Michuzi,
Naomba email yangu iwe private. Naomba uweke hii kwenye mada yako. Nina kaswali kamoja tu.

 Kwa nini wanaume hasahasa wa kitanzania hawawezi ku express feelings zao kwa wake zao au waume zao; Ukiwaacha ndio wanaanza eti ooh ninakupenda, ooh sirudii tena na mambo kebekebe. Kwa nini?? Why??

Sent on the Now Network™ from my Sprint® BlackBerry

Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. Samahani, hivi wanaume nao wana waume??

    ReplyDelete
  2. mdau,
    wanaume kuexpress feelings zao kwa WAUME ZAO???!!! Mhh
    Gordon.

    ReplyDelete
  3. kabla ya watu hawajakusukutua naomba kwanza ujisafishe matongotongo yako usijeukawachafua vinywa vyao!
    WANAUME WA KITANZANIA HAWAWEZI KUJIEXPRESS FEELINGS ZAO KWA WAKE ZAO AU WAUME ZAO?!
    Huna adabu wee! yaani wanaume wa kitz tunaoana?!
    pus, paka, nyau!
    nakuweka kiporo, nawaachia makuli wakiamka UTASHAAA!

    ReplyDelete
  4. Dunga DungaApril 20, 2009

    what kind of nonsense!

    hata wanawake huwa hawaexpress chochote. i have dated 16 girls so far na sikuona expression yoyote ya maneno (verbal) zaidi ya mimi mwenyewe kuwa mchokozi kusoma body language na kusukuma kingi nikiona njia nyeupe.

    at least wanaume huwa tunaexpress feelings KWA MANENO wakati tunakutongozeni, na pia KWA MANENO during the relationship especially pale tunapotaka ngono, na pia KWA FEDHA mara kwa mara kama vile kukunulieni zawadi na kuwatoeni out.

    Out of curiosity wewe uliyetuma hii nonsense umeshakuwa na mahusiano na wanaume wangapi wa Kitanzania?

    ReplyDelete
  5. hawawezi ku express feelings zao kwa wake zao au waume zao? sikujua wanaume wakibongo nao wanaolewa siku hizi.....

    ReplyDelete
  6. sasa na wewe hueleweki..umewazungumzia wanaume iweje uweke tena waume zao au wanaume wana waume zao pia???? Wanaume wengi wanapenda kutikisa kiberiti kama kimejaa, wakikikuta kipo mdebwedo basi watakuokukanyaga weee bila huruma lakini wakio kimejaa ndio nisamehe utapewa.


    Hawapendagi kujishusha hao wanapenda kuwa JUUUUU hata kama wamekosa.....

    ReplyDelete
  7. KUTOJIAMINI,INFERIORITY COMPLEX,DHARAU KAMA ILIVO TAMADUNI MWANAMKE NI KITU TU,

    nk nk.

    unamaanisha nini unaposema wanaume wa kiTz afu wasema hawaonyeshi mapenzi kwa waume zao?

    ReplyDelete
  8. Mdau, pole kwa yaliyokukuta maana umeandika kwa jazba!

    Mimi kwa maoni yangu, siwezi kusema kwamba wapenzi wote huwa hawaambiani kuwa wanapendana kama wanapendana. Uzoefu wangu na mume wangu tangu tukiwa marafiki tuliambiana pale tulipohisi hisia za kimapenzi zimeshamiri. Mpaka leo, huwa haipiti wiki bila mmoja kumwambia mwenzie kwamba "Nakupenda". Kikubwa ninachokiona sana kwa hao unaowasema wewe ni kiburi cha kutotaka kuonekana "dhaifu wa mapenzi". Kwa wale wenye imani hizo, huwa nawaonea huruma sana. maana wakati unambania mwenzio, hujui pia nawe kama unapendwa au la! Kwa hiyo wewe pia ningekuuliza, ulimwambia ?? au ulikuwa unasubiri aanze yeye?

    Salaam,

    Dada

    ReplyDelete
  9. michuzi,huyu kaachwa! ngoja nimuimbie!!

    kuachwa,kuachwa ni shughuli pevu*2
    mbaya zaidi pale mwenzio ana nenepa wee unakonda*2

    Note:inategema,usitegemee mimi mwanaume wa kibongo kukupa too much attentions wakati wewe huonyeshi feelings zozote.inabidi unijengee confidence,na hiyo confidence itatokana na trust na upendo wa dhati,sisi ugonjwa wetu ni mdogo tu ni kuonyeshwa upendo tu na security kwamba hakuna mazingira tata! what you gie is what u get dada yangu.uki ni win mbona hivyo vitu ni vidogo tu!

