Bro. Michuzi,
kwanza salaam. Pole na uchovu uchovu wa vekesheni, japo watu huwa wanapumzika na wala hawasikiki wakichukua vekesheni!
Well nina swali la kizushi kwani Kiswahili kinanipa utata kinakua kila siku na hasa ukiwa mbali na nyumbani inakuwa vigumu kuelewa maana ya baadhi ya maneno mapya na matumizi yake.
Swali langu ni kwamba
(i) Nini maana ya FISADI?
(ii) Nini maana ya MLA – RUSHWA”
(iii) JE NINI TOFAUTI YA MLA- RUSHWA NA FISADI?
(iv) Hivi katika hawa wawili ni yupi mwenye athari katika maendeleo ya maisha ya mwanadamu, na yupi wa kukabiliwa kwanza?
. Maswali yangu ni ya kizushi lakini kwa msaada wa wachambuzi na wataalamu wa lugha ya Kiswahili nina matumaini kwamba nitapata majibu yatakayotufungua macho baadhi yetu tunaojifunza misamiati ya Kiswahili.
Nashukuru kwa blogu ya jamii na ninasubiri majibu kwa hamu kubwa kisha tutaendeleza mjadala huu na kufikia kiini cha maswali yangu.Ninaomba rekebisha Kiswahili changu kama kibovu.
Wako Mdau Steve
USA
steve nadhani fisaidi ni mfujaji wa pesa, au mtuanayetumia pesa za umma kwa manufaa yake binafsi, na mla rusha, ni anayepokea hongo au pesa kwa njia isiyo halali, lakin nadhani sijaeleza vizuri ila maswali yenyewe yanajieleza vizuri tu kama ulivyoyanukuu
ReplyDeleteUkitazama Kamusi ya Kiswahili sanifu wametafsiri neni FISADI:Mtu mbaya,mtongozaji,mharibifu,mpotevu,mwasherati.
ReplyDeleteRushwa:Kupokea fedha au kitu cha thamani kinachotolewa na kupewa mtu mwenye madaraka ya jmabo fulani ili mtoaji apatiwe upendeleo.
Hivyo ndivyo kamusi ya kiswahili sanifu inavyo tafsiri maneno hayo.
Kuelezea tofauti ya maneno hayo na yupi mwenye athari wewe mwenyewe kwa kutumia akilia yako ya kuzaliwa anagalia tafsiri ya maneno hayo kisha anaglia tofauti zake na upime
nashukuru kwa swali lako la kipuuzi,
ReplyDeletefisadi ni mtu anayejilimbikizia mali au fedha za serikali,NGO au watu waliompa madaraka kuwasimamia kinyume na sheria/haki kwa manufaa yake mwenyewe
mlarushwa ni mtu/muajiriwa aliye na wadhifa wakughulikia maswala fulani kisheria lkn anatoa huduma kwa kupokea/kuomba fedha,vitu au uchi kwa anayestahili au asiyestahili kupata huduma.
nijuavyo mimi
scientist
Kiswahili kimechukua maneno mengi toka lugha mbali mbali hususan lugha ya Kiarabu. Japo mara nyingi utakuta tafsiri ya neno katika kiswahili inatofautiana na ile ya Kiarabu kwa mfano ghorofa, safina, fuska n.k. maana ya neno fisadi lipo karibu sana na maana yake kwa kiarabu. Kwa ufahamu wangu "fisad" ni noun inayotokana na neno la Kiarabu "fasad" (au wingi faasidin) likimaanisha corruption. Kwa maelezo zaidi angalia http://en.wikipedia.org/wiki/Fasad
ReplyDelete... Mdau kweli kabisa. tupo wengi tunaoathirika na ugumu wa kiswahili - japo lugha yetu.
