nanihii akiendeleza libeneke makao makuu ya google sehemu inayojulikana kama sillicon valley (kimatumbi chake usiniulize; sijui) hapa san francisco leo
vekesheni bila mikonozzzz haikamilikigi. hapa nanihii akiwa na wadau wanaokula nondozzz za udaktari (miaka 12!) katika chuo kikuu cha stanford university kilichopo san francisco. mdau ulieniazima pambazzzz (jina kapuni) asante kwa msaada kwenye tuta. maana ningeumbuka...


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 58 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2009

    hahahahahaaaaaa.michuzi unatuua sana.sasa mie nimempenda huyo dada wa pili kulia kwako.mpe email yangu. michaelpeter2008@yahoo.com

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2009

    Oyaa noma mtu mzimaa umembagua huyo kiti moto...next time uache ubaguzi wa rangi..Oooops sorry inawezekana michuzi ushamba ulikuwa unakusumbua lack of technical knowledge ukidhani ukimshika huyo unapata MAFUA YA SHWAINI...Noooooooooooo huwezipata.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2009

    mithupu miyeyusho! harusi za watu hapa bongo unakula fulanazzzz lakini hao wanyamulenge unawavalia suti??? Aaaaaaaaaaaaah acha hizo kaka!tehe tehe........

    ReplyDelete
  4. Nanihii hizo pamba "usipime" umetoka mswano kweli kweli hasa kwenye hilo "google"

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2009

    hiiii!!! balozi wa nanii?? umependeza wewe,tena umetoka chicha

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2009

    Michu umesahau flanaz Bongo tutakutumia,tupatie Address tu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2009

    udaktari miaka 12!!!!?????????

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 19, 2009

    Michuzi leo umependeza sana...utafikiri unaenda kuoa mhaya vilee....very nice!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 19, 2009

    Ndugu nanihii, mwenzio familia yetu hatuna daktari, ni vyema uni-introduce kwa hawa mabinti, nione kama investment inaweza kufanyika.

    ReplyDelete
  10. www.tanzaniasports.comMay 19, 2009

    Faza umependeza sana!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 19, 2009

    Silicon valley haipo San fransisco, ipo mbele ya san jose ni miji tofauti kabisa au kwa sababu uliingilia San franscisco basi kila mji kwako ni Sanfransisco.
    ANY WAY karibu sana BAY AREA

    ReplyDelete
  12. lakini wewe balozi shauri yako na watoto wa watu,mama balozi akiona hii si atajua ndiyo kisa hukutaka kumchua?
    halafu ile fulazzzz uliicha wapi jana wewe
    Anyway bro tuna kutakia kila kheri huko ,waambie hao mabinti wasome sana bwana hata majina yao huja tuwekea.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 19, 2009

    miaka 12???????
    nini icho wanasomea?udaktari wa kitu gani
    ebu acha fix weweeee

    yes konozzzzz kwa totozzzz

    mh!!michu unaasili ya "UHAYA"au mkeo ana asili yake??sasa ndo nini eti umepozi picha google pale ionekane
    hahahahaaaaaa

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 19, 2009

    12 years!!!!!
    for Mars or.......

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 19, 2009

    Jamani naomba msaada eti Pambazz ndio nini? yaani slang nyingine za kwetu zimenipiga chenga huku niliko!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 19, 2009

    Wenzetu huko US inachukua angalau miaka 12 kusomea Medical Doctor. Yaani miaka 4 kwa degree ya kwanza, kwa wale ambao degree yao ya kwanza haikuwa ya sayans basi inawalazimu wachukue masomo ya pre-med(Biology,Chemistry,Anatomy nk) kwa 1-1.5year, kisha ndipo unaweza kuingia medical school ambayo itakuchukua miaka 4 tena kumaliza.Baada ya hapo inabidi kumalizia kipengele cha mwisho cha residence kama vile daktari mwanafunzi ambacho nacho ni miaka 3 hadi 6 kutegemea na umesomea udaktari wa nini

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 19, 2009

    UKITAKA KUJUA WACHONGA VINYWA WENGI WA UGHAIBUNI NI ZERO YAANI... HAWAJUI SAVING WAO STAREHE TU. SASA MICHUZI YUPO HUKO HAKUNA ANAYEMKARIBISHA.... KIMYAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 19, 2009

    Mtajuaje na yeye kafika ofisi za google!! Tunakushukuru mdau uliyemuazima kaka yetu pamba maana hali ya fulanazz ilikuwa mbaya

    ReplyDelete
  19. Kazi ya braza michu ni kutuhabarisha mambo mbalimbali tena fasta fasta, sioni tatizo akituletea pic yake yuko google, je mheshimiwa jk akipigwa picha hapo pia mtasema anawaonyesha, acheni ushamba! kwa hiyo watu wasikongoli picha kisa unaonyeshwa, kama wewe unapajua sio wote, na mimi kesho ntaenda kupiga picha kwenye mapyramid nimtumie aweke humu useme tunakuonyesha! Alaaaa!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 19, 2009

    12 yrs ni pamoja na kuwa professor!

