Zanzibar International Film Festival/Tamasha la Nchi za Jahazi kwa muda mrefu sasa limekua likitoa nafasi za mafunzo ya muda mfupi (Training Workshops) kwa wadau wa filamu nchini na pia kutoa nafasi kwa soko la filamu la Africa mashariki kwa ulimwengu.
Ikiwa sasa tuko katika Tamasha la 12 la nchi za majahazi, ZIFF imeendelea kunadi na kukuza soko hili la filamu, ZIFF inatambua mahitaji ya kiwanda kizima cha filamu ili kikue na kufikia malengo tuyatakayo. Lakini kumekuwa na mwamko mdogo sana kwa wadau ama washiriki wa fani hii, ukiangalia kiwanda hichi hakina watu wenye ujuzi upasao (Professionalism) na ndio maana kimekua kikizalisha ilimradi kazi tena zisizo na ubora.
Mwaka huu tena ZIFF inatoa nafasi ya mafunzo ya muda mfupi kwa wadau na washiriki wa soko/kiwanda cha filamu. Tunaomba watu wajitokeze kutuma maombi yao ili kuweza kushiriki. Pia tunaomba wadau/washiriki wasisite kuuliza maswali pale wapohisi hawajaelewa au panawatatiza.
Naambatanisha Tangazo la Warsha za Mafunzo ya muda mfupi ili kuwajulisha wadau/washiriki nini kinaendelea katika ZIFF 2009 na pia kuwaomba washiriki.
Nashukuru kwa vyombo vya habari kwa kuwa mstari wa mble kuzungumzia soko na kiwanda cha filamu kwa upana lakini tukumbuke bila elimu kiwanda hichi kitakufa.
Ahsante kaka Michuzi kwa msaada wako mkubwa katika kiwanda/soko la Filamu.
WORKSHOP/CONFERENCE/FORUMS AT ZIFF 2009
27th June – 3rd July, 2009 - Film Production for Children Workshop by DFI15 Participants (10 From Mainland, 5 Zanzibar), Application Deadline 25th May, 2009For Film Makers/Producers Only.
28th June – 5th July, 09 - Screenwriting Workshop by Maisha Film Lab9 Participants: Application Deadline 21st May, 2009For Script Writers Only.
2nd July, 2009 - Acting for Camera by Ntare Mwine and Danny Glover (USA)20 Participants (15 from Tanzania Mainland/East Africa, 5 from ZanzibarFor Actors Only.Application Deadline 25th May, 2009.
2nd- 3rd July 09 - Tourism Conference by ZIFFFor All Tour Operators in Tanzania (Zanzibar and Mainland)Apply now for this special opportunity.
Deadline for Application 1st June, 2009
3rd July, 2009 - African Film Makers/Producers Forum by ZIFF/TAIPAFor East African Film Makers/Producers
Application Deadline 1st June, 2009
3rd July, 2009 - Wild Life filming by South African WildlifeFor all Wildlife Film Makers/Producers Application Deadline 1st June, 2009
4th July, 2009 – Development Film Workshop by GTZFor All Film Makers/Producers/Media Houses.25 Participants (15 from Mainland, 10 from Zanzibar and East Africa)Application Deadline 1st May, 2009
Wako katika Filamu,
Daniel NyalusiEvents Coordinator/Film Programs
Zanzibar International Film Festival 2009
I wish I could be there. There is some good stuff going on at ZIFF this year. I hope my fellow Bongo actors will take full advantage of these wonderful opportunities.
ReplyDelete- Chemi
Daniel Nyalusi,
ReplyDeleteKazi nzuri sana mnayofanya ZIFF. Mimi nasoma utalii huku Ughaibuni lakini natarajia kuja huko nyumbani wiki inayokuja kwa ajili ya kukusanya data za utafiti wangu. Nimeona mna program moja ya Tourism Conference 2nd-3rd July, ningependa sana kuhudhuria kwenye hii conference. Nimejaribu kuangalia website yenu, lakini sikupata info za kutosha na baadhi ya pages hazifunguki, hakuna pia contacts details zenu(simu, email address). Ninapenda kufahamu nanma ya kujiregester na mahali ambapo hii conference itafanyika. Kama unaweza tafadhali naomba wasiliana na mimi kupitia hii email ckumbayaro@yahoo.com.
Cheers,
Mdau
Hongera ZIFF.Kila la heri kwa mwaka huu na miaka ijayo.
ReplyDeleteNeno halisi linalopaswa kutumika hapa ni 'Tasnia' na si 'Kiwanda'. yaani tasnia ya filamu na si kiwanda cha filamu.Kiwanda ni sehemu fulani kuna uzalishaji wa bidhaa, kuna mashine, motor fan belt, conveyor belt na kelele mbali mbali zinazohusika na uzalishaji huo. Au zaidi na zaidi siku hizi kwa sababu ya utumikaji wa TEKNOHAMA katika kila aina ya uzalishaji basi kelele zianaelekea kupungua na vitaa taa vitufe na keyboard na screen vinakuwa vingi.
Lakini tasnia ni shughuli kwa ujumla za aina fulani za kiuchumi- kwa hiyo unaweza ukasema tasnia ya utangazaji (kwa maana ya broadcasting industry), tasnia ya filamu (yaani film industry), tasnia ya benki (banking industry)na kadhalika. Najua ndugu zangu wa vyombo vya habari kama Clouds na hasa Captain Habash wamechangia katika matumizi ya 'kiwanda' kama ulivyotumia wewe lakini naamini ni matumizi potofu na neno linalotkiwa kutumika hapa ni 'tasnia'.
Kiwanda ni lazima kiwe kiwanda fulani yaani labda cha konyagi kule chang'ombe au Tanzania Printers cha uchapishaji. Tasnia inajumuisha shughuli zote za aina maaluum kama vile za uchapishaji, utengenezanaji vinywaji na kama hivyo; yaani, kwa mfano, Tanzania Printers, Jamana, DTP, zote zimo katika tasnia ya uchapishaji lakini kila kampuni iliyotajwa hapo ina kiwanda chake.