
:1). Mchinjaji akiwajibika huku akiwa pekupeku, wao wanaamini kutokuvaa viatu kunaifanya floor yao kuwa hygienic
2). Kuku waliochinjwa wakiwa wamewekwa kwenye floor ambayo ni chafu na inakanyagwa na miguu ya watu tena michafu
3). Kuku wakisubiria hukumu yao huku wakishuhudia wenzao waliochinjwa wakikukuruka pembeni yao, Mchinjaji wakati mwingine huchinja hata kuku 6 kwa mpigo huku wengine wakishuhudia wenzao wanavyotolewa roho!
4). Damu, kinyesi, manyoya na matumbo yakiwa yametupwa ovyo5). Chemba ya maji machafu ikiwa jirani kabisa na kuku
6). Tope na uchafu vikiwa vimezagaa ovyo kwenye floor
mdauMR. AHMED VIRIYALA
mdauMR. AHMED VIRIYALA
Dar es Salaam, Tanzania
Vichafu ndio vitamu mwanangu!!!
ReplyDeleteWewe wa wapi??
Mzawa
ya kaisari muachie..................................................................
ReplyDeleteukimchunguza kuku humli
wewe buruza tu usafi utafanya kwako
ReplyDeletehaki za wanyama jamani, wanahisia kama sisi si vizuri na si uungwana
ReplyDeleteUkimchunguza sana kuku huwezi kumla.
ReplyDeleteDuh! hii kweli kubwa yao. Afadhali umeweka humu kama jj halioni basi watabidi waje wasome humu wajue kuna watu wanajua tofauti kati ya uchafu na usafi.
ReplyDeleteWatu wako miguu chini na wao si wataugua pia? I hope wakimaliza shift wanaoga kabla ya kwenda majumbani mwao
inatia chefu chefu sana!mbaya sana kwa mtindo huu-kipindupindu kikitokea wapenda kuku kazi ipo!
ReplyDeleteMmmmh i am speechless!!!!
ReplyDeleteMungu atunusuru hata apron zao chafu!
ReplyDeleteWatu inabidi kuchinjia kuku manyumbani kwao..Bwana afya wako wapi hapo???????!!!
ReplyDeleteHali inatisha, ila nchi bado changa taratibu tu ipo siku tutakuwa na consumer association na machinjio kama hayo yataisha. Watu wa afya wanaenda ambapo mtu anavunja sheria kubwa ili wachukue rushwa, lakini machinjio ya kuku hawajali.
ReplyDeleteKwamba wanatoa viatu kwa vile wanaamini ndio usafi uliwauliza? Waislam wakichinja kuku wanatoa viatu regardless.
ReplyDeleteNa kuchinja kuku sita kwa mpigo ni pointless, sioni inahusiana vipi na usafi. Hukuwa na haja ya kutia tia chumvi nyingi, the picture was self-explanatory, kuweka kuku chini is bad enough, period.
Hii picha imeniacha hooiii sana!!! Ndo maana inabidi ununue kuku ukamchinje mwenyewe ktk mazingira uyapendayo wewe yaani kiusafi/kuvaa au kuvua viatu/kuvaa apron au kuka uchi..inakuwa juu yako wewe mwenyewe-amasivyo hiyo ndo hali halisi yenyewe...mmmmmmm makubwa hayo mwanangu..TZ tambarare..
ReplyDeletejamani hiyo balaa, lkn hapo kuna watu wanagombea kabisa hao viumbe na mtu akikosa anjilaumu mbaya mno!!
ReplyDeleteIts Neyma
KWA MNAOISHI KATIKATI YA JIJI HAPO NI PACHAFU LAKINI KWA TUNAOISHI USWAZI PANAFANANA NA TUNAKOISHI TOFAUTI NI KUWA HAPO HAKUNA VIROBA VYA VINYESI VYA BINAADAMU. UCHAFU NI JADI YETU, SOKO LABUGURUNI NI CHA KUPINDUKIA, TEMEKE VIVYOHIVYO NA MASOKO YOTE NI MACHAFU, LAKINI MADIWANI WA DAR AMBAO KARIBU WOTE NI WA CCM WANANG'AA WALIVYOTAKATA.
ReplyDeleteRafiki mbona unateleza, hivi umeshafikia umwinyi wa kuchinjiwa kuku! kwa familia yako umenunua sana ni kuku wawili, kuna haja ya kuchinjiwa kweli my friend?Labda ingekuwa zama zile unaitwa..... lakini Ahmed kuna haja ya kuchinjiwa kuku!
