wananchi wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali kuunga juhuhudi za kupiga vita matumizi ya tumbaku duniani katika sherehe zilizofanyika jana kitaifa eneo la Horiri – Rombo mkoani Kilimanjaro mpakani mwa Kenya na Tanzania.
wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali kuunga juhuhudi za kupiga vita matumizi ya tumbaku duniani katika sherehe zilizofanyika jana kitaifa eneo la Horiri – Rombo mkoani Kilimanjaro mpakani mwa Kenya na Tanzania.

Mwanafunzi wa shule ya msingi Gunule ambayo iko Horiri wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro Twaha Bakari akiwa amebeba bango lenye ujumbe wa kupiga vita matumizi ya tumbaku katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kuttotumia tumbaku duniani

wahudhuriaji kwenye sherehe hizo
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya Kutotumia tumbaku duniani wakifuatilia kwa makini ngoma na michezo mbalimbali iliyokuwa ikionyeshwa katika viwanja vya Horiri wilayani Rombo –Kilimanjaro.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2009

    I think we should raise taxes on Bia na Sigara! Thats the only way kupunguza namba ya watumiaji tumbaku na walevi. Yaani sales tax ya hivyo vitu iwe 50%.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2009

    Natamani watu waandamane namna hii kupinga ufisadi!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2009

    mambo ya kuiga tu. Tanzania tuna matatizo mengi ya kushughulikia siyo kuacha kuvuta tumbaku. Na wale ndugu walima tumbaku kule Namtumbo mtawasaidiaje watu wakiacha kuvuta tumbaku?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2009

    kuna umuhimu gani wa kuwatumia wanafunzi katika maandamano haya?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2009

    Wewe unaesema vita hivi ni vya kuiga ni mbumbumbu ! Unajua matatizo mangapi tuliyonayo yanasababishwa na utumiaji tumbaku ? Fuatilia vizuri ujue serikali inatumia mamiliono mangapi kutibu wagonjwa wanaotokana na matumizi ya tumbaku.Unajua watoto wanavyoathiriwa na asma, na magonjwa mengine ?

    Fuatilia ujue hali za kiafya wa hao waliopo Namtumbo,au wale kule iringa wanaolima tumbaku, na uone pia jinsi gani wananyonywa ! Wanaofaidika ni wengine...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2009

    Nyie mnaosema wanaandamana kwa nini na kwanini wantumia wanafunzi. Hivi mnajua madhara ya second smoking. Watoto wengi bongo mapafu yao kama ya wazee kumbe wanishi na watu wnaovuta sigara kutwa kucha

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2009

    kama serikali inaona uvutaji una madhara kwa binadamu basi ipige marufuku na iache siasa zake.
    kila siku utasikia serikali inatumia gharama nyingi kutibu. uwingi wa gharama sio kigezo ingesema inapata hasara tungeielewa. ifanye hivii ichukue pato litokanalo na tumbaku itoe hizo gharama then ituambie hiyo balance ni nini... iache kupiga kelele
    ingefanya kama alivyofanya Maximo kwangu mimi Chuji, Bobani na master Kaseja hapo ingeeleweka msimamo wake

    Chuji
    Ilala

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2009

    NANI KASEMA.....NYOOOOO. YAANI NIACHE KUBWILA TUMBAKU LANGU AAAAAAAAAACHOOOO AH! NGOJA NIANZE UPYA.
    YAANI NI...AAAAACHOOOOOOO. HUU UGOLO KIBOKO WA MZEE KITUMBO.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 01, 2009

    Yote Tisa spelling mistake kwenye bango ...'wolrd'..badala ya 'world' ....kwenye bango -(picha ya kwanza).... du! inabidi wakasome waelimike kabla ya kwenda kwenye maandamano,- ...hivi hawa walimaliza primary school?.... manake hizi spelling exercise ni za darasa la 2..!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 02, 2009

    Kwanini watu waandamane ili watu waache kutumia tumbaku ilihali serikali bado inasisitiza zao la tumbaku, dawa ni KUWACHA KULIMA TUMBAKU halafu tuone kama watu watatumia tumbaku.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 02, 2009

    Kumbe ilikuwa WOLRD NO SMOKING DAY pia? I thought it was just WORLD NO SMOKING DAY!!!!!

    Mdau, Boston, US

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 02, 2009

    namuona Lemunge, Arawa, shirima na Laswai....wanarepresent Rombo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...