sehemu ya hotuba ya JK alipokutana na wadau wa los angeles leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 62 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2009

    Safi Sana Kikwete, nanukuu "KAMA MMECHAGUA KUKAA NJE KAENI TU HUKU HUKU..." mwisho wa kunukuu.
    Sirudi N'GO.... Kama raisi wa nchi anasema kaeni sasa kuna atakayenishawishi nisikae Mtoni... aaa wapi.. Kila la kheri.

    MDauz

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2009

    Duh Kikwete kasema watu wanakula Huku na huku

    1.Kikwete Mpeni Kura nyengine Ila Zanzibar Karume atoke atafutwe mtu kama Kikwete. wala Seif sharrifu hafai watafute mtu mwengine awe Cuf ila sio Seif.

    Kikwete anaelewa kasema na kakiri unaweza kuwa raia sehemu unayotaka Huru FULLSTOP NUKTA.

    na ameweka ukweli hapo wamaongezi yake hafichi.

    Kikwete ananiangusha kitu kimoja nimetizama sana akijielezea kwa kiengereza anasitasita ila ni mtu mmoja anaongea ya maana na anasema ukweli kama kitu sio kizuri sio kizuri. hafichi makucha. Kikwete Inshallah utaonana nao tena usijali. Michuzi kumbe tukiona Blog kimya alafu upo nchi fulani kikwete anakuja huko eh.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2009

    Hapo mnatunyima wamatumbi tu. Wajanja wa kariakoo wate wana passport mbili.(WAINDI)

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2009

    hao wasomi ni wasomi uchwala tu. Ni wivu tu hakuna chochote. hicho ndicho kitatumaliza watanzania ndio maana hatuendelei wivu umetujaa sana. badala kufikiria point tunafikiria watakula huku na huku what a stupid point from a so called educated person.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2009

    Tusirudi bwana bondo kuna malaria saana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2009

    Mbona watu wanasimama na kupiga kelele kabla ya raisi hajamaliza kuongea..Hii ni heshima mbaya

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2009

    hakuna uraia wa nchi mbili! Nyie wabeba mabox vipi? mnataka huku na huku! chagueni moja Bongo au Ughaibu full stop.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2009

    Hao so called wasomi bado wako na kasumba zilezile za kizamani hawakuwai kufungua macho, wanachojua niCCM na Nyerere hoyeee, wavivu wa kufikiri, wamefubaa akili awawezi kwenda na wakati hata kidogo na ndo maana TZ tuko masikini wa yote

    Tunaitaji new generation ya wasomi, hawa wa Nyerere jhawana jipya wangeondoka tu na mwalimu wao

    ReplyDelete
  9. MwakipesileMay 20, 2009

    Hebu turudi nyuma kidogo. kwa sasa nani anaye komba na kutunyonya na kuibia nchi yetu ni watanzania wenyewe wenye uraia wa Tanzania. Na ninani anayewekeza Tanzania na kufungua biashara ni watu wa nje ndio wanao wekeza na kuwa na mitaji mikubwa. Sasa basi iwapo tunaita watu wa nchi nyingine waje kwa sababu wana mitaji kwa nini tusiwaruhusu watanzania wenzetu wenye uraia wa nchi nyingine waje kuwekeza nyumbani kama watanzania tu wa kawaida na kuacha faida yote nyumbani hapa, kinyume na wawekezaji wa kigeni ambao wanatorosha faida yote na kujenga kwao. Mimi nina amini kabisa mtanzania mwenye urai wa nchi mbili na amewekeza nyumbani hatahamisha faida na kuweka nje ya nchi atajenga nyumbani.Ni kweli swali la usalama wa taifa lipo na utaratibu ufanywe kuwawezesha watanzania wenye urai wa nchi nyingine watoe michango yao nyumbani. mfano wamarekani huwezi ukawa rais wa nchi hii au kuwa na cheo kikubwa sana jeshini kama hukuwa raia wa kuzaliwa. Na sisi tunaweza sema kwamba ni wale tu ambao uraia wao wa kwanza ulikuwa wa kitanzania-kuzaliwa- ndio wanaweza kupata dual citizenship vinginevyo ni NO!.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 20, 2009

    Mkweleanatabu kweli kweli yeye mwenyewe mbona ughaibuni atoki kwa maana anapapenda sasa kulikoni anatubania na anawasahau wale wahindi wa kariakooo

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 20, 2009

    Mimi mtanzania ninaye hishi hapa Los angeles na mmoja wa watu walihudhuria kikao hicho.

    Sikuridhishwa na majibu yaliyo fafanualiwa na Rais.Eti..!!tunataka huku na huku..na kuendelea kusema kama itimisho ni "wivu".

    Jamani..mimi ninabeba mabox hapa iliniweze kulipa ada yangu ya shule na mkopo wa shule.Nikimaliza shule yangu ya robotics science nafikiria kupata uzoefu kwa muda kabla sijaamua kurudi Tanzania ambako hata sijui nani ataniajiri na hiyo taaluma.Kwa hiyo mimi nimebadilisha uraia iliniweze kuajiriwa na aerospace industry.

    Nifanyaje!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 20, 2009

    Mheshimiwa Raisi Kikwete ameongelea tu jinsi raia wa nchi mbili watakavyofaidi kwa kula huku na huko, lakini je Tanzania na watanzania wangeweza pia kufaidika? hili swala hakuliongelea, nchi kama India wana kitu fulani wanaita NRI yaani non resident indian, ukiingia tu wanakupa visa fulani ambayo ipo tofauti na viza nyingine, viza hiyo inakuruhusu kukaa pale unavyotaka na kukupa haki fulani nyingi tu.

    Mtanzania mwenye uraia wa kimarekani au wa sweden je akiteremka tanzania ni fedha ngapi za kigeni huacha pale? akiamua kujenga nyumba je ni mafundi wangapi wanajipatia ajira?