ReplyDeletendio mana wengine tunaenda sokon kuku mzima-mzima wambeba au unachinjiwa apo na mtu unamwona kwa ustaarabu na usafi wote!!
ReplyDeleteiki cha mtoto,machinjio ya ng'ombe na mbuzi (machinjioni)umefika wee annon?
mbpna utagairi kula nyama!!
usafi kwa mbongo F++
waliotumia msemo "ukimchunguza kuku utashindwa kumla" wamepotea kimaana ya msemo huu, ukimchunguza kuku alacho apitapo na alalapo na mengine afanyayo mwenyewe kuku, sio afikishwapo na binaadamu. mnadhani kuku kama angelikuwa na uwezo angelikubali kumalizia maisha yake sehemu kama hiyo?
ReplyDeletekumuelimisha mchangiaji wa May 19, 2009 6:28 AM, na wengine wote, kuvua viatu kwa waislamu wanapochinja hakumaanishi kuwa waislamu wanaruhusu uchafu kama huo uliopo kwenye picha. katika sheria za kiislamu unatakiwa mahali unapochinja pawe safi, na unavua viatu kwa heshima kwa kuwa wanatumia miguu yao kuzuia mabawa na miguu ya kuku wakati wa kuchinja. ni kuepuka israfu ya kukanyaga chakula kwa viatu. wanatakiwa kuchinja mmoja mmoja na kukosha kisu na mahali wanapomchinjia kabla ya kuchinja mwengine. kwa mantiki hiyo kama utaona kuwa picha hizo hazifati kabisa sheria za kiislamu.
ReplyDeletemtowa maoni wa May 19, 2009 6:28 AM, sijui kwa nini umeona umuhimu wa kutaja waislamu. hata hivyo nakukumbusha tu kuwa waislamu hawasimami wima wakichinja. wanamuweka kuku chini, wanamuelekeza kibla na kuinama kumchinja. tena wanachinja mmoja mmoja hadi akate roho na sio katakata kama msumeno.
ReplyDeleteNdiyo maana wengine huwa wananunua na kwenda kuchinja wenyewe ugumu upo wapi?
ReplyDeletewaislam..kibra
ReplyDeletenani kasema nenda machinjio yote uone km kuna izo sheria gani sijui mwataja apa
watu wamechoka kufata dini/sheria
ni hayo
mdau wa May 19, 2009 3:18 PM una akili finyu kweli au ni mdogo sana? hukuambiwa kama wanaochinja wanafata sheria za kiislamu au la, kilichosemwa ni kuwa sheria ya kiislamu ni kuelekea kibla. sasa hao wa machinjoni kama wanafata au hawafati sio kosa la dini ya kiislamu. wacha pumba na soma uzuri kinachoandikwa.
ReplyDeleteSijasema Waislam ni wachafu au sijui wanageukia kibla sijui wanachinja wameinama, wameinuka, wanasoma dua, I ain't said none of that.
ReplyDeleteNimesema, Waislam wakichinja kuku wanavua viatu, na kwamba mpiga picha asitudanganye, unless aliwauliuza wakamwambia, kwamba wanavua viatu kwa vile wanaamini ndio usafi. Nope. Ni dini. And as y'all saw them old folks got vibandiko in dey heads, ni Waislam na hivyo watavua viatu regardless.
Au Waislam huwa hawavui viatu wakichinja kuku?
Sisi ni wachafu kwa asili na tunaendekeza tabia hii kama tungekua hatutaki hali hii tungeweza kuikomesha mara moja kwa kususia kula vitoweo vinavyotoka maeneo kama hayo lakini.............!Ukipata muda tembelea jiko na choo cha hoteli unayo pata maakuli!
ReplyDeletemdau wa May 20, 2009 3:44 AM nakubaliana sana na points zako zote ila sikubaliani kuwa tu wamevaa vibandeko ndio u-conclude kuwa hao ni waislamu. kibandeko sio uislamu na kuna watu tele wanavaa vibandeko na sio waislamu. pia labda hivyo walivyovaa hapo ni vile vya kufata health and safety rules na ndio maana hata unaona wamevaa aproni. Nimesema labda kwa kuwa sina uhakika kama ambavyo wewe huna uhakika kama hao jamaa ni waislamu au sio.
ReplyDeleteanyway tusitoke sana kwenye point muhimu, nayo ni kuwa sehemu za machinjoni ni chafu na watu wa jiji ni lazima waliangalie suali hili haraka.
mr fish