Ama kweli Kuishi kwingi ni  kuona mengi! 
The Ngoma Africa alimanusra wamfikishe PAKA  kwa pilato wakati wa Pasaka!

Ni kweli kwamba wengi walifurahia Pasaka, na si uwongo kwamba  na mabalozi wetu Ngoma Africa au sauti ya zahabu kutoka afrika mashariki nao walikuwa na party yao ya faragha ya wenyewe kwa wenyewe, ambayo hawakutaka mtu mwingine asiyekuwamo katika kikosi hiko cha FFU kuwemo!

Lakini katika party kiongozi wao Ras Makunja alikuwa hayupo,alikuwa bize na maandalizi mengine muhimu kama kawaida yake.

Baada ya Pasaka kwisha jumanne ya 14 watu wote wameanza kazi katika maofisi yao! Kiongozi wa ngoma afrika Bw.Kichwa Ngumu Ras makunja asubui na mapema anapigiwa simu na wakili wa bendi yao hili aende kuleta muafaka kati ya wanamziki wake na Raia moja wa kijerumani ambaye anamiliki PAKA anayedahiwa kuiba mishikaki ya wanamziki hao walipokuwa wakibabque! 

Yaani unaambiwa kama sio kiongozi wa bendi hiyo kuifuta kesi hiyo,tayari PAKA huyo angetinga mbele ya Pilato kwa kosa la kukwapua mishikaki ya wazee wa kukaanga mbuyu.

Japokuwa wenyewe soo hili walitaka liwe siri.....lakini baadhi ya wanamziki walikuwa
wakimlalamikia kiongozi wao kwanini ? why?? alifuta kesi wakati akijua kuwa ughaibuni kila kitu kinafuata mkondo wa sheria???????

hakaaaa!!!!huo udaku mie simo
 
Mdau Msemakweli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 57 mpaka sasa

  1. Vicha wetu?vipi tena jamani ?kwani huyo paka akupewa mwaliko!

    ReplyDelete
  2. Ndio machizi wetu waswahili wanasema unapokuwa Roma lazima ufuate taratibu za warumi,hapa hamkukosea mmefuata taratibu za kisheria lakini ole wenu kama mngempiga huyo paka hizi habari zingekuwa zingine hapa,muwe na utaratubu huo huo,japokuwa akili zenu mnazijua wenyewe

    ReplyDelete
  3. Sasa nyie kweli mnawazimu! jamni
    PAKA ! inamaana kweli mlikuwa serious na hii kesi???

    ReplyDelete
  4. Sasa ngoma africa jamani?
    mbona paty yenyewe ni hamtaki wageni kwani kuna vilaji gani?ndani ya paty hiyo,si mnaona paka kakuzidi kete akiingia na kuchukua chake,nyinyi wenyewe mmeijua njia ya kwa wakili

    ReplyDelete
  5. E! bwana mdau ras makunja,kesi vipi?mbona mpya na umeamua kuwaminyia wadogo zako? si ungeacha tu waende paka shume kwa pilato?

    ReplyDelete
  6. ah machizi wetu? kiasi palikuwa shwali hapa? KWANZA POLENI SANA KWA PAKA SHUME KUCHUKUA PANDE LA NYAMA CHOMA? HALAFU NAJUA KAMA SIO
    KAKA YENU RAS MAKUNJA,HILI TAYARI LILIKUWA SOOO LA KIMATAIFA

    ReplyDelete
  7. kw!kw!kw! paka hana uwoga? ndani ya kambi ya FFU anajipendelea kwa minofu? mungu bariki vingivyo tungesikia paka nae kakaangwa

    ReplyDelete
  8. hapa kweli huyu paka amewaonea!
    hii kesi ingeenda tu mbele ya pilato,halafu tungesikia mwisho wake,hivi kwani kuna jela ya wanyama kama paka au mbwa huko ughaibuni

    ReplyDelete
  9. kaka braza ras makunja,si ungeacha tu hili soo liende mbele kwa mbele

    ReplyDelete
  10. katika siku mliokamilisha siku yangu ni leo!!!! hivi nyinyi ngoma afrika kila siku nawasikia nyimbo zenu zinanigusa na mara nyingine kutoa machozi kwa kile mnachokilalamikia! lakini hii ya leo mungu wangu! imebidi nicheke kiasi cha kutoa machozi!!!
    yaani hii kesi mngekwenda nayo mbele kweli????
    kwa sababu nyama si mngenunua tu harafu yakaisha

    ReplyDelete
  11. washikaji? hawa jamaa noma sana!
    hii ni kali ya aina yake,ndio tuseme hapa haki ya kisheria lazima ingepatikana?

