Marehemu Mama Martha Sinkara

Familia ya Nyingo “Lingalangala” wa Houston, Texas insikitika  kuwajulisha ndugu jamaa na marafiki popote pale duniani kuwa Mama yetu Mpendwa Martha Sinkara amefariki dunia nyumbani kwake Ludewa Iringa tarehe 22/4/2009. 

Taratibu zote za mazishi zimefanyika  huko huko Ludewa tarehe 24/4/2009. Kwa wote wenye mapenzi mema tunaomba sala zenu ili Mwenyezi Mungu amjalie neema katika safari yake hii ya mwisho.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe milele. 
Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Poleni wafiwa kazi ya mungu haina makosa. tunaamini atakuwa amefika kweye ile safari ya uzima wa milele Amen.

    ReplyDelete
  2. R.I.P mother! Poleni ndugu!

    ReplyDelete
  3. I personally know her.
    She is a strong woman and nice one.
    The mama Lingalangala-I like her
    Bye mama
    Pole kwa familia yake
    Tuko wote Houston ila nilikuwa sijajua kama mpo Houston.
    Nitawatafuta kuwapa pole wafiwa
    Poleni Lingalangala woooote Tanzania

    ReplyDelete
  4. NG'INGO AU NYINGO???
    poleni wanyalukolo wa kuboma,inguluvi itange

    amen

    ReplyDelete
  5. Mungu amlaze mahali pema mama yetu mpendwa mama lingalangala tulikupenda sana na tutakukumbuka kwa uchesh,busara na tabasamu la upendo la kila wakati.Mwenyezi Mungu awape moyo wa ustahimilivu wafiwa wote tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu na MUNGU AMJALIE PUMZIKO LA AMANI NA TUKIZIDI KUMKUMBUKA NA BABA YETU MPENDWA LINGALANGALA,AMINA

    ReplyDelete
  6. Poleni sana ndugu, kufiwa mzazi inauma sana. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi, Amen.

    ReplyDelete
  7. Tunaomba contacts za wana familia wa Houston
    Tunamfahamu huyo mama na tunapenda kuwapa pole

    ReplyDelete
  8. Poleni wafiwa wote.
    Je, ni kweli kuwa kuna msiba mwingine wa yule wakili maarufu wa DSM aitwae Moses Maira uliotokea huko Houston? Wadau tufahamisheni.

    ReplyDelete
  9. Poleni sana wafiwa.
    Mungu amlaze mahali pema peponi. Amina.

    ReplyDelete
  10. Yes Maira amefariki Houston
    Ni habari za kweli

    ReplyDelete
  11. watoto wa late mzee maira tunaomba update za taratibe za kuaga mwili hapa houston...please tungependa kuhudhuria tafadhali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...