Marehemu Mzee Ramadhani Abu Ally

Familia ya marehemu Mzee Ramadhani Abu Ally na Mama Joyce Abu inasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa, Mzee Ramadhani Abu Ally, aliyefariki alhamisi tarehe 23 April 2009 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu Mzee Abu Ally alizikwa Ijumaa 24 April 2009 katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

Mpendwa mzee wetu, utakumbukwa daima na mkeo mama Joyce Abu; watoto wako: Ali (Tabora, Tanzania), Hanifa, Malilo, Hashim, Omari na Tunu (Dar es Salaam, Tanzania); Peter (Vienna, Austria), Mariam (New-York, USA), Ndema (Geneva, Switzerland), Dotto-Sharon (Washington DC, USA); wakwe zako: Mrs Ali, Sultani, Bakari, Mrs Hashim, Renate, Habib, Jameson; wajukuu zako na pia ndugu jamaa na marafiki.

Arobaini ya marehemu itafanyika nyumbani kwake, Dar es Salaam siku ya Jumapili tarehe 31 May 2009.

Familia ya marehemu Mzee Abu Ally inapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru kwa dhati ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa nasi na kutupa moyo katika kipindi kigumu cha ugonjwa wa mzee wetu hadi kufariki kwake.

Shukurani za pekee pia ziwaendee madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam kwa jitihada zao katika matibabu kwa mpendwa baba yetu. Pia familia inatoa shukurani za dhati kwa Watanzania wa Uswisi na Jumuiya yake (TAS) kwa ufariji kwa wafiwa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mzee Abu Ally mahala pema peponi. Amen!
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kapumzike kwa amani baba yetu mpendwa Mzee Abu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2009

    Inna lillahi wa inna ilayhi rajiun.
    Poleni sana Maryam Abu na familia kwa jumla, Inshaallah Mwenyeezi Mungu atawapa moyo wa subira na Inshaallah marehem ampe kauli thabit, amtiliye nuru kaburi lake na amlaze mahali pema peponi Amin.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...