Hi
Vipi kaka na pia mh balozi wa nanihii na nanihii...,hongera sana kwa libeneke maana una2saidia saaanaa.
Sasa me msaada ninaouomba kupitia hii blog yako ya jamii ni kwamba me ni mtanzania halisi ambaye kwa sasa niko nakula nondo ya uongozi wa biashara hapa United Kingdom na panapo majaaliwa nategemea kukamilisha nondo yangu soon then natarajia kurudi nyumbani Tanzania kusaidiana na boyz 2 men (JK) kulijenga taifa letu,sasa msaada wangu ni kama ifuatavyo:-
KUNA KIPINDI NILIKUTANA NA MTANZANIA MWENZANGU HAPAHAPA UK TUKAWA TUNAONGEA MASWALA KIBAO NA TUKAFIKIA POINT YA UKIRUDI NYUMBANI UNARUDI VIPI NDIPO AKANIDOKEZEA KWAMBA KAMA UKO UGHAIBUNI KIMASOMO UKIMALIZA MASOMO YAKO NA KUPATA SHAHADA YAKO WAKATI UNARUDI HOME UNAWEZA KUNUNUWA GARI HUKU KWA MFANO HAPA UK NA KULIINGIZA BONGO BILA KULILIPIA USHURU AU KAMA UTALIPA BASI UTALILIPIA KIDOGO TU NA PIA AKANIAMBIA YA KWAMBA UNARUHUSIWA KUINGIZA GARI MOJA,TV MOJA,RADIO MOJA YAANI KILA KI2 KIWE KIMOJAKIMOJA.....
Sasa wadau me hapo ndipo naomba msaada wenu mnisaidie kunifahamisha kama kweli hii sheria ipo kwetu ama vipi na kama kweli ipo inakuwakuwaje naomba kwa yeyote mwenye kufahamu anifafanulie tafadhali kupitia e-mail yangu hapo chini maana nina kindinga changu nimekinunuwa sasa ni mwezi wa pili na ni cha mwaka 1998 ndo nataka mwishoni mwa mwaka huu niende nacho hm japo kinisaidie kuepuka na kupigana vikumbo pale posta mpya chini ya mkungu.
Kaka balozi wa nanihii tafadhali naomba nitolee hii katika blog yako wadau waweze kunisaidia.Tafadhalini wadau naomba msaada wenu.
Mdau
ftyu80@yahoo.co.uk
kila mtanzania ana hinsi ya kukuelewesha , nenda katika mtandao wa TRA, yaani tanzania revenue authority utapata kila kitu wengi ni waongo.
ReplyDeleteUnaruhusiwa kuingiza vyote ulivyovitaja kama "personal effects" bila kulipia ushuru wowote ilimradi uwe na ushahidi kwamba umekuwa ukivimiliki kwa muda usiopungua mwaka mmoja kabla ya kurujea nyumbani; hivyo huwezi kununua gari tu mara unaporejea nyumbani na kutegemea kupata unafuu huo wa kutolipa kodi!
ReplyDeletekindinga cha 98 bongo? hiyo miaka 10 hapo imegonga tayari
ReplyDeleteNdugu yangu usipende kusikiliza maneno ya mdomoni, mara nyingine huwa ni ya kufikirika. Waandikie TRA email, mailto:info@tra.go.tz watakujibu, ila inaweza kuchukua mwezi, andika email usipojibiwa mandika tena mpaka wanajibu, mimmi nilisha wahi kuwa na swali kama hilo wakati naagiza gari kwa mara ya kwanza, walinijibu vizuri wakanipa na mchanganuo(formula) na sheria zao hivyo nikaweza ku jipanga vizuri.
ReplyDeleteHabari za jioni...Habari hizo ni za kweli kabisaaa, ukiwa majuu kama mwanafunzi na unagari sasa umeamua kurudi TZ unaweza shusha gari bandarini kwa bure/bila kulipa ushuru wa aina yoyote ile..Lakini mie ningekuwa wewe ningecheki na bandari kwani mambo yanabadilika kila kukicha, haya ni yakweli mwaka jana (namjua binti aliyeshusha Benz yake hakulipa hata chembe) alivyoosema yeye ni mwana funzi na akaonyesha documents kadhaa aliweza kukwepa ushuru...but just have someone verify this before hand....thanks... ASANTE MICHUZI KWA LIBENEKE HILI ZURI SANA..