    ReplyDelete
  10. "Kwa nini WANAUME hasahasa wa kitanzania hawawezi ku express feelings zao kwa wake zao au WAUME zao" !!!!!!!!!!!?????????????????
    mbona sikuelewi braza. wanaume wana waume au ndo mambo ya huko uliko mdau mmeruhusiwa kuolewa au kuoana?

    ReplyDelete
  11. Hivi nyie hebu komeni mnamchambua mwenzenu bila aibu!!!! Hajakosea huyo kwani nyie hamjaona wanaume wana waumezao hapa Tanzania?? Wapo kibao?? Nenda Lango la jiji au sehemu zozozote za starehe utawaona tuu mume na mke wajinsia moja.. Mwaya hao wanaume wanaoshindwa kujiexpress their feelings ni MADOMO ZEGE..

    ReplyDelete
  12. Haja kosea huyooo msimuhukumu jamani...Anaowazungumzia ni MASHOGA haoo babu hebu eleweni....Mnajitoa fahamu hakuna waume na waume zao…..Haluuuuu najuta kusikia........

    ReplyDelete
  13. NautiakasiApril 20, 2009

    Ha ha ha Utajuuuuuta kumfahamu, kukataliwa kubaya jamani, mwacheni ahangaike...!Sabah Salum Muchacho anawimbo wake mmoja anasema "..hujarogwa mlimwengu usitafute sababu, hiyo ni fimbo ya mungu yakushika adabu, unalia kwa uchungu, haina wakukujibu, kanighufuia Mungu jaza yangu ni thawabu, lililobaki uchekwe wewe siwakupewa pole...." weweeeeeeeee, ndo basi tena unamakinda ya mbwa wajisifu una ng'ombe!?

    ReplyDelete
  14. uwoga na kutojiamini,domo zege

    siku izi totoz zimeenda skuli,exposed life,kazi swafi,pesa nje,zinachonga kinoma nk nk

    yan jameni ukitaka kuingia shurti mwanaume ujikaze aswaaa yan ukimuendea ovyo mbona UTAJUUUUTA KUMFUATA??
    lets be ourselves vijana!lets speak out dont shy away

    ReplyDelete
  15. *..wahenga wanalongaaa: 'mapenzi ni kikoa, nipe nikupe'...

    *mdau kauli zako zimelalia mrengo mmoja...kama maoni ya wengi humu ndani kuwa 'labuda' umefura kwa jazba zimekujaa na aghalabu hizo ni dalili za mtu 'aliyetendwa'..poleee mwakwetu!!!...

    ReplyDelete
  16. Wachangiaji wote nimeyafurahia maoni yenu. Mimi sina cha kupunguza au kuongeza. Kila la kheri.

    ReplyDelete
  17. Mbona unafanya generalization kwa wanaume wote hata usiowajua?Ili upate jibu sahihi jiulize wewe kwa nini wanaume unaokuwa nao(sijui mpaka sasa ushafikisha wangapi)hawaexpress feelings zao kwako(sijui we ni mke au mume wao)?na inawezekana tatizo sio hao wanaume inawezekana ni wewe ndo maana wanakuwa hivyo unavyowaona kwako,period.

    ReplyDelete
  18. wanaume wa kitz hawawezi kuexpress feelings zao kwa WAKE zao? Waliwezaje kuwafanya wawe wake zao(kuwaoa)kama hawakuweza kuexpress feelings zao?
    Unawalinganisha na wanaume wa nchi gani ambao pia wamekua ni waume zako? Ukikubali kuolewa lazima uwe tayari kulala bila chupi...wewe unataka expression gani tena zaidi ya kuolewa? au hujui unaposema wanaume kwa wake zao unamaanisha nini mdau? Wewe umeexpress feelings zako kwake yeye Mtz akakuogopa au?

    ReplyDelete
  19. bro Michuzi mbona simwelewi huyu dada? Anabip au anapiga????????