    Serikali ya Tanzania still has a lot of improving potentials, watanzania walio nje wanaweza kutumika vizuri sana kuisaidia nchi, the government shouldnt give them a cold shoulder, both are going to loose something. No matter what your nationality is, as long as you were born and grew up as a Tanzanian u will always be a tanzanian. You will speak different languages but swahili will flow better, the memories of school will be with u, memories with friends etc etc.

    If they really care abouit the welfare of Tanzania and Tanzanians they will then consider tanzanians living abroad, but is there much to expect of the government? do they even care of Tanzanians who are in Dar es salaam? then why all of a sudden would they start to care about tanzanians living abroad?

    They just dont give a darn about anybody.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 21, 2009

    Nilisikitishwa na yule Rastafarians aliyefariki hivi majuzi alijitolea kwa moyo wote akafundisha vyuo mbali mbali akaomba uraia kwa miaka mingi lakini wakamkatalia hivi ilikuwa ni kwanini? Au kwasababu hakujua kutoa rushwa kama wahindi?(nadhani alikuwa anaitwa Dk. Ken)
    Inasikitisha siasa za zidumu fikra SAHIHI za mwenyekiti wa CCM bado zinaendelea. Miaka za nyuma vitu kama TV, magari na maendeleo mengine vilikuwa vinazuiliwa kwasababu vilikuwa ni anasa. Hata nasikia mambo ya kupata passport ilikuwa ni taabu sana mpaka miaka ya karibuni watu ndio wameanza kusafiri safiri.
    Dual citizenship ina faida nyingi ikiwa ni pamoja na Taifa kutopoteza wataalamu wake bali kuweza kutumia utaalamu wao kusaidia kuendeleza taifa, Pia kuna faida mbali mbali katika uchumi na biashara. Pia ni nafasi ya ku expose taifa na wananchi na kuwa katika level moja na mataifa mengine.
    Mataifa mengi yenye kungangania mfumo wa urai moja utagundua ni mataifa ya kikomunist kama China na North Korea hivyo hakuna jambo la ajabu kwa CCM kuendelea kuminya wananchi.
    Hofu kubwa ilikuwa ni kuwapa Wahindi uraia wa nchi mbili lakini nadhani hilo lingeweza kutafutiwa ufumbuzi. Natumaini haya ni mawazo ya JK na iko labda Bunge linalowakilisha wananchi litakuwa na uwezo wa kuliangalia na kulijadili hili suala kwa makini zaidi na ikishindikana leo milango tu itafunguka huko mbeleni kama ilivyokuwa kwa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, passport kwa wananchi, TV, biashara huria, na mengineyo mengi.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 21, 2009

    Kama Rais anasema "mtakula huku na huku" na ni mtu aliyeshauriwa na "wasomi" (sijui wa wasomi wa umbeya au majungu) Tanzania haitokuja iendelee. Watu wanaomba uraia wa nchi mbili ili waweze endeleza nchi si kula huku na huku.
    Sijawahi kuona raisi na wasomi wake wana mawazo finyu namna hii.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 21, 2009

    Kiingilio hiki hapa
    http://www.lawac.org/reservationforms/Kikwete-web.pdf

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 21, 2009

    Du sijaelewa kabisa..Hivi JK kaja vekesheni kama michuzi au michuzi kaja kikazi..kureport safari ya JK.....
    Mdau hapo juu wajua kabisa kwamba Tanzania english ni second language afu unasema eti rais anasisita....wewe yaani kukaaa kwako US miaka 10 ukibeba box na kithungu chako cha broken ushaona ushafika...TAARIFA YAKO...KUONGEA KITHUNGU SIYO KUWA NA ELIMU..Wanugu wangapi wanaongea kithungu lakini kichwani mbumbumbu..wabeba box msituangushe bwana na ushamba wa kuongea kiingereza bwana

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 21, 2009

    OYAAAAAAAAAAAAAAAAA Mashakaaaaaaaaaaaaaaaa upo wapiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
    Pleale tunakusubiri hapa utufanyie analysis.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 21, 2009

    Please John Mashaka Come On Where are you? we are waiting for your comments here.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 21, 2009

    hakuna point hata moja hapa. kuanzia kwa aliyetoa hotuba, wasikilizaji hadi watoa maoni hakuna pointi kabisa.
    huyo nae katumia kodi zetu zoooote kuja kongea na wapiga box!! kisha akatumia kodi zetu kuiona gugo!!!
    ama kweli usiombee kuifahamu nchi inayoitwa tanzania. kila siku presha itakuwa inapandaa inashuka!!
    Asifiwe, TZ

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 21, 2009

    Wadau,
    Mimi nahisi Mheshimiwa Raisi hakutaka kuelezea tatizo la uraia wa nchi liko wapi? Kwa kweli analijua.Mimi sijawahi kusikia watu wa Tanganyika wakipinga suala la uraia wa nchi mbili. Tatizo ambalo Mh Raisi hakutaka kulisema ni kuwa wanaopinga suala hili ni viongozi wa CCM Zanzibar. Hao ndio wanaojifanya kuwa ni wapenzi wakubwa wa mapinduzi na wanahisi uraia wa nchi mbili utasababisha watu ambao walikimbia wakati wa mapinduzi kurudi. Unajua viongozi wa Zanzibar wanawahusisha Wazanzibari walioko nje na upinzani. Sasa wanaona kuleta uraia wa nchi mbili ni kuwafanya wapinzani walioko nje kurudi Zanzibar na "kusababisha fujo". Ni woga wa mtoto mwari tu.
    Sasa CCM Bara unajua hawataki kuwaudhi CCM Zanzibar hata kidogo kwa kuogopa CUF kushika serikali Zanzibar.
    Hilo ndio tatizo. Anaebisha aseme ni lini na wapi watanganyika wamekuwa wakipinga uraia wa nchi mbili? Suala la kusema eti watu wanataka kula huku na huku alikuwa anataka kuchekesha watu tu sio kweli.
    Ndimi robo mzenji/robo mbongo/robo mbeba boksi huku Detroit.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 21, 2009