ReplyDeleteKwa maelezo ya kwanza hapo juu najua wadau watasema ni mhaya. We subiri tu. Umetikisa kiberiti.
ReplyDeleteLabda kama ulikuwa unawajaribu kuona wadau watatoa maoni ya namna gani. Yangu ni macho tu.
Subiriiiiiiii------------------uone-------
Mhhhhhhhhh!!!!!miaka sita iliopita nilikuwa bongo.bandarini kuna mambo ya ajabu sana.Kwani kama ulivyo sema kuwa utalipia kidogo,hoo!!!Iko hivi gari kwa kipindi kile ikiingia ina kaa pale bandarini kwa muda wa wiki mbili bila malipo wakati una malizia ur paper works/kazi za makaratasi ambazo ukizembea zaweza chukua miezi miwili.
ReplyDeleteSasa basi kwa kipindi kile baada ya hizo wikimbili.Kinacho fuata kama Gari haija toka unalipia bandari Tshs 10,000 kwa kila siku ambayo imezidi zile wiki mbili,This ni first.
Pili akitokea mtu akiipenda gari yako pale bandari watakuzungusha mpaka ukate tamaa ili ainunue huyo jamaa siku ya mnada,una weza konda ndani ya miezi mitatu unapo ingia tu bongo.
Third kuna kutumia clearing and forwading.hapa sasa kuna mbwembwe balaa hawa jamaa wana weza poteza karatasi yako muhimu makusudi na kusababisha malipo zaidi.Tegemea haya mambo ila kama una mtu katika JK system sijui.
Kwani hata mimi niko nje hapa huwa nafikiria sana lakini naona kama nitapata pesa nirudi nayo home tu na vitu niuze vyote.
Napenda sana kufahamu sheria mpya ya sasa ambayo ina weza kuwa nzuri lakini utekelezaji wakeni sifuri.Hapa ndio utagundua kuwa majirani wanao hitaji ardhi ya Tanzania wao wanafaidi sana kwani ile bandari ya mombasa waliyopewa wanafunzi wako exempted/dutyoff kwa kila kitu.{MDAU}
Sinauhakika kama bado inaendelea hiyo exemption kwa watu waliotaka masomani au la. Nilipotaka kusoma UK miaka hiyo walikuwa wakihesabu kitu kikubwa kwa unit moja moja bure walikuwa wanaviita kama " personal effect" kwa mfano friji 1,compter 1,TV 1, cherehani1,washer1, dryer1. Wakikuta umebeba zaid ya moja basi itachargiwa ushuru wa kawaida. Sina uhakika na gari, mie nilipata expection ya percentage fuluni sikumbuki kama mtumishi wa serikali.
ReplyDeletewasiliana na mwenyekiti wa watanzania uk anaitwa abuu faraj atakusaidia.
ReplyDeleteau swift freight cheki www.tzuk.com.
Mdau, haka ka sheria bongo kapo, ila navyojua mimi, ili kuwalinda ma expat wa kibongo tuliopo huku ughaibuni tusipoteze mali zetu tulizonazo huku aidha mikataba ikiisha au vingenevyo, serekali iliweka sheria kuwa mtu unaruhusiwa kurudi na mali zako home (Sio za biashara na ndo maana wakasema kila kitu kimoja) bila ushuru ila tu viwe katika jina lako katika kipindi kisichopungua mwaka mmoja.
ReplyDeleteNadhani ni hivo, kama nimekosea, wadau watarekebisha.
KUHUSU GARI KAMA SHERIA HAJABADILIKA UNATAKIWA UWE UMEKAA NALO UK KWA ZAIDI YA MIEZI 12.. ZAIDI YA MIEZI 12 MAANA YAKE UNA KADI YA UMILIKI WA GARI HILE KWA ZAIDI YA MIEZI 12 NA LIWE NA MOT CERTIFICATE.
ReplyDeleteLAKINI UNGEFIKIRIA KUHUSU KAZI, KWANI TANZANIA SIKU HIZI KAZI KUPATA NI NGUMU KAZI ZIMESHIKILIWA NA WAGENI KAMA WAKENYA,WAGANDA NA RWANDA...KATIKA HILI NADHANI KK AMESHINDWA SIELEWI KWANINI ASITEMBELEE SIKU MOJA OFISI KUBWA KADHAA AJIONEE MWENYEWE UCHAFU HUU, WATANZANIA WENGI WASOMI WANASHINDWA KUPATA KAZI, KWANI WAGENI WANAPEANA KAZI WENYEWE KWA WENYEWE. WATANZANIA HAWANA HAKI KATIKA NCHI YAO WENYEWE.
