Askofu Mkuu Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es salaam Muadhama Polycarp Pengo akiongoza akinyunyizia matawi katika ibada ya Jumapili ya Matawi jana kanisa la Mtakatifu Joseph Dar. Wakristo wamekuwa katika mfungo wa siku 40 ambapo hii ndiyo wiki ya mwisho ambapo itafuatia Ijumaa kuu (Siku ambayo Yesu anasulubiwa) na Jumapili ya Pasaka (Siku Yesu anafufuka) na sikukuu itafikia kilele siku ya Jumatatu ya Paska.

Globu ya Jamii inawatakia wadau wote Wiki Takatifu njema


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Du! Brother michuzi umenifurahisha kweli leo. Yaani Ijumaa kuu Nabii Issa anasulubiwa, na Jumapili ya Pasaka Yesu anafufuka. Sasa hao ni watu wawili tofauti ama la. Naamini huo ni ubunifu wako wa kutaka kumuunga mkono Alhaji Ali Hassan Mwinyi kwa hotuba yake aliyotoa siku ya Maulid (ambapo jamaa alimpinga kwa kumpiga kofi)kuwa Wakristu na Waislam wa Tanzania tushirikiane kwa kila jambo. Tofauti za kidini hazita lijenga bali kulibomoa taifa letu.
    Nakutakia Heri ya Juma Kuu wewe na wadau wako wote

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi naikumbuka sana ile picha aliyopiga mwandishi mmoja wa gazeti la Majira anaitwa Abdul Njaidi ilitoka kwenye gazeti la majira la tarehe 14 July 1999.Hakika kuna miujiza jamani pale st.Joseph yaliyotokea kwenye picha ile hata yeye alibaki mdomo wazi, picha aliyoipiga yeye mwenyewe alishangaa object nyingine iliyokua kulia kwake mbali kabisa ikitokea pia kwenye hiyo picha.
    Prepare urself for the Easter those who believe

    ReplyDelete
  3. Wadau samahani mimi nina swali hua najiuliza siku nyingi. Hivi jina haswa la huyu Bwana pengo ni lipi? Yaani namaanisha majina, bila cheo. Na ninaomba ufafanuzi kuhusu mpangilio wake, maana nashindwa kuelewa kabisa! Asanteni sana!

    ReplyDelete
  4. Nabii yusuf radhi za mwenzi mungu zimshukie juu yake Amin

    ReplyDelete
  5. Kaka michuzi hebu tuweke sawa wadau
    katika sentensi yako hii(Ijumaa siku ambayo nabii Issa anasulubiwa na Jumapili ya pasaka siku Yesu anafufuka).kuna walakini katika sentesi yako hapa hunajaribu kuonyesha kwanba tukio la ijumaa na la jumapili ni vitu viwili tofauti. tafadhali fafanua, kuna mengi yamejificha katika hili.

    ReplyDelete
  6. anaitwa mwadhama polycap cardinal pengo
    mwadhama ni cheo
    cadinal ni cheo
    majina yake ni polycap pengo

    ReplyDelete
  7. Michuzi yaani we machale kweli umeshabadilisha? mbona umefuta nabii issa au unaogopa kupigwa kibao kama Mheshimiwa?

    Mdau
    Kijitonyama

    ReplyDelete
  8. Michuzi hata usipo post hii hamna neno mi nakufagilia kwa ku edit kwamba aliyesulubiwa na aliyefufuka ni mtu huyo huyo mmoja, ilikuwa inakonfyuzi..

    Koku

    ReplyDelete
  9. ..Mitchu,ulikuwa ukijifagilia?..mwanangu ungezaliwa katika 'jografia nyingine' kama latin amerika ungekwitwa 'Jesus'..

    ReplyDelete
  10. MICHUZI NA WEWE PIA PASAKA NJEMA!
    ASANTE SANA MICHUZI KWA KUWA MTU WA WATU NA KUWAPENDA WATANZANIA WOTE BILA KUBAGUA.ASANTE NA TENA PASAKA NJEMA.

    ReplyDelete
  11. KILELE CHA PASAKA NI JUMAPILI.
    MICHIZI BWANA!!
    I DO NOT GET THE JOKE HERE, MARA ISSA MARA JUMATATU.
    IKIZINGATIWA WEWE SI MKRISTU, NA HII MADA NI NGUMU KATIKA MCHANGAYIKO WA MADHEHEBU, MI NAONA UNATAFUTIA WATU SABABU YA KUSEMA.

