wasanii wenye ulemavu super convoy (shoto) na mmasai wa njano wakifanya vitu vyao kwenye sherehe ya send-off katika ukumbi wa holland hall uliopo msimbazi centre jijini dar. awali madansa hawa walikuwa na kundi la tot ila sasa hawana ajira na wanajitafutia riziki kwa kutoa burudani kama hivi, badala ya kuwa omba omba mitaani. globu ya jamii inawafagilia sana wadau kama hawa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. This is supper!

    Hawa wamekuwa ni mfano wa kuigwa...sio kama wengine wanaong'ang'ana na 'Umatonya' usio na mpango katikati ya majiji...

    ReplyDelete
  2. Hii safi sana Michu.Thanks.
    Mdau
    USA.

    ReplyDelete
  3. Lakini sio vizuri kuwatupia pesa hapo chini....wangeweka chombo.

    ReplyDelete
  4. Kuna mwenzao mmoja anaitwa Pajero Punk yuko wapi siku hizi?

    Jamaa wanajituma sana ni mfano mzuri kwa jamii kwamba ukiwa mlemavu si kigezo cha kushindwa kujitegemea.Banza Stone (le general) aliwatumia sana hawa jamaa enzi za achimenengule

    ReplyDelete
  5. MICHUZI, UNAWEZA KUANIKA NAMBA ZAO ZA SIMU HAPA KWENYE BLOG YETU? AU TUAMBIE TUTAWASILIANA NAO VIPI. MIMI HUPENDA KULA NA WATU KAMA HAWA HASA NYAKATI ZA PASAKA, EID, KRISMAS, NK. SIYO LAZIMA NIKAE NAO. NIKIWA NA VIJISENTI NAWATUMIA MOJA KWA MOJA BILA HIYANA.
    MUNGU KAWAJALIA VIPAJI HAWA, SI UTANI...

    MSOMAJI,
    UNITED STATES OF AMERICA a.k.a USA

    ReplyDelete
  6. Watu kama hawa wangekua na sehemu nakupatiwa ajira ila ndio hivyo tz yetu, hao wenye mikono na miguu tu wenye ajira ni wachache ije kua hawa

    ReplyDelete
  7. Hivi hata wheel chair hazipatikani kwa bei rahisi? Nakuunga mkono mdau hapo juu, hembu wekeni mawasiliano yao ya simu, email ili tuwachangie angalau wapate wheel chair kuliko kusotesha mikono yao chini kama hivyo.

    ReplyDelete
  8. Mimi nitawatafutia vimashati tuwili tutatu wawe uniform na kama watapenda vikaptula jamani kaka naniiih weka contact zao nakuja summer uko mdau
    Uk

    ReplyDelete
  9. Embu acheni kujishaua, kwani sehemu za walemavu hamzijui? nendeni Bongo kwenye vituo vya watoto yatima na walemavu mkawasaidie sio kujifanya mnataka kutoa msaa nyuma ya pazia, ooooh UK, siojui USA, ndugu zako ushawasaidia au unataka kujionyesha tu??, Mtoa sadaka Bora ni yule atoae kwa mkono wa kulia Huku wa kushoto haujui nini kinaendelea.
    Walemavu wangapi wanahitaji msaada, hamjasaidia, mpaka Michuzi Apost hapa ndio mnaanza kuwa na moyo wa Huruma sio!!

    ReplyDelete
  10. Inapendeza kuona vilema hawako nyuma ktk kujitafutia riziki. Tunaomba contacts tafadhali.

    ReplyDelete
  11. i saw some kinda of wardrobe mulfunction au macho yangu kwikwi...! shughuli kwelikweli

    ReplyDelete
  12. Gospel nothing more

    ReplyDelete
  13. Anony wa April 17, 2009 6:17 PM

    Usiwahukumu watu maadamu wanataka kusaidia. Hata kama hawafanyi vile wewe unavyotaka, lakini wakiwasaidia hawa walemavu ni makosa? Mbona una akili finyu ndugu yangu. Wazungu wanasema 'information is power'. Si kweli kuwa kila wakati unafikiria kuwasaidia walemavu. Hadi saa zingine uamshwe. Kwanini wewe ukiombwa na mtu njiani unampa msaada, wakati huohuo hujasaidia nyumbani unakotoka? Acha kupima mizani isiyo hata na maana!
    Kwa hivo ungefurahi hao vilema wasisaidiwe? Afterall, naamini anayetoa ni chaguo lake, atoe kwa nani, na kwanini. Usimchagulie.

    Mbona hujamtukana Michuzi, wewe mshikaji unayejua sana. Maana ungeanza na Michuzi aliyetuwekea picha kuwa anajishaua, kama unadhani hilo neno lako lina maana sana! Una roho ya kutu. Kuwahukumu hao washikaji, tayari nawe unstahili hukumu, maana udhanio ni mafarisayo wanaweza wasiwe, maana nia yao anayeipima ni Mungu tu, si wewe! Wabongo, wabongo, wabongo! Sina hamu nao. Ingekuwa kifurushi, watu wenye roho ya kwanini kama wewe, natupa baharini na jiwe kuzamisha kabisa...... Aaaaaaaaaaa grrrrrrrrr!!!

    ReplyDelete
  14. Imekuwa vizuri kuwa baadhi ya vipaji vya kweli kama hivi vinaanza kukubalika.Maana hapo awali ingekuwa ni ubatili.Kwani huyu dada mwimbaji anakubalika hata na sisi waislamu kwani mungu ni mmoja lakini dini anayotokea waliwahikumuwekea vikwazo vya imani.Na sasa tusubiri kuona baada ya hawa jamaa kwani ibilisi wengi wako katika dini.Ila hapa ni mfano mzuri na wa kuigwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...