    HAIWEZEKANI MTANZANIA ANAEOMBA KUWA NA URAIA WA NCHI MBILI AONWE KAMA MTU MWENYE TAMAAA YA HUKU NA HUKU WAKATI HAO WAGENI AMBAO HAWANA HATA URAIA WA TANZANIA WANAFAIDIKA TANZANIA NA NCHI ZAO.RAISI ALITAKIWA KUANGALIA KWAMBA SWALA LA URAIA WA NCHI MBILI NI VIZURI KWA NCHI KWANI WATANZANIA WATAWEZA KUJA KUWEKEZA NA WAO SIO LAZIMA WAGENI TU WAWEKEZE.RAISI UNAPOKUWA NA FIKRA YA MITAANI NDIO TATIZO LENYEWE.
    VIONGOZI WETU SIO WATU WA KUCHAMBUA MAMBO TATIZO.
    INAKUWAJE WATOTO WENU WANA URAIA WA NCHI MBILI SISI WATOTO WA KAJAMBA NANI ISHINDIKANE?
    MDA mzawa

    ReplyDelete
  22. Kaka Michu asante sana tena sana kwa hii klipu. Kama ina transkriptu naomba unitumie kwenye barua pepe. Naandika pepa kuhusu hii mada ya uraia pacha na nitahitaji kumnukuu rasmi Mheshimiwa Rais kuhusu kula huku na huko. Alafu pole sana na lile sakata la KLM. Nakutakia Vekesheni njema huko Marikani. Inshallah tutaonana ukirudi kula na huku Bongo Tambarare. Kila la heri!

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 21, 2009

    Mashaka atauletea maneno mengi tu yasiyo na tija.

    Raia ameongelea kifupi mno- labda kwa ajili ya mazingira yenyewe. Ukweli ni kwamba katika swala la brain drain tunapoteza watu wengi ambao kwa sababu ya pochi watakaa nje na kama masharti ya kukaa nje ni uraia basi wtauchukua. Naamini kama watanzania wengi ambao wana skills zenye utashi wa kimataifa wangeweza kukaa nje bila matatizo wapate pochi na kuendelea na pasipoti moja tu ya TZ bila matatizo au bugdha za kiuhamiaji au disadvantage zingine wangefanya hivyo na kubaki huko.Lakini kuondoa matatizo na bugdha anajipatia pasipoti ya kigeni ili wakae kwa usalama zaidi na convenience.
    Sasa swali ni kwamba je tuko tayari kuona watu wetu wanaondoka tu wanaondoka kwa sababu we cannot afford to pay them for their skills? Ni muhimu JK na watu wake kama hawataki uaraia wa nchi mbili wawe na mkakati wa kupunguza brain drain walau maana tutabaki nyuma tu kila siku kama watu wetu wenye uwezo tunawaangalia wakitumika kuleta maendeleo nje. Kwa mafano kwa nini tusiwe na international register ya watanzania wenye rare skills za kimataifa na wao wawe wa kwanza kutafutwa kwa ajili ya kazi yoyote ambayo kwa kawaida angepewa expatriate? Najua Jamaica wanafanya hivyo; na si kazi kubwa kuwa na register ya namna hiyo kw akutumia TEKNOHAMA. Kwa hiyo hawa jamaa sijui wawekezaji SONGAS, SAB, COCACOLA wasilete mgeni hapa nchini kabla ya kwanza kudhihirisha kwamba hakuna mtanzania mwenye uwezo popote kwenye hiyo register ambae ana uwezo na kuitaka hiyo kazi. Alafu wasilete longo longo hawa wawekezaji wa kumlipa mtanzania kidogo kwa kazi sawa kwa sababu ni mtanzania- maana hiyo ipo hivi sasa.Kitu kama hiki kitapunguza brain drain na kuwabakiza watanzania hapa.
    Pili JK na watu wake waangalie immigration procedures za kwetu na kupunguza maspana boi wanaoingia hapa kutoka South Africa na kwingineko kama maexpatriate- wapo hao walikuwepo Sea Cliff Hotel, walikuwepo TBL. Kazi ambazo waTZ wanaziweza. Hapa immigration omeshindwa kazi mpaka sasa.
    Vile vile TIC isiwape vibali eti mwekezaji wa kiwanda cha pipi (alikuwepo mmoja ambae vile vile alikuwa anachoma pizza karibu sana na TMJ mikocheni siyo Saverio), restaurant ya kuchoma tandoori Chicken ( alikuwepo mmoja Upanga karibu na Jamati). Hapa TIC ina kazi bado.Hawa wanabana tu nafasi za watanzania. Watu kama hawa tunaowaruhusu hapa kweli hawaleti tija na hawa ndiyo hasa wanakula huku na huku.Inatakiwa tulete maexpatriate madaktari, mainjinia, investors wenye international brands kuja hapa. Lakini hii haileti maana kama nchi inao, walau kiasi, watalaam wa aina hii na inshindwa kuwaretain alafu inakubali wageni tena kufanya kazi ambazo watanzania wamekwenda kufanya nje!
    Alafu kuna mchangiaji mmoja amezungumza idea nzuri nadhani kwamba JK na timu yake iangalie uwezekano wa waTZ kuwa na dual citizenshio na siyo wageni kuwa na paspoti ya pili ya kitanzania.
    Lazima hili swala tuliangalie katika muktadha wa kuweza kubakiza nyumbani skills za kuweza kuleta maendeleo na tusiendelee kuzipoteza.
    Balozi wa nanhii: naomba kujenga hoja katika globu yalo tukufu kama ilivyoainishwa hapo juu!!!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 21, 2009

    Mwakipesile

    Umeongea jambo la msingi sana.