    ReplyDelete
  20. Huyo sijui ni kaka ama dada?
    Lakini nafikiri pia wanawake wa ki-Tanzania hawahitaji expression yoyote sababu hawakawii kukuita oo huyu Bushoke,Je waujua huo wimbo unaoelezea mtu alipofanya hiyo"expression" ikamtokea puani maana dada kaamka asubuhi kaenda kwa shoga yake unasikia anajitapa oo hana bao hapa ,hageuzi na maneno mengi ya kejeli ambayo yanaonyesha mtu akikujali we unaona unamburuza.
    Je nyie wanawake wa KTZ mnafanya hivyo maana nyie ndio mnaongoza kuwa na mpenzi ya chipsi kuku tu.
    na utajuta kumfahamu aliyekumwaga nyooo!Na naona hujabahatika kukutana na wanaojua kuji-express watu mpaka wanatoa chozi nini wewe?
    Siku nyingine kabla ya kutuma ulichoandika soma kwanzanza maana wadau wameshindwa kukuelewa.
    Agaton jp

    ReplyDelete
  21. Alichotaka kusema hapo ni kwamba.
    Watanzania wake kwa waume (wengi)huwa hawonyeshi feelings zao kiwazi.

    Ukweli ni kwamba watanzania kwa ujumla ni wasiri sana na wengi wana aibu sana, also very conservative.

    Kwahiyo dada/kaka uliye uliza hilo swali, kama wewe ni mtanzania then u will just know how to go about it we(tanzanians)know...our instincts talk more than words somehow we get along....am I right folks?
    Grandma

    ReplyDelete
  22. Wabongo tuna tabia moja mbaya ya kukurupuka. Huyu mdau aliuliza swali la kizushi hajasema kuwa yeye ni mwanamume au mwanamke. Sasa wengine mnapotoa hoja kwa kumshambulia kama mwanamke, mnakosea. Ni kukurupuka. Jadili swali (toa hoja) bila kumshambulia muuliza swali. Leo ni swali la kizushi, kesho tutapata lisilo la kizushi na mwenendo wetu utakuwa huo huo. Ndugu zanguni tujenge tabia ya nguvu ya hoja badala ya hoja ya nguvu!

    ReplyDelete
  23. Najua Mtoto mrembo ulimwacha mumeo ukijua hakupendi, sasa umegundua anakupenda unajuuta kumwacha baaday akugundua anakupenda na unamlauumu kwa kuto-express feeling zake mapema.
    be careful utajuuuuta kumfahamu mwanamme mwingine baada ya kumwacha mmeo rudi tu kwake kwani umegundua anakupenda.

    ReplyDelete
  24. Pole dada kwa yaliyokupata mpaka ukawa a maswali kama hayo uliyouliza hapa. Mara nyingi mila na desturi zetu watanzaia pia hapa zinachangia kidogo, yaani desturi zetu hayo mambo ya kujieleza au kuwa waziii hasa kwa wanawake yalikuwa hayapo na kwa wanaume pia wao ni kufanya vitu vyao kimywakimya huku akiangalia unapokeaje, kwa bahati mbaya nawe ukiwa hujielezi yeye anapata picha kuwa unaridhika na yanayoendelea pale, sasa kama ulivyosema unapomuacha ndio anaanza kubebeleza, hapo huwa anakuwa anashtuka amaa kumbe mbona bado namuhitaji? nawe pale unakuwa ndo umemuelewesha kwa kuwa wazi kisawasawa nae anabembeleza kisawasawa, sasa wewe ungempa tu nafasi nyingine ili uone kama somo limeeleweka au vipi,ingawa sielewi vizuri unamaana gani hapa, bali kwa kukisia tu nadhani bado hujakutana na wanaume wachangamfu wajuzi na watundu kwenye mapenzi. Kwa ushauri tu kwanza nawe ueleweke pale unapoona kuna urafiki wa karibu unaanza, nawe ujiongeze, chokoza mada kwa gia za maswali au kujieleza, utani,kuwa wazi wewe kwanza na kwa kutumia busara, pia mgomo baridi kidogo unapendeza, ukizidisha shaurilo utakuta shilingi hiyoooo inadumbukia chooni mwan-dada, kumbuka love is allways to give then take, Pia kumbuka unyumba ni mapatano bibi wewe na mumeo kubembelezana. Dada kama ulikosea mwanzo rekebisha tu hujachelewa utafurahia maisha kama baadhi ya wanawake wenzio wanavyofurahi, Niishie hapa bi dada niwaachie na wengine wenye ushauri wa kukusaidia wakupatie ila uvumilie kidogo maana kila mtu ana ufundishaji wake hapa, wewe utachagua litakalokujenga.