    ReplyDelete
  12. ukisikia mgeni anafuata taratibu zilizowekwa na wenyeji wake ndio hivi! usichuke sheria mkononi.
    nyinyi waungwana sana Ze Ngoma Afrika,eh hile shutuma yenu na baba wa kambo vipi?

    ReplyDelete
  13. WEWE? PAKA WA KIZUNGU KWANINI?
    UMEKULA MSHIKAKI WA WATOTO WA USWAHILINI? UJUI HIYO NI HATARI?
    KAMA WANGEKUPIGA MAWE

    ReplyDelete
  14. hello! kaka braza ras makunja,nasikia baba wa kambo kakununulia miwani mipya ya zahabu?
    tena umekuwa mtu mkimya sana,sijasikia madongo mapya siku hizi.

    ReplyDelete
  15. unajua ulayahakuna mambo ya kibongo
    heti umpige paka wa mtu kwa kuchukulia kitoweo,unaachotakiwa kufanya ni kama hawa ffu wetu lazima uwe na wakili wa kutetea haki yako,lakini kama wangedhubutu kupiga japo kofi mwenye paka angewashitaki wao kwa kunyanyasa mnyama.wamefuata sheria na wangelipwa fedha,sema tu huyu kiongozi wao labda kataka pasiwepo uhusiano mbaya ndani ya jamii ya ughaibuni.
    Hongereni sana

    ReplyDelete
  16. sasa wadau? hapa kidogo pananiacha mdomo wazi? yaani mishikaki ingemfikisha paka mbele ya hakimu?
    kwamba kafanya uharibifu wa mahakuli ya waungwana FFU?

    ReplyDelete
  17. te!te!te! kama siyo mkaka braza wao ras makunja,tunavyowajua wajamaa lingukuwa soooo tena sooo lisilikwisha mpaka haki ingetolewa,
    paka kajipenyeza katika paty ya watu wa shoka bila ya mwaliko,mungu wangu yamemalizika.
    mkaka braza huo na moyo huo huo
    ukubwa jiwe

    ReplyDelete
  18. ughaibuni heti paka na mbwa wana haki kuliko mgeni,lakini sheria hizi za kijinga jinga ni ulaya tu,hapa kwetu watu hawana time ya kuweka sheria ya haki ya wanyama..
    kwanza mpaka mwenyewe anajua wazi kuwa akila nyama ya mlalahoi atakiona cha moto

    ReplyDelete
  19. kaka zetu ngoma africa kweli wachoyo! paka naye mmehamua kwenda naye mbele ya sheria?
    msalieni mungu jamani

    ReplyDelete
  20. paka huyu vipi? kaka makunja
    amevamia kambi yako na kupora mnofu wa ffu?
    au alivyosikia ras ni msamalia mwema basi alijipenyeza tu? na kukuta msamalia mwema haupo bali majeshi ndio yanachoma choma?

    ReplyDelete
  21. Hivi nyie hamjui kuwa wenyeji wanachukia sana wageni. Huyo PAKA angelikuwa amepigwa na wao wangekipata cha moto. Make angewafungulia mashtaka hizo gharama wangezilipa na nini? Make angewaambia matumizi ya PAKA ni makubwa kuliko ya binadamu. Hawa kaka wana akili sana. Hizi nchi za ULAYA na MAREKANI hawana mchezo kwa mnyama wao. Na huyu mtu angewaambia kuwa wangemshitaki police akalipa kuliko kumpiga PAKA hapa sio utani.