HUU NI WAKATI MUAFAKA WA KK KUSHUGULIA HILI SUALA MWENYEWE KWANI TIMU YAKE IMEFELI KUFANYA KAZI KWA NIAMBA YA WANANCHI WA TANZANIA.
Ndugu yangu habari za kuingiza hiyo mizigo ni kwamba kama wewe ni dent basi inabidi ilo gari lako uwe umalinunua miezi kumi na mbili iliyopiata kabla ya kuanza kulisafirisha.Kinyume na apo utalipia ushuru kama kawaida
ReplyDeletewewe 3.45am,vipi wewe,huyo hawezi kuwa mhaya,maana mhaya lazima angetoa kitu show room yaani brand new na sio gari la miaka kumi iliyopita.mhaya anajua fika kwamba haya magari ya zamani ndio yanayoleta environmental pollution kujazajaza micarbondioxide mjini.hii mutu lazima itakuwa hii mikabila ya ajabu ajabu isiyojua maana ya kutunza mazingira
ReplyDeleteJamani mimi nafikiri hii ipo wazi issue ya gari ni utata sana labda upate bahati. Hii nina maanisha kwamba kama unaona gari yako haujawa nayo zaidi ya miezi kumi na mbili (Mwaka) basi sidhani kama utapenda kufoji makaratasi maana utaenda kupata usmbufu na kujuta kuliko ungechukua hela yako ukaenda kununua Bongo (Mawazo tuu)
ReplyDeleteKuhusu personal effect bado zipo pale pale ila ndio kwa kila kitu kiwe kimoja kimoja na nasisitiza uwe na uthibitisho wa kuwa umevimiliki kwa muda wa fulani na sio umevinunua tuu ukaenda navyo lazima wata kula kichwa.
Kiujumla washkaji wa Customs ni nomaaaaa yaani wananjaa zaidi hata ya matrafiki wa barabarani na hasa wakijua umetoka nchi kama Uingereza basi wanajua umekuja nazo
Kuna kamsemo nilikakuta kwamba "kama wasipokukamua leo basi watakuwa wamefanya sana kosa pindi pale utakapo ingia ofisini na kuanza ufisadi wa kodi za wananchi"
Kila la kheri ila the best way nafikiri ni kucheki karibu na watu wa TRA na Bandari.
Ukweli upo kwenye sheria ya East African Community Customs Management Act, 2004. fifth schedule, Part B -General Exemptions kipengele cha 5 -Passengers' Baggage and personal effects;
ReplyDeleteWewe msomi, jisomee hapo chini na ujipimie mwenyewe. Sheria hii inatumika East Africa kote, hakuna cha Kenya wanasamehe wanafunzi wala nini, kila mtu atajisemea hapa, huo ndio ukweli.
5. Passengers' Baggage and personal effects
(1) Goods imported by passengers arriving from places outside the Partner States shall, subject to the limitations and conditions specified in the following paragraphs:
The goods shall be:
(a) the property of and accompany the passenger, except as provided in para- graph 7;
(b) for the personal or household use of the passenger in a Partner State; and
(c) of such kinds and in such quantities as the proper officer may allow.
(2) Notwithstanding paragraph (1)(c), the following goods shall not be exempted
185
No. 1
East African Community Customs Management
2005
under this item:-
(a) alcoholic beverages of all kinds, perfumes, spirits and tobacco and manu- factures thereof, except as provided in paragraphs 6 and 7 of this item;
(b) fabrics in piece;
(c) motor vehicles, except as provided in paragraph (3) and (4);
(d) any trade goods or goods for sale or disposal to other persons.
(3) Subject to paragraphs (1) and (2) of this item, the following goods may be exempted under this item when imported, as baggage by a person on first arrival in a Partner State whom the proper officer is satisfied is bona fide changing residence from
a place outside a Partner State to a place within a Partner State, where the person has neither been granted an exemption under this paragraph nor resided in a Partner State before his arrival other than on temporary non resident visits:
(a) wearing apparel;
(b) personal and household effects of any kind which were in his personal or household use in his former place of residence;
(c) one motor vehicle, "(excluding buses and minibuses of seating capacity of more than 13 passengers and load carrying vehicles of load carrying capac- ity exceeding two tonnes)" which the passenger has personally owned and used outside a Partner State for at least twelve months (excluding the peri- od of the voyage in the case of shipment):
Provided that the person has attained the age of eighteen years.
