Miezi,wiki na sasa zimebaki,siku na saa kadhaa ile MEMORIAL REUNION ya Wabongo itakayo wakutanisha Wabongo kutoka sehemu mbali mbali hapa,Marekani,Canada na kungineko duniani,itakayofanyika kwa mara ya kwanza Washington Dc  kuanzia may 22 na kuhitimishwa may 24
 
Kutakuwa na Mechi ya mpira wa miguu inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa kabumbu kati ya Bongo United Fc v/s Houston stars itakayochezwa,jumamosi may 23 kwenye viwanja Fairland Recreation Park,Greencastle Rd.mechi hii ni kiporo ya mechi iliyochezwa Houston mwaka jana Thanksgiving na timu hizi zilitoka sare ya 3-3 baada mechi kuchezwa dakika 120.
 
Mechi inatarajiwa kuwa ngumu ingawa kila upande unadai ushindi,mbali na mechi hii ya mpira wa miguu,kutakua na mpira wa kikapu,Pazi,Vijana na Don Bosco,Nyama choma.
 
Karibuni sana Wabongo wote popote pale mlipo,hii Reunion sio ya kuhadithiwa,jaribu kila uwezalo na wewe uwe mmoja ya wale watakao hadithia,hii reunion ya Wabongo ya kwanza na ya aina yake,fika ukutane na rafiki yako wa siku nyingi.
 
Kama maelezo zaidi kama hotels,address za wapi maraha,starehe na mambo yasiokua ya lazima,sehemu za michezo na nyama choma,Direction na makadhalika pliz visit 
www.wabongoreuniondc.com 
au piga simu 
240 441 2380,
240 715 2077,
301 300 2742

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2009

    Kueni mtunze watoto wenu. Kila siku ni party party. Hivi hamjui mnazeeka. Kama hukutanua ukiwa kijana basi tena. Hamwoni aibu na umri wenu huo?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2009

    watoto pia wanakutana na wototo wenzao kaka tuli

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2009

    HUU UPUMBAVU TULIUFANYA ZAMANI SASA NI MUDA WA KUANGALIA MAENDELEO SIO PARTY TU.HAKUNA LA MAANA NI UPUUZI MPUTU. KALAGABAHO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...