    ReplyDelete
  22. eh ngoma afrika hili lilikuwa deal la nguvu,lazima mngelipwa kifuta machozi,si mnajua hawa wanyama kama paka na mbwa huko ulaya wanakuwa na bima ya fidia wanapofanya uharibifu.
    ndio sema tu huyo kaka bro kayaingilia kati

    ReplyDelete
  23. we acha tuu jamaa wanujua ULAYA ukikitaka kukiona cha mtemakuni piga mnyama PAKA! au MBWA! wangechukua hasira za kibongo bongo sasa hivi tungesoma mengine magazetini,bora walivyompeleka POLISI

    ReplyDelete
  24. LAKINI KATIKA HII PATY YA VICHAA WETU!!!MBONA WENYEWE TU? KULIKUWA NA NINI? WALICHUKUA WANAKIFICHA AU MJADALA GANI ? ULIOTAKIWA USIENDE NJE YA NGOMA AFRIKA??
    KWA SABABU ISIWE WALIKUWA WANAMZENGWE WA KUTOKA NA SERA MBAYA YA KULETA ZOGO NDANI YA JAMII?SI WATU WAKUFANYA NAO MCHEZO KATIKA KAZI YAO

    ReplyDelete
  25. Hapana lazima kulikuwa na jambo ndani ya paty hii,sidhani kama hilikuwa paty tuu,labda walikuwa wanakaanga mbuyu mpya,Mungu akapeleka kiumbe hiki PAKA na mbuyu zao zikavurugwa na kesi ya paka

    ReplyDelete
  26. PAKA ANAPOJIPENDELEA NA MNOFU RAHA TUPU,WAKAANGA MBUYU ! MBUYU AZIKAANGIKI PAKA KALA KITOWEWO

    ReplyDelete
  27. Kaka braza ras,pole sana kazi leo hapo PAKA kala kitowewo cha ffu?
    vipi? sasa PAKA kala mishikaki inamaana ffu walibaki na chachandu tu? bila ya mishikaki kazi hakuna
    kaka

    ReplyDelete
  28. RASTA HARUHUSIWI KULA NYAMA
    NI MKOSI TOKA KWA MIZIMU YA HAILE NA BOB MARLEY
    KESI INGEKUKWA MBAYA ZAIDI KWAO.
    NAYAJUA HAYA MAMBO YA MIZIMU YA MARASTA

    ReplyDelete
  29. hi wakaanga mbuyu sasa hii inakuaje?paka anaondoka na asusa?
    kwa nini msimshughulikie,sheria ingefuata baadaye

    ReplyDelete
  30. sasa wewe unawalaumu kuwa vichaa wachoyo wamshitaki paka mbele ya sheria! kumbe ulitaka wafanye nini?
    ughaibuni mnyama analindwa kisheria,na kafanya madhara ya kula
    mishikaki ya watu lazima ashitakiwe

    ReplyDelete
  31. mimi nakubaliana na moja ya wachangaiji hapo juu,hawa lazima walikuwa wanakaanga mbuyu mpya,hili wakitoka basi piga au ua zogo kubwa atupati usingizi,lakini mungu kampeleka kiumbe PAKA kazua mambo mengine mbuyu zimechelewa kukaangwa

    ReplyDelete
  32. Kaka braza Makunja wewe hodari sana wakurusha madongo na kukaanga mbuyu ! haya mambo yapo ndani ya nyumba yako? jikaangie mwenyewe tukusikie,tena watoto wako mwenyewe wamechoma nyama wakati we haupo mara PAKA kawalaza na njaa ffu,kaanga sasa ?

    ReplyDelete
  33. paka ni paka tu awe wa ulaya au wa
    uswahilini,sasa paka kaondoka na nofu la FFU? ingekuwa hapa kwetu oh! tungesema paka wa uswazi wana njaa,sasa huyo si paka wa uzunguni?
    vipi ?kaibia nofu la ffu?

    ReplyDelete
  34. kaka ras Pokea wimbo mpya huu
    Nyau! Nyau ! Nyau kala minofu!
    ya ffu.
    Kaka braza pole sana na zogo hili,lakini waenga walisema kila mpuliza moto cheche umrukia mwenyewe,sasa hapa naona mambo makubwa,sasa MADONGO ya kisa hiki yatakuaje? wewe hodari ya kuimba wenzako tena upitwi na jambo tayari ushaenda kurekodi,sasa hili vipi???

