KUNA HABARI KWAMBA HUKU KWETU TEGETA KUNA KIZAAZAA CHA AINA YAKE.

 UVUMI UMEENEA KWAMBA KATIKA ZOO ILIYOKO HUKU SIMBA WAWILI WAMETOWEKA NA HAWAJULIKANI WALIPO. 

NIKIWA MKUU WA HII NANIHII NAFANYA JITIHADA ZA KUPATA UKWELI WA HABARI HII NA KAMA NI KWELI NIJIUNGE KATIKA MSAKO. 

DAH! UKUBWA NAO SAA INGINE BALAA. MAANA WENZETU WAMEATHIRIKA NA MABOMU, SIE SIMBA!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2009

    JANA JUMATANO USIKU NILIKUWA NIKIANGALIA LUNINGA KWA BAHATI NZURI UKAONESHWA MKUTANO WA KAMPENI YA CCM NA MHE. MALECELA AKIHUTUBIA, HAMADI! LIKAPITA GARI LA CUF, DUH! WANANCHI WAKAACHA KUMSIKILIZA MALECELA NA KUANZA KULIFUATA GARI LA CUF HUKU WAKISHANGILIA JAMBO LILILOMFADHAISHA SANA MHE. JOHN. SASA TAMBWE NA MWENZAKO KAZI KWENU KANUSHENI NA HILO MDAI KUWA MWANDISHI ALIPANDIKIZA PICHA MBILI, HII SI NDIYO KAZI YA PROPAGANDA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2009

    kaka michu acha kuturusha roho watu wa tegeta na mbezi, nasikia sasa hivi mbagala nyumba unaweza kununua hata kwa milioni moja tu, sasa kama huku kwetu kuna simba basi wasipopatikana hata bure utapata nyumba ya nguvu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2009

    we hapo juu una matatizo ya akuli mkuu wa wilaya ya kwetu huku kaleta taarifa za kuogofya wewe unatuletea mambo ya siasa we vipi?inaonekana nyinyi ndio mnaoshinda vijiweni kuhubiri siasa badala ya kufanya kazi..kutoroka kwa simba na huo upuuzi unaotuletea ni tofauti..nakupa pole sio muda wote tunajadili siasa...we wa wapi!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 14, 2009

    Mimi pia ni mkazi wa tegeta na nimesikia hizo habari. Anayejua ukweli wa hili swala tunaomba atuhakikishie ili tufahamu ukweli.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 14, 2009

    Vita ni vita. Wewe mzee wa nanihii unaenda huko ujashabaa au ujapeleka tu na hizo camera zako???Hebu jitulize ungojee taarifa bado tunakuhitaji....Au umesomea mgambo?? Ungeenda manyara kwanza kufanya mazoezi ndipo uende kuwasaka la sivyo jitulize tuu waache wataalamu wa shughuli hiyo waende au nenda nao ila uwe close na mwenye shaba usijetupa camera zako..
    Pia huu ulioutoa kaka ni mchango mmojawapo katika jamii kujulisha umma kuwa kunatukio la namna hii kwani najua watu wengi huangalia blog yako...

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 14, 2009

    T he t he t he Tegeta upo mwaka huu!!!! No comment, Close my mouth. Pole sana kama uko huko. nenda kikamilifu kama huko usije ukiwa huna camera wala mkono. Nawasikitikia watoto tuu huko bora hata watu wazima kdg lkn watoto hata kujitahidi kujiokoa hawawazi. Wazazi kuweni makini na watoto jamani. Mzazi mlinde mwana wa mwenzio mfanye kama wako. (Mwana wa mwenzio ni wako). Jamii za huko ambazo hazipati huduma za blog zifikishiwe taarifa haraka waweze kuwa makini laa sivyo majanga mengine yatatokea/

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 14, 2009

    HILI NILIJUA NI BOMU LINAALONGOJEA KULIPA,HII SI ZOO NI JUST HOLDING GROUND KWA AJIRI YA EXPORT,LAKINI INASHANGAZA HATA HIYO WIZARA IMETOAJE KIBALI CHA ZOO KWENYE MAKAZI YA WATU,KIBAYA ZAIDI MMILIKI WA HII ZOO FEKI YAELEKEA KULISHA KUNAMSHINDA WANYAMA WANAKUFA SANA NA WIKI ILIYOPITA FISI HAPA WALITOROKA WAKAUWAWA ,WATU WAMEKAA KIMYA,HUU NI UFISADI WA KUWAPA WATU LESENI KWENYE MAZINGIRA YA KUTISHA WAKATI PALE HAPAFAI KABISA KWASABAU IMEZUNGUKWA NA MAKAZI YA WATU,TUNAOMBA SERIKALI IFUTILIE MBALI HII ZO FEKI NI HATARI KWA MAISHA YA WATU NA NI HATARI KWA WANYAMA WANAOKUFA BORA WARUDISHWE KWENYE MAZINGIRA YAO

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 14, 2009

    Habari hii imekanushwa jana na wahusika wa zoo hiyo kupitia TBC1 na tumeonyeshwa simba 2 wakiwa katika banda wamefungiwa

