CHINI KULIA ANGALIA TARAKIMU HIZO. IKIFIKA 6,000,000 TU  WAKATI UPO HEWANI BASI WEWE NDIYE MSHINDI. KATIKA KOPMYUTA YAKO PALE JUU PANA KIDUDE KIMEANDIKWA 'Prt Sc Sys Rq' AMBACH UTAKIBOFYA;  KISHA  NENDA 'START' KISHA TAFUTA 'PAINT' KWENYE 'ACCESSORIES' AMBAPO BAADA YA HAPO UTARUDI KWENYE  'EDIT' BOFYA 'PASTE' NA KISHA 'SAVE'. KITU NA BOXI! HUO UKURASA UNA-ATTACH KWENYE EMAIL YAKO NA KUTUMA. MAMBO KWISHNEY! SI VIBAYA UKAANZA TIZI LA NAMNA YA KUFANYA HIVYO SASA KWANI SAFARI HII TASWIRA YA AINA YOYOTE HAITOKUBALIWA....

WADAU WAPENDWA,

NACHUKUA NAFASI HII KUWAKUMBUSHA KWAMBA MDAU WA MILIONI 6 ANAKARIBIA NA INSHAAAAAAALLAH PANAPO MAJAALIWA MFADHILI ATAPATIKANA KARIBUNI NA KUTOA DONGE NONO KWA MSHINDI.

 KWA SASA NAOMBA NISIMTAJE HUYO MFADHILI WALA ZAWADI NONO AMBAYO AMEAHIDI KUTOA.  ILA KWA SASA  NAOMBA NIWAHAKIKISHIE KWAMBA AMEPATIKANA MFADHILI MMOJA NA KWAMBA YUKO TAYARI KUZIDISHA DAU LA SAFARI HII  NA HUENDA LIKAZIDI LILE LA KAWAIDA LA DOLA 500 KWA MSHINDI. HIVYO KAENI MKAO WA KULA.

WADAU WENGI WAMEKUWA WAKIULIZA MDAU WA MILIONI 6 ANAPATIKANA VIPI; NI SIMPO SANA. WEWE ENDELEA KUPERUZI GLOBU YA JAMII KILA MARA HUKU UKITUPIA JICHO UPANDE WA KULIA KULE CHINI KABISA NA ANGALIA TARAKIMU. ZIKIGOTA 6,000,000 WAKATI WEWE UPO KATIKA LIBENEKE, BASI UJUE UMEULA. TUMA HUO UKURASA KWA ANUANI YA EMAIL YA issamichuzi@gmail.com 
NA MAMBO YOTE YATAKUWA MSWANO KWANI WEWE NDIYE UTAYEKUWA MSHINDI.

KANYABOYA AMA KUUZIANA MBUZI KWENYE GUNIA  SIO TU HAIRUHUSIWI  BALI PIA HAITOFUA DAFU MAANA JOPO LA MAJAJI NA BATALIONI YA MAFUNDI MCHUINDO WAKO TAYARI KUCHEZA NAZO. HIVYO USIJISUMBUE KUGHUSHI KWA KUINGIZA  INGIZO SILO, KWANI HAUTAONA MWANGA WA JUA NA UTAISHIA KULALAMA KAMA PAPA AMA NYANGUMI WA NCHI KAVU.

-MICHUZI


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. BajunGirlMay 06, 2009

    sawa,kaka michuzi twasubiri.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2009

    mimi ni msomaji mkuu wa blog hii. ninaamini nina mchango mkubwa sana wa mawazo yanayoweza kuikwamua taifa letu. tatizo ni kutoijua teknolojia hii ninayoweza kuniunganisha na watanzania wenzangu duniani kote. si mimi peke yangu, tuko wengi. tunaomba utupe maelekezo ya jinsi ya kutoa maoni yetu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2009

    tuko pamoja kaka michuzi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2009

    usanii mwengine unakuja huo.

    ReplyDelete
  5. Mdau, OmanMay 06, 2009

    michuzi eeh, icho kidubwasha kilichoandikwa sijui prt sc sys mi sikioni, ebu tuelekezane vyema, si unajua tena mashikoro haya!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2009

    mheshimiwa naomba link ya mwimbo wa mwasinti nalivua pendo kwenye yotube tafadhali tuko mbali na nyumbani.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2009

    Mmmhh hapa sijui kama ufisadi hautahusika!! any way shida yangu naombeni tu mniambie hiyo kitufe ya prt sc sys ipo wapi!!!! mi natumia internet explore as web browser

    nkya
    a-town

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 06, 2009

    Michuzi
    Haya mambo ya kuwa mtu wa 6M hayana maana kama huduma unayotoa kwenye blog hii ya jamii. Lete vitu achana na DECI za kimawazo ama upatu wa Mengi na Manji bwana!
    wewe ni mtaaluma fanya taaluma

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 06, 2009

    naomba niulize wadau au michuzi mwenyewe.Kwani kuna vigezo gani vyakumpata huyo mshindi wa M6

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 06, 2009

    kigezo lazima uwe mtoto wa fisadi..ukiwa fisadi nyangumi au papa hupati kitu!
    ndivyo nilivyoelewa toka kwa kamisaa Michuzi

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 08, 2009

    Mimi sio mtoto wa Papa wala nyangumi..mimi mtoto wa sisimizi kila mmoja ananionea. Mimi nikichangia maoni nikiweka jina langu sijui inakuwaje sioni Michuzi ukizitoa hadi nikaamua kutoa maoni bila kuweka jina ndio nikawa nayaona. Je mimi unanichukulia vipi na mimi ni mchangiaji mada kila mara katika blog yako? Au itakuwa ndio vile vile kuzidi kuonewa?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 08, 2009

    Hakika ni vuna vuna...tunatafuta weeee hicho kitufe cha prt sc sys..hatukioni...Tufanyie upendeleo basi uikuze hicho kitufe tukione au tuelekeze vizuri..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...