Mheshimia habari za kazi,
Mimi nilikuwa mmoja kati ya abiria waliokuwa wakisafiri hivi karibuni toka Dar es salaam kuelekea Tanga, nilishangazwa baada ya basi tulilopanda kusimama ghafla baada ya kusafiri kwa masaa kadhaa.
Nilipohoji abiria mwenzangu akasema kuwa hivi ni kituo cha kwenda kujisaidia, kwa mshangao sikuona jengo lolote kama choo, ila kundi la watu wanawake kwa wanaume waliteremka ndani ya basi na kuingia mwituni kujisaidia, ama kuchimba dawa kama wenyewe ilivyosikia wakisema.
sasa mdau wangu, sijui serikali yetu hii tunayopiga kelele kila leo lina msaada gani kwa wananchi angalau hata vyoo vya kulipia katika vituo vya mabasi, maana wakati mwengine unaweza safiri na watoto au waja wazito ambao wanahitaji kutumia choo mara kwa mara.
si dhani ni jambo la busara kama ningesafiri na mama mkwe nianze kumtafutia kichaka ili ajisaidie kama picha inavyoonyesha
huyu naye??
ReplyDeletenani hajui mama mkwe huwa anachimba dawa...
KWA KWELI NI AIBU NA SI USTARABU UKIZINGATIA BAADA YA KUJISAIDIA HAKUNA HATA MMOJA AMBAYE ATANAWA AU KUSAFISHA MIKONO YAKE NA AMETOKA KUSHIKA NANII.
ReplyDeleteWalahi tena hii habari ya kupiga watu picha wakiwa wanachimba dawa, mtu utakujaoteshwa nundu bila sababu. Faraha yenyewe ya kuchimba dawa ndogo, tena mtu ufyatue foto, ohooo ho. Chondechonde, haya we.
ReplyDeletetatizo hakuna public toilet. msafara wa mkuu wenyewe huwa unasimama kwa ajili ya machimbo
ReplyDeleteardhi inaitaji kurutubishwa
ReplyDeleteJijini Dar kwenyewe vyoo hakuna ndio unategemea Serikali ijenge vyoo maporini?
ReplyDeleteWatu wengine bwana!
ReplyDeleteKwa maana hiyo unataka serikali ichimbe vyoo huko maporini! Kiazi Kweli! Kwanza kuchimba dawa huko porini ni faida pia kwa mazingira! Misitu inapata mbolea na baada ya decomposition ya hizo vitu, matokeo yake unapata nutrient recycling! Nakupa shule mwana jivi au urine ni baya tu linapokuwa katika mazingira anayoishi binadamu lakini likiwa huko porini hiyo ni mbolea!
Basi kama hivyo hata nguchiro, na mbweha,tembo, simba na nyani nao pia tuwachibie choo manake na wao wanachafua mazingira!!!
hata ukijenga vyoo, unadhani mtanzania atalipa ili apate pahala pa kufanya haja ndogo? jamaa watazunguka nyuma ya ukuta wa choo na kumaliza shuhuli zao :)
ReplyDeleteACHENI KUTETEA SERIKALI.MISAADA KIBAO INATOLEWA INAMANA HELA ZA KUIBIWA NA MAFISADI ZIPO LAKINI HELA ZA KUJENGA VYOO KWA RAIA KUSAIDIA AFYA ZAO HAKUNA? SIO LAZIMA VYOO VIWE VYA KULIPIA ,SERIKALI INAWEZA KUJENGA VYOO NA IKAAJILI MTU WA KUSAFISHA NA KULINDA CHOO HILI KIWE KATIKA HALI YA USAFI NA USALAMA KWA RAIA.AU NDIO BAJETI HAITOSHI KUTOA AJIRA KAMA HIZO LAKINI INATOSHA KUWAONGEZEA WABUNGE MISHAHARA?
ReplyDeleteHIVI VITU VIDOGO NA TUKIENDELEA KUTOA COMMENTS ZA AJABU AJABU NDIO TUTAENDELEA KUBAKI MIAKA NENDA RUDI TUNAKOJOA VICHOCHORONI NA KWENYE MISITU TUKIAMINI KWAMBA SERIKALI HAIWEZI KUJENGA VYOO AU MTANZANIA HAITAJI HUDUMA YA CHOO KWANI ANAWEZA KUJISAIDIA POPOTE PALE.
