyofanya unamng'ang'ania hebu nikuulize swali, unampenda kwa nini? dada dunia ya sasa mapenzi hayalipi bills bahati mbaya sana inaonekana kwamba unamtegemea huyo jamaa ndio maana anakutenda hivyo. Amka, tafuta kazi na jitegemee huo ndio ushauri wangu.
    Get out and Fast.....

    ReplyDelete
  17. Kama ni kweli hii hali imekutokea pole sana kwa sababu si kosa lako ni kosa la moyo wako kukubali kupenda. Ila ukweli ni kwamba tangu mwanzo ulikwisha kosea labda kama jamaa alikudanganya ati hana msichana yeyote anayeishi nae, lakini kama ulikua ukifahamu tangu awali basi umefanya kosa kubwa sana.
    Pia kitu kingine ulichokosea ni kukubali kumpa mwili wako kabla ya wakati yaani ndoa. Sasa jamaa ameshakupa watoto wawili na hana kinachomfunga kidini ni rahisi kukuacha, kwani ni wazi jamaa alikutamani, hakukupenda. Anapoenda ndipo alipokua na upendo wa kweli. Pole sana dada ila ukweli kwa sasa siwezi kukushauri zaidi ya kukupa pole na kukuomba uchague mawili.
    Ama umuache urejee kuishi maisha ya awali na kumrejea mola wako
    Au uvumilie na kuendeleza uzinzi ukitumai kwamba ipo siku utaitwa mke

    ReplyDelete
  18. wewe kwani uliambiwa yuko au wako hebu kaa pembeni utubie makosa unaliyofanya kwakujuwa,na ulee watoto km riski utapata nyengine uyo mwanamke hana haja ya mke wandoa shida yako huduma tu,

    ReplyDelete
  19. Mtaka kuolewa hubana. We ulishaachia sasa unataka kuolewa ili iweje?

    Sisi wanaume huoa kupata ulichotoa, sasa kishapatikana kwa nini gharama za kuoa?

    ReplyDelete
  20. Daah, umaskini unawaponza dada zetu. Yaani wewe dada pamoja na historia ya huyo jamaa wewe ukamkubali, ukidhani wewe ni mwanamke sana kuliko waliokutangulia? Basi kitanda umekitandika hivyo ukilalie hala hala msife na ukimwi tu!!

    Mdau, Boston, US.

    ReplyDelete
  21. Kuna usemi wa kiswahili unasema.."UKIPENDA BOGA PENDA NA UA LAKE"...nadhani hata wewe dada unaufahamu uu.
    Nikirudi katika upande wa taaluma zaidi kwa taarifa yako hutambuliki kisheria na kama mke wa huyo bwana so neno wake wenza halihusiki hapo.
    Pili kama uliridhika na mapungufu yake tangu mlipokutana na ukijua kwamba alikuwa na wanawake wawili na amezaa nao pia sioni sababu ya wewe kushangaa kuwa hata wewe hana haja ya kukuona.Pengine ndo tabia yake nda ndo alivyo jamaa.Labda uchunguze pia familia yake.
    Dada kama vipi hulali basi endelea kukesha na jamaa na pengine mpo zaidi ya watatu... peleleza!
    Kwa ushauri nenda kwa Washauri wa familia utapata ushauri zaidi.

    ReplyDelete
  22. Kama unauwezo wa kujitegemea anza chukua wanao miaka hii sio ya kushare tena magonjwa.

    ReplyDelete
  23. Shoga pole.Ulikuwa una jua kama ana watoto, sasa muacha akadiskas juu ya watoto wake, ndio umesha lowa. lakini kwa magonjwa haya ya kimwi, jikaze umuwache dada.Madame

    ReplyDelete
  24. wewe unampenda halafu unauliza. bananeni tu hapo hapo. kupanga ni kuchagua. unavuna ulichopanda.

    ReplyDelete
  25. MAPENZI NI UPOFU WALA HAINA HAJA YA KUULIZA JIBU LIKO WAZI DADA.

    ReplyDelete
  26. Ungeondoka na watoto. Halafu ungeenda kwa daktari na upime. Pia, usifunge ndoa tena isipokuwa uwe unajua mwanaume ni safi na hajaishi na wanawake wengine!

    ReplyDelete
  27. Mwanaume huyu ana matatizo wengi. Unaweza kupata mwanaume mbora! Mwambie aondoke ile aende kwa huo wanawake wengine wawili

    ReplyDelete
  28. mwambie aengeze wa nne, mpumbavu we, ata haya huoni, unajua zinaa tu

    ReplyDelete
  29. Pole dada.

