Mmarekani anayeishi Denmark, Bobby Ricketts ambaye ni mtaalamu wa saksafoni na muziki wa Soul, Funk na Jazz, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana baada ya kutoa mafunzo ya jinsi ya kupiga vyombo vya muziki na kuimba kwa wasanii wa kikundi cha Tanzania House of Talent (THT). Mafunzo hayo ya Bobby Ricketts yanafanyika kwa wiki moja.
Mmarekani anayeishi Denmark, Bobby Ricketts ambaye ni mtaalamu wa saksafoni na muziki wa Soul, Funk na Jazz, akiwatazama wasanii wa kikundi cha Tanzania House of Talent (THT) walipotumbuiza, Dar es Salaam jana baada ya kutoa mafunzo ya jinsi ya kupiga vyombo vya muziki na kuimba kwa wasanii hao. Mafunzo hayo ya Bobby Ricketts yanafanyika kwa wiki moja.

Baadhi ya wasanii wa kikundi cha Tanzania House of Talent (THT) wakifanya mazoezi Dar es Salaam jana baada ya kupewa mafunzo ya jinsi ya kupiga vyombo vya muziki na kuimba, na Mmarekani anayeishi Denmark, Bobby Ricketts ambaye ni mtaalamu wa saksafoni na muziki wa Soul, Funk na Jazz. Mafunzo hayo ya Bobby Ricketts yanafanyika kwa wiki moja.

Bobby Ricketts awapiga msasa THT
MSANII mahiri kutoka Marekani, Bobby Ricketts yuko nchini kuwapa mafunzo ya jinsi ya kutumia vyombo vya muziki na kuimba, wasanii wa kikundi cha Tanzania House of Talent (THT).
Bobby Ricketts anayeishi Denmark, ambaye ni mtaalamu wa saksafoni katika muziki wa Soul, Funk na Jazz, alianza kutoa semina ya wiki moja kwa wasanii hao, kwa lengo la kuwasaidia kufikia malengo yao ya kuwa wasanii mahiri duniani.
"Lengo langu ni kuhakikisha wasanii wa THT wanatimiza ndoto yao, kwani wana vipaji ambavyo havina budi kuendelezwa katika muziki, kucheza dansi na maigizo," alisema Ricketts.
Rebecca Young, Meneja wa THT pia alisema: "Tunaona fahari kwa Ricketts kujitolea kuendesha semina kwa wasanii wetu ili waweze kukomaa zaidi katika fani."
THT imedhihirisha sanaa ni njia bora ya kufikisha ujumbe kwa jamii, na kikundi hicho kimedhihirisha kina uwezo wa kutumia njia hiyo kufikisha ujumbe kuhusu mada mbalimbali kwa njia ya sanaa jukwaani, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya UKIMWI.
THT wanatoa elimu hiyo kwa njia ya sanaa ikiwa ni pamoja na ujumbe kupitia muziki, dansi na ngoma, na kimekuwa kikidhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain.
Kikundi cha THT kilianzishwa mwaka 2005 na kinaundwa na vijana wapatao 45 wenye umri kati ya miaka 14 na 24. Kundi hilo la vijana limekuwa likitoa burudani maridhawa katika matukio mbalimbali nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. mmarekani anayeishi denmark, mmarekani anayeishi denmark, mmarekani anayeishi denmark ...

    ReplyDelete
  2. Jamani kwani big deal mtu kuwa mmarekani? Hadithi nzima ni mmarekani anayeishi Denmark, mmarekani anayeishi Denmark...kwani wangesema tu "Msaanii mahahariri kutoka Denmark isingekua habari nzuri? Au umaarufu wake ungepungua

    ReplyDelete
  3. Huyu jamaa mtaalamu au anataka kuja kujenga Resume tu? Ohh nimewahi kufundisha Bongo blah blah

    ReplyDelete
  4. si unajua tena nyumbani kasumba, ukitoka nje ya mipaka unaakili hata kama ni mmarekani anayesafisha vinanda na gitaa dernmark. Halafu hawa wadogo zangu mbona wamejikakamua kiasi hicho wasijewakashindwa kupumua.

    ReplyDelete
  5. LAZIMA UITAJE MAREKANI WEWE.

    ReplyDelete
  6. Jamani eeh, kunradhi,

    Mi huyo Jamaa wa kimarekani NIMEM-MAINDI alivyoalivyo, hiyo misuli yake ya mkononi!

    Inaelekea akiku... duh, basi tu sina jinsi.

    Salam zake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...