Home
Unlabelled
PSI kuzindua ATM za kondomu wiki ijayo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
RUKSA KWA MAANA UCHANGU DOA
ReplyDeleteKIMTINO PIA RUKSA MAANA CONDOM
SI ZIPO BWELELEEE
Kaka si vibaya kukosoana hiyo sio ATM inaitwa condom vending machine labda kama ulikuwa unatumia lugha zako za siku zote za utani kama badala ya blog unasema glob ni hayo tu
ReplyDeleteSawa ila kuweka na kuangalia ili zisiwekwe ambazo hata muda wa matumizi umekwisha, maana tunaongoza kwa kuweka mambo ila hatuna uangalizi wowote
ReplyDeleteWaafrica haswa Watanzania sijui mtajua kujiheshimu lini.huwa mnajifanya kutangaza sana hizi condom nyie wenyewe hamtumii na mnasambaza magonjwa mnategemea wenzenu ndio watumie.
ReplyDeleteKujitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mmeathirika sana kama vile ni sifa unatuharibia jina sana duniani.Mbona ulaya watu wana kufa kwa HIV/AIDS lakini huwezikuta wanajitangaza kuwa wao wanaongoza.Elimisheni watu wa hapo nchini sio kwa kujitangaza watu tunaogopeka duniani.{MDAU}
Kama tukiwa na fikra kama za mchangiaji wa mwanzo sidhani kama Watanzania tutakuja endelea, angalia ndugu yangu kwa wenzetu hizo vending machine ziko toilets especially za kike na kuna condom za aina zote, sasa wewe unaposema eti ooh ukimwi hautaisha, kwani sababu ya kuwekwa hizo machine ili watu waambukizane ukimwi? Tupo kwa ajili ya kuambiana ukweli kama mtu anatoa maoni ambayo hayana msingi wowote. Hebu fikiria hivi kwanza: Kuna watu wanashindwa kununua condom kwa aibu na wengine wanashindwa kutumia condom kwa sababu maduka yanakuwa yamefungwa, sasa kukiwa na hizo machines hopeful zitakuwa sehemu nzuri na ambayo mtu anaweza pata huduma anapohitaji. Tuangalie vya kuchangia jamani manake sasa imezidi!
ReplyDeleteTanzanians we are geting lost, even in America where I lives, I never seen such a vending machines. this is gona catalize fonication to many include young kids. Guys we better do some moves to stop that. lazima kuna mafisadi wanakula cha ju hapo.
ReplyDeletemkereketwa
Kaka hizo ATM zako labda waweke ndani ya vyoo vya mahoteli, lakini wakiweka sehemu za wazi hawampati mtu.
ReplyDeleteNani anaependa kuwangiwa?
We imajin ndo hiyo ATM iko pale NBC Posta au pale Posta Mpya!
Khaa!
This is keeeewwwlllll!!!i just need to know hizi vending machines i hope ziko toilet and not just any coridors eyyy!!ARE THEY flavoured??naomba kwa msisitizo waziweke sana hapo kempinski dar!
ReplyDeleteWe anonymous wa 2:49 AM si lazima uandike Kingereza ilhal grammatically uko ICU, maana duh! Even in America where I LIVES, I never seen such A VENDING MACHINES! wacha weeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
ReplyDeleteKwendeni zenu msilete mambo ya itikadi kali hapa, wengi wetu tunaona aibu kununua kondomu pharmacy au supermarket hasa panapokuwa na mwanamama wa makamo kama cashier this is a gd thing tena ziwekwe vyooni kwenye mabaa na pubs!
ReplyDeleteooooh mwenyezi ooooh tuepushe na huu ufilauni
ReplyDeletemtaziweka wapi???
watu kwanza hawazipendi/hawatumii
heeeeeeeee!!!
ReplyDeleteupupu...shenzy
ReplyDeleteWANAPOTEZA MUDA..how can you eat a sweet with its cover,its not a raining season so i dont need a raincoat watsoever.lol
ReplyDeleteAnony 2:49 AM, May 15th
ReplyDeleteKama unataka kuwadanganya watu, jaribu kutumia lugha unayoijua. Hupo Marekani bali Gongo la Mboto, Dar. kwa kuwa siku hizi Internet cafe ziko kila kona ya Mji, usijitie kuw a umepanchi. Wewe bado mchovu, na sisi huku Ulaya bado tutatesa sana.
Kama unahitaji kusaidiwa na Kiingereza, uliza waliosoma au utaibika.
Ni msaada mzuri kwa wanojali afya zao. Ni vizuri machine ziwekwe vyooni kwa ajili ya privacy.