ReplyDeleteMy stab:
Fisadi = mharibifu. Mtu yeyote anayefanya ndivyo sivyo... anayepotosha malengo au kuzuia malengo yaliyokubalika yasifikiwe kwa namna yoyote ile; iwe anajua au hajui huyo ni fisadi! Tofauti kidogo na "mfuska" ambaye ni mtongozaji, mwasherati na/au mzinzi.
Mla rushwa... ni yeyote anayepokea hongo au chochote (ikiwa ni pamoja na vitu kama sifa au "ujiko") kwa minajili ya kuzuia haki isitendeke. mtoa rushwa... anayetoa hongo.
Nani mbaya... wote dugu moja... wote ni ma "axis of evil" wa kikweli kweli. cheers
Heee hee heee. Fisadi ninavyoelewa mimi ni jitu linalo fusa bila uhalali wowote. Kama ushajaribu kucheza gudugudu au kamali ukafuswa fedha zako kimbinumbinu ndio ufisadi wenyewe huo. Kwa hawa jamaa zetu wanaotuomba kura ili wale ndio huohuo ufisadi mtu achukua tanesco yote kimbinumbinu nyie mwafuswa hele zenu tuu. Mpokea rushwa ni kamavile changu doa yaani yeye hana mme maalum wala msimamo. ´Mfano rahisi trafik atakuwekea mkwara ukimpa hela analegeza. Kwa jamii wote fisadi na mla rushwa ni maadui wa kubwa kutegemea na madaraka walionayo. kwamfano fisadi anaweza kumuhonga malarushwa akapata mkataba wa miaka hamsini kuinyonya tanzania. Kama una maswsali ya ziada njoo hapa pacific manundu nitakufahamisha.
ReplyDeleteNeno fisadi linavyotumika sasa hivi ni tofauti kabisa na maana yake halisi. Kwa maana yake halisi mtu kama Manji siyo fisadi lakini kwa maana hii mpya ambayo bado siyo rasmi kwenye lugha ya kiswahili unaweza kumuita hivyo. Kwa mfano wale old school wanaweza kuelewa maana ya neno mshkaji hapo zamani lilikuwa na maana ya mtu ambaye una uhusiano naye kimapenzi lakini siku hizi mshkaji ni mtu wa karibu kwako au rafiki.
ReplyDeleteAnony number mbili umetulia saana.Hayo ndiyo majibu halisi ya hayo maneno mawili.Neno fisadi has nothing to do with "Material wealth" ,its fisadi kiwembe.Rushwa is what about all material wealth...!!!
ReplyDeleteThanks,
Mdau,
Ughaibuni.
hahahaha wewe anonymous wa 7:30pm umenichekesha sana wewe ndiyeumejua kuelezea maana halisi ya fisadi na mla rushwa, na wewe u nayesema asante kwa swali lako la kipuuzi mpuuzi ni wewe unayejifanya unajua kumbe kichwani maji matupu, mshambawewe wewe unaoenekana unasifa zote hizi mbili fisadi na mlarushwa hahahahah
ReplyDeleteMay 30, 2009 12:50 PM ametulia sana na amelinganisha na maisha halisi ya kitanzania.ametumia general knowledge na maana halisi inayotumiwa na serikali kwa maneno hayo. na anaeleweka kuliko wote
ReplyDeleteWewe SCIENTIST huruhusiwi wala hupaswi kuambia mwenzako anauliza maswali ya KIPUUZI kwani jua kuwa Kuuliza si ujinga wala upuuzi...Yeye si kila kitu anafahamu napia nahakika hata wewe Si kila kitu unafahamu. Kila mmoja anayo right ya kuuliza na Michuzi ameona ni swali lenye msingi ndipo akaliweka laasivyo asingeliweka ..Tusipende kuwavunja moyo wenzetu kama wewe unajiona unajua waache wenzako wanaojua kidogo wajue zaidi....
ReplyDeleteBlog ya hii ipo kwaajili ya kuelimisha, kuburudisha, kutuhabarisha.