MDAU MZAWA
Vyoo ni muhimu jamani. miaka nenda rudi watu wanchimba dawa kila siku wanahama hama baada ya maeneo kuanza kunua. Fikiria mabsi ya kutoka mbeya, iringa, songea to Morogoro. Wote hawa wanachimba dawa. Serikali au watu wawekeza. Kila basi likisimama mwenye basi ndiyo analipa kwa ajili ya abiria wake. Inawezekana kabisa. Halafu watu hawanawi mikono. Kama umeharisha ndiyo basi tena.
ReplyDeleteNilipoenda Zimbabwe, basi likasimama na watu walienda kuchimba dawa porini, tena manyasi mafupi. Nilipoenda Jamaica, mkoani, basi ilisimama na watu walienda kwenye majani kuchimba dawa. Ndio Third World.
ReplyDeletembolea...
ReplyDeleteUnajua `tabia' za watu hazijifichi, `ubinafsi na choyo' zipo kwa kila mtu, ni swala la nani mwepesi wa kumuonyesha mwenzake.
ReplyDeleteKiongozi kama mtu mwingine anayo hiyo tabia. Kama yeye hawezi akakufikiria wewe kama hujifikirii mwenyewe. Kwanza ulipewa tiketi ya kumwezesha, ukamkabidhi yeye, manake unamwamini. Lakini kumwamini huko hakuwezi kumfanya yeye akajua kila kitu.
Maana yangu ni kuwa, hoja kama hizi tunazizarau, hatuwapi changamoto viongozi wetu,mfano, swala la usafi, wewe ukila ndizi, ukinywa maji unatupa takataka ovyo, kesho na keshokutwa unalalamika,mitaro imeziba, hukumbuki kuwa chanzo ni wewe. Hii yote ni ubinafsi.Unajifikiria mwenyewe, kukidhi haja yako, bila kufikiria wengine au madhara ya baadaye.
Unaona hoja za watu kuhusu swala hili la kuchimba dawa, wanaona ni mzaha, kwasababu yeye halimgusi. Lakini tukumbuke huko tunakochimba dawa huenda kuna watu wanaishi, wanawinda au wanapita. Fikiria ghafla anakutana na hicho ulichokiacha! Kuna kipindupindu nk.
Tabia zetu tukitaka ziwe safi tuwe kila tunachokifanya tunafikiria upande wa pili. Je nikifanya hivi hakitamuathiri mwingine.
Kuna umuhimu kwakweli kila kituo kuwe na vyoo, kila umbali fulani kuwa na namna ya kuhifadhi uchafu wetu, ili tusiathiri mazingira. Na hili tutaliweza kama kila viongozi wa maeneo wataanzisha harakati hizi. Inaweza ikawa mradi wa kijiji. Lakini nafikiri hata hili tunasubiri wafadhili, watusaidie.
M3
Mimi ningependa kuwashauri Madereva na hao makona...Waweke utaratibu kwani naamini ktka hizo njia wanazopita sio maporini tuu wanapita wanapita katika vijiji vya watu ktk stendi za mikoa za daladala..hivyo basi wasiwe wanasimamisha mabasi msituni kwani pia ni hatari pale ambapo mtu utajikuta unachimba dawa, wasimame sehemu za stand hata za daladala kwani kunavyoo vya kulipia watoe madakika kadhaa watu wajisaidie kisha waondoke...
ReplyDeleteKusimama simama njiani watu kuonesha sehemu nyeti wengine wako na watoto wao na wakwe zao ndio nini hivyo..Hasa wanaume anaweza akasimama umbali sio mrefu na basi lilipopaki yeye anamwaga supu tuu wakwe, wamama, watoto wanamtizama...Sio vizuri...Sio utamaduni wa Muafrika huuu...
Then tabia nyingine mimi naamini ni mtu kujiendekeza utakuta mtu anatoka Dar hadi Morogoro eti anasimama njiani kujisaidia...Kwanini watu kabla hamjaondoka msijisaidie then ujizuie hadi utakapofika???? Dar na Moro kuna umbali gani wa kushindwa kujizuia???? Kuna umbali gani wa wewe hadi kuanza kula kula na kunywa njiani hadi ipelekee wewe kusikia haja kubwa na ndogo???
Hali kadhalika Tanga na Dar hakuna umbali saana wa wewe kulaaa na kunywaa hadi usikie haja...Vumilia...Ukijenga tabia ya kuwa na muda wa kwenda chooni basi ndivyo mwili wako utakavyokuwa unafuata utaratibu huo...Usizoeshe mwili tabia za kwenda chooni ovyo ovyo na kula ovyo ovyo...