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 14, 2009

    Huyo alieyeandika mambo ya siasa nadhani ana matatizo.
    Mimi ni mkazi wa Tegeta na nimeshahoji sana mtu kupewa kibali cha zoo ktkt makazi ya raia.
    Jana tumelala kwa hofu ukizingatia mie ni jirani na zoo.
    Yaani tangu mwenye nchi hii aondoke,matatizo yanazidi kuongezeka

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 14, 2009

    Mkuu wa nanii, Mimi ni mkazi wa Tegeta Nyaishozi, simba kweli wapo wawili wametokea sehemu za wazohill na jana mmoja kaonekana saa 10 jioni kwenye shule moja ya mama Sitta akipita uwanjani na usiku kaonekana maeneo yanaitwa machakani kwa hiyo msilete mambo ya uzushi wala nini ni kweli wapo na hawajatokea katika ZOO wanajua wenyewe walikotoea hivyo watu wote wajihadhari

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 14, 2009

    KAAZİ KWELİ KWELİ :))))))) NDO NCHİ YETU LKN

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 14, 2009

    - KITENDAWILI!: mkuu wa nanihii, hawa Simba mbona kazi rahisi tuuu.. watafuteni hawa watu wanne. mkiwapata, basi watu wa tegete ambaeni huku mwalala vi-baraza-ni, raha mustarehee!...

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 14, 2009

    Ngoja tutafute kikosi cha Morani wetu, kazi hiyo ndogo, tutajikumbusha masuala ya jando.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 14, 2009

    Hapa swali ni kwa serikali kupitia wizara yake ya mali halisi na Utalii. Kwa nini Mtu apewe kibali cha kuweka Zoo kwenye makazi ya watu. Hata hao simba alioonyeshwa kwenye TV wao kwenye mabanda.Ipo siku watawakosesha amani wakazi wa Tegeta. Mambo ya mikataba mibovu ipo mingi sana JK ndio kama hii bado kazi ipo kuweka nchi sawa. Kuna watendaji wanaendelea kukuangusha. Kesho utasikia Uzembe mingine.Plz Fire them ;tutapata waadilifu

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 14, 2009

    dah! safari hii wakazi wa dar mziki mtaucheza MBAGALA ELEVEN haijaisha tena SIMBA siwatanii ila mtaona kila aina ya rangi zilizopo duniani

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 14, 2009

    Kaka michuzi nafikiri umefika wakati vyombo husika viwajibike, kuanzia watu wa maliasiri wanatoa vibari vya kutengeneza zoos without consideration ya vigezo husika. Pale maliasiri MPINGO HOUSE pamejaa ufisadi panahitaji kufumuliwa ili tuepukane na matatizo haya. Ndiyo maana hawataki kuwaajiri vijana wa UDSM wakijua fika hawataki challenges hat they need old ways techniques za miaka 47 iliyopita!! So mimi nafikiri kwa suala hili wote waliohusika tanhu mchakato wa awali wa kutoa kibali mpaka hapo simba walipotoloka wakamatwe na kufunguliwa mashitaka this is negligency ya hali ya juu. Mdau ZOOLOGY AND WILDLIFE SCIENCE UDSM!!! NYAGONDE

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 14, 2009

    Haya Yanga, Simba wako wawili tu si kumi na mmoja.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 15, 2009

    ebu jamani tuache mambo ya kizamani.. mimi ni mkazi wa tegeta karibu na ZOO na huwa napeleka watoto wangu sehemu ile.. wenzetu nchi za nje wameendelea na wana ZOO nyingi sana lakini sisi watanzania wa hapa dar tumepata ZOO mbili tu,moja tegeta na nyingine kigamboni..kweli tutawafikia wazungu kwa njia hii...!!!???

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 15, 2009

    duuuu.. hii ya leo kali..!! simba katoka ZOO bila kutudhuru sisi wa njiani..huyo simba haoni???

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 16, 2009

    na kweli sasa huu ni uzushi.. nondo zile za banda la simba na lile liukuta likubwa kuzunguruka ile ZOO kote,simba watatokaje? Hii Zoo ya Tegeta ndiyo sehemu pekee ya karibu ambayo naweza kupeleka wanafunzi wa shule yangu kujifunza wanyama...mnataka kila wiki tuende Mikumi?? Mbona hii Zoo imejengwa kimakini kiasi kuwa kama mnyama atatoka Bandani atabaki eneo la humo humo Zoo. Cha msingi kabla ya kutoa comments za uzushi kuhusu Zoo hii sisi watazamaji twende tuione.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 16, 2009

    haaa haa haa eti simba.. eti watoto msitoke nje..eti simba kala mtu mbona hizo taarifa hamna polisi!!!. kama mbagala habari zao ziko wazi na hizi za simba zingefika polisi na wale waathirika LAZIMA wangedai wasaidiwe na wangeonyeshwa kwenye TV wakiwa hospitali.tusiwekane kiroho juu bila sababu jamani