    Mi nahisi we unamuhitaji huyo bwana kuliko ye anavokuhitaji wewe. Kuoa au kutooa sio issue kwani bado mtakuwa the same kundi la wanawake kwa mwanaume mmoja. Nashawishika kuamini kama isingekuwa unamuhitaji (kifedha) ungesha anza mbele.

    Stastically speaking, hio ni kawaida sana. At any time (t), mwanaume mmoja anatembea na wanawake watatu (wastani) na mwanamke mmoja anatembea na mwanaume wawili (wastani). Tofauti kati ya mwanaume wako na wengine ni kuwa ye anakwambia kuwa sasa naenda lala na wenzio wakati wanaume wengine wanaenda kwa siri.

    Hivo wala usijali, wala usiumize kichwa kumwambia atumie condom kwani hatotumia. Sali omba tu msikubwe na lile gonjwa. By the way, hakuna tafiti zinazo onesha kuwa walio ambukizwa ni wazinzi kuliko ambao hawaja ambukizwa. Life goes on.

    ReplyDelete
  30. wewe ndio hujatulia sio huyo mwanaume.
    1.kwanini ulimpa wakati unajua kuna wawili kabla yako na hawajaolewa?
    2.Kwanini ulirudia kuzaa mtoto wa pili kwa njia hiyo ya kuziniwa kama wewe una dini?
    3. Unamtegemea kwa kiasi gani? yaani wewe una uwezo wa kifedha kuishi bila kumtegemea yeye kulea watoto?
    Kama jibu ni ndio, usiondoke ataingiza mwanamke mwingine bali mkazie na bana usimpe tena. kapime na tunza wanao.
    Kama analeta fujo anataka kwa nguvu kawaone viongozi wa dini waambie umechoka kuziniwa, na akikubali kuoa mkapime, mkipima kama safi kazi unayo, unahakikisha unamchisha asitamani hata hao wa mwanzo. kama una afya njema mbona huyo unamchosha kwa kumpa mpaka anapepesuka tuone ataenda wapi? ala analeta ufuska enzi hizi za ukimwi?

    ReplyDelete
  31. Kuna msemo kwa kimombo unasema hivi " A BABY CAN PLAY WITH ITS MOTHER'S BREASTS BUT NOT WITH ITS FATHER'S TESTICLES". Huyo mwanaume ni mfupa uliomshinda fisi, huuwezi!

    ReplyDelete
  32. unatupotezea muda hujui unachotaka kama ulivyowaibia wenzako ukajiona wewe mjanja na wenzio hivyohivyo,unasema mawazo ya kujenga na sio ya kubomoe kunachokinachojenga hapo? be srious usisingizie uislamu kabisa wote nyie wazinzi na dini zote zinakemea

    ReplyDelete
  33. Jamani, hebu tuseme ukweli. mapenzi ni upofu na wanaume ni wadanganyifu saaaana. Wangapi mnaomsema huyu dada mzinzi, au mjinga na nyinyi mna situation kama hiyo au mbaya zaidi? hebu tokeni hapa na muwe wakweli. Mijanadume mengi huwa wadanganyifu na waharibifu hasa akili zao zikihamia katikati ya miguu

    ReplyDelete
  34. tuliza moyo wako, tafakari na mwombe mungu akupe ufumbuzi hapa unatafuta waosha vinywa wapate nafasi, wao pia hawajatulia.

    ReplyDelete
  35. nanukuu "uishi na mwanaume asiyeishi na mwanamke mwingine"

    UTAMJUAJE?????wee annon apo juu?

    khaaaa

    ReplyDelete
  36. muislamu? hivi kweli kuna hata haja ya kutaja imani yake hapa? analala na wanawake watatu bila ya kuwaoa na ana watoto wa nje ya ndoa watatu, hivi kweli unadhani anafata amri za din yake au ana jina tu la kiislamu. hata angelikuwa ni kristo basi mtu angeliuliza imani yake. JINA HALIMAANISHI IMANI YA DINI.

    ReplyDelete
  37. Huyo nasikitika kusema ni Muislam jina, anaishi na vimada watatu hajawaoa anazini tu.
    Wewe mshauri mfunge ndoa kwani mwishoni mtahukumiwa wote kama wazinzi

    ReplyDelete
  38. Kuna mtu katowa Comment bila kusoma juu naona wengine wanashindwa kueelewa Anasema wanawake wanazalilishwa? Hapana hapo wote wanajizalilisha kwa mwenyezimungu. Jengine analalamika kwamba ana hate when man say because he is muslim wachak ujifanya kiengereza kinapanda,

    Kiswahili juu umeshindwa kusoma Huyo mwanamke na huyo mwanaume na hao wasichana manake si mwanamke wala si mwanaume wote hawapo kwenye kitu kinaitwa NDOA wote wanafanya UZINZI haifai kabisaaaaaaaa.