    ReplyDelete
  21. afande midakoMay 19, 2009

    umesahau kumshukuru na aliye kuazima kaMAC na sijui kama unajua kukatumia au ulipigia picha tu?

    udaktari upo wa aina nyingi, nahisi jamaa haongelei uphysician may be ni Phd ya biology/phyisics nk ambapo wanataka watoke na principle mpya

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 19, 2009

    Kwa ufafanuzi tu, Stanford University ipo katika mji wa Palo Alto. Ni mji mdogo uliopo kati ya (sio katikati ya) San Francisco na San Jose.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 19, 2009

    Kaka Michuzi,
    Ahsante kwa kutuhabarisha juu ya mambo unayoona kwa picha pande zote unazotia mguu. Maana tunajifunza mengi.

    Ila komenti(Ya Pili) kama ya Anony May 19, 2009 2:18PM uwe unazitia kapuni, maana ni komenti zisizofaa kabisa katika dunia ya sasa na wala hazichekeshi.

    Mimi naamini Michuzi ulielemewa na mzigo wa comments lukuki ndio maana utani wa ajabu wa Anony wa pili ukapenya na kuifikia blogu ya Jamii.

    Mdau
    Mbagala Kibonde Maji

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 19, 2009

    Bro Michu tafuta mzungu au mnugu uoe ili upate makaratasi. Nakwambia next time ukisafiri kwenda ughaibuni hautahitaji kupiga foleni nje ya balozi, maana utakua na gamba la kueleweka.

    Usizubae Michuzi.

    Halafu kitu kingine, ebu jaribu kwenda kwenye golden gate bridge halafu ning'inia kwenye daraja ujitie unataka kujitupa majini. Utaonekana "live" California nzima na probably kwenye CNN dunia nzima. Au vipi kaka Michu?

    Take it easy people!!!! LOL..

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 19, 2009

    nanihii usisahu kuja tu sumu ya yule simba aliyetoroka mana sijatoka ndani mpaka leo!!!!! mana huko kutakua na sumu ya ukweli

    ReplyDelete
  26. ChakubangaMay 19, 2009

    Wewe Michuzi,uliingia tu,branch ya Google hapa Stanford University sio makao makuu yenyewe-:).Acha kuwapiga ngwala ya kiini macho wananchi wa blog...
    Chakubanga

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 19, 2009

    Karibu mzee wa fulanazz ndani ya kiwanja! Umependeza na suti hiyo lakini inaonekana ya kibongo! teteeee!
    Inabidi utembelee sehemu mbalimbali za marekani sio San Francisco pekee kwani wewe kila mji marekani unaita San Francisco!
    Nipigie simu # hii 574.993.1266 tuongee.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 19, 2009

    Michuzi, huyo wa kushoto ndiyo yule mdogo wetu anayesoma uganda,anaonekana msongo kweli.Kulikoni kaka michuzi,umenenepa sana usoni...umpandishwa cheo nini kuwa mkuu wa mkoa!

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 19, 2009

    Udaktari ni miaka 7.

    Minne medical school, mitatu residence.

    Ukitaka kupasua vichwa na mengineyo hiyo ni specialization ya ubingwa, huwezi ukaihesabu katika miaka ya usomi wa udaktari wa kawaida.

    Ile miaka minne ya degree ya kwanza (liberal arts) sio masomo ya udaktari. Ile inaweza kuwa ya kitu chochote, History, Music, chochote, almuradi ujazie masomo ya msingi ya Sayansi. Hiyo degree huwezi kuiita ni sehemu ya miaka ya udaktari. Udaktari unaanzia medical school.

    Na hakuna degree inayoitwa pred-med. Ukisoma, kwa mfano, Freshman Zoology au Sophomore Organic Chemistry wakati wa hii liberal arts degree inayoitwa "pre-med" utasoma biology ile ile na organic chemistry ile ile anayosoma mtu wa Bachelor of Science in Marine Biology ambae yeye hataiita pre-med. Hakuna kitu kama pre-med biology.