    Kwa kuongezea mimi nasema Rais JK sio Intellectual kabisa, huwezi kuzungumzia hoja ya msingi kama Uraia wa nchi 2 kwa hoja dhaifu namna ile.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 21, 2009

    mbona raisi wetu unaongea kama vile hutaki hili jambo. wacha izo excuse zako za wasomi kupinga. kama kweli ulitaka dual citizenship ungefanya bidii ili awo wasomi bandia wakubali na wewe. ebu angalia hizo nchi nyingine walioruhusu uraia wa nchi mbili walifanyaje. watanzania mlio nje wekeni pesa zenu mliko kwasababu haina aja ya kufikiria mtastaafu nyumbani.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 21, 2009

    MWANAKIJIJI TUNAKUSUBILI .

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 21, 2009

    Hivi hamjamjua rais wetu mpaka anamaliza term yake ya kwanza!? Huwa hana majibu ya mswali/kero za wananchi. Anabaki kusingizia wengine na kuchekacheka tu. Mbona hakusema mtazamo wake YEYE KAMA RAIS na binafsi ni nini? Siasa siasa tu!! Halafu, L.A sio mahali pa kwenda kutangaza utalii wa TZ right now, waste of money. People are worried about foreclousures right now! Strategy baba !

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 21, 2009

    Watanzania acheni uvivu, someni academic papers kuhusu suala la uraia wa nchi mbili muelewe wenyewe, msisubiri kutafuniwa na mtu anayeimba nyimbo za kasuku kutoka kwenye majarida. Ndiyo maana Wakenya wanatuzomea.

    ReplyDelete
  29. Wabongo kila kitu wanacheka.

    Wanaletewa bad news wanacheka.

    Wanapigwa kidongo cha kula huku na huku wanacheka.

    Wanaambiwa Membe alijebeba ujumbe wao kwa Watanzania kashindwa kuwashawishi nyumbani wanacheka.

    Wanaambiwa uchumi ume slow down wanacheka.

    Na hawa ndio wamekaa huko US wa vijijini sijui ndio itakuwaje

    Kazeni sura Wabongo nyinyi... mtakufa na mikazi ya schedule na mi stress na mi bills huko... nyie jichekesheni tu

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 21, 2009

    Kuna watu wengine akili zao hazina akili. Wewe umepata uraia wa US sasa uraia wa Tanzania wa nini? Wewe kichaa nini? Huku ni kupotezena muda kabisa. Ukiwa na uraia wa Marekani unakuwa na nafasi kubwa sana ya kufanya biashara bongo kuliko hata wabongo wenyewe. Mashaka anataka ipite ili agombee urais sijui nani alimwambia aoe limama la kizungu.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 21, 2009

    HIZI AFARI ZA MAREKANI ZISIZOISHA MBONA HAZITULETEI MANUFAA YOYOTE? HIVI NI KWELI UMASIKINI WA NCHI HII UTAONDOLEWA KWA SAFARI ZA MAREKANI? HIVI KWELI GOOGLE, MICROSOFT NA YAHOO WATAWEZA KUONDOA UMASIKINI WA WATANZANIA? JK ANAONGOZA KWA SAFARI ZA NJE HAPA DUNIANI LAKINI TANZANIA BADO INAONGOZA KWA KUOMBAOMBA HAPA AFRIKA LICHA YA KUWA NA RASLIMALI NYINGI. WAKATI TUKILALAMIKIA SAFARI ZA JK, CCM INAZIONA SAFARI HIZO NDICHO KIPIMO CHA UFANISI KATIKA KUONGOZA NCHI! AIBU.WATANZANIA TUBADILIKE TUJUE NI NANI ANATUFAA AU HATUFAI KUONGOZA NCHI ILI TUVUKE KWENYE HILI DIMBWI LA UMASIKINI ULIOKITHIRI. KWAKO MJOMBA JK, HAO WATANZANI HATA WAKIRUDI WOTE SIKU UTAKAPOPATA NAFASI YA KURUDI HAWATAWEZA KUUBADILI UCHUMI WA TANZANIA, MIMI NAONA WITO WAKO NI WAKUTAPATAPA TU; BADILI MFUMO WA KUTAWALA UWE ENDELEVU NA SI UFAHARI WA CHAMA CHA CCM KUSHIKA MADARAKA. NAWE MICHUZI, USISAHAU KUNILETEA KUKU WA KUKAANGA WA KINTINKU (KENTUCKY) WALAHI SIJAWAHI KUWALA TANGU NIZALIWE. VAKESHENI NJEMA. SAMAHANI NILISAHAU, VIPI ILE BLOG MBOFUMBOFU MMEWEZA KUIGUNDUA HUKO GOOGLE?

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 21, 2009

    Napenda kuchangia baadhi ya waliotoa maoni wanajiona ni wasomi saanna mpaka kutumia lugha kuwa alivyosema Raisi au washauri wake eti kuwa ni(stupid point)Hivi wewe ni nani? Unajiona bora ni mwerevu jaribu hata kugombea nafasi yyt kama utapata wacha huku hata huko ughaibuni uliko kujuwa kiingereza basi nongwa? Wacheni kusannifu viongozi, eti uhuru wa kutoa mawazo, ziko Nchi zinakubali Uraia wa Nchi zaidi ya moja, hapa kwetu bado ni mpaka bunge lipitishe hiyo Sheria na mchakato upo, naona wewe pia utalilia jinsia zote mbili ili ufaidi Poleni. Nawe mbeba maboksi ukimaliza kutosheka na masomo njoo utaukana uraia huo wa huko utapewa wa Huku Tafuta kisomo kwanza halafu uje kuna taratibu zake Karibu sana

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 21, 2009

    nimechoka kabisa...
    yan aya ndo majibu ya rais Kikwete?

