Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (kushoto) wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wa zamani ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, William Lukuvi (Kulia) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma leo kuhudhuria kikao cha bunge kilicbhoanza leo na kinatarajiwa kuchukua siku 10.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. karibuni dom lakini mh waziri naona anaipenda hiyo pozi ya mikono mfukoni.

    ReplyDelete
  2. Mtoto wa mkulima anaonekana mwenye mawazo mengi kweli siku hizi ... kuna nini kinamsumbua jamani?

    ReplyDelete
  3. Kwenye mikakati ya UFISADI karibu.

    ReplyDelete
  4. Mchungaji Deci mbaroni

    2009-04-21 21:33:19
    Na Sharon Sauwa na Romana Mallya


    Mchungaji wa Kanisa la Kipentekoste la Kimara jijini Dar es Salaam, Issack Kalenge, amekamatwa na Polisi wakati akihutubia wateja wa Development Enterpreneurship for Community Initiatives (Deci) katika makao makuu ya taasisi hiyo Mabibo.

    Akizungumza kwa njia ya simu jijini Dar es Salaam jana, Mchungaji huyo alisema polisi walimweleza kuwa wamemkamata kwa shtaka la kuhutubia mkutano bila kibali, jambo ambalo halina ukweli.

    Alisema Polisi walimhoji kwa zaidi ya saa tatu katika kituo cha Polisi cha Magomeni ambapo aliwaeleza kuwa hakuwa anahutubia mkutano bali walifika pale kwa ajili ya kupashana habari kuhusiana na mkutano wao wa Jumamosi na kuhusu kufungua mashitaka mahakamani.

    ``Pale ni ofisini kwetu ambapo tumekuwa tukikutana kujadiliana mara kwa mara sasa hata kama tunakutana kupashana habari basi tuombe kibali haiwezekani,``alisema na kuongeza Polisi walimruhusu kujidhamini mwenyewe na kurudi tena kituoni hapo Aprili 23, mwaka huu.

    Mchungaji huyo alijikuta akiingia mikononi mwa Polisi mara aliposhika kipaza sauti na kuanza kuwahutubia wateja wa kampuni hiyo waliokusanyika mapema katika makao makuu ya taasisi hiyo Mabibo jijini Dar es Salaam jana asubuhi.

    Wateja hao walikusanyika katika mkutano wao, uliolenga kujadili juu ya kukukusanyika katika mkutano utakaofanyika Jumamosi na kufungua kesi mahakamani kudai haki zao ambazo zitakosekana kutokana na hatua ya Serikali ya kufunga akaunti zao na Serikali.

    Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema mchungaji huyo kwa kutumia kipaza sauti, alisikika akiwahutubia wateja hao kwa lengo la kuwahamasisha kujiandikisha katika orodha ambayo itatumika kuufikisha mahakamani uongozi wa Deci baada ya kufunga shughuli zake.

    Walisema wakati akihutubia wateja hao, alisikika akimtaja Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo kuwa alibariki shughuli za taasisi hiyo kwa kufungua tawi mojawapo mkoani Morogoro na kwamba anapaswa kujiuzulu wadhifa wake.

    Walisema baada ya kutamka kauli hiyo ghafla Kamanda wa Wilaya ya Kipolisi Magomeni (OCD), Omar Chambo, alimkamata mkono aliokuwa ameshikilia kipaza sauti hicho.

    Hata hivyo, walisema wakati akiendelea na zoezi la kumkamata mchungaji huyo, ghafla OCD, aliteleza na kudondoka chini huku akifuatiwa na mtuhumiwa.

    Nipashe ilishuhudia Mchungaji akiwa chini ya ulinzi ambapo wateja wa Deci walipokwenda kwa nia kumwekea dhamana katika Kituo cha Polisi Urafiki, waliambiwa kuwa waende Magomeni.

    ``Sisi hatunaye mtu wa Deci hapa labda mwende Magomeni muonane OCD kule,`` alisikika mmoja wa askari akiwaambia wateja waliofika katika Kituo hicho cha Urafiki wakitaka kumdhamini mtuhumiwa huyo.

    Katika ofisi hiyo kulikuwa na ulinzi wa askari polisi wakiwa na silaha huku maofisa wa taasisi hiyo wakiwahimiza wateja kuondoka katika eneo hilo kwa sababu hawatakiwi.

    ``Wewe ni mteja ama ni mfanyakazi wa Deci, hamtakiwi hapa ondokeni,``alisikika mmoja wa walinzi katika ofisi hiyo akiwaambia waandishi wa habari na wapiga picha huku akihangaika kufunga uzio wa kamba katika eneo hilo.

