Mambo Vipi Issa Michuzi?
Je hii ni halali? Majuzi mkazi mmoja wa Iringa alikuta Mbwa Kagongwa Katikati ya Barabara na yeye akakimbilia kisu na kumvuta mbwa pembeni mwa barabara na kuanza kumchuna kwa ajili ya kitoweo. Kuna wapita njia alitaka kumpiga kwa kitendo hicho cha, wengine wakaishia kumkodolea macho tu, tena wengine watoto wadogo. Hii imekaaje?
Mdau Iringa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2009

    hata huku ufipino ukienda vibaya kwenye hoteli utakula kitoweo cha dog.dawa ni kuagiza kuku tu ukiona majina yanakuchanganya kwenye menu unayopewa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2009

    Mbona wachina wanakula? Iyo nyama poa tu