Wadau mnaposema ukiwa mwanafunzi unakuwa exempted, mbona hamfafanui vizuri. Ni documents gani zinazotumika . Kama niko nje kama mkazi wa kudumu au raia na nakwenda shule. Je nahesabika kuwa ni mwanfunzi for TRA purpose?
ReplyDeleteMdau Ubena Zamosi.
SHERIA ZA FORODHA ZINASEMA KUWA KAMA UMEKAA NJE ZAIDI YA MIAKA MITATU UNARUHUSIWA KUJA NA PERSON EFFECTS ZAKO ZOTE BILA KULIPIA USHURU,INA MAANA HUWEZI KULIPA USHURU KILA KITU KAMA MAFRIJI,VITANDA,GARI,MAGODORO MAKOLOKOLO YAKO YOTE,HIVYO KIJANA USIBABAIKE JAZA CONTNAINER HATA MABAKURI YAKO YOTE
ReplyDeleteje akina sisi tulikuja kupiga boksi vipi? nimekaa huku miaka ushee na mwaka huu nimeamua kurudi nyumbani kutuliza mgongo for good, nami nitasamehewa?
ReplyDeletewewe unawasifia wahaya. wahaya wote ni waganda wa kagera. muhaya ana nini si ni waganda hao?? nyie wahaya kwani ni watanzania?? si basi tu nyerere ilijishaua??. nyie kwenu uganda ndo mana hata lugha yenu na kiganda ni kitu kimoja acheni kutusumbua na nchi yetu waganda wanyankole nyie.
ReplyDeletemi nikiwa na ofisi siwezi ajili mganda wa kagera?
NIMESIKITISHWA SANA KUSIKIA KUWA WAGENI WAMECHUKUWA KAZI NA WAZAWA WAKAKOSA KAZI HIYO SIO HAKI HATA KIDOGO
ReplyDeleteNYIE WASOMI KAMA MPO NENDENI MKAMUONE RAISI WA NCHI NA MPE MALALAMIKO YENU DUNIA NZIMA INAMPA KIPAUMBELE RAIA KWANZA.
HII HAIKUBARIKI NA KAMA MTASHANGAA BASI ILA IMENIUMA SANA HUWEZI WEWE UKAENDA KENYA NA UKAPATA KAZI WAKATI WATU WAO HAWANA KAZI
IKIBIDI HATA KUANDAMANA ANDAMANENI
MPAKA MSIKILIZWE
THAT IS NOT FAIR AT ALL
ANON 4:20.
ReplyDeleteLet me educate u a bit sababu??
Kwanza kabisa wewe mpumbavu, yani crack-head, lakini kwasababu nataka uweze kujitambua japo kidog ngoja nikuelimishe!
1. Office ambayo crack-head kama wewe anaweza kupata sijuhi kama utaweza kuafford muhaya yeyeto labda crack-heads kama wewe.
2.Isipokua wewe nimpumbavu sana atleast u have some idea on past HISTORY, makofi kwa pumbavu hili!!!!!!!
lakini wewe pumbavu hiyo history yenyewe, dont think u passed it! kuna kitu kinaitwa bantu languages kasome vizuri, kisha upige mswaki alafu ndio uje kukenua kwenye blog.
Francis Mulokozi concerned Muhaya.
Mambo ya Makabila yaishie kwenye utani jamani, kha! Mawazo, fikra mufilisi za kikabila zikae mbali na blog yetu na nchi yetu tafadhali!!!
ReplyDeleteWewe Ano's 4:20. Hii ni lugha ya Kibantu. Usiseme kitu kama ukijui. Halafu unapoaandika sentensi jaribu kuweka anza na herufi kubwa, kituo cha kufunga sentensi. Kujidai mnajua kiswahili kumbe hamna lolote. Na jitahidi kujua ni wakati gani unatakiwa kutumia alama ya kuuliza. Sisi ni watanzania harisi.
ReplyDeleteMdau jibu la swali lako utalipata hapa http://www.tra.go.tz/documents/RETURNING%20RESIDENT.pdf
ReplyDeleteUShauri kwa wengine, Jifunzeni kuwa watafiti na kutumia vyombo husika kupata majibu ya myatafutayo...