    ReplyDelete
  35. EH! NGOMA AFRICA ! POLENI SANA
    NDIO SASA HIVI NARUDI KUBEBA BOX!!
    NAKUTA HILI SOO HAPA BARAZANI!
    SASA IMEKUWAJE TENA WAKAANGA MBUYU WANGU? MBONA HUYU PAKA ANAKUAANGIENI MBUYU NYINYI?
    NASIKIA KALA MINOFU YENU? ISTOSHE NAONA KAKA BRAZA NAE KATUMIA BUSARA ZA KIBONGO KUFUTA KESI!
    MNGEVUTA KITU KIDOGO KWA MMILIKI WA PAKA TENA! EURO

    ReplyDelete
  36. leo leo paka kala nyama ya majeshi!
    do noma kweli! PAKA WA KIZUNGU kala mishikaki ya wajumbe wa mambo! wenyewe kuchokoa chokoa mambo na visa vya uswahilini.

    ReplyDelete
  37. Wanasayansi na wataalamu wa tabia za wanyama,wanasema PAKA na FARASI ni wanyama welevu tena wanautambuzi wa hakili ya hali ya juu! katika kesi hii ya hawa vijana na PAKA aliyewalia mishikaki,lazima paka alijua katikai mkasanyiko huo kuna jambo na mahakuli lazima yatakuwepo kitu kama nyama,katika utambuzi wake huo naona alichukua hatua ya kujenga urafiki wa mda na moja wa vijana hao,naisi kitu kama hiko lazima kilikupo.
    Hatua hiliyofuata Paka huyo labda alitumia upenyo huo kwa kujialika mwenyewe na kuona hakutumpiwa ata kipande cha nyama,kama ni hivyo paka lazima ajipendelee kwa kuchukua chake.
    Na hawa walalamikaji nao wakaitumia nafasi hiyo kuitumia sheria kuwa paka huyo kawaharibia starehe zao kwa kuingilia chakula.
    JAMAA WELEVU UGENINI

    ReplyDelete
  38. hello wajumbe msilete gozi gozi hapa,hawa vijana wetu ffu wameliwa mishikaki yao,cha kutia uchungu kamanda wa kikosi kaifuta kesi kwa kigezo cha usamalia mwema,lakini

    ReplyDelete
  39. eh! hakuna anaeleta gozi gozi wala nini?hila tunachouliza paka kaingiaje kwenye kambi ya makomando?je kama yule paka angekuwa na kombora au milipuko?inamaana kikosi kizima cha wakaanga mbuyu kingeteketea? hili nao lazima tulizingatie tusiongelee paka kala nyama tu

    ReplyDelete
  40. wewe mtoa Anony hapo juu vipi?
    TUSILETE GOZI GOZI? LAZIMA GOZI
    LAZIMA TULETE KWA SABABU MISHIKAKI
    IMESHALIWA NA NYAU
    LILILOBAKIA NI GOZI TU AMBALO KAKA BRAZA MAKUNJA LAZIMA ALITUNGIE WIMBO NA KULIKAANGIA MBUYU

    ReplyDelete
  41. sasa kaka ras makunja kesi hii vipi? umeifuta au kuna deal gani?na mwenye PAKA? nauliaza kwani wewe maarufu kwa kukomalia kichwa mambo ya jamii hili haki itendeke sasa kesi hii haraka sana umeifuta na BABA WA KAMBO ulikuwa mstari wa mbele kulikoni?????

    ReplyDelete
  42. hi!mwe!mwe mwe kweli huyo mwenzetu hapo kanena jambo la maaa usalama wa FFU ,kama yule nyau angefungwa mlipuko inamaana tungewapoteza wacheza LIGWARIDE ??? maana usalama vichaa wetu nao muhimu kutokana na kazi yao ya kukipaka choo pale wanapochoshwa na longo longo

    ReplyDelete
  43. HELLO! WAJUMBE NI KWELI KUHUSU UASLAMA KUNA MCHANGIAJI HAPO JUU KAONGELEA SWALA LA TABIA YA WENYE ROHO MBAYA WANATUIA HATA WANYAMA KUWAFUNGA KOMBORA,HILI NALO TULITILIE MANANI TUKIZANGATIA HAWA WANAMZIKI WENYEWE LABDA HAWAJIJUI DARAJA GANI ?WANALO KATIKA JAMII,MCHANGO WAO KATIKA KUYASHIKIA BANGO MAOVU YAMEWAFANYA KUWA MAARUFU NA PENGINE KUWA NA AMAADUI! AU NDIO TUSEME BONGO ATUJAFIKIA KIWANGO CHA KUWACHUKULIA WASANII KUWA WANASAUTI YA JUU KATIKA JAMII?????

