baraka chibiliti katuletea hii kutusalimia toka italy
Home
Unlabelled
dawa ya wanaodengua kupokea simu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Sio bongo tu hata ulaya,watu hata hufikia wakati wanajipigia simu bora kuonyesha kuwa wanasimu ya bei kubwa.Unakuta simuina ita wala haipokelewi mpaka kero.Aksante mdau{MDAU}
ReplyDeleteHII INAFURAHISHA!
ReplyDeleteMDAU,
UGHAIBUNI
sasa jamaa anapaparika nini? dawa yake achukue huyo demu na mwenzake basi. tatizo hapo sio simu SIM card kama ipo fiti tunanunuwa nyengine. Ila hao madada wape mambooooo. XXXXX.
ReplyDeleteAkome na maringo mbuzi. Mlio wenyewe mbaya halafu anapigia kelele watu. Kuna siku kwenye mkutano simu ya mtu ilianza kulia kama mbwa anabweka, pata picha huko katikati ya watu.
ReplyDeleteMhh, kama hiyo ni dawa, tutapata wenye ngeu wengi
ReplyDeleteMh, Chibiriti hiyo ni safi sana lakini usiwadanganye wabongo, ulaya ni ulaya watu hawachukui sheria mkononi kafanye hivyo Bongo hahahahah utabadishwa jina soon sio Chirbiriti tena bali Marehemu live kwenye bar
ReplyDeleteChibiliti sasa unataka kutuletea balaa na mauaji Bongo. Hayo mambo yanawezekana hukohuko Italy, huku umtumbukizie mtu simu yake kwenye glasi ya bia si unatafuta kifo....!!!!!!
ReplyDeletehicho kitu kinaonekana kimetengenezwa,sababu ukiangalia,hao wahusika wanaangaliana,kupeana ishara.
ReplyDeleteumetupaka matope hapo!!!
huyo jamaa ni rafiki yako
Mdau Napoli.
chibi hujatulia
ReplyDeleteKwa kweli hii ni CHiboko.
ReplyDeleteNisaidieni ndugu zanguni. Mimi sijawahi kuona hata video moja ktk hizi zinazo posiwa. natumia laptop aina ya HP na nipo bongo hapa hapa. Je natakiwa nifanyeje? Manaake nikibonyeza ile 'play' inaniambia buffering halafu inanipa ujumbe kuwa video is currently unavailable. please try later.
ReplyDeleteHelp!
SAFI CHIBILITI
ReplyDeleteMDAU DARWINI
Nimecheka mpaka mbavu ya mwisho ndio maana siachi kutembelea hii site, asanteni wadau kwa hii style
ReplyDeletewewe wa anony wa 10:28 hujui kuchanganua mambo nini? hao si kwamba wanaangaliana kupeana ishra. ni kwamba jamaa nia yake ni kuwakoga wale mademu, akaiweka simu mezani ili watoto waione wamzimike, sasa akawa anawaangalia kuona kama minjonjo yake inawafikia kweli au la. mimi ni mwanaume lakini niliwahi kuwa narafiki yangu ana tabia za kishamba kama hizo, akivaa kiatu kizuri akakaa kwenye kiti basi utamuona anapandisha suruali akijifanya labda anajikuna kwenye soksi huku anawaangalia nyie kuona kama kama mnakiona haswa kile kiatu bomba, vivyo akiwa na simu bomba, akiwa na pete yake kubwa ya dhahabu akaingia kiwanya chenye totoz kali kama pale regents basi ndo utamjua yeye ni nani, manake mkone wenye pete ndo unatumika kuinulia glasi na ni lazima awe akiwaface mademu wakati huo, akipigiwa simu wakati glasi iko mdomoni hapo ndo mtakoma wenyewe manake anatoa simu kwa mkona wa kulia lakini ni lazima aongelee kwa kutumia ule mkono wenye god ring kubwa na anaongea kwa sauti mademu waone ile simu kali na mkono ulioishika una pete kubwa ya dhahabu kali.