    Sasa nyinyi kina dada wawili, medicala ethics zinataka integrity, msijifagilie uongo uongo kwa Michuzi, unless Michuzi hakuwaeleweni, au Michuzi mwenyewe ame present kiholela holela tu kitu mlichomwambia kwa usahihi na ufafanuzi. Unajua tena Wabongo hatuzingatii communication.

    ReplyDelete
  30. Kweli kaka Michu umechemsha. Stanford University iko Palo Alto, sio San Francisco. Nakutuma uende pale ofisi ya admissions GSB uwaambie waache kuleta zao za kuleta maana wameni-ding kuingia kitivo chao...hahaha! All I can do is player hate...lol!

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 19, 2009

    MICHUZIIIII UKIRUDI NAOMBA UNILETEE LAPUTOPU MBILI NA SIMU YENYE MEMORI KADI NA PILASIMA TIVI IINCHE "50" NA JEZI YA HESHEEM THABEET SIO KOBE BIRIANTI AU LA YALE MAMBO YAKO PALE KWA CHIFU NITAMWAMBIA ASIKUFANYIE TENA, UMEONA HUJAWAGA KWA MZEE NANIHU NDOMANA NDEGE ZILIKUPA TABU. FUROMU XNGINDOMBUNDINGO'NDINGA'SI sijui jina ndio linafanya mpaka leo PASIPOTI SIPATI? Eti BW MICHU.

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 19, 2009

    Mzee wa mikonozi, mbona the same ladies Prezident wa URT naye amepiga mikonoz nao, inakuwaje?

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 19, 2009

    mswahili akijua kitu bwana shida sana,sa we unayejifanya unajua Stanford Uni ilipo pamoja na vitongoji vyake ukinyamaza itakupunguzia nini au ilimradi ukosoe,umkoseshe raha mwenzako.unaniudhi kweli!!
    w pamoja nakujua ilipo ushawahi hata kuingia au mbwembwe tu!!

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 19, 2009

    Oya mtaalam wa BAY AREA (Anon wa May 19, 2009 2:57 PM) mbona humalizii kwamba bay area actually ni SAN FRANCISCO BAY AREA? Na kwamba San Jose iko SOUTH END ya SAN FRANCISCO BAY AREA? Sasa michuzi kakosea nini? Nchi za watu hizo acheni kuzijua sana, unapajua mbagala kibonde maji wewe? *****!

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 19, 2009

    michu mbona umevua pete ya ndoa??!!!

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 20, 2009

    Hata mie nipo na aliyesema Michuzi uwe unatizama Maoni ya watu wengine hata mie comment yake sioni kuchekesha, ni kashfa tu kaweka manake mara michuzi mshamba mara kambaguwa huyo, Jamaa hapo hapo anasema michuzi hatopata Mafuwa ya Swain sasa nani hapo anatumia Ubaguzi? kama sio wewe. lack of technical knowledge neno hilo naona umejitupia mwenyewe ndio umejilenga. Ustarabu jamani. usiwe kama wale watu wa Bongo Search.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 20, 2009

    Asante mdau wa Mbagala Kibonde maji.
    Komenti kama za huyo Naony wa May 19, 2:18pm ni za aibu. Ukimdhihaki mtu kwa sababu ya asili yake (alivyoumbwa) unamkosoa Muumba wake. Lakini ukimdhihaki mtu kwa tabia yake anayoweza kubadilisha (mfano uvivu, ubaguzi wa rangi) ni sawa.

    Ntibadyuza

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 20, 2009

    Tusidanganyane humu, Medical School US ni miaka 4 tu. Hayo mahesabu mnayopiga sijui ya degree ya kwanza, sijui mwaka 1 wa biology ni mda wa kufanya prerequisites na mtu ukiwa unafanya pre-reqs huwezi kujidai uko Med-School. Unaweza maliza hayo madarasa ya pre-reqs na ukaishilia kwenda kusomea kuigiza, so tusidanganyane jamani

    Ni sawasawa na mtahiniwa wa Muhimbili aseme kasoma miaka 12 Medical School kwamba kabla ya kusomea udaktari hapo Muhimbili ambako kumemcosti miaka 5 alianzia high school (form 5&6 = miaka 2), na kabla ya ku-qualify kusomea PCB alisomea shule ya mkondo wa sayansi O-level (form 1-4 = miaka 4), na kabla ya kuanza ku-practice udaktari alifanya internship (1 year). Ukijumlisha yote hiyo unapata 12.

    Medical school US ni miaka 4, full stop!!!