    ReplyDelete
  44. paka si alidhani jamaa marastafarian ndo mana akajimegea tu zagazaga!ye alijua huo ndio msosi pekee unaomfaa kwani rasta hali nyama!

    ReplyDelete
  45. Sasa wewe anony
    unayezungumuzia usalama wa wanamziki! sasa hawa wanapokuwaga jukwaani si wanapewaga ulinzi wa kutosha na hapo hapo washabiki wanawazidi nguvu walinzi!
    Sasa hapa leo Paka nae kawazidi nguvu washikaji kwa kuchukua fungu lake minofu ya mishikaki.
    Uoni kuwa mungu pekee yake ndiye anayelinda viumbe wake.
    hawa wanamziki nao wanalindwa na mungu

    ReplyDelete
  46. PAKA kumbe huko ulaya nako kuna
    mapaka wezi kama bongo? basi kumbe
    bora bongo tambarale,paka wa bongo mpaka uwamegee ndio wanakula

    ReplyDelete
  47. Hawana maana haoo mngempeleka tu huyo pka mahakamani mkalipwe,maana hawa watu wa hizi nchi bora wakulaze njaa mgeni lakini sio mbwa au paka hapa nilipo mimi kuna bibi saa 12 asubuhi utasikia eti anaongea na paka na mbwa hana cha mjukuu wala nini toka nije hapa ni mwaka sasa yeye na mbwa na paka tu
    ahhh binadamu lazima achukue nafasi yake bwana.
    mdau jp

    ReplyDelete
  48. vichaa wetu poleni sana kwa kulazwa na njaa na paka shume,ndio ulimwengu paka nae kakuombeni udugu.

    ReplyDelete
  49. YAANI WEWE ACHA TUU
    PAKA KAFANYAZIA MISHIKAKI YA WAUNGWANA? HALAFU KAKA BRAZA ANAWASALITI FFU KWA KUFUTA KESI!HETI MAMBO YASIZUE MZOZO? SASA MBONA TUMEYASIKIA KUWA PAKA KAJIRUSHA KATIKA PATY YENYE ULINZI MKALI! TENA NDANI YA KAMBI YA FFU!
    PAKA SHUPAVU KULIKO WAZEE WA KUKAANGA MBUYU

    ReplyDelete
  50. Hiiiiii!!!!PAKA KAWAZIDI KETE FFU
    Hongera balozi michuzi kwa kisa hiki,jamaa na umarufu wao wote mbele ya paka hawana ujanja

    ReplyDelete
  51. hao maras vipi nofu hjilo. ndo maana paka katimua nao vumbi. Makunja hakualikwa angegoma manofu kuletwa hapo.

    ReplyDelete
  52. duh kumbe marasi mnatamani sana manofu na hiyo dini yetu. mnajifungia ndani kiongozi wenu asijue. bora nyau kawaumbua.

    poleni sana

    ReplyDelete
  53. PAKA ALIWAONA WENZIE WAKIJIBURDISHA NDIO AKATINGA NAO SASA IWEJE MNAMTOSA,HHHAHAHA UTANI KIDOGO

    ReplyDelete
  54. MARASTA GANI WANAKULA NYAMA

    ReplyDelete
  55. sidhani ka niwote marasta pale!
    lakini Ras Makunja mwenyewe huyo niwazi anajulikana kuwa ni VEGITERIAN ni mtu wa kula mboga mboga kwa miaka mingi ndio maana kila siku yupo vile vile

    ReplyDelete
  56. SIO WOTE WANAMZIKI WA NGOMA AFRIKA NI MARASTA! NI RAS MAKUNJA TU NDIYE LABDA ASIYEKULA MINOFU HUYU ANAJULIKANA WAZI KUWA NI MLAJI WA MBOGA MBOGA ZA MAJANI NA ATUMII ULEVI WA AINA YOYOTE!!!!LAKINI VITU VINAVYOTOKA MODOMONI MWAKE!!!
    MARA NI NYINGI NI MWALIKO WA USHALI

    ReplyDelete
  57. Katika paty ya minofu ndio maana Ras Makunja kaikwepa kajua lazima kungekuwa na zogo la nyama !si yeye mwenyewe ni vegiterian na kawachia uwanja nduguze wajifarague mara paka katibua raha zote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...