Balozi Amina Salum Ali


Jumuiya ya Watanzania Jimbo la Michigan wanayofuraha kumkaribisha Balozi wa Umoja wa Afrika kwa Marekani Mheshimiwa Amina Salum Ali kwa chakula cha jioni.

SIKU: Jumanne tarehe 19 Mei, 2009
Saa: 12:00 Jioni (Saa za Marekani ya Mashariki):



Kwa vile tayari ana ratiba nyingine baada ya chakula cha jioni, shughuli itaanza juu ya alama.



Mahali: Makao Makuu ya TAMI


22255 Hessel st,


Detroit MI 48219.



Balozi Amina Ali ni mwakilishi wa kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani nafasi ambayo aliteuliwa miaka miwili iliyopita na hivyo kumuweka katika kundi la Watanzania wachache walio katika uongozi wa juu wa medani za kidiplomasia za kimataifa.
Tunayofuraha kwa ugeni huu mashuhuri.
Kutokana na mahali ambapo chakula hicho kitaandaliwa wale wote ambao wangependa kushiriki nasi katika jioni hiyo wawasiliane nasi kwa maelezo zaidi au maelekezo ya jinsi ya kufika:



Mwenyekiti wa TAMI:
Mr. Ayub Mfinanga - (586) 354 -5479 au
Katibu wa TAMIMr. Ben - (248) 242 2520
Asanteni.
NB: TAMI ni chama rasmi kinachowaunganisha Watanzania waishio katika jimbo la Michigan hususan eneo mama (metropolitan area) la Detroit, na maeneo jirani na kimeandikishwa rasmi kama chama cha hiari na kujitolea kwa mujibu wa sheria ya kodi ya Marekani 501(c). Uanachama ni kwa kuomba uanachama na kulipa ada za uanachama zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. southamptonMay 18, 2009

    duh mama kazeeka sasa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2009

    Kazeeka wapi wewe!!!? Mama bado analipa kabisa... Napenda watu wazima wanaovutia kama huyu, hata kuchumbia naweza(subjective)! Be careful with subjective claims kid!

    ReplyDelete
  3. southamptonMay 19, 2009

    i know she is still awakened, but not the way she used 2b when she was as a minister of state in the foreign affairs incharge of Regional cooperation,i usd to maintain her telephone direct line fron posta na simu company, she was so beatiful,nw mhh...

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2009

    Miaka inasonga mbele. Kila saa moja inapotick ndio muda unakatika.Halafu mtu mwingine anategemea muonekano wako uwe wa mwaka 1980's mweee! Kuzeeka ni process ambayo kila mtu kwa wakati wake atapitia, na kuzeeka si dhambi na binadamu huna amri na hiyo process jamani!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2009

    Kazeeka au hajazeeka the fact remains there - she is beautiful and lovely!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2009

    go mama go tanzania...

    hureeeey Tz hureeeey mwanamke

    ndio tunaotaka tuoe

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2009

    mwanamke mazingira...

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 19, 2009

    sasa wewe mzazi wa lulu (southampton May 19, 2009 7:31 AM) hapo ndio unasema nini?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2009

    Hijab yake kasahau wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...