Kuku tunaokula....Wikiendi hii nilienda kununua kitoweo cha kuku pale Kisutu 'Soko Mjinga', na hii ndio hali halisi niliyoikuta kwenye 'mahakama' yao ya kuku. Watu wa Mamlaka za usafi na afya mpo?!
:1). Mchinjaji akiwajibika huku akiwa pekupeku, wao wanaamini kutokuvaa viatu kunaifanya floor yao kuwa hygienic
2). Kuku waliochinjwa wakiwa wamewekwa kwenye floor ambayo ni chafu na inakanyagwa na miguu ya watu tena michafu
3). Kuku wakisubiria hukumu yao huku wakishuhudia wenzao waliochinjwa wakikukuruka pembeni yao, Mchinjaji wakati mwingine huchinja hata kuku 6 kwa mpigo huku wengine wakishuhudia wenzao wanavyotolewa roho!
4). Damu, kinyesi, manyoya na matumbo yakiwa yametupwa ovyo5). Chemba ya maji machafu ikiwa jirani kabisa na kuku
6). Tope na uchafu vikiwa vimezagaa ovyo kwenye floor

mdauMR. AHMED VIRIYALA
Dar es Salaam, Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2009

    Vichafu ndio vitamu mwanangu!!!
    Wewe wa wapi??
    Mzawa

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2009

    ya kaisari muachie..................................................................
    ukimchunguza kuku humli

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2009

    wewe buruza tu usafi utafanya kwako

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2009

    haki za wanyama jamani, wanahisia kama sisi si vizuri na si uungwana

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 18, 2009

    Ukimchunguza sana kuku huwezi kumla.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 18, 2009

    Duh! hii kweli kubwa yao. Afadhali umeweka humu kama jj halioni basi watabidi waje wasome humu wajue kuna watu wanajua tofauti kati ya uchafu na usafi.

    Watu wako miguu chini na wao si wataugua pia? I hope wakimaliza shift wanaoga kabla ya kwenda majumbani mwao

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 18, 2009

    inatia chefu chefu sana!mbaya sana kwa mtindo huu-kipindupindu kikitokea wapenda kuku kazi ipo!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 18, 2009

    Mmmmh i am speechless!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 18, 2009

    Mungu atunusuru hata apron zao chafu!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 18, 2009

    Watu inabidi kuchinjia kuku manyumbani kwao..Bwana afya wako wapi hapo???????!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 19, 2009

    Hali inatisha, ila nchi bado changa taratibu tu ipo siku tutakuwa na consumer association na machinjio kama hayo yataisha. Watu wa afya wanaenda ambapo mtu anavunja sheria kubwa ili wachukue rushwa, lakini machinjio ya kuku hawajali.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 19, 2009

    Kwamba wanatoa viatu kwa vile wanaamini ndio usafi uliwauliza? Waislam wakichinja kuku wanatoa viatu regardless.

    Na kuchinja kuku sita kwa mpigo ni pointless, sioni inahusiana vipi na usafi. Hukuwa na haja ya kutia tia chumvi nyingi, the picture was self-explanatory, kuweka kuku chini is bad enough, period.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 19, 2009

    Hii picha imeniacha hooiii sana!!! Ndo maana inabidi ununue kuku ukamchinje mwenyewe ktk mazingira uyapendayo wewe yaani kiusafi/kuvaa au kuvua viatu/kuvaa apron au kuka uchi..inakuwa juu yako wewe mwenyewe-amasivyo hiyo ndo hali halisi yenyewe...mmmmmmm makubwa hayo mwanangu..TZ tambarare..

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 19, 2009

    jamani hiyo balaa, lkn hapo kuna watu wanagombea kabisa hao viumbe na mtu akikosa anjilaumu mbaya mno!!

    Its Neyma

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 19, 2009

    KWA MNAOISHI KATIKATI YA JIJI HAPO NI PACHAFU LAKINI KWA TUNAOISHI USWAZI PANAFANANA NA TUNAKOISHI TOFAUTI NI KUWA HAPO HAKUNA VIROBA VYA VINYESI VYA BINAADAMU. UCHAFU NI JADI YETU, SOKO LABUGURUNI NI CHA KUPINDUKIA, TEMEKE VIVYOHIVYO NA MASOKO YOTE NI MACHAFU, LAKINI MADIWANI WA DAR AMBAO KARIBU WOTE NI WA CCM WANANG'AA WALIVYOTAKATA.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 19, 2009