    Mwanamke ondoka mtizame mwanao subiri kuolewa na MWANAUME akajifunze tabia na dini yake inavyotaka. mnatambaza magonjwa tu.

    SOMENI KWANZA KABLA HAMJA WEKA MAONI.

    ReplyDelete
  39. WOTE HUMU NI WAZINZI NA WANAWAKE SISI UDHAIFU WETU TUNASINGIZIA WANAUME! ALIWAFANYIA WENZIE MAKOSA WACHA NA YEYE YAMKUTE,ALIJIONA YEYE MALKIA

    ReplyDelete
  40. Nafikiri WATANZANIA mpaka hapo mliona SOMO 1.Mwanamke huyu alijuwa kama huyo KAKA alikuwa na wanawake akazalisha nje akachukuwa nafasi sijui alijuwa kapata? HAJAOLEWA KAANZA UZINZI wao bila CONDOM 2.MWANAUME HUYO NAYE ANAKITU ANAFICHA KAPIMENI.

    WADAU FUNDISHO HAPO LINAONESHA MILA DESTURI NA DINI ZETU NDOMANA ZINAPENDA NDOA MKUTANE SIO MNAVAMIANA KABLA KUJUWANA VIZURI SANA, FIKISHANENI KWA WAZAZI MJITAMBULISHE MUOANE HAIWEZEKANI VUMILIANENI.

    MSIWAIGE HAO JUU NDOMANA MTIHANI UMEWAPATA KWANI HATA KWENYE NDOA UPO ILA MUNGU NDIO ANAHUKUMU. HAO WAO WASHAANZA KUJIHUKUMU NAFSI ZAO.

    MIE NAWAONEA HURUMA WATOTO MUNGU AWASAIDIE.

    HUYO MWANAMKE KAYATAKA NA MWANAUME HANA HESHIMA WALA FUTURE ANAONEKANA NDIO BAADAE WANAJISIFU VIBINGWA NA WATOTO, WATOTO UKIZAA KIZINZI HAWAESABIWI KAMA WAKO. HAPO ZAMBI MWANAMKE NA MWANAMME, WATOTO THWAWABU TU ILA WASIJE KURUSI UPUUZI WENU.

    ReplyDelete
  41. kwa kifupi, labda niseme kwamba kati yenu wote hakuna mwenye haki.
    Wote ni wazinifu, na unachotakiwa kufanya ni kuacha hiyo zinaa na kuomba toba kwa mola wako na atakusamehe.
    Pili kama hofu ni watoto inategemea wewe ni wa dini gani kwa waislamu mtoto aliyepatikana nje ya taratibu ya NDOA huwa ni mali ya mwanamke na hana nafasi ya kumrithi huyo Mwanaume kwa chochote kile.

    Nakushauri ondoka katafute namna nyingine ya maisha ili usizidi kumuudhi Mwenyezimungu, ili akupokee vizuri siku utakayokwenda kwake.

    Ondoa shaka Mola atakusaidia kwakuwa bado upo hai na anakupa riziki yako.

    Asante

    ReplyDelete
  42. yaani mimi nakushangaa unajaribu hata kuuliza ushauri.Hakuna ushauri wowote wewe ni kufungasha virago vyako.Sijui unasubiri nini hasa ukifikiria jamaa hataki kuoa.Achana nae usipoteze muda wako.

    ReplyDelete
  43. mpaka dakika hii ulipoandika hili swali bado ulikua unaishi nae?maduka ya sumu huyajui?je zile za panya wanapitisha kwenye vibaiskeli?nashauri ujaribu ile itakusaidia.

    ReplyDelete
  44. mpaka dakika hii ulipoandika hili swali bado ulikua unaishi nae?maduka ya sumu huyajui?je zile za panya wanapitisha kwenye vibaiskeli?nashauri ujaribu ile itakusaidia.

    ReplyDelete
  45. Yamekukuta na wewe, wakati unawanyang'anya wenzako ulijiona bombaa kuwazidi, sasa hilo ndo jawabu lako.
    Ninawasiwasi kama kweli una miaka 35, wenye miaka hiyo si wajinga hivyo.
    Hapa hakuna ushauri juu yako ni kuku zomea tuu It is too late kwako.

    Zaidi iwe fundisho kwa wote wanaopenda short cuts

    GJK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...