Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Robin Goetzsche alipowasili kwenye kiwanda cha kampuni hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kuzindua mtambo mpya wa kisasa wa kufungasha bia.Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TBL, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda (wa pili kushoto) akibonyeza kitufe kuzindua mtambo mpya wa kisasa wa kufungasha bia katika kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kunshoto ni Meneja wa kiwanda hicho, Bw. Salvatory Rweyemamu. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa (TBL), Bw. Robin Goetzsche na wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.William Lukuvi (wa tatu kulia), Waziri wa Viwanda, Buiashara na Masoko, Dkt.Mary Nagu.

Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda (kushoto) akiangalia zawadi ya bilauri aliyozawadiwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Robin Goetzsche (katikati) baada kuzindua mtambo mpya wa kisasa wa kufungasha bia katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Bi. Dorris Malulu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2009

    Wiki mbili tu waziri huyo kakataza watu wasinywe pombe.Pombe ambazo uhuzwa kwa bei nafuu. sasa apo bila buku shing mbili ujagusa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2009

    Nimefurahishwa sana na huyo kijana kupewa nafasi ya kuongoza moja ya makampuni makubwa nchini.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2009

    huyu slavatory rweyemamu ndo yule wa ikulu au majina tu yanafanana??

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2009

    ASANTE KWA KUTUONESHA KUWA UNAJUA MANENO YA KISWAHILI, BILAURI HUTENGENEZWA KWA CHUMA NA GILSI HUTENGENEZWA KWA KIOO VYOMBO HIVYO VIWILI VINAFANANA KWA UMBILE NA MATUMIZI; SASA GILASI KUIITA BILAURI SI KUENDELEZA KISWAHILI BALI NI KUPOTOSHA KISWAHILI. NINAJUA KWA WALIODANDIA NJIANI KISWAHILI BILA KUJUA KILIKOTOKA VIDOLE VYAO VITAWAWASHA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2009

    NINGEKUA WAZIRI MKUU NINGEULIZA HIZI GLASS MNATEGENEZA WAPI BONGO AU NJE,KAMA NJE KWANINI SIO BONGO..NAWAPENI MUDA MNIPE FEEDBACK HARAKA....

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2009

    KUUZA POMBE KWA WATANZANIA ONLY NI KUJIUA.. NA KUHARIBU FAMILIA ZETU. LAZIMA TANZANIA IUZE POMBE ZAKE NCHI ZA NJE.. TBL KUTAKA KUUZA POMBE TANZANIA ONLY SIO MAENDELELO.
    TBL ANGALIA MFANO WA BUD, STELLA AU PERONI.. ZIPO DUNIA ZIMA.. ACHA UPUMBAVU.. MAENDELEO SIO HAYO UNAYOFANYA HAPO TANZANIA.. UNAUWA WATANZANIA TUU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...