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 16, 2009

    Kuzusha jambo la uongo kama hili ni ufisadi pia. nimetembelea Zoo ya Tegeta jana na nikawakuta Simba 2 wapo na wana afya nzuri.
    nafurahi sana sasa DAR tuna ZOO ya Wanyama ambayo imejengwa kwa kuzingatia usalama. huyu mtu aliyeanzisha uzushi huu ana lake jambo.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 16, 2009

    HUYU ANAYESEMA KUWA TUACHE USHAMBA YAELEKEA YEY HAJUI KITU MAY BE ANASIKIA TU ZOO ZA ULAYA ZOO GANI ULAYA ZILIZOPO KWENYE MAKAZI YA RAIA???? MIMI NAISHI TEGETA HII SI ZOO NI UCHAFU,KUMBUKA MIEZI KAMA SIKOSEI 2 HIVI JANI ALITOROKA KWANYE HII ZOO FAKE AMETUHARIBIA MALI SANA NA UCHAVUZI WA KILA AINA HATIMAYE TULICHANGA LAKI ILI VIJANA WAHAKIKISHE ANAUWAWA,VILE VILE KUMBUKA WANYAMA NA NDEGE WANA MAGONJWA YA AJABU,MAFUA YA NDEGE YAKITOKEA HAPO KWENYE HII ZOO FAKE ILIYO KWENYE MAKAZI YA WATU ITAKUWAJE???? KIAMA KINGINE HIVYO WEWE NDIYO UNAMTAZAMO SIYO WA KISASA NA USIO WA KISHULE NA HUJUI ZOO ZA WAZUNGU ZIPOJE,TEMBEA UONE,NAOMBA SERIKALI ITUONDOLEE HUU UCHAFU KWENYE MAKAZI YA WATU

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 16, 2009

    Mara Simba , mara Nyani katoroka Zoo na eti zilichangwa laki ili watoto kumuua , mara eti fisi walitoka yote hii ni uzushi mtupu!

    Nyani wote waliokuwa katika msitu wa Tegeta Makaburini wametawanyika baada ya kufyekwa eneo lote lile. Itakuwaje wawe mali ya Zoo saana huyu mkazi wa Tegeta angeomba msaada Maliasili ili hawa Nyani wawindwe.

    Huyu anayesema Zoo ya Tegeta ni uchafu ndiye Mzushi wa habari na ana lake jambo.

    Sisi walimu tunashukuru Zoo kuwa hapo Tegeta tena ina Wanyama wanaofaa kufundishia.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 16, 2009

    hivi ni issue ya Zoo au uzushi wa Simba katoroka Zoo? maana huyu jamaa anayesema yeye katembea sana anajua mambo ya zoo mbona zoo ya Tegeta iko Km27 toka City Centre lakini Ulaya kuna Zoo nyingi tu ambazo kutoka city centre 2km ama walking distance . mfano:

    1) Bristol Zoo
    Address Clifton
    Telephone
    How to Find it: From the City Centre follow the signs to Clifton. The zoo is on the B4468 about 2 miles from the centre of town
    Open: All year from 9.00 am
    Prices:
    Area: 5 hectares 12 acres
    No of Species No of Animals Star Rating
    Mammals 67 444 Conservation **
    Birds 109 418 Enclosures **
    Reptiles 27 162 Education ** *
    Amphibians 2 15 Recreation **
    Fish Research **
    Total 205 1039

    2) London Zoo
    Address Outer Circle, Regent's Park, London
    Telephone 020-7722 3333
    How to Find it: The nearest underground is Camden Town - from which the zoo is a ten minute walk. Regent's Park station is further but the walk is more pleasant. Various busses By British Rail - the nearest station is Euston. Take the Underground (Northern Line) from Euston to Camden Town By Bus - No. 274 and C2. By car - Zoo's car park is on the Outer Circle of Regent's Park. £5 for Zoo visitors. Pay and display parking also available on the Outer Circle
    Open: All year from 10.00 am
    Prices: Adult £9 Child (3-14) £7 Under 3s FREE Student/Senior Citizen/Disabled £8
    Area: 15 Ha 36 Acres
    No of Species No of Animals Star Rating
    Mammals 89 781 Conservation ** *
    Birds 138 690 Enclosures **
    Reptiles 101 486 Education ** * *
    Amphibians 21 124 Recreation ** *
    Fish 177 3312 Research ** * *
    Total 526 5393

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 17, 2009

    Jamani hili sio swala la mchezo hii ni hatari kabisa. Wewe Anony hapo juu ni kwamba kinachotakiwa ni umakini wa mmiliki wa hiyo zoo. Je kweli ameweka ulinzi wa kutosha kuhakikisha wanyama hawaendi nje ya mazingira yale. Nchi za Ulaya wanajua jinsi ya kuweka tahadhari za kiusalama kwa namna yoyote ile na teknologia ipo ya kuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo swala la kuweka zoo kwenye makazi ya watu is not an issue to them because they can handle all pressure. MTU MMOJA KATAJA KUWA WANAWEKA WANYAMA HAPO KWA MUDA KUSUDI WAWASAFIRISHE, HII INAWEZA KUWA NI KWELI LAKINI INAHITAJI UTHIBITISHO. MAANA UFISADI TANZANIA NI KILA KONA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...