Heshima yako mkuu wa nanii, tunashukuru sana kaka kwa kutupa uhuru wakutuma maoni yetu kwenye blog ya jamii, na kweli imekuwa blog ya jamii kutokana na kuweka mambo yanayotokea katika jamii.
tatizo langu lipokwa kituo kimoja cha luninga cha hapa nchini, hicho kituo kilikuwa nasifa ya kutuonyesha mpira na kilikuwa kituo namba moja nchini, tokeamiaka hile na wewe mkuu ulikuwa mmoja wa watangazaji kwenye kituohicho..
nakumbuka kwenye mashindano ya uero 96 yaliyofanyika uingerezawewe ulikuwa mmoja wa watangaziji na wewe kama sikosei ndio uliyemletamchambuzi wa mpira Dr Licky Abdallah.
watu waliipenda sana na hasasiku za mpira lakini sasa hivi wamekuwa hovyo hasa baada ya kufunguachannel nyingine sasa hivi wanadai wanaonyesha mpira bila zengwelakini wanazengwe kupita maelezo wanachelewa kutuonyesha mpira.
pili wanatuonyesha mechi za team za uingereza tu, najua uingereza ndio ligiyenye wapenzi wengi nchini lakini wangetuonyesha mechi nzuri ya sikuhiyo. nilikuwa naomba kama wameshindwa kutuonyesha mpira live bila zengwe basi watuambie. wanatuboa kweli.
Mdau Omary

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Kaka tatizo lao kubwa channel 10 ni kuwa wanatudanganya watu wazima wameweka vipindi vya dini ndio priority kwao. Mtu unasubilia mpira tangu 9.45pm wanaanza kurusha almost half time wanasahau siku hizi kila mtu anweza kupata live results na akajua wanatuongopea. Kuweni wastaarabu.

    ReplyDelete
  2. vumbi nitamu sana hasa ukichanganya na dawa ya mbu mambo mswano au hamuoni watu bongo walivyonenepa??

    labda mseme mafuriko hayo ndiyo nayaheshimu lakini ujanja ni kujenga vilimani tu kama waruguru,wasambaa,wachaga wa mitaa furani,hapo utakuwa umeyakomesha mafuriko

    ReplyDelete
  3. DUNIANI KUNA MAMBO SAWASAWA NA BAHARI KUNA PAPA NA NYANGUMI TENA WALE WA HATARI----------------------------------------------------------------------------------EMVI MAPENZI MELI YA WAPENDANAO NAHODHA MIMI NA MICHUZI--------------------------------------------HAMTUWEZI

    ReplyDelete
  4. michuzi na wadaau sio mahakimu kesi hii ipeleke kisutu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Mdau ukiyepost hii mada, napenda kukufahamisha kuwa popote pale duniani ukitaka kitu kizuri ni lazima ukigharamie, kinyume cha hapo endelea kuangalia vipindi ambavyo waendesha TV wanakupangia.

    Ukitaka kuangalia mechi live nk, itabidi uingie katika mpango wa kulipia kupitia DSTV-MuultiChoice.

    Nadhani kwa maelezo haya machache nimekusaidia sasa unaweza kufanya research kutoka upande wako

    ReplyDelete
  6. SASA UNASHITAKI AU VIPI?KAMA UNA SHIDA PUNGUZA JAZBA KUWA MPOLE,SIO KUPAYUKA TU,KAMA UNAONA UNAKUZINGUA NENDA KANUNUE CARD KISHA UCHAGUE MECHI UNAYOTAKA.

    TUWEKEE MAMBO YA MAN YUUUUUUUU MICHUZI

    MAN YUUUUUUUU OYEEEEEEEE

    ReplyDelete
  7. mkuu unachanganya halali na haram tuzo pointi poa ndovu laaa

    ReplyDelete
  8. Kwani wamekulazimisha kuangalia? wewe unataka vya bure hii TV ni ya baba yako? hicho kipindi wanakuonyesha free bado unalalamika, nenda kalipie uone kama watakuzingua, hivyo vituo vya TV vinaendesha kwa fedha na sio maji or air

    ReplyDelete
  9. Mechi za bure online.Justin.tv/bigitivo.Unaweza ku-search kwa kutumia timu zinazocheza siku hiyo katika search window juu kulia.
    BTW-Tumewapiga ubaya Villareal.Jumamosi zamu ya Chelsea kupata dozi halafu Liverpool, then Man U ktk (ligi,FA cup,Champ league) mwaka huu tunatesa tunatesa. Eli kilema tunatesa.Awilo longomba tunatesa,Jojo wear tunatesa.

    ReplyDelete
  10. Yaani watu wanajua kuchemsha kweli sasa unalaumu nini humu, na je Michuzi atasaidia nini? wewe unaangalia mpira bure kisha unataka uwapangie waonyeshe nini. Je ujuhi wao wapo kibiashara pia na wanajali faida ili waweze kukurushia angalau huo mpira unaouona nusu.

    Fuata ushauri wa wadau kama uridhiki na uonyeshaji wao nenda kanunue card za DSTV

    ReplyDelete
  11. TATIZO LAKO MDAU UNAPENDA BUREEEEE
    CHANNEL 10 NAO WANANUNUA HAKI YA KURUSHA MICHEZO HIVYO INABIDI WAWEKE MATANGAZO KIBAO ILI KUPATA FAIDA.

    BINAFSI NAWAPA PONGEZI NYINGI WAMETUSAIDIA KUONA UEF BILA ZENGWE. NA KWA SASA NAJIDAI NA DISH

    SASA WEWE NA UBAHIRI WAKO UTAKOMA KURINGA
    CHANEL 10 HOYEEEEEEEEEEEE!
    MARARAMIKO YAKO HAYANA MASHIKO.

    ReplyDelete
  12. BURE GHALI! Huu msemo una maana kubwa sana kwa mwenye kutafakari. Ukitaka kuepuka kero yote hiyo mzee jiunge na DSTV sio kama utaona gemu moja, we wabofya tu na kuchagua uangalie ipi; Serie A, La Liga, Portuguese and Brazil Leagues, Premier league ndio kabisa unaweza kuangalia hata game 4 kwa wakati mmoja kama TV yako ina PnP na still there's SO MUCH MORE to choose; music, movies, documentaries etc!!. Raha yote hiyo kwa $74 tu kwa mwezi! ni nyingi kwa usiye nazo au usiyejua starehe ya TV na soka!

    ReplyDelete
  13. Suala hapa sio kutaka vya bure-tatizo ni kuwa kwa nini wajifagilie na wadanganye umma ambao hawajui ukweli kuwa mechi ni live wakati ni marudio.Huko ni kujidhalilisha wao wenyewe.Kama hawawezi waache watu watafute mbinu nyingine ila sio kudanganya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...