Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein akiongoza kikao cha Kamati ya pamoja ya
Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ofisini
kwake jijini Dar leo. Kushoto kwake ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
na kulia kwake ni Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha.
Picha na mdau Hilary Bujiku wa Ofisi ya Waziri Mkuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2009

    sasa hiyo miua mezani ya nini? kipimo cha uzalendo sio bendera ya taifa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2009

    Hayo maua mezani kuna siku mtu ataweka bomu. Acheni mimie sitawi siyo kuing'oang'oa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2009

    Je viongozi wa Tanganyika wapo wapi hapo ktk kuvungumzia kero za muungano?

    Nafikiri mkutano ungeweza kuangalia vipi kero za muungano kama serikali ya Tanganyika ingekuwepo badala ya kuwakilishwa na Serikali ya muungano, hii siyo balansi nzuri katika mizania ya Muungano.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2009

    Jamani, jamani acheni kujifanya mnauchambua muungano nyinyi wakuu wa nchi, hayo mambo waachieni wanasheria kwani wao watapitia neno hadi neno. Anyway kila la heri tunasubiri ripoti yenu wewe Makamu na waziri Pinda.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2009

    Pinda amelala, wanamboa sana hao wazenj hapa anajiuliza mkuu kikao kitaisha saa ngapi? wazenj kwa ku-deka jamani kuweni wakubwa sasa miaka 40 ya muungano bado tunalialia tu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2009

    mnapoteza muda na hela za watu bure, hakuna lolote mtakaloamua kama vipi hizo hela za posho tumieni kukarabati mashule, kila mtu atondoka na lake alilokuja nalo. kama muungano soo kila mtu aende kimpango wake tuone

    ReplyDelete
  7. Na kero ya mafuta msiisahau tafadhali!!!1

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2009

    meza imejaa mauwa kama bustani hawana hata pa kuweka mafaili yao... hehe

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2009

    mdau wa May 20, 2009 1:54 AM mawazo yetu ni kama sawia hapo, ila mimi nilijiuliza hivi ni wangapi kati ya wanakamati kutoka katika serikali ya muungano ni wadanganyika na wangapi ni wazanzibari?

    pia hivi kweli hawa wote lengo lao si moja tu? wote wananufaika na mfumo uliopo sasa unadhani kuna atakaeafiki mabadiliko yeyote?

    suali hili linatakiwa lijadiliwe na kuongozwa na independent body na sio wanasiasa na viongozi wa nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...