kikosi cha Yanga
Kikosi cha Simba

Ni kwamba ile mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa jumapili April 26 ikiwa ni moja ya sherehe za muungano, homa imezidi kupanda miongoni ya wachezaji na washabiki wakitambiana kila mmoja akivutia kwake.

Hii imekuja baada ya mechi ya Simba na Yanga  nyumbani Tanzania kutoka droo ya  2-2, na  kila timu hapa imesema  imetumwa kumalizia kazi iliyokuwa imebakizwa na Simba/Yanga Tanzania.
 
kambi za timu zote ni shwari isipokua Yanga golikipa Dedy Luba ameumia mkono baada ya kungongana na Kheri Kheri kwenye mazoezi. Kocha wa Yanga Meya ameingiwa na wasiwasi wa kumkosa kipa huyo. Kwa upande wa wachezaji wengine amesema wapo fiti na wanaendelea vizuri na mazoezi na atatangaza kikosi ijumaa
 
Kambi ya Simba inaendelea vizuri chini ya kocha mchezaji Libe, na wamemrudisha kipa Hiraly aliyekuwa ameihama timu kwa kisingizio cha kua benchi muda mrefu na habari ndani ya kambi hiyo zina sema huenda wakamrudisha Londa ambaye kwa sasa yupo Tanzania kwa Shughuli za kifamilia. Lakini Mkakile(Bamchawi) alipoulizwa alikataa kuthibitisha habari hizi kwa kusema haya ni mambo ya ndani ya uongozi wa Simba.

Wakati huo huo Yule mchezaji wa kiungo wa Simba ambae kwa sasa yupo Atlanta Elvis Dotto Mnyamuru atakuja maalum kwa mechi hio jumapili.
 
kocha mchezaji wa Simba alipoulizwa kikosi gani kitashuka dimbani,alisema sasa hivi ni mapema kutangaza kikosi kwani wacheaji wote wapo kwenye ari na mazoezi yamepamba moto na kuongezea kusema  'lazima tuigalegaze Yanga mwaka huu...'
 
Mgeni wa heshima kwenye mechi hii atakua msaidizi balozi mh Switebert Mkama.

 Mechi itachezewa kwenye wanja letu la Taifa la zamani (Meadowbrook park),saa kumi na moja jioni(5:00pm) pia Nyama choma itakuwepo. hivyo washabiki manaombwa kuja kwa wingi na kuwa watulivu kwani inategemewa kuwa  mechi itakuwa nzuri na burudani tosha kuadhimisha Muungano day

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mzee mwenyewe Abul Daudi Munisi aka "kandoya" simba damu tangu miaka ya 80...Nakuna ndani ya uzi wa Msimbazi, fanya mambo jumapali, nitakua hapo. Unikumbusha Mbali(Mwereni)
    Classmate
    G.Msangi aka samora

    ReplyDelete
  2. michuzi wee fala kwa kubania comment yangu! lakini message delivered any way!

    ReplyDelete
  3. wabongo bwana,,, kikweli kuishi ni kuishi tu, kama mpo USA kuleni maisha na muenjoy good time kama tunavyowapata kwenye michuz blog
    big up guys

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...