
Hayati Ramadhani Faraji
Kufuatia msiba mzito wa ndugu yetu Ramadhani Faraji a.k.a Rama bwela,uliotokea hapa barcelona siku ya ijumaa tarehe 02 april mwaka huu wa 2009, tungependa kuwafahamisha watazania wote wanaoishi ndani na nje ya Spain ya kwamba utaratibu wa kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinaendelea.
Siku na mahali itakapofanyika shughuli ya kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwa mazishi mtajulishwa mara tu itakapo julikana. Jumuia ya watanzania hapa Barcelona inakaribisha mchango wa hali na mali katika kufanyikisha shughuli hii.
kwa maelezo zaidi waweza wasiliana na wahusika wafuatao
Brown E.B simu namba 0034699600531
au
A.S.Kwanza simu namba 0034608654084
pia tunatoa rambirambi za dhati kwa familia na ndugu wa marehemu na kuwaomba subira na uvumilivu wakati mipango ya kumsafirisha marehemu zikiendelea.
MOLA AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMINA


Poleni sana wafiwa na watanzania wote wa hapo barcelona, Mwenyeezi Mungu atawapa subira katika kipindi hiki kigumu na Inshaallah Mwenyeezi Mungu atamweka marehem mahala pema AMIN.
ReplyDeleteNaomba kuuliza bwana Brown E. B. ni Brown E. Balige au?
HAYATI
ReplyDeletesamahani na poleni sana wafiwa
amen
dahh poleni , ni kazi ya mungu , safari yetu sote , mungu amlaze pema peponi amin
ReplyDelete