JK akikaribishwa Malkia Magrethe wa pili (Magrethe II) katika kasri ya malkia kuhudhuria chakula maalum cha mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake

Na Mwandishi Maalumu

RAIS Jakaya Kikwete ameondoka nchini na tayari amewasili nchini Denmark kwa ziara ya kikazi. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Rais Kikwete na ujumbe wake watahudhuria Mkutano wa Tume ya Denmark-Afrika.

Rais Kikwete ni mjumbe katika Tume hiyo ambayo Mwenyekiti wake ni Waziri Mkuu wa Denmark, Anders Fogh Rasmussen.

Wajumbe wengine wa Tume hiyo ni pamoja na wakuu wa nchi na serikali, wanasiasa, wataalamu wa sekta mbalimbali, wawakilishi wa jumuiya za kimataifa na kikanda pamoja na wawakilishi wa jumuiya ya kibiashara, taasisi zisizokuwa za kiserikali na wasomi.

Taarifa ya Ikulu ilisema mada kuu ya Tume hiyo ni Vijana na Ajira katika Afrika, na ripoti ya mwisho ya Tume hiyo itaelekeza nguvu zake katika kupendekeza mkakati wa jinsi ya kuongeza nguvu za misaada ya kimataifa hasa katika maeneo ya vijana na ajira.

“Pia ripoti hiyo itapendekeza mikakati mipya ya kupunguza umasikini, kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi na jinsi vijana wa Afrika wanavyoweza kumiliki na kuongoza jitihada zao za maendeleo chini ya mwelekeo mzima wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa (UN),” ilisema.

Mbali na kuhudhuria mkutano wa Tume hiyo, Rais Kikwete pia atakutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Wamiliki Meli wa Denmark wakiwakilishwa na Mtendaji Mkuu na Rais wa chama hicho, Peter Bjerre-gaard ambaye alikutana naye jana hotelini kwake.

Rais pia leo alikula chakula cha mchana na Malkia wa Denmark na mumewe, Prince Consort kwenye Kasri ya Fredenborg. Rais ataondoka Denmark kesho na moja kwa moja  atkwenda Afrika Kusini ambako atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Jacob Zuma kuwa Rais mpya wa nchi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2009

    yes!!Can't wait to read JK's memoirs maana mpaka saa hivi simuelewi naona vilio vyetu havisikii!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2009

    Mtalii wetu huyoooooo, achanja mbuga!Hatukuwezi mkwere!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2009

    Dah Ebana Mshikaji Unasafiriii Simchezo. Poa Lakini Tutafanyaje

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2009

    Sahihisho mkuu wa wilaya ya nanihii.
    Anders Fogh Rasmusen alishajiudhuru uwaziri mkuu wa Denmark. Kwa sasa ameajiriwa NATO ni general Secretary kama sikosei. Waziri mkuu mpya ni Lars Lokke Rasmusen.
    Na wewe umekuja Vekeshen Dk?Maana ktk hii misafara ya wazito huwa hukosekani.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2009

    TULIKUWA NA HELSINKI PROCESS, IKAJA BLAIR COMMISSION FOR AFRICA, SASA HII DENMARK-AFRICA COMMISSION......MATUNDA YAKO WAPI?????????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...