    ReplyDelete
  12. Mdau wa April 06, 2009 3:10 PM nashukuru kwa kunijulisha. Sasa kama ni hivyo, kwa nini wanachanganya majina na vyeo? nina maana, kwa nini wanapangilia cheo+jina+cheo+jina? Kwa nini isiwe vyeo + majina? Kwa mfano huwezi kusema "Mheshimiwa Jakaya Mwenyekiti Kikwete", itakua haileti maana. Au kuna sababu maalum!
    Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  13. Mheshimiwa aliyeshika mic ni classmate wetu tulipokuwa pale Visiga Seminary sasa ni Rev Fr Vincent Mpwaji ambaye ni Katibu wa Cardinal na Jimbo kuu la Dar es salaam. Keep it up mzee ,joe

    ReplyDelete
  14. Madu Cardiff kumbe na wewe unasumbuliwa na lugha kama mimi?

    ReplyDelete
  15. Mkuu wa wilaya ya naniii, mimi ni mkristo lakini ukweli ni kuwa hizi sikuu ni sanaa tu za binadamu ukisoma biblia yote hakuna sehemu inasema jumapili ya pasaka. Pasaka yenyewe ilikuwa alhamis alipokula mkate na divai na kisha Yuda kumsaliti hiyo ndio ilikuwa pasaka lakini hii ya jumapili haimo kwenye biblia. huo ndio ukweli mkuu wa wilaya, usiibanie michuzi hii ni blog ya jamii mwenye hoja ya kusema hii pasaka ya jumapili iko kwenye biblia aweke

    ReplyDelete
  16. Mdau unayeulizia cheo cha Kardinali, ni kwamba hicho ni cheo cha juu kabisa (chini ya Papa, ambaye ni kiongozi wa Makardinali wengine na Kanisa kwa ujumla). Pana anachaguliwa na Ma-kardinali miongoni mwao (Conclave). Kwa hiyo, unlike vyeo vingine ambavyo ukivipata unaweza kuviacha au kupanda juu zaidi (kama rais, m-kiti, waziri,Rev, n.k), u-Kardinali ni cheo cha kudumu na hicho huwa kinakuwa sehemu ya jina lako (kama Middle name hata kwenye passport).Hata wakistaafu (au kujiuzuru sababu ya umri mkubwa) bado wanabaki na hicho cheo hadi Mungu akiamua kuwachukua. Ndio maana anaitwa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (or H.E. Polycarp Cardinal Pengo).

    ReplyDelete
  17. Kujibu swali:

    Jina lake ni Polycarp Pengo. Hayo ya Mhadhama na Kadinali ni vyeo tu. Na mpangilio unaotumika ni desturi tu. Kwa mfano Baba Mt wa Sasa (Benedict wa 16) jina lake halisi ni Joseph Retzinger. Hivyo kabla ya kuwa Papa aliitwa Mhadhama Joseph Kadino Retzinger. au marehemu Kadinol Rugambwa, jina lake ni Laurian Rugambwa na aliitwa Mhadhama Laurian Kadino Rugambwa.

    Nyongeza: Pengo kwa asili ni mtu wa Mwazye- Sumbawanga - Rukwa, , amezaliwa, kukua na kusomea huko. Ni matunda ya Kaengesa seminari.Ni padri wa shirika la Mapadri weupe(Missionaries of africa aka White fathers) amewahi pia kuwa askofu wa iliyokuwa diocese ya Nachingwea

    Nawakilisha

    ReplyDelete
  18. Kujibu swali:

    Jina lake ni Polycarp Pengo. Hayo ya Mhadhama na Kadinali ni vyeo tu. Na mpangilio unaotumika ni desturi tu. Kwa mfano Baba Mt wa Sasa (Benedict wa 16) jina lake halisi ni Joseph Retzinger. Hivyo kabla ya kuwa Papa aliitwa Mhadhama Joseph Kadino Retzinger. au marehemu Kadinol Rugambwa, jina lake ni Laurian Rugambwa na aliitwa Mhadhama Laurian Kadino Rugambwa.

    Nyongeza: Pengo kwa asili ni mtu wa Mwazye- Sumbawanga - Rukwa, , amezaliwa, kukua na kusomea huko. Ni matunda ya Kaengesa seminari.Ni padri wa shirika la Mapadri weupe(Missionaries of africa aka White fathers) amewahi pia kuwa askofu wa iliyokuwa diocese ya Nachingwea

    Nawakilisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...