Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanda Peter akiongea na wahariri leo ofisini kwake Dar

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema shughuli za Kampuni ya DECI (Development Enterprenueurship Community Initiative) za wanachama kuweka fedha kupata faida marudufu ni sawa na upatu na ni kinyume cha sheria za nchi.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ofisini kwake jijini Dar es
Salaam leo (Jumanne Apr. 14, 2009) alisema ndiyo maana Serikali imeunda timu ya kuingalia DECI na kuchukua hatua bila kuwaathiri wanachama wa DECI.

“Hakuna cha maono wala ufunuo, DECI ni upatu tu. DECI siyo mkombozi ni
ujanja ujanja ambao ambao lazima utaleta matatizo hatimaye,” alisema.

Shughuli za upatu ni kinyume cha sheria Na. 8 ya mwaka 2006, iliyoidhinishwa
na Rais Januari 5, mwaka 2007, kuwa ni kosa kuendesha shughuli za upatu
ambao hauna usalama wa fedha watu wazochanga, aliongeza.

Alisema kuwa timu iliyoundwa na serikali kuangalia shughuli za DECI ina
wataalamu kutoka Benki Kuu, Wakala wa  Soko la Mitaji na Dhamana (Capital
Markets Authority) na Idara ya Polisi.

DECI ilianza shughuli zake nchini mwaka 2007 na iliandikishwa kwa Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA).

Waziri Mkuu alisema DECI ilianzishwa kama chama cha kuweka na kukopa, lakini baadaye ikawa inaendesha upatu na kwamba ina wanachama zaidi ya 430,000 na ina ofisi 46 katika mikoa 18 kati ya 26 nchini, kwa mujibu wa taarifa
alizopata.

Benki ina akiba ya Sh. bilioni 1, lakini fedha ambazo zimezungushwa kupitia
DECI ni Sh. bilioni 13 ambazo zilitolewa na kuchukuliwa na wanachama kama
faida.

Kuhusu suala la ardhi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Waziri Mkuu
alisema kuwa suala la ardhi linatawaliwa na sheria za kila nchi na siyo la
ushirikiano katika jumuiya.

Alisema suala ardhi, kama vile la hoja ya mtu akiikaa katika nchi moja kwa
mfululizo kwa miaka mitano apate uraia wa nchi hiyo, ni masuala ambayo
hayawezi yakachukuliwa kwa pupa na Tanzania lazima iyaangalie kwa makini.

Kuhusu udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma ambavyo baadhi yao
vilifungwa kwa muda kutokana na suala la uchangiaji, Waziri Mkuu alisema
udahili umekwenda vizuri na kunavigezo vipya vya kujua uwezo wa mwanafunzo kucjangia kiasi gani.

Waziri Mkuu pia alisema Tanzania isisite kuhusu kuwaruhusu wakulima wakubwa binafsi kuwekeza katika kilimo cha kisasa cha kibiashara kwani bado kuna ardhi kubwa yenye rutuba lakini haijaguswa.

Alisema kinachotakiwa ni kuwa na Benki ya Ardhi ili muwekezaji akitaka
kuwekeza katika kilimo anapewa ardhi ambayo kwa mfumo wa Tanzania ni ya
Serikali na inatolewa kwa kukodishwa kwa masharti maalum.

Kuhusu uvunjifu wa amani huko Tarime na maeneo mengine katika mkoa wa Mara, Waziri Mkuu alisema Serikali imepanga kuwa na mkoa wa kipolisi wilayani Tarime ili kuimarisha ulinzi.

Vilevile, inafaa kutenga eneo la amani la watu kuweza kukimbilia kama vile
kuwa na kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika maeneo yenye magomvi.

Kuhusu maagizo ya Waziri Mkuu kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) kuangalia hesabu za Kituo cha Mabasi cha Ubungo na Soko la
Kariakoo, Waziri Mkuu alisema kazi hiyo imekwishaanza na kwamba amepewa muda wa kutosha kuikamilisha.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kuna Vifungu vingi vinazuia ufisadi lakini vingozi wetu asilimia 97 ni mafisadi,

    ReplyDelete
  2. Jamani hii DECI si ndiyo ile ile SPA ya miaka ile. Wachache wa kwanza walibahatisha. Waliobaki wote wakaingizwa mjini. Sasa imeibuka na jina jipya?

    ReplyDelete
  3. (US Blogger)

    Asante PM kwa kuweka hili swala wazi manake huu wizi ungeumiza wengi bila ya Serikali kuingilia.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa Pinda,

    Asante kwa ufafanuzi na kuweka mambo sawa kuhusu DECI.