Miili ya wanyama wote tukiwemo sisi inatabia jinsi utakavyo izoesha ndivyo itakavyo kuwa..
Tufikikirie suala la kuwekewa public toilets nyingi ktk stand za mabasi makubwa/daladala kila mkoa / kila wilaya....tusifikirie kuwekewa public toilets misituni huo ni ulimbukeni..Sisi Watanzania tulivyo wastaarabu je kwa wale wenyekuchafua kwa kuacha mzigo pembeni ya choo na wasio flash/mwagia maji mizigo yao itakuwaje...Atakayeshughulikia choo kiwe kisafi huko misituni atakuwa nani.....TUNAIOMBA SERIKALI ISAIDIE VYOO VISHUGHULIKIWE KUJENGWA KTKA VITUO VYA MABASI/ MIJINI ambapo panaweza kuajiriwa watu wa kusafisha na mahali ambapo kako busy patakuwa na wateja wa kulipia wa kutosha wakiwemo pia wasafiri ili choo kiweze kujiendesha na kulipa mshahara wa msafishaji chenyewe na kununua dawa chenyewe. Wenye mabasi pia wawe wanatumia vyoo hivyo...
ReplyDeleteMmmmmh!!! Halafu unasimama porini unashika sehemu zako nyeti supu supu zinakudondokea then unarudi zako mambo swaaafi ktka basi unanunua chakula unakula haunawi hata mikono na pia kusalimiana au kumpa mtu kitu...Aisee WaTZ...Bacteria wa afya tunawependaga wenyewe inaonyesha..
ReplyDeleteNa wale wenzangu wa kushusha mzigo then kufuta na majani na makaratasi mpoooooo???? Je mnanawaaaa mtokapo porini????
Ipo siku mtu atajifutia majani ya kuwasha aka UPUPU or NDAFII ndipo atakoma
mkuu nakupongeza kwa kazi nzuli kuhusu kuchimba dawa wenye mabasi pia ndio wanatakiwa kuweka vyoo kwenye mabasi mbona huku ulaya mabasi yanavyoo ndani sioni kwanini ya bongo awawezi kuweka msilaumu selikali kila kitu huu ni ujinga kila kitu selikali uchafu pia ni selikali ? angalia mazingira dar es salaam yanasikitisha tuache uchafu jamani wabongo sio kila kitu selikali
ReplyDeleteUnashangaa nini?? Hii ndo bongoland
ReplyDeleteKWAHIO DADA CHEMI NA WEWE UKAENDA KUCHIMBA DAWA KWENYE NYASI FUPI? AU ILIKUA OK KWA VILE ULLIKUWA NA SANITIZER? KUWA THIRD WORLD COUNTRIES ISIMAANISHE VITU VIDOGO KAMA HIVI TUVIZARAU.MAGONJWA MENGI HAKUNA SABABU BINADAMU KUPOTEZA MAISHA KWA UGONJWA WA KIPINDU PINDU KWA VILE NI 3RD WORLD COUNTRY.MAMBO MENGINE YANAWEZA KUTATULIWA SEMA KWA VILE SISI RAIAI WENYEWE TUNAONA NI SAWA TU HAMNA TATIZO KUJISAIDIA VICHOCHORONI NA MISITUNI NDIO MAANA HATA VIONGOZI HAWAJALI PIA.SERIKALI KUJENGA VYOO NDIO KUTOA AJIRA YENYEWE HAPO JAMANI.
ReplyDeleteHuyo Dreva na Konda wake ndio wazembe na wachafu. Mabasi mengi ya kwenda Tanga yanasimama kwenye mahoteli na abiria wanapata nafasi ya kujisaidia na kupata chochote kama soda nk. Hiyo kampuni ya basi hilo inapaswa kushitakiwa kwa uchafuzi wa mazingira na kukiuka sheria inayowataka wasafirishaji kusimamisha basi mahali penye huduma za jamii
ReplyDeleteKaka hayo ndio mazingira tuliokulia na tunaendelea nayo, tusiwe na kashfa kwa sababu tunaishi katika nchi za watu, pia kaka sio ustaarabu katika mazingira kama yale kuchukua picha, au kuishi nje ndio kunawafanya wabongo wote wajinga? kumbuka ulikotoka na ujifunze ustaarabu
ReplyDelete