ReplyDeleteWatanzania muwe wenye kupenda kuelimika hii ni changamoto ya kupambana na ukimwi. Kwa wenye akili timamu hawatojali mwenye kampuni anatumia kifaa au hatumii bali ataangalia uhitaji wake wa kifaa hicho.
Hapa kuna mawili tu either kuacha uasherati au kutumia kifaa. Hizi machine zitawasaidia sana wastaarabu wanaojali afya zao.
Hizo nchi za nje zinazosemekana kuwa hakuna machine za condom ni zipi? tuongee kwa ushahidi, kuna maeneo maalum ktk nchi hizi ambayo machine za pads za wanawake pamoja na condom zinapatika. Na isitoshe condom zinapatikana ktk kila surgery (zahanati) na hizi zahanati ziko kwenye maeneo yote ya makazi ya watu, hivyo mtu unapohitaji, ni kiasi cha kwenda dirishani kuomba na huwa zinagawiwa kwa wingi za kukutosha kwa kipindi unachotaka.
Hakuna machine za condom kwa sababu condom ziko available na wenzetu hawana tabia za kushangaana katika vitu vya kimaendeleo.
Naomba tuchangie hoja kimaendeleo ili tuwasaidie ndugu zetu wengine kama siss tumeshakata tamaa.
Swala hapa ni wapi ziwekwe na si kwamba hazitapata wateja.
Huu ni wizi mtupu.Kwanza mnachochoea uzinziiiiiiiiiiii. Kutuletea hizo ITM za kondomu kwanini msituletee ITM za kuwafichua mapapa na manyangumi.
ReplyDeleteAlaah kumbe nimegundua aliyemuwasha mzee Mwinyi Kibao alikuwa sahihi.
Habari ndio hiyo.
BRO MICHU NAULIZA HIVI ILISUALA WAKUU WA NCHI WANALIJUA JAMANIII NAONA SASA HATA WASIOTAKA KUZINI WATAHITAJI KUZINI NA NCHI YETU SIJUI KAMA ITAENDELEA.JAMANI SIKILA WANACHO KISEMA WAZUNGU NDO KIZURİ,FIKIRI BRO MICHU KAMA HIZI MASHINE ZITAFUNGWA MPAKA VIJIJI JAMANI WATU WATAMALIKA KWA UKIMWI JAMANII,Mdau Dr
ReplyDeleteMI SASA NATAKA NIMSIKIE KIONGOZI YOYOTE AROPOKE KUWA TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA!!!
ReplyDeleteWENZETU WAMEIGA MAMBO YA MAANA NA SASA WAMEENDELEA KIUCHUMI NA KIJAMII.
SISI HUKO, SHOMBO TUPU, VIONGOZI NYAMAFU KABISA, KAZI TU KUIIBIA NCHI WAKISHINDWA KUISAIDIA JAMII DHIDI YA MAAFA!
UKIMWI NI MAAFA NAMBARI MOJA HASA HUKO KATIKA ULIMWENGU WA TATU, NA UNAMALIZA WATU HASA!
HUKU ULAYA HATA HUWASIKII TENA WAKIUZUNGUMZIA, SABABU HAWAJALI TENA NA WAMESHINDWA KUUDHIBITI!
INABIDI KILA MTU AJICHUNGE MWENYEWE!
HUKO SASA WANAKULETEENI BIASHARA YA MIPIRA, SASA IUZWE KIHOLELA. NANI ATAHAKIKISHA UBORA WAKE KAMA HAIPASUKI MTU AKIWA KARIBU NA KUPIGA GOLI?
AU MMESHASAHAU JINSI BIDHAA FEKI ZILIVYOZAGAA MITAANI? NANI ATAKUHAKIKISHIENI UBORA WA KONDOMU ZITAZOUZWA?
MAANA HAPA UK PAKITI YA MIPIRA 12 INAFIKA MPAKA £9, HUKO MTAUZIANAJE?
SASA ZIKISHALETWA HIZO MASHINE, MHESHIMIWA RAISI TUTAMWOMBA BAADA YA MWAKA MMOJA AADHIMISHE FAIDA YAKE KITAIFA DESEMBA 1 KWA KUTOA TAKWIMU MPYA ZA UENEA KWA UKIMWI.
JAMAA WABONGO MPAKA LINI NYINYI MTAACHA KUIGA HATA YASIYOFAA KUIGWA?
JAMAA MSIPOKUWA MAKINI BONGO ITATEKETEZWA KWA LAANA YA NGONO SI MUDA MREFU UJAO.
MUNGU ATULINDE, Amin.
Mndengereko, Ukerewe
Am kweli kila mtu na macho yake! nyinyi imeshikilia ATM mimi macho yangu yametua kwa huyo dada! du jamani kuna mtu ana email? michuzi vipi?
ReplyDelete