    ReplyDelete
  25. Mfano mimi ni mumeo, nakutwanga mangumi na naku-treat vibaya kila kukicha au sikuonyeshi kabisa mapenzi lakini kila siku na-express what u called FEELINGS eti "Oh mamsapu I love u, nakuona kwenye glasi nikinywa maji, nakuona kwenye tonge nikila ugali" we itakusaidia nini na itasaidia nini mapenzi yetu. Mapenzi ni kuonyeshana mahaba sio kupeana kauli zisizotoka deep in your hear! kama umeachwa pole da Kiboga! utajuuuuuta kuingilia mapenzi!!

    ReplyDelete
  26. pole

    sasa sikia usipende kuamini zile movies zinazoonyeshwa na wazungu,wafilipino,au hollywood movies etc,,,mapenzi yale ni uongo ndo maana zaitwa muviz,,,
    penzi ni lako na mwandani wako full stop,,,hakuna cha kitchen party,jando wala shangazi ni wawili tuu ndo mtaendeleza penzi

    kwani adi mumeoana ilikuaje?sii mmeonyeshana FEELINGS tayari?au me ndo sielewi??

    kaaazi kweli ili swali

    ReplyDelete
  27. Mh, mbona kiila mtu anatetea jinsia yake mara ooh wanaume hivi mara ooh wanawake hivi.. hatujibu swali kama mdau mmoja alivyosema hapo juu.

    Kwa kuchangia hoja, mi naona ni malezi yetu ndio yanayotufanya tuwe hivi. Pia wanawake katika mahusiano wanapenda waume wao waweze kujali details ndogo ndogo kitu ambacho wanaume hawaoni na si kosa lao. Hata wanaume wengine wakiwemo wazungu hawajaweza kumwelewa mwanamke ktk mapenzi mpaka leo hii. Mwingine ukimwambia unampenda kosa, ila ukimnunulia gari.. aah unampenda kuliko. Ni marefu kwa kweli mi yananichanganyaga

    ReplyDelete
  28. Si suala la wanaume peke yao, bali ni suala lililojengeka kutokana na mila na tamaduni wa watanzania walio wengi bila kujali kwamba ni wanaume au wanawake. Watanzania walio wengi hawana utamaduni wa kuelezea hisia zao waziwazi(SIO KOSA) bali hisia zetu ziko kimatendo zaidi kuliko maneno. Ndiomaana mara nyingi hata akina dada wengi wanapotokea kuwapenda wapenzi wao lakini wanaumia moyoni bila kuwaambia kilicho moyoni mwao. Pia ieleweke kwamba sio kosa. Watanzania tunaonyesha sana hisia zetu za mapenzi (KIMATENDO) ni utamaduni huu ndugu yangu.
    Mdau wa Mila

    ReplyDelete
  29. huyu anaonekana ni dada na kishaachwa, ndio maana ana jazba ivi, ni kweli w'ume hawaaminiki, kwasababu mapenzi yao yapo apo ilipokutana miguu kwa mbele kidogo, na w'ake mapenzi yao yapo moyoni, na ndo mana ukimuacha we unaumia na y hajali

    ReplyDelete
  30. Wadau waliohoji suala la wanaume wa Kitanzania kuonyesha mapenzi kwa waume zao wametoa conclusion japo haijasemwa. Kuna maswali ya kizushi hayastahili kujibiwa. Hili ni mojawapo.

    ReplyDelete
  31. HAYA MNAANZA KUNIBOA TENA, KWANI CHA AJABU KITU GANI ALICHOANDIKA HUYO MDAU HAPO, MNAJIFANYA BONGO HAKUNA GAYS, MBONA SASA HIVI HICHO SIO KITU CHA KUSHANGAA JAMANI, OOH ETI KAKOSEA, KAKOSEA KITU GANI, ANAMAANISHA WANAUME WENYE WANAWAKE, NA WANAUME WANAOTEMBEA NA WANAUME WENZAO PERIO, SASA MNASHANGAA KITU GANI, JIBUNI SWALI KAMA MNA MAJIBU, KAMA HAMNA JIBU KAENI KIMYA!