SHERIA NI NZURI,LAKINI KUNA TATIZO MOJA.KWA WENGI WETU AMBAO TUMEKAA NJE KWA MUDA MREFU TUNAELEWA.ILI UWEZE KUINGIA KWENYE MFUMO SAWA NA WENZAKO WA HUKU,INABIDI UFANYE ADJUSTMENT ZA HARAKA HARAKA. INAPOKUJA KWENYE SUALA LA USAFIRI,UTAJIKUTA UNAISHIA KWENYE PALE UWEZO WAKO MDOGO UNAPOFIKIA. HUWEZI KUJILINGANISHA NA WENYEJI KIFEDHA. UTAPATA USAFIRI AMBAO NI SECOND HAND KWA KWELI.
ReplyDeleteUTAJITAHIDI KUFANYA KILA KITU SAWA,PAMOJA NA KUTUNZA KIDOGO UKIPATACHO ILI UWEZE KURUDI NYUMBANI NA AKIBA YAKO AU HATA USAFIRI. KWA MAANA HIYO MARA NYINGA UNAJIKUTA UNAWEZA KUTUNZA FEDHA ZA KUNUNULIA GARI LILILO KWENYE HALI NZURI KIPINDI AMBACHO UMEMALIZA MASOMO NA UNAKARIBIA KURUDI NYUMBANI. KAMA KUNA UWEZEKANO,SHERIA INGERUHUSU MTU ANAYERUDI NYUMBANI AWEZE KUSAMEHEWA USHURU HATA KAMA GARI HILO AMENUNUA WIKI MOJA KABLA YA KUANZA KURUDI NYUMBANI.HII NI BAADA YA KUTHIBITISHA KUWA ALIKUWA MASOMONI AU NJE YA NCHI KWA MWAKA MMOJA NA ZAIDI. PIA ITASAIDIA WATU WAWEZE KUINGIZA MAGARI YASIYOMACHAKAVU SANA TOFAUTI NA YALE AMBAYO WAMEKUWA WAKITUMIA KIPINDI KIREFU WALIPOKUWA NJE.WENYEWE TUNAJIJUA NI MAGARI YA AINA GARI TUNATUMIA TUKIWA HUKU.SI VYEMA TUKAPELEKA MAGONJWA HAYO TENA NYUMBANI !!
Raia yeyote wa tanzania anaruhusiwa exemption kama anarudi nyumbani ali mradi awe alikuwa nje ya nchi kwa zaidi ya mwaka mmoja, haijalishi kama alikuwa nje kikazi au kimasomo. Watakachoomba proof ni passport yako ili wacheki kama hujarudi ndani ya mwaka mmoja. na gari uwe umelimiliki kwa zmwaka mmoja ndiyo unapewa full exemption otherwise kama utaonyesha umelinunua muda chini ya mwaka still utapewa exemption ya percentage fulani , nadhani ni 20 percent off. Make sure una risiti maana wale jamaa huthaminisha kwa bei ya juu sana kama exemption ikishindikana.
ReplyDeleteasante
ReplyDeletegari la mwaka 1998 unazidi kutujazia pollution bongo...ebooo
uza njoo mtupu ununue huku
ivi nyie wahaya mna nini???
hawa wala vumbi wasikukatishe tamaa we peleka gari lako. hayo magari wanayokuambia ukanunulie bongo ni ex Japanese car, choka mbaya na mengi ni ya 1995 na yameenda mileage kibao, wewe nenda na lako la uk nauhakika hata kama ni la 98 nina uhakika ni 100% better than yaliyo kwenye show room za bongo. Trust me i've done my reseach.
ReplyDeleteWadau mnasahau kitu kimoja muhimu, yes bidhaa uwe umekaa nazo mwaka, ila na wewe uwe una ushahidi that ulikuwa ughaibuni kama mwanafunzi si chini ya miaka mitatu. Ila, kupata info zote, bora uende ktk website ulizotajiwa hapo juu. ahsante
ReplyDeleteNdugu ni ngumu sana kutoa mizigo kwa bandari ya bongo cha kufanya wewe kama gari umeshatumia hapa Uk mwaka mmoja pitisha holili kila kitu ni rahisi sana wala hakuna kuangaika kama bongo.
ReplyDeleteAll the best.