makamu mwenyekiti wa chama cha netiboli nchini (chaneta) shy-rose bhanji akielezea masikitiko ya chama chake dhidi ya hatua ya BBC kutangaza kutembeza bakuli kwa chama hicho kuomba misaada ya maharage na vyakula vingine ili kufanikisha mashindano ya taifa cup mwaka huu, badala ya kutangaza milioni 50 ambazo shy-rose anadai waliweza kukusanya toka kwa wadau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. sasa mama Bhanji analalamika nini kutoa ni moyo kwani kachumbari na maharagwe si nao mchango?...

    ReplyDelete
  2. Anyway mimi sielewi exactly BBC walitangaza nini so sitawasupport waloa kuwapinga. Ila hata mimi binafsi nilikuwa sipendezwi kabisa na tangazo la radio la kutembeza bakuli la Chaneta. Kwamba tunahitaji msaada wa maharage, mchele, unga, nyanya, chumvi, vitungu na hata mkaa jamani? Kwangu mimi hili tangazo lilikuwa linaidhalilisha pia hata nchi/serikali at large si Chaneta na wizara ya michezo peke yake.

    Infact ningekuwa waziri wa michezo ningeresign kabisa. Mpaka sasa sielewi jukumu la wizara ya wizara husika kwenye michezo isiyoweza kujiendesha yenyewe kwa viingilio kama netball ni nini? shame on us kwa kweli

    Michuzi hakuna tusi hapo iache iende kama ilivyo mkuu.

    ReplyDelete
  3. Kuomba omba kubaya sana
    Kuomba omba kubaya sana
    Usiombe
    Usiombe
    Jitegemee

    ReplyDelete
  4. So what? didnt they get what they requested for?

    ReplyDelete
  5. nilifikiri Shy wamo kumbe mh, hivi waTz tunaona sifa saaaana kuombaomba kila saa na kila kitu?kwa nini hatuna mawazo ya kujitegemea au njia mbadala za kujizalishia kipato? utadhani kuomba ni fasheni wakati ni fedheha, kada mzima wa chama tawala na afisa wa benki kubwa huna namna ya kukisaida kwa mawazo chama cha michezo mpaka uombe kachumbari? hii ni aibu. Nilikosana na rafiki yangu mpendwa kisa nilikataa kumchangia mchango a ujenzi wa kaburi la dada yake! lakini nilisema amenipunguzia mashuzi, tujue majukumu yetu ya kibinafsi, kijamii na kitaifa. Tuamkeeeeee

    ReplyDelete
  6. Ingawa sikusikia hili tangazo la BBC lakini nafikiri BBC walichofanya ni kutafuta attention ya umma, kama jinsi kampuni kubwa za utangazaji za ulaya na marekani wanavyotangaza kuhusu africa aslimia kubwa utakuta kama sio kuhusu vita basi ni njaa, UKIMWI au rushwa wakati kuna mambo kibao mazuri Africa.
    Lakini labda kwao sio 'news' sana
    si unajua mbwa akimngáta mtu sio news sana lakini mtu akimng'ata mbwa ni news?

    ReplyDelete
  7. Jamani mnapogawana vyeo muwe mnawapa wataalamu wa kuongea kazi ya "u-spokesperson". Manaake Hizo press conference za Bongo Kila siku Mi Huwa Hoi, manaake ni vichekesho vitupu, from wanaouliza mpaka wanaojubu hayo maswali.. Mwe!!!
    KISWAHILI LUGHA YA TAIFA
    HILI LUGHA YA TAIFAAAAAA.

    ReplyDelete
  8. Big-up kwa Shyrose Bhanji, BBC habari zao ni kuangalia upungufu zaidi ya mazuri.

    Huu ni mtindo wa vyombo vya habari vya magharibi, kutokuona au kukubali kuwa watanzania wakihamasishwa kama hii issue ya 'maharage na kachumbari' watanzania wakaongeza na pesa taslimu Tshs 50 millioni.

    Generali Idi Amini aliitisha harambee ya kuwasaidia Waingereza waliokuwa na hali ngumu ya njaa na uchumi miaka ya 1970, na waganda wakajitikoza kuchangia mbuzi, kuku, matoke n.k lakini Waingereza wakakataa msaada huo kutokana na fikra za kikoloni.

    Hivyo sisi tunajua BBC siku zote habari nzuri toka Afrika hazirushwi hewani, kila siku ni habari mbaya tu, asante kwa Shyrose kuwapa 'vidonge vyao' BBC.
    Mdau
    Jijini London

    ReplyDelete
  9. Huyu Bhanji anabana pua anavyoongea au masikio yangu? Analalamika bure tu, sasa kama wameandika Watu wemetoa maharage tatizo liko wapi? Millioni 50 sawa lakini wenyewe (BBC) wametaka stori ya maharage, kama unataka kuandikia stori ya millioni 50 basi anzisha shirika lako la habari mama

    ReplyDelete
  10. Mama Bhanji bila shaka unajua kuwa uandishi ni biashara na mhariri anangalia habari gani itauza gazeti au itavuta matangazo kwenye Lunginga: Hivyo hbari ya maharage na viazi kama mchango ndiyo ilikuwa habri ya kueleta mvuto! Kumbuka ulivyokuwa nuwa jinsi ulivyo kuwa unasema habari ambazo pengine hata wewe ulijua kuwa utekelezaji wake ni ndoto tu! Basi tulia unyolewe na bakuri lako ulilotembeza za maharage na kachumbari! kwekwekwe...heehee ..Bhaji mwana wee unachekesha

    ReplyDelete
  11. Hawa wote wawili walitaka kutuchekesha tu, huyo muuliza swali na Bhanji wote comedians. Swali la kizushi na jibu la kizushi.

    ReplyDelete
  12. mkuu wa wilaya wa ------ baadae!!
    mtanambia wadau

    mark my words!

    ningeuliza apa swali ila michu angebana saaaana abt uyu dada,,,

    ok ok

    ReplyDelete
  13. Aje kwangu mimi Abbas nitampa shilingi 5M...0713617834

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...