    "eti muwaachie wawekezaji na serikali wawekeze ktk maswala fulani nyie jengeni ili ndugu zetu waone manufaa ya nyie kuwa nje"BBC

    Yesu tusaidie

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 21, 2009

    wee annon
    kama abaoa je?watu waendelee msikiliza?

    afu uyo mjinga apo eti bongo malaria nyingi!!kaa uko nje milele uone,heri z=sie tuwe tunatalii tu nje na kurudi bongo sweety

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 21, 2009

    msirudi bongo badilisheni kabisa uraia mkae nje

    no dual citizenship Tz

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 21, 2009

    nimeshitushwa sio na uamuzi wa serikali kukataa uraia wa nchi mbili bali sababu alizozitowa rais wa taifa. unbelievable.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 21, 2009

    Mimi nadhani suala la uraia wa nchi 2 kwa Tanzania linahitaji muda kidogo na siyo wakati wa kuwalaumu wasomi waliopo Tanzania. Sikubaliani na watu wa nje wanaposema kwamba wanataka urai wa nchi mbili ili walete maendeleo nyumbani. Kimsingi wao hawana moyo wa kusaidia nchi na ndiyo maana wameamua hata kusaliti urai wao. Inatakiwa tuwapongeze wote waliopo bongo kwa kukubali kufanya kazi nyumbani ili kujenga nchi yao pamoja na kuhudumia ndugu zao. Mimi sioni ni kwa nini watu wa nje wanashindwa hata kuwasaidia ndugu zao waliopo nyumbani kwa kisingizio tu siyo raia tena wa tz. Kibaya zaidi kwapo ambao walienda kupitia kodi za walalaho, lakini hawakurudi nyumbani ili kuwahudumia baada ya shule zao. Chagueni uraia 1. Hongereni wasomi wote mliopo Bongo kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kubaki nyumbani ili kuijenga nchi, ila nawaombeni acheni rushwa ili wananchi wafaidi maendeleo yao.

    ReplyDelete
  38. Jasmin AlkharimMay 21, 2009

    Do, wadau, anagalau nimefurahishwa na mahojiano haya ya rais kuhusu uraia wa nchi mbili. Dr. Shayo wa UK aliiweka vizuri sana hoja hii pale aliposema kuna mambo ya msingi ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi. Anagalau Dr. shayo inaonekana anakubaliana na hoja ya rais Jakaya Kikwete

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 21, 2009

    Balozi, mbona hukumvuta sana yule demu katika video yako, ulipitiza katikati ya mabitozi wawili na kumtoa demu vizuri tu huku akikuangalia kidizaini na my hasbandi wake karibu yake akikupa kijicho cha wifu fulani.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 21, 2009

    Asante Mheshimiwa Raisi kwa maoni yako kuhusu uraia wa nchi mbili. Sisi wenye pasi mbili huwa hatusumbuliwi na serikali yako tunapokuja kuona familia zetu, tunashukuru. Tunalipa ada ya viza na tunasaidia maendeleo ya nchi kwa kutumia fedha zetu nyumbani.

    Kwa kuwa nchi ni masikini, inazalisha dola milioni 350 tu mpaka leo, ambayo ni sawa sawa na mazao ya mvinyo TU ya Chile huko Marekani ya Kusini, utakubaliana na mimi kuwa kuna faida nyingi kuliko hasara kutuwezesha sisi wenye pasi mbili kuja nyumbani na kuleta fikira na mawazo mepya katika uchumi. Inaonekana halisi kuwa elimu bado ni duni Tanzania kama watakataa bungeni kutupa ruhusa ya kuwa na pasi mbili kihalali. Kama ina madhara yoyote, kwa nini nchi tajiri nyingi (Canada, USA, UK) na zinazoendelea nyingi (India, Brazil, Philippines) zimeruhusu pasi mbili? Je, usalama wao ni mdogo kuliko Tanzania? Sababu za usalama hazingii kichwani kwa wasomi kama sisi kwa kuwa Tanzania hakuna kitakachohatarisha usalama wake wakati "wakubwa" kama Marekani na Brazil wameruhusu. Sababu za wivu zimeniudhisha sana Mheshimiwa Raisi, inaonyesha dhaliti kuwa sisi tuko nyuma sana kimawazo na kielimu, hii ni sababu isiyo na msingi maalumu. Anayefaidika na elimu yetu ni nchi za nje zilizotuchukua kw akuona faida ya elimu yetu, na hamna hata siku moja Mtanzania atachagua pasi ya Tanzania ukimpa afanye uchaguzi. Maamuzi ya swala hili ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.

    Shukurani.
    Max, mdau wa Japan

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 21, 2009

    hatuwezi wote kujazana tz kugawana umaskini,uraia wa nchi mbili ni muhimu tunawasaidia wa nyumbani na kutoa nafasi ya ajira kwa waliopo tz.
    kwetu sisi wanafunzi imekuwa ni ngumu sana huku nje kpata nafasi ya internship kwasababu si raia, na hata kwenye interview huku hata kama unavigezo wanakudisqualify mapema na mwishowe una degree unaishia kubeba box,tax kwa ma foreigner ipo juu sana, xul fee for non-EU members ni juu sana ndo maana wengi wanaishia kusoma vyuo vya ajabu ajabu japokuwa wametimiza masharti ya kupata uraia wa nchi husika

    sasa sijui wasomi wetu wanaakili sana kuliko wa nchi zingine duniani au?

    hivi yule muhindi aliye kuja kugombea u miss tz aliukana uraia wake na kuchukua utz? maana aliishi tz mwakammoja tu akaingia miss tz

    tungoje mpk lini?

    nasubirini wale watoto mliowapeleka football academy nje wote mje kuskia wafaransa au warabu

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 21, 2009

    I wish ningekuwa hapo nikamtwanga maswali. Anamaanisha nini kula huku na huku? Nia yetu ni kurudi kwetu na kujenga nchi yetu. Kula, ni wao tu wanaokula watanzania wote wa kawaida ni walala hoi. Hapo hapo anasema kwamba anatuelewa kuwa tunaishi huku kwa ajili ya kuwapatia watoto wetu elimu nzuri.