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 20, 2009

    Michu we kichwa sana. Ungepeleka konozz kwa mtasha basi angekufungulia law suit ya kushika nyeti zake bila kukuruhusu lakini Wabongo hawana hizo. Enjoy your stay.

    ReplyDelete
  40. Karibu sana balozi wa nanii, take your time, enjoy yourself, this is AMERICA, you came on right time....spring---summer time, its beautiful.Hope, you gonna love it and learn one or two things, take a lot of pics.

    kusafiri ni shule.

    ReplyDelete
  41. Gloria ChecheMay 20, 2009

    Namwona Christine Karamagi..
    the second girl from left,
    she very intelligent yaani kichwa kichwa sana tangia IST mpaka Academic International School..
    i think she be doing computer science at stanford..thou aint sure...all i know, we was schoolmates at both schools Academic and IST..
    girl tutafutane basi....lol

    ...mdau
    Gloria Cheche from Harvard University

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 20, 2009

    Kama "Medical school US ni miaka 4, full stop!!!" hata mie ningeenda. Maana hapa Bongo imenishinda ni miaka 5 "full stop!!!" baada ya kumaliza high school.
    Mdau Bunju

    ReplyDelete
  43. MagazetiMay 20, 2009

    Sasa Michuzi unataka watu sasa ku-twitter....badala ya blog...yaani what are you doing?

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 20, 2009

    Mzee wa fulanazzzzzzzzz najua walioko huko wamezoea kubeba mabox na kusoma miaka ishirini bila kurudi nyumbani na muda kama wako wa kutanua hawaupati so keep it up brother dear!!!! NAJUA UNAWATESA HUKO NA NYUMBANI HUKU PIA. NA UNAJULIKANA KOTE. WAO WAKO WAPI NA WANA SIFA GANI MBALI YA KUJUA MIJI YA WATU TUU. RUDINI NYUMBANI NYIE VIBEGA WA TANZANIA. NA NIMPONGEZE DR.MBAKISYA ALINANINE ONYANGO KWA KUTUNUKIWA TUZO HUKO, NA HASHIM THABEET NA WENGINEO WANAORUSHA BENDERA YA TANZANIA NJE YA NCHI VILIVYO. Braza michuzi endeleza libeneke

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 20, 2009

    Michu umependeza sana..nimeona hizo picha za hao wadada wako na nanii vipi kulikoni vekesheni yako inagongana na safari zake kila mahali?
    Enjoy ur stay

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 20, 2009

    annon 3.53pm
    4 degree ya kwanza
    1-1.5 kama hujasomea sayansi biol
    4 medical school
    3-6 yrs internship???

    #so wamanisha degree ya kwanza yaitwa general degree au?ambayo inakua na masomo gani sasa??
    4 yrs medical sch ndo specialty mf physician,gyne etc?
    internship ndo imeniacha hoi khaaa

    asante annon kwa kuniweka bayana.jibu na ayo basi

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 20, 2009

    wee annon uko nchi gani ujui kiswazi chetu siku izi??

    pambaz ni nguo za kufa mtu,km misupu izo suti

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 20, 2009

    annon 8.22 pm...asante sana kwa KUELEWESHA KWA UMAKINI

    khaaa michuzi nawe?uwe makini kusikiliza au usipost vitu apa kiholela adi ubate usahihi,wee ushaona wapi udaktari miaka 12??ata urusi tu uingereza HAKUNA 12yrs

    me dokta so i was shocked to read this!!

    kweli communication zero adi michu

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 20, 2009

    ni kweli hauna pete ya ndoa!!!!

    ReplyDelete
  50. Mh. Nanihii, kuwa mwangalifu na baadhi ya comments nyingine hazipendezi kuwepo. Zaidi ukirudi bora utumie ule usafiri wetu wa usiku

    ReplyDelete
  51. PhatlorenzoMay 20, 2009

    Anon wa May 20 9:20 AM
    Duh unaonekana uko bitter sana na watu walioko nje as if uliwahi kunyimwa visa ulipokuwa mdogo. Tatizo lako ni kwamba unafanya generalization. Sio kila aliyeko nje ya nchi ni "m-beba mabox", kama ambavyo sio kila aliyeko nyumbani ni "mnuka kikwapa". Si umewaona hao watanzania kwenye picha ya Mi-Soup wanaosoma Stanford. Unaijua admission criteria yake let alone price tag ya kusoma hapo? Kwa taarifa yako kuna watanzania wengi tu wasomi na wenye professional careers za maana hapa U.S. lakini hakuna anayeosha mdomo. Hata ukisoma postings zao utajua hawafanani na wewe.

    Phatlorenzo-Minnesota

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 21, 2009

    Phatlorenzo-Minnesota kwani shida iko wapi mwana???? mbona kujitetea kwingi wewe mkimbizi wa kiuchumi??. piga box osha wazee osha vyoo lakini mwisho ukumbuke kurudi kwenu huko si kwenu mtakuta mwana si wenu siku mkirudi ohoo!!
    acha kujitetea. wale wenye maisha mazuri huko ni watoto wa balili na watoto wa fisadiz wengine!!
    piga box piga box piga box mwana zikusanye uje uzitumie utese huku make huko mnasave tu hamtumii. piga box mwana!
    Asifiwe, TZ

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 21, 2009

    12 f#*&%$# years watu wanasomesha watoto wao udaktari in the U.S. Kweli pesa ya walipa kodi wa TZ ina nguvu!

    ReplyDelete
  54. PhatlorenzoMay 21, 2009

    Dear Asifiwe....
    Haya mkuu nimekuelewa..nitafanya kama ulivyoelekeza. Ngoja nirudi kubeba Box hapa maana muda wa break umeisha. Next time.
    Phatlorenzo-MN

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 21, 2009

    blaza michuzi huyo wa kulia sio wende aman huyo aliyeongozaga form four kwa kupata A masomo yooote kumi na tatu kweli, amefika stanford? kweli huyo balaa mungu amuongoze afaulu vizuri arudi kututibu wananchi wenzake wa tanzania, kweli hicho chuo balaa watanzania wako hao tu??? kinaonekana sio vile vyetu vya sie wabeba mabox wakusoma kwa timing..........

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 21, 2009

    12 years kwa maana ya miaka ya elimu ya juu baada ya kumaliza high school ni sawa kwa kusomea udaktari US.

    Breakdown
    Basic degree(ya kitu chochote lakini sanasana ya sayansi - 4 yrs)

    Medical school yenyewe - 4 yrs

    Specialization(au residency ambayo ni lazima kwa US ili upractice, 3-7yrs)

    sasa ukijumlisha hapo, tangu mtu anapomaliza high school marekani mpaka aje kuanza kupractice ni shule ya kati ya miaka 11-15 ya university level education)

    MICHUZI YOU ARE RIGHT!

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 22, 2009

    KAKA NANIHII MI NAPENDA SANA ULIVYO FREE NA MAISHA YAKO SABABU UPO KAMA WEWE NA SIYO KUIGA MTU,WE KAMA UMEPIGA PICHA KUTUONESHA WEKA DONT WORRY COZ UR ALWAYS DOIN A GREAT JOB,NAAMINI WE SIYO BITOZ NA NDIO MANA UKASEMA UMEAZIMWA NGUO,WABONGO ALWAYS NI WANAFIKI NDIO MANA WANAKAZANA KUANGALIA MAKOSA TU MARA ETI UJAALIKWA KOKOTE,MARA SIO KILA MJI UPO SAN FR,MARA UDAKTARI SIYO MIAKA YOTE HIYO ETC,VITU HIVYO ANYBODY CAN GOOGLE AND TELL SASA YA NINIMTU KUJIFANYA ANAJUA SANA?WABONGO NDIO MANA HATA KUKAA NAO MTAA MMOJA HUKU MTONI HUWA SIMIND SABABU MAMBO YA TANDALE YANAANZA KINOMA NA WAKATI TUPO BARA LINGINE HUKU,DAMN!!DO UR THANG MAN DONT GIVE A HELL ABT HATERS!

    ReplyDelete
  58. jamani wabongo kwa KUNGANGANIA mambo yasiyo na umuhimu kivile hatujambo..sasa kama Stanford iko Palo Alto au San Fran au San Jose au Mountain View inaongeza au inapunguza nini? mweee!!

    Ni kweli hakuna degree inayoitwa Pre-Med na u-MD sio 12 years hizo ni songombingo za kuwazingua. Ni mwendo wa liberal arts ila unadeclare major mwaka wa tatu na unakomaa nayo mwaka huo na wa nne halafu baada ya hiyo degree ndo unajimuvuzisha kwenye specialization.

    Mie ndo niko hapa mwaka wa kwanza prospective economics major, ni nondoz kwenda mbele ila ndo ivo aint no quitter. Kwa hiyo mbongo aliyeko mitaa hii akijisikia kuhang out anishootie email on elupimo@stanford.edu

    cheers

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...