    Rafiki mbona unateleza, hivi umeshafikia umwinyi wa kuchinjiwa kuku! kwa familia yako umenunua sana ni kuku wawili, kuna haja ya kuchinjiwa kweli my friend?Labda ingekuwa zama zile unaitwa..... lakini Ahmed kuna haja ya kuchinjiwa kuku!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 19, 2009

    ndio mana wengine tunaenda sokon kuku mzima-mzima wambeba au unachinjiwa apo na mtu unamwona kwa ustaarabu na usafi wote!!

    iki cha mtoto,machinjio ya ng'ombe na mbuzi (machinjioni)umefika wee annon?
    mbpna utagairi kula nyama!!

    usafi kwa mbongo F++

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 19, 2009

    waliotumia msemo "ukimchunguza kuku utashindwa kumla" wamepotea kimaana ya msemo huu, ukimchunguza kuku alacho apitapo na alalapo na mengine afanyayo mwenyewe kuku, sio afikishwapo na binaadamu. mnadhani kuku kama angelikuwa na uwezo angelikubali kumalizia maisha yake sehemu kama hiyo?

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 19, 2009

    kumuelimisha mchangiaji wa May 19, 2009 6:28 AM, na wengine wote, kuvua viatu kwa waislamu wanapochinja hakumaanishi kuwa waislamu wanaruhusu uchafu kama huo uliopo kwenye picha. katika sheria za kiislamu unatakiwa mahali unapochinja pawe safi, na unavua viatu kwa heshima kwa kuwa wanatumia miguu yao kuzuia mabawa na miguu ya kuku wakati wa kuchinja. ni kuepuka israfu ya kukanyaga chakula kwa viatu. wanatakiwa kuchinja mmoja mmoja na kukosha kisu na mahali wanapomchinjia kabla ya kuchinja mwengine. kwa mantiki hiyo kama utaona kuwa picha hizo hazifati kabisa sheria za kiislamu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 19, 2009

    mtowa maoni wa May 19, 2009 6:28 AM, sijui kwa nini umeona umuhimu wa kutaja waislamu. hata hivyo nakukumbusha tu kuwa waislamu hawasimami wima wakichinja. wanamuweka kuku chini, wanamuelekeza kibla na kuinama kumchinja. tena wanachinja mmoja mmoja hadi akate roho na sio katakata kama msumeno.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 19, 2009

    Ndiyo maana wengine huwa wananunua na kwenda kuchinja wenyewe ugumu upo wapi?

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 19, 2009

    waislam..kibra
    nani kasema nenda machinjio yote uone km kuna izo sheria gani sijui mwataja apa

    watu wamechoka kufata dini/sheria

    ni hayo

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 19, 2009

    mdau wa May 19, 2009 3:18 PM una akili finyu kweli au ni mdogo sana? hukuambiwa kama wanaochinja wanafata sheria za kiislamu au la, kilichosemwa ni kuwa sheria ya kiislamu ni kuelekea kibla. sasa hao wa machinjoni kama wanafata au hawafati sio kosa la dini ya kiislamu. wacha pumba na soma uzuri kinachoandikwa.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 20, 2009

    Sijasema Waislam ni wachafu au sijui wanageukia kibla sijui wanachinja wameinama, wameinuka, wanasoma dua, I ain't said none of that.

    Nimesema, Waislam wakichinja kuku wanavua viatu, na kwamba mpiga picha asitudanganye, unless aliwauliuza wakamwambia, kwamba wanavua viatu kwa vile wanaamini ndio usafi. Nope. Ni dini. And as y'all saw them old folks got vibandiko in dey heads, ni Waislam na hivyo watavua viatu regardless.

    Au Waislam huwa hawavui viatu wakichinja kuku?

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 20, 2009

    Sisi ni wachafu kwa asili na tunaendekeza tabia hii kama tungekua hatutaki hali hii tungeweza kuikomesha mara moja kwa kususia kula vitoweo vinavyotoka maeneo kama hayo lakini.............!Ukipata muda tembelea jiko na choo cha hoteli unayo pata maakuli!

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 20, 2009

    mdau wa May 20, 2009 3:44 AM nakubaliana sana na points zako zote ila sikubaliani kuwa tu wamevaa vibandeko ndio u-conclude kuwa hao ni waislamu. kibandeko sio uislamu na kuna watu tele wanavaa vibandeko na sio waislamu. pia labda hivyo walivyovaa hapo ni vile vya kufata health and safety rules na ndio maana hata unaona wamevaa aproni. Nimesema labda kwa kuwa sina uhakika kama ambavyo wewe huna uhakika kama hao jamaa ni waislamu au sio.

    anyway tusitoke sana kwenye point muhimu, nayo ni kuwa sehemu za machinjoni ni chafu na watu wa jiji ni lazima waliangalie suali hili haraka.

    mr fish

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...