    ReplyDelete
  32. NIMEGUNDUA KUWA WENGI WENU MLIOCHANGIA HAPA NI WANAUME, TENA WENYE UPEO WA KISHAMBA SANA, KWANI WENGI MMEMTUKANA HUYO MUULIZA SWALI NA KUMKEJELI BILA KUJUA KUWA ANATAKA MSAADA WENU NA SIO MATUSI YENU, UNAJUA NDIO MAANA KAAULIZA SWALI HILI KWASABABU WENGI MLIOCHANGIA(HASA WANAUME)NDIO NYIE ANAOWAZUNGUMZIA KWENYE SWALI LAKE. WANAUME WENGI WA KITANZANIA BADO WANA MTAZAMO WA KICONSERVATIVE KWENYE MAPENZI, WANADHANI KILA MWANAMKE NI CHANGU, AU GOLD DIGGER WANASAHAU KWAMBA WAPO WANAWAKE WENGI WAZURI TU WALIOLELEWA VIZURI WENYE MAADILI, ELIMU NA KUJITUMA, HII INAWAPONZAGA SANA, KAMA HUYO MJINGA HAPO JUU ALIYECOMMENT ETI WANAWAKE WENGI MNA MAPENZI YA CHIPS KUKU, HIVI HAO WANAWAKE MNAWATOAGA WAPI JAMANI? HAMJUI KUTONGOZA, NA KAMA MTATONGOZA MKABAHATIKA KUOA MNAANZA KUJISAHAU SANA KWENYE NDOA ZENU NA KUACHA KUEXPRESS MAPENZI KWA WAKE ZENU KWA SABABU YA MTAZAMO KUWA KILA MWANAMKE ANAPENDA PESA TU, UNAJUA HATA KUMSHIKA MKEO MKONO WAKATI MNATEMBEA NI EXPRESSION YA MAPENZI, AU KUMSAIDIA KUPIGA PASI, NI VITU VIDOGO VIDOGO KAMA HIVYO, WHETHER HUYO MUULIZA SWALI NI MWANAUME AU MWANAMKE ISSUE NI KWAMBA MNAOGOPA KUJIEXPRESS FEELINGS ZENU, KUBALINI HIVYO MSAIDIWE!

    ReplyDelete
  33. umeachwa kwa vijibwa, umebwagwa kwa vijibwa,
    amerudi tena kwangu, nakualika rusha roho,

    ReplyDelete
  34. aliyekwambia hawaelezi feeling zao nani? nenda Musoma, kaolewe na mkurya. utapigwa mpaka uote manundu, hiyo ndo jinsi ya kuexpress feeling.

    halafu hiyo research umefanya wapi, au waliokuaproach unawana generalize.

    hivi karne hii bado watu wanatoa assumption kama research? hivi feeling zako unaweza kizifanya za watu wote? sijui wewe ni kaka au dada; lakini ukiwa na hasira usiandike. pata muda wa kutulia ndo ujue nini cha kusema mbele za watu.

    anyway msamehe huyo ni mkurya na una bahati angekuwasha kibao kama jinsi ya kuonyesha upendo.

    ReplyDelete
  35. jamani sijaelewa huyu jamaa anamaanisha nini anaposema kuexpress feeling. nadhani ni neno pana sana. ni pana sana hata halijadiliki.

    ReplyDelete
  36. wadau mi kwa uelewa wangu nadhani mdau mwenzetu anazungumzia romance, jinsi wenzetu mataifa ya magharibi wanavyoonyesha kisses waziwazi mfano naweza mkiss mume wangu mbele ya wazazi wangu na no aibu,kumsifia wife au mume mbele ya wazazi wa pande zote 2, kupeana roses etc, ndo hoja yake kama sikosei. kama ndivyo basi naweza sema ni swala la tamaduni tofauti hapa. mfano wenzetu wa magharibi akimpenda mtu anasema na kama hampendi anamwambia waziwazi, lkn tofauti ipo kwetu sana mfano mmoja wa wana ndoa anacheat na utakuta baadhi ya ndg na marafiki wanaelewa lkn wanatoa support kwa asilimia kubwa kuhusu uzinzi.

    ReplyDelete
  37. hahahhahahaaaa uwiiiii mbavu zangu

    sawasawa annons!!!kuna watu umu wana vichwa vibovu,hizi stress jamani?????
    sasa wewe utafananishaje romance za wazungu,waarabu,wachina,wabrazil na AFRIKA tena Tz na S.Afrika??

    aya tuendeleze libeneke

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...