    Hata hivyo, wateja hao waliondoka kituoni hapo huku wakiwatukana waandishi wa habari kwamba wanatumia mgogoro huo katika kufanya biashara yao ya magazeti.

    ``Wewe tumekuona tunakusihi usithubutu kufika katika ofisi za Deci ,`` walisikika wateja hao wakimwambia mmoja wa wapiga picha aliyewapiga picha kituoni hapo.

    Katika hatua nyingine, Mchungaji Kalenge alisema kikao cha kamati yake kilichofanyika jana, kimeamua kuwashitaki wakurugenzi wa taasisi hiyo, baraza la wadhamini la taasisi hiyo ambalo ni Baraza la Makanisa ya Kipentekoste linaloongozwa na Askofu Sylivester Gamanywa.

    Alipohojiwa ni kwanini wameamua kubadili uamuzi wao wa kuishtaki serikali, alisema kuwa wameamua kubadilisha watu wa kuwashtaki baada ya kubaini kuwa Serikali na uongozi wa Deci lao ni moja tu na kwamba hawataweza kupata taarifa muhimu kwa ajili ya kuandaa mashtaka.

    Alisema kesi hiyo inatarajiwa kufunguliwa kesho kutwa Mahakama Kuu katika Kitengo cha Biashara na kwamba mashtaka yatakuwa ni kuvunja mkataba kinyemela na kusitisha ghafla shughuli za kupanda na kuvuna hatua ambayo imewaathiri wateja.

    ``Hawa viongozi wa Deci ni wahuni wamefunga ndoa na Serikali, sisi tumeamua kuwapeleka mahakamani wao kwa sababu tunazo nyaraka ambazo zinaweza kutusaidia katika ushahidi, lakini kwa upande wa serikali itakuwa vigumu kwa sababu hatuna ushirikiano na uongozi,\"alisema.

    Kova awaambia ama zao ama zake
    Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limewapiga marufuku wanachama wa kampuni ya Development Enterpreneurship Community Initiative (DECI) kukaa vikundi au kufanya maandamano bila kibali kuanzia sasa.

    Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana kuwa hawapo tayari kuruhusu wanachama hao kukaa katika vikundi kwani vitakuwa na lengo la kuashiria uvunjifu wa amani.

    Kamanda Kova aliwataka wanachama hao wakati wakisubiri suala lao likiendelea kushughulikiwa wakae kwa utulivu na sio kutoka majumbani mwao na kuweka vikundi kwenye ofisi hizo au mahali pengine.

    Kadhalika, Kamanda Kova alisema wameamua kuimaisha ulinzi zaidi baada ya kugundua kuwa kuna baadhi ya watu wamelichukulia suala hilo kisiasa na kutaka kuharibu amani iliyokuwepo kwa kujiweka katika makundi yanayotaka kufanya maandamano.

    ``Nachotaka kusema ni kwamba suala hili lipo katika mtiririko, halihitaji maandamano wala watu kukaa kwenye makundi kulijadili, muachane na fikra potofu za kuliweka katika siasa au kiitikadi, msubiri maamuzi,``alisema.

    Kamanda Kova aliwataka wale wanaotaka kuandamana juu ya suala hilo waombe kibali maalumu kwa ajili hiyo na sio kukutana kinyemela.

    Juzi Waziri wa Fedha na Uchumi, aliviambia vyombo vya habari kwamba akaunti za Deci pamoja na viongozi zimeshikiliwa na serikali kwa lengo la kulinda fedha za wananchi ambazo waliwekeza katika upatu huo.

    Habari zilizotufikia wakati tukienda mitamboni jana usiku, zikidai kwamba, viongozi kadhaa wa Deci walikuwa wametiwa mbaroni.

    Hata hivyo, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, alikataa kuzungumzia suala hilo.

    Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Said Mwema alisema alikuwa nje ya ofisi kwa siku nzima ya jana hivyo pia asingeweza kuzungumza lolote kuhusiana na hilo.

    Hata hivyo, vyanzo vya habari vilidai kwamba, uongozi wa Deci jana mchana ulikuwa ofisini kwa DCI kwa ajili ya mahojiano.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  5. mambo ya ngoso mwachie ngoso, hapa tunachokijua na kujadili ni ganda tu risasi wala hatuijui, hivi hamjiulizi miaka yooote hiyo hao wanakuja juu sasa kukamata na kuongea walikuwa hawaijui deci? Kalaghao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...