
CHINI KULIA ANGALIA TARAKIMU HIZO. IKIFIKA 6,000,000 TU WAKATI UPO HEWANI BASI WEWE NDIYE MSHINDI. KATIKA KOPMYUTA YAKO PALE JUU PANA KIDUDE KIMEANDIKWA 'Prt Sc Sys Rq' AMBACH UTAKIBOFYA; KISHA NENDA 'START' KISHA TAFUTA 'PAINT' KWENYE 'ACCESSORIES' AMBAPO BAADA YA HAPO UTARUDI KWENYE 'EDIT' BOFYA 'PASTE' NA KISHA 'SAVE'. KITU NA BOXI! HUO UKURASA UNA-ATTACH KWENYE EMAIL YAKO NA KUTUMA. MAMBO KWISHNEY! SI VIBAYA UKAANZA TIZI LA NAMNA YA KUFANYA HIVYO SASA KWANI SAFARI HII TASWIRA YA AINA YOYOTE HAITOKUBALIWA....
WADAU WAPENDWA,
NACHUKUA NAFASI HII KUWAKUMBUSHA KWAMBA MDAU WA MILIONI 6 ANAKARIBIA NA INSHAAAAAAALLAH PANAPO MAJAALIWA MFADHILI ATAPATIKANA KARIBUNI NA KUTOA DONGE NONO KWA MSHINDI.
KWA SASA NAOMBA NISIMTAJE HUYO MFADHILI WALA ZAWADI NONO AMBAYO AMEAHIDI KUTOA. ILA KWA SASA NAOMBA NIWAHAKIKISHIE KWAMBA AMEPATIKANA MFADHILI MMOJA NA KWAMBA YUKO TAYARI KUZIDISHA DAU LA SAFARI HII NA HUENDA LIKAZIDI LILE LA KAWAIDA LA DOLA 500 KWA MSHINDI. HIVYO KAENI MKAO WA KULA.
WADAU WENGI WAMEKUWA WAKIULIZA MDAU WA MILIONI 6 ANAPATIKANA VIPI; NI SIMPO SANA. WEWE ENDELEA KUPERUZI GLOBU YA JAMII KILA MARA HUKU UKITUPIA JICHO UPANDE WA KULIA KULE CHINI KABISA NA ANGALIA TARAKIMU. ZIKIGOTA 6,000,000 WAKATI WEWE UPO KATIKA LIBENEKE, BASI UJUE UMEULA. TUMA HUO UKURASA KWA ANUANI YA EMAIL YA issamichuzi@gmail.com
NA MAMBO YOTE YATAKUWA MSWANO KWANI WEWE NDIYE UTAYEKUWA MSHINDI.
KANYABOYA AMA KUUZIANA MBUZI KWENYE GUNIA SIO TU HAIRUHUSIWI BALI PIA HAITOFUA DAFU MAANA JOPO LA MAJAJI NA BATALIONI YA MAFUNDI MCHUINDO WAKO TAYARI KUCHEZA NAZO. HIVYO USIJISUMBUE KUGHUSHI KWA KUINGIZA INGIZO SILO, KWANI HAUTAONA MWANGA WA JUA NA UTAISHIA KULALAMA KAMA PAPA AMA NYANGUMI WA NCHI KAVU.
-MICHUZI
sawa,kaka michuzi twasubiri.
ReplyDeletemimi ni msomaji mkuu wa blog hii. ninaamini nina mchango mkubwa sana wa mawazo yanayoweza kuikwamua taifa letu. tatizo ni kutoijua teknolojia hii ninayoweza kuniunganisha na watanzania wenzangu duniani kote. si mimi peke yangu, tuko wengi. tunaomba utupe maelekezo ya jinsi ya kutoa maoni yetu.
ReplyDeletetuko pamoja kaka michuzi
ReplyDeleteusanii mwengine unakuja huo.
ReplyDeletemichuzi eeh, icho kidubwasha kilichoandikwa sijui prt sc sys mi sikioni, ebu tuelekezane vyema, si unajua tena mashikoro haya!
ReplyDeletemheshimiwa naomba link ya mwimbo wa mwasinti nalivua pendo kwenye yotube tafadhali tuko mbali na nyumbani.
ReplyDeleteMmmhh hapa sijui kama ufisadi hautahusika!! any way shida yangu naombeni tu mniambie hiyo kitufe ya prt sc sys ipo wapi!!!! mi natumia internet explore as web browser
ReplyDeletenkya
a-town
Michuzi
ReplyDeleteHaya mambo ya kuwa mtu wa 6M hayana maana kama huduma unayotoa kwenye blog hii ya jamii. Lete vitu achana na DECI za kimawazo ama upatu wa Mengi na Manji bwana!
wewe ni mtaaluma fanya taaluma
naomba niulize wadau au michuzi mwenyewe.Kwani kuna vigezo gani vyakumpata huyo mshindi wa M6
ReplyDeletekigezo lazima uwe mtoto wa fisadi..ukiwa fisadi nyangumi au papa hupati kitu!
ReplyDeletendivyo nilivyoelewa toka kwa kamisaa Michuzi
Mimi sio mtoto wa Papa wala nyangumi..mimi mtoto wa sisimizi kila mmoja ananionea. Mimi nikichangia maoni nikiweka jina langu sijui inakuwaje sioni Michuzi ukizitoa hadi nikaamua kutoa maoni bila kuweka jina ndio nikawa nayaona. Je mimi unanichukulia vipi na mimi ni mchangiaji mada kila mara katika blog yako? Au itakuwa ndio vile vile kuzidi kuonewa?
ReplyDeleteHakika ni vuna vuna...tunatafuta weeee hicho kitufe cha prt sc sys..hatukioni...Tufanyie upendeleo basi uikuze hicho kitufe tukione au tuelekeze vizuri..
ReplyDelete