    Umetumia vema usomi wako wa sheria, na mamlaka yako ya u-PM kumaliza danadana katika utapeli huu wa DECI.

    Sasa naomba uwageukie waliokwiba mabilioni ya wananchi hapo BoT kieleweke kabla ya uchaguzi wa 2010.

    La sivyo danadana za watu kuuza sura mahakamani hazitatufikisha popote, na wengine tushaanza kuamini kwamba viongozi wetu mnavuta muda tu mpaka uchaguzi wa 2010 upite.

    Siku njema

    ReplyDelete
  5. Nakuunga mkono ndugu yangu hapo juu,Maana bongo likitokea jambo ambalo linaathiri shughuli za wakubwa{hao mifisadi}Basi hatua za harka zinachukuliwa lakini upande wao utasikia ooo kuna tume sijui miezi 6 sijui mwaka alimradi wajisahaulishe na jambo hilo,
    Hayo yote ni sababu ya kulinda hizo saccos zao kwani hilo silinajulikana na wakatunga na sheria kabisaaaa,
    tafuteni njia mbadala ya kusaidia hiyo deci ijiendeshe kwani si linawezekana kama walikuwapo kwa miaka 2 sasa ina maana wanaweza kujiendesha ziangaliwe kasoro zirekebishwe libeneke liendelee.
    mdau jp

    ReplyDelete
  6. AFANAAALEKII NAJUTA KUWAAHAM WAWAMBIE WANANCHI NINI WAFANYE KWA MTAJI UPI NI BORA NA UTAWASAIDIA KAZI AU KILIMO PIA VIZURI IKIWA SERIKALI WAMELIONA HILO NAOMBA KUWE NA NJIA MBADALA ILI NAFUU YA MAISHA IPATIKANE
    DUNDA

    ReplyDelete
  7. suala la ardhi nawashauri watanzania tusikubali ardhi yenu kufanywa ya jumuiya ya afrika mashariki kwani wakenya ardhi ipo wapi?TUSILEGEZE MSIMAMO HATUHITAJI ARDHI YAO ILIYO JANGWA NA WAO WASITAKE ARDHI YETU.Nimesikitika kusoma standard la Kenya kuwa kuna matajiri wa Kenya ambao wameshanunua ardhi huko Tanzania na wanawaajiri watanzania kulima BANGI na kuiuza nchini na kwao Kenya.Jamani tukishakubali ardhi kuwa ya jumuiya ya Africa mashariki tumekwisha tutakuwa watumwa katika nchi yetu na wengi wetu tutaishi katika slums,je hamjaona Kenya wanavyotaka kunyang'anyana Ekari moja tu ya kisiwa cha Migingo na Uganda kiasi kwamba wanataka jeshi lao lipelekwe kisiwani humo..TUKATAE NCHI YET KUUZWA.WATOTO WETU WATARITHI NINI?

    ReplyDelete
  8. Hiyo ni "pyramid" ni hatari kwa wananchi na serikali ya Tanzania. Watakao naswa ndali watalia, kwa uhakika wataibiwa. Mimi nishashuhudia kitendo kama hicho na watuwengi walipoteza pesa, nyumba, ardhi nk.
    Huo ni utapeli wa hali ya juu.

    ReplyDelete
  9. Lakini Nina wasiwasi na Data alizotumia Mheshimiwa Pinda.

    Billion 13 kwa watu 430,000 ni pesa ndogo saana kwa mtu mmoja mmoja ni kama 30,000 .... ambayo watu isingewasumbua.

    Kuna data zaidi zimejificha.

    ReplyDelete
  10. billion moja tu bank sasa hivi....weweeee watu wameshaibiwa hapo.....huyo anayesema kuna data zimejificha hamna lolote....huo ndio ukweli....kuna watu wanawalisha wenzao hapo....billioni 13 zimetoka kwa hao hao zinahamishiwa kwa hao hao tena.....ni hela inazungushwa tu hapo

    sasa ukitaka kujua wameliwa waambie wooote waseme kila mtu kawekeza shilling ngapi hapo na jumla yake ni more than billion 13 na zote wanakula wakuu wa DECI.....

    MADOFF fraud hiyo....uzuri wa madoff ni kuwa yeye ni jela tu na akipitiswa mitaani yupo na bullet proof vest yake na hamna wa kumwendea bagamoyo huko ....hapa bongo watu wakianza safari za bagamoyo hao wakuu wa deci watapuputika weeeeeee hata hayo majumba wasiyaenjoy....watch out people

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...