ReplyDeletewanaume wa jinsi hiyo wapo wengi bahati nzuri mademu wa kisasa wanajua mikogo yote hiyo na wanaweza kukupa shit kwa kuhama sehemu waliyokaa. kwa hiyo huyo bwana anawaangalia mademu kujiridhisha kama wanaiona simu kali. na mademu nao wajanja wamemuonyesha kuwa hawakogwi na simu. ofcourse hiyo ni action imepangwa ila lengo ni kutoa ujumbe kuwa vitu hivyo vipo sana!!! nenda dar uone wanaume malimbukeni waliopata hela ukubwani wanavyojishaua. au wabeba box wakirudi likizo uone wanavyojishaua utakuta wanapokea simu na kuanza haloo, enhee, ah unajua sikuweza kuja bado nimechoka sbabu ndo kwanza nimeingia jana usiku sana na klm unajua pale ohare airpot chi-town au chicago tulichelewa sana kuondoka halafu ndege ilipata matatizo ikabidi tutue kwa dharura jackson hazfield airport pale a-town yani atlanta tukabadilishiwa ndege ndo tukaanza safari ya kwenda schiphol airport amsterdam na penyewe tulikaa sana kabla haujaanza safari ya bongo yani hapa nilipo nimechoka kinoma. yani sintarudia tena kukata ticketi northwest airlines na likizo yangu ikiisha nikitaka kurudi states safari hii nakata BA kutoka dar halafu nikifika london nitaunganisha kwa Delta airlines hadi JFK kennedy NY si unajua mambo ya NY mzee? halafu kutoka pale ndo nitashuka chicago kabla sijaeleka nyumbani champaigne urbana ambako hata nategemea kuhama niende kushi durham north carolina!! lakini usijali mzee nitakuja kesho si bado upo sinza palepale palestina? hamna noma ntakuja pia unipeleke viwanja vya bongo nikaone kama vinafikia vile vya kwetu kule chicago." ntakuja kesho usikonde ila ntakuja mida ya joni sababu asubuhi ntakuwa bize pale bandari na wakala wangu nashughulikia kutoa gali langu hammer limeshafika si unajua bongo sina gali la kutembelea?? pia mzee mzee nitafutie mteja nikitaka kurudi home states itabidi hili hammer nilibane kimtindo si unajua tena?? haloo sikupatipati vizuri hapa nilipo kuna kelele za daladala nitakupigia baadae si unajua hii simu yangu mambo ya blackberry ikiwa inasachi mtandao wa internet huwa haitaki kelele ndo maana hata kuongea sikusikii vizuri, hizi bwana sikujua kama hazifunction vizuri huku africa inauma sana sababu nimeinunua bei mbaya sana kule texas.""
kwa hiyo bwana ujue watu wa aina hiyo wapo na wakuwa wamekusudia kuwachota totoz kalikali.
Ahsante
hao mademu 2 na hao jamaa 2 wote wako pamoja.ni msg poa lkn m2 asiyekujua ughaibuni hawezi kufanya hivyo hata kidogo.
ReplyDeletetena ukifanya hivyo ndo utakuwa umempa ulaji maana utamnunulia simu mpya na gharama za hapa na pale kibao.
hiyo imepangwa tu kiaina.alafu kwanza simu yenyewe wala haikuita kwa sana kumfanya mtu asiyekujua kuitumbukiza ktk glasi.
ANON May 15, 2009 2:10 PM
ReplyDeleteKutokana na maelezo yako tatizo halitokani na aina ya pc unayotumia,bali linaweza kuwa ni tatizo la speed/bandwidth ya mtandao wako.Jaribu kuangalia hilo.
Tried to Help,
NdafU.
Mdau wa Tarehe May 15, 2009 2:10 PM, unatakiwa kudownload Adobe flash player ili uone hizi videos, nenda hapautaipata free
ReplyDeletehttp://get.adobe.com/flashplayer/
Kila la kheri.
Asanteni sana mlionisaidia ili niweze kuziona hizi video. Kweli nimefanikiwa baada ya ku download hiyo flash player.
ReplyDeleteThanks for the help