    Je yeye anafanya nini kupandisha kiwango cha elimu? Wakati tunasikia kuwa kuna ma professor wengi wenye vyeti vya fake wanaofundisha kwenye vyou vyetu. Kwa nini asiwaruhusu watanzania walioqualified na wanaopenda nchi yao (kuliko wakenya wanaotuvamia kila siku) kuja kufundisha na kuinua kiwango cha elimu nchini? Mfano mwingine ni picha iliyotolewa na Michuzijr juzi inayoonyesha bweni la wanafunzi 25, hata kuku hawapashwi kulala humo.

    Wewe anonymouns wa 11:35 unayesema ulikuwa hapo na sasa unatuuliza sisi ufanye nini kwanini hukumbandika maswali? Au bado una kasumba ya kuwaogopa viongozi wetu???

    ReplyDelete
  43. I think it will be more wise to establish a Diaspora commitee which can cooperate directly with the goverment or an institute part of Foreign Ministry, with or without dual citizenship.
    Sababu ni nyingi tuu ambazo we can both benefit , serikali na sisi waishio nje ya nchi.

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 21, 2009

    the whole speech has no coherent meaning, my fellows tanzanians could you explain to what did he me say as a chief of state??

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 21, 2009

    I hope akija DC atakutana na wabongo. Maana tunasikia tu ooooh Rais wenu alikuwa hapa na alikutana na watanzania kwenye dinner kwa balozi. Jamani hiyo dinner hatuitaki lakini angalau mtupe fursa na sisi watu wakawaida kukutana na rais wetu. Maana nasikia tuu kuwa atakuwa hapa DC, au ndiyo kaisha pita (as usual). Haya mambo ndiyo yanarudisha maendeleo. Hata kukutana na Rais ni big deal, ni RAIS WA WATANZANIA WOTE!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 21, 2009

    sa yale matawi ya CCM nje(UK) yanachukua wanachama kwa vigezo gani?maana wengi mle waburundi,wanyarwanda na wasomali.Ina maana hao jamaa wote hawaqualify kuwa wanachama kama katiba ya nchi hairuhusu uraia wa nchi mbili.WALIJIRIPUA ILI WAWEZE KUISHI UK.

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 21, 2009

    Kula nini kunakotokana na kuwa raia wa nchi mbili? Tanzania nimezaliwa Ughaibuni natafuta,na katika kutafuta kwa vizuri tunatengeneza karatasi litusaidie kutafuta vizuri.

    ReplyDelete
  48. Napenda kuongezea kidogo tu kwenye huu mjadala wa uraia wa nchi mbili.

    Ukifanya uchunguzi, utaona kuwa nchi zinatofautiana katika masharti yao ya uraia wa nchi mbili. Ziko nchi ambazo hazina masharti magumu, na ziko ambazo masharti yake ni magumu.

    Marekani ni nchi mmoja ambayo nimeona ina masharti magumu. Hii ni pamoja na kiapo ambacho mtu anaapishwa wakati wa kuchukua uraia wa Marekani. Katika kiapo hiki, mtu anaukana uraia wa nchi alikotoka, na anakana kutii amri za rais wa nchi ile, na anaapa kuwa kuanzia sasa yeye atamtambua na kutii amri za rais wa Marekani tu.

    Nawaomba wadau muangalie hiki kiapo cha uraia wa Marekani. Ni kizito. Lakini, kama nilivyosema, nchi zingine hazina kiapo kama hiki.

    Vile vile, Marekani inawakumbusha raia wake kuwa mtu anayeamua mwenyewe kwa hiari yake kuomba uraia wa nchi nyingine, anajiingiza katika hatari ya kupoteza uraia wake wa Marekani. Marekani ina wasi wasi mwingi kuhusu raia wake wanaoomba uraia wa nchi zingine.

    Narudia, hapa nimetoa mfano wa Marekani tu. Nchi nyingine, kama vile za Ulaya, Australia, na kadhalika zina mitazamo tofauti, na zingine hazina matatizo kama haya ya Marekani. Kwa hivi, suala hili tunapolijadili, labda tungelijadili kwa kuangalia pia ni nchi gani tunazoongelea.

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 21, 2009

    Jamani eeeeey tulioko nje tuendelee kujenga family zetu achaneni na hii serikali ambayo sina uhakika inawauliza wasomi wapi wenye fikra finyu kuhusu hili swala la uraia. Chukua uraia wako wa nchi uliopo rudisha ganda lao la kijani na ukitaka kwenda nyumbani kaombe visa it is that simple. Nikimaliza kusomesha watoto wangu na wandugu zangu ambao hawana uwe wa kuwalipia watoto private schools au kupata sacholarship za serikali ambazo sijui huwa zinagawjwe. Maana nakumbuka nilipomaliza form six with second division ya science nilienda wizarani kuomba scholarship ya udaktari au unesi mzazi wangu akaambiwa kuwa eti nimefanya vizuri sana hivyo nina chance kubwa ya kuchaguliwa kwenda mlimani au muhumbili hivyo wanawapa hizo scholarship watu ambao hawatachaguliwa hapa nyumbani (waliofeli), mwanangu upo hapo??? I could not believe it and true I ended up going to mlimani na nikachukua ganda langu na nilipochukua ganda tuu nikapaa majuu kwa msaada wa mwanafamilia aliyenauraia wa nje! Bila hivyo ningekuwa nasota bongo kama wenzangu niliomaliza nao! Huu ndiyo umuhimu wa kuwa na uraia wa nchi mbili. The time I have been here nimesaidia sana watoto wa family yangu angalau kuwafikisha form four. Bill za laki laki uongo hazinishindi maana dola sasa karibu Tshs 1350! So you need couple of hundreds kumsomesha mtu bongo. Mengi yataweza kufanyika kama issue hii itangaliwa kwa mtazamo mpya na siyo mambo ya wivu. WATANZANIA TULIONJE YA NCHI TUJENGE FAMILIA ZETU NA HATIMAYE TUTALIJENGS TAIFA LETU! MUNGU IBARIKI TANZANIA NA KUWAPA WASOMI WETU MWANGA WA KUCHAMBUA MAMBO KWA KUFUATA MISINGI MUHIMU YA MAISHA.

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 21, 2009

    Mheshimiwa alikuwa anawaonea aibu tu wadau..ila ukweli ni kwamba huwezi kuwa mchezaji wa timu mbili chagua timu moja tucheze mpira..na wote mnaotaka uraia wa nchi mbili ni ma snitch..ma selfish...ma traitors...na mbaya zaidi hamna akili..nasoma zangu UK narudi Bongo nyumbani baaaaaaaab...mnachotaka mkusanye viji dola vyenu na vi pounds ..mkatanue bongo ..mjifanye mmetoka Ulaya kumbe ma stress kila siku..Magomeni namba moja sio LA..A..NY..wala London...rudini kwenu wote mnaopenda starehe za kijinga...

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 21, 2009

    Naomba Mheshimiwa JK atufafanulie nini maana ya kula huku na huku. Mimi nilikuwapo Bongo nimechoooka ile mbaya sikuwahi kula chochote nauli tu ya daladala jasho linakutoka. Huku abroad sidhani hata kama kuna mtu anakula kwani watu wako hoi na mashift ya kazi au masomo. Hapa kuna imani potofu ya kwamba tukiwa nje kuna fungu maalumu lililotengwa na serekali kwa ajili ya kutupa pesa wageni. Hapana sio hivyo hata mtu akila ni kwa jasho kweli kweli mtu anakuwa yaya aweze kula. Huo usemi wako wa kirahisi wa kula huku na huku unasikitisha sana. Na kula ya Bongo inatokea wapi wakati hata ajira zenyewe hakuna? Na penye ajira kipato hakitoshelezi mahitaji. Nimeichunguza sana hotuba yako na majibu yako yalikuwa ni ya kisiasa na yasiyo na ukweli ndani yake. Na kama mtoa maoni mmoja alivyosema watanzania kazi ni kucheka cheka tu mkiambiwa nakupiga risasi sasa unacheka na makofi juu.

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 22, 2009

    WEWE WACHA PUMBA,UNAJUA KIINGEREZA AU UNAUNGANISHA UNGANISHA, MPAKA UMKOSOE RAIS WAKO? WASAIDIE WAMATUMBI WENZAKO FALA WEWE

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 22, 2009

    NILITEGEMEA RAIS ANGETOA HOJA NZITO,KULA HUKU NA HUKO...SIJAELEWA MAANA YAKE NI NINI? MIMI KAMA MTANZANIA NILIYESOMA HADI KWENYE LEVEL YA UDAKTARI KATIKA NCHI HII HUWEZI KUNIAMBIA ETI NIUKATAE URAIA WA USA HALAFU NISIENDE TANZANIA AMBAKO NIMEZALIWA NA WAZAZI WANGU WANAISHI HUKO...KWELI HAIWEZEKANI.RAIS HAKUPASWA ASIKILIZE MANENO YA MITAANI YA WASOMI UCHWARA WANAOTAKA WATANZANIA WOTE WARUDI KUJAZANA HUKO BILA KAZI ETI KWA AJILI YA KU-KEEP URAIA WAO.MHESHIMIWA RAIS HUJAAINISHA FAIDA ZA URAIA WA NCHI MBILI VS HASARA ZAKE.UKWELI UNAONEKA...HATUFAIDI TUNAFANYA KAZI HALALI NA HAKUNA MTU ALIYEKATAZWA KUJA MAREKANI KUSOMA NA KUFANYA KAZI ILA JITIHADA ZAKO.

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 22, 2009

    Sisi wamarekani wenye asili ya ki-Tanzania tunafurahi kuona wasomi mbalimbali mnatoa maoni yenu kuhusu uraia wa nchi mbili.Tutaendelea kusaidia Tanzania kwa kuendelea kuwatumia pesa ndugu na jamaa zetu waoishi huko ambapo bado tunaona ni nyumbani.Hatupendi kuwa wamarekani laki wabebabox wenzangu mtakubaliana na mimi kuwa ukiwa mmarekani utachota pesa ya hapa kilaini sana(haina guarantee)Sasa Mh Kikwete anaposema Hatuewezi kufaidi huku na huku halafu anatusisitiza tukajenge na kuwekeza nyumbani ili kuinua uchumi wa nchi anamaana gani?Tuinue uchumi wa nyumbani wapi ili nani afaidi?Tumekwenda kumsikiliza kwa matumaini ya kuendelea kubaki watanzania wa kuzaliwa na wamarekani wa kuhamia japokuwa Mh raisi ametukana na kusisitiza tuwekeze nyumbani ambako tutapokelewa kama foreighn investers.Nikijenga kiwanda Makambako siku mambo yakiharibika nikipewa masaa 24 kuondoka sintaondoka na kiwanda changu ingawa hakufafanua ni nani atakayefaidi kutoka kiwandani kwangu.Tumezaliwa Tanzania,tunaipenda Tanzania na tutaendelea kusaidia Tanzania.Tungependa sana kubaki watanzania laki umaskini ndiyo uliyotufanya tuukane utanzania kwa sababu Marekani inamkaribisha mtu yeyote anayetaka kutajirika.Kwanini mataifa mengine watajirishwe na Marekani na siyo Watanzania?Ila suala alilosisitiza Mh rais la kuhamisha utajiri wa hapa kupeleka nyumbani bado sijaelewa.Naomba mjadala uendelee.Mungu zibariki Tanzania na Marekani.

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 22, 2009

    Mbona tukituma pesa western union mnazikimbilia? Hizo pesa si zimesomesha watoto wanaojenga nchi hap Bongo? Bila sisi kuzituma inakuwaje? Hamjui tumesacrifice sana ili ndugu na majamaa waishi vizuri? Kwa vile mambo yamebadilika? Kwa vile sabuni siku hizi zipo watu wanaoga wanatakata? mbona miaka ya zamani hata kipande cha kuogea taabu kupata mnasubiri tuwatumie. Wacha tu msitudharau tulio nje tumewajengea taifa.!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  56. We mdau wa Marekani wa herufi kubwa we uliyesema umesoma mpaka udaktari, nashangaa hujui kwamba si lazima uwe raia wa Tanzania ndio uingie Tanzania kusalimu babu zako.

    Umekana uraia wa Tanzanua, sawa, tafuta Visa njoo usalimie nchi yako ya asili.

    Tatizo liko wapi?

    ReplyDelete
  57. Waungwana,
    NImesikiliza "clip"... sikuwepo kwenye mkutano, lakini nadhani madongo mengine kwa kweli hayastahili. nilichoelewa ni 3 things: 1. Hoja haikupokelewa vizuri na "wasomi" 2. Ni maoni yake Raisi kwamba hoja hii bado ina "merit" and 3. Tutaendelea kufundishana na kueleweshana... translation... bado kunakazi ya kueleweshanathe debate is on the table. hayo madongo sioni uhalali wake.
    Baada ya kusema hivyo, nadhani kuna haja ya wadau kujaribu kujadili hoja hii kwa uwazi. sio tu kwa faida yetu, bali hat akwa wakina "Membe" ambao amefika mahali hawana point za kuitetea. Nimeishi Marekani kwa miaka takribani 14, na leo naishi Dar (mwaka wa pili sasa) bottom line: ni kwa "wasomi" kufikiria namna ya kuweka mikakati ya kuja kujichukulia nchi yao kiuchumi. Uraia wa nchi mbili huendani hoja... lakini sidhani kutakuw ana faida yoyote kwa mtu binafsi, iwapo hata sasa mtu bado hujaweza hata kufikiria ni nini cha kufanya ku "take advantage of your current status". Unaishi US, UK or wherever... tayari una nafasi kubwa ya ku-make a difference kuliko 97.5% ya watanzania ambao wapo hapa Bongo. My wish ni kwamba wabongo tutapunguza "uswazi" na kuanza kudiscuss "real" issues ambazo "control yake ipo mikononi mwetu! - Peace

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 22, 2009

    God verdommer!! kula huku na huku maana yake ni nini?
    Halafu mbongo aliyechukua uraia wa nchi nyingine akipanda chati kwenye nchi za kigeni, ndio wakina Kikwete kwanza kujisifia.
    SIFIA ULICHOUNDA
    Tukiwa na uraia mara mbili kitu tutachakula Bongo ninini kama sio kuja tu kuwasaidia ndugu zetu ambao wamebanwa mbavu na mafisadi hata kufurukuta hawawezi.
    Kikwete anaogopa kwamba watanzania waliokua nje hawaupendi uongozi wake kwahio wakati wakupiga kura watarejea nakupewa haki yakupiga kura na kumuondosha madarakani.

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 23, 2009

    I will just go back to visit but will NEVER open up a business or anything... my life here in the US is way better than when I was there. I am very educated and make over 1000000K a year so even without their citizenship, I will still survive. to many of you in here go back to college educate yourselves and fall back. By the way, am I the only one who has noticed that JK smiles all the time? does he ever get MAD/SERIOUS??

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 24, 2009

    NIMESIKITISHWA SANA SANA NA MAWAZO YA RAIS KIKWETE KATIKA HOTOBA YAKE KUWEKA MBELE SUALA LA KULA HUKU NA HUKU NI KWASABABU MAWAZO YAKE NI RUSHWA TU NANI ANAKULA HUKU NA HUKU? MH!! KIKWETE NAOMBA AFUTE KAULI HIYO INAMAANA MBAYA SANA KWA WATANZANIA SI WOTE NI WALA RUSHWA NAUNGANA NA WATOA MAONI HAPO JUU KUKATAA URAIA WA NJI MBILI SI BUSARA FANYA UTAFITI WA KINA MSOMI MWENZANGU UJE NA MAWAZO ENDELEVU DUNIA INAKIMBIA SANA!!!

    MDAU/MBEBABOX UK.

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 26, 2009

    Ka Michuzi nategemea utampa JK asome au hata assistant wake... kwa kweli mambo ya mbagala yanasikitisha sana kwanini wasitibiwe na serikali wale watoto waliopatwa na matatizo ya kutokusikia baada ya yale mabomu? au wewe mwenzetu uliye jirani sana na JK kwanini usimwombe for the sake of the those poor children? mwenzetu kutwa mnasafiri im sure hiyo trip moja ikikatwa itatibia wale watoto ingekuwa ni ulaya wale ni wangekuwa mamilionea ama kweli kukaa hapa bongo kunahitaji moyo, Pls kaka michuzi saidia, please. ulaya watu huwa wanachangia kwenye kila kitu lakini swala kama hili nashindwa kuelewa kwanini halifanyiwi chochote... kaka michuzi tafadhali sana saidia kadri unavyoweza tunajua una kontact nyingi please tuko chini ya miguu yako.

    ReplyDelete
  62. AnonymousJuly 24, 2010

    Karume na Seif ndio wakombozi wa Zanzibar na si Kikwete wala mtanganyika mwengine yoyote. SEIF NA KARUME KWA ZANZIBAR BORA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...