Mkuuwa Majeshi na maafisa waandamizi wake wakipozi na viongozi wa African Life Assurance baada ya kkupokea ubani kwa ajili ya wanajeshi waliopoteza maisha katika ajali ya mabomu mbagala
Kampuni ya African Life Assurance (T) Ltd imetoa msaada wa Tshs 6,000,000 (milioni sita) kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davies Mwamunyange ikiwa ni rambirambi zao kwa Familia Sita za Wanajeshi Waliopoteza maisha katika ajali ya milipuko ya Mabomu Mbagala DSM. Pichani Mkuu wa Idara ya Wateja Taasisi na Mahusiano wa kampuni hiyo, Julius Magabe, akimkabidhi hundi hiyo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davies Mwamunyange.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2009

    Heheee jamani victor fungo alishakuwa mkubwa namna hiy jeshini!!hongera zako fungo

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2009

    Michuzi,
    naomba kuuliza kwanini makao makuu ya JWTZ yamefanana sana na shule ya sekondari Tambaza?? labda wadau wa blog yako wanaweza kunifafanulia suala hili.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2009

    Jamani mbona sijasikia kama kuna mkuu yeyote either serikalini au jeshini kuwajibika kwa kujiuzulu au kushtakiwa kuhusu tukio hili tukio ambalo limeleta janga kubwa kiasi hiki kwa wananchi na wanajeshi wa eneo hilo?
    Can someone be accountable or forced to be for their actions of being irrisponsible in their decisions and plans?
    Nchi zingine hakuna upuuzi kama huo; kifo cha mtu mmoja tu ni sokomoko licha ya wote hao waliokufa Tanzania and all we see are those officials visiting the victims is hospitals na kuwapa visenti vya kuwasaidia in search of media coverage?!!
    Viongozi wengine hawatapata fundisho kwa kutowajibika kwao kwani hata likitokea janga lingine lolote; litatupwa tu kapuni and life goes on....
    This is unbeliavable!!

    J.
    Toronto.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2009

    J Toronto, kuwajibika sawa, lakini tusubiri matokeo ya tume. Watu hawawezi kulipuka tu na kujiuzulu bila sababu. Majenerali wa JW wako makini, hawafanyi mambo kwa kubahatisha. Na kama ni ajali, ni ajali tu, kumlazimisha jenerali ajiuzulu ni kuitia nchi hasara kwani majenerali wetu hawatengenezwi kwa miaka kumi kama ilivyo katika nchi zingine. In Tz it takes more than 30 years to make a general.Tuvute subira tutaelezwa kilichotokea ndiyo tanze kuulizana wa kuwajibika.

    Echo November

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 13, 2009

    Echo November sikuwa na maana kuwa nataka majenerali wawajibike/wajiuzulu...nina maana yeyote yule; mmoja au kumi wa ranki tofauti jeshini wanaohusika na suala la usalama na uelewa wa hatari ya mabomu hayo kuwa katika maeneo hayo yenye raia na wakati gani yaliyochakaa yalipuliwe katika mpangilio fulani kwa kuzingatia usalama wa wote.
    Hiyo tume tunaisubiri japo inaweza kuchukua miaka na wala matokeo yake tusiyasikie vilivyo....with the system there?!... marehemu hana haki.
    Lakini ingekuwa hapa Canada hao majenerali wangejiendea likizo zenye malipo kwa muda kwani kuna kuwajibika hapa na legal system ingewalipa hao victims mamilioni ya $$$$$$.

    J.
    Toronto

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2009

    Wee Echo, wee hivi unadhani tume hiyo itamhoji generali akiwa madarakani. Ni vyema majenerari na mawaziri wenye dhamana waachie ngazi ili tume iwe huru. Tulishuhudia kule india baada ya lile shambulio, mara moja kiongozi mwenye dhamana alijiuzulu hakusubiri tume iundwe hata kidogo.
    kwani maoni ya tume yatatoka mbiguni?? Mbona majibu yanajulikana, ni swala la kiufundi tu.
    Sasa maamuzi ya kuyateketeza mabomu 75 ulitoka wapi? kwa nini utolewe baada ya kuuwa watanzania hawa maskini tena wa MBAGARA!!! Inasikitisha sana. Wala siwafagilii hawa viongozi wanaokumbatiana.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2009

    mchangiaji, mbona unasema watanzania hawa maskini tena wa mbagala? yaani ina maana maskini wengine wana nafuu kuliko maskini wa mbagala? hebu nifafanulie, mbona watu wanaoishi mbagala wanadharaulika? labda kwa kutumia nafasi hii tunaweza kuchangia mbagala ina tofauti gani na sehemu nyingine za Dar

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2009

    Jamani mi sidhani kama kuna mtu atajiuzulu hapa, Waziri mhusika ni mtoto wa mzee ruksa ambaye anaandaliwa kugombea urais Zanzibar 2010 ambayo ni mwakani tu, halafu ang'atuke kwa hili, mkuu wa majeshi ni rafiki mkubwa wa JK. Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi.

    Amin

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 14, 2009

    Wachangiaji wote hapo juu naona mnaishi katika ulimwengu wa uwajibikaji.
    Mara uko Canada, mwingine UK, mwingine US...sisi watanzania tumechoka na urembo wenu wa sanaa!! hivi mtakuwa lini...mnataka sisi waTanazania tuwe tunaiga kila kitu kwa sababu mko huko...tunasheria zetu, tutachunguza kwa utaratibu tulio uweka kisheria na kimsingi..na kama mnataka tusikilize ujinga wenu huo rudini nyumbani mkafanye kazi..wazembe tu kwa kuwa muko nje ndo mnajifanya mnajua kila kitu...ajali ya mbagala itachunguzwa kama ajali zingine bila ushabiki wenu huo.

    Walikufa niwatanzania wenzetu na ilituuma sana na tunasikitika...wewe unayefikilia kuwa tunafurahia unamatatizo, tutafanya kama utaratibu wetu ulivyo na nauhakika haki itatendeka.

    Nyie mkishafika nje ya nchi kila kitu mnajifanya kujua...kama mko shule someni mmalize mje mtumie elimu zenu hapa...siyo ushabiki na kujifanya mnajua kila kitu.

    Poleni sana mbumbumbu nyie. kaeni na mawazo yenu hayo ya kukopi na kupest..

    mfano unataka kusema kwakuwa mabomu yamelipuka kwa sababu ya joto kali waziri wa ulinzi ajiuzuru...unaakili kweli wewe...eti kwasababu umepata access ya internet.....pole malimbukeni nyie

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 14, 2009

    Serikali pia ikubuke kumsaidia Coplo Edwin aliyekuwa katika mapambano ya ujambazi Kariakoo...Jamani coplo huyu anataabika kwani risasi ipo karibu na moyo wake...Muhimbili wamekataa kumtibu ameambiwa arudi nyumbani...Serikali, Wewe mmiliki wa BUREAU uliyekuwa unaibiwa changia hata kamilioni kamoja ktk zile zilizookolewa na polisi hao basi, Watanzania wenye uwezo tunaomba mumsaidie Coplo huyu akatibiwe aokoe maisha yake...Kwani alikuwa katika moja ya kuokoa jamii kwa ujumla katika kutokomeza ujambazi..........Hakika hii tutakuwa tunakatisha tamaa mapolisi ktk kudhibiti uhalifu...Kwani atajijua akienda akilikanyaga tuu hakuna atakayemsaidia...DUH inatiisha aibu watanzania......Kutunukiwa watunukiwe wengine je hawa waliojitoa kimasomaso kama wako vitani wanafikiriwa vipi?............TAFAKARI....HAKI POLISI

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 14, 2009

    wewe unayewaita wachangiaji wenzio malimbukeni na kupinga uwajibikaji, ni wasi wasi na upeo wako wa mambo ya kisasa. Kama ni kamanda basi pole sana najua ni kwa sababu ya jinsi ulivyolelewa na sehemu kubwa ya maisha yako ni huko YA NDIYO AFANDE!! Hapa tunaongelea "issue" na sio Jeshi.
    Kama unafuatilia vizuri zoezi linaloendelea huko MBAGALA la kuteketeza mabomu, wananchi walihakikishiwa kuwa hakutakuwa na athari yoyote, wasiwe na wasiwasi, wao wakae mita 50 tu kutoka kambini... na UPUUUZI MWINGINE....
    Sasa kama wewe si mbumbubu na limbukeni utakuwa na lugha gani ya kuwaeleza hawa WAHANGA wa MBAGALA kwa adha wanayosababishiwa na watu WABABAISHAJI.
    Huku kubebana kutatumaliza watanzania. Ubabaishaji umo hata ndani ya jeshi lenyewe kuanzia wanavyoajiri na kuteua makamanda, elimu duni kwa wahusika na kadhalika na haya ndiyo matokeo yake. Tuombe mungu wasije wakatutia aibu huko DARFUR. Naomba tuwe watulivu tupo ktk kipindi cha mpito. Makamanda punguzeni jazba hii blog ya jamii. Hata hayo mabom yanatoka ulaya, mafunzo ya kwenda Darfur yanatoka USA, hivyo usitudharau eti tunacopy na ku-paste. Limbukeni mkubwa wee!!kaa chini.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 14, 2009

    Sasa Mbagala mnaigeuza kuwa Deal, mnazidi kutuangamiza ili mwendelee kunufaika kwa namna mnavyojua wenyewe. Msitutoe kafara. Tena mnanichefua sana suala hili mnapolichukulia kisiasa. Wewe waziri mwenye dhamana juzi tu, unaongea bila hata aibu kwa kujiamini.... sitaki kunukuu maneno yako. Leo hii tena yale yale tunaendelea kwenda makaburini.
    "SHAME ON YOU". JK kuwa mkali, chukua hatua hata kama ni jeshi, wewe ndiye Amiri jeshi mkuu, achana na ....,...
    Ipitie upya tume iliundwa, nina wasi wasi nayo kama kweli una uchungu na watu wako. Kwa kuwa ukweli unaujua, kazi kwako.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 14, 2009

    khaaaa wee annon
    yani kwa mipesa yooote iyo polisi walonayo,wanainchi nani wachange kumlipia jamaa aliyekuwa kazini??si sehemu na jukumu lake mwajiri kumfidia mfanyakazi wake??

    kwanza polisi wenyewe ndo "zombe's"

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 14, 2009

    jamani hivi mmeiangaliapicha ya kwanza mstari wa nyuma huyo afande mwenye combat badala ya kuangalia mbele kamkodolea macho mdada wa watu mh

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 15, 2009

    Huyu mdau asiyetaka viongozi wa jeshi wawajibike kwa uzembe wao nadhani ni mwanajeshi na ndiye yule yule Echo kama sikosei.

    Tafadhali usiite yaliyotokea Mbagala "ajali". Sikubaliani na nyie hata kidogo; semeni tu "TUKIO" la Mbagala kwani ni uzembe wa hali ya juu.
    Wala msimuhusishe Mwenyezi Mungu kwamba kapenda...Ni Uzembe wa Jeshi. Najua ukweli unauma lakini kumbukeni kutowajibika kwenu kumezua balaa and you have destroyed the lives of those poor ophans; widows and widowers.
    Inaelekea umezoea yes yes sir kwamba hata hujua how to discuss issues kwa ustaarabu!
    Iko siku mtawajibika tu kwani maisha yanabadilika na Watanzania wanafungua macho.

    J.
    Toronto.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 15, 2009

    viongozi hongereni kwa misaada. mungu awajalie mkamalizie majumba yenu ya kifahari na zinazobaki mzitumie kumalizia kuhamishia watoto wenu kwenye vyuo vya marekani!!! ubalozi wa marekani na wenyewe ukitoa msaada wake basi ukatumike vizuri katika kujaza stock zenu za magari ya kifahari na zitakazobaki nyingine mjazie zile account zenu nje na nyingine mzitumie kwenye kwa tiketi, kulipa hoteli na tiketi za mamiss mnapoenda kula uroda kule london, kingston na kwingineko.
    mungu wabariki viongozi wetu waoengezee nguvu za kuendelea kuwafanya watanzania maskini.
    Amen.
    Ahsanteni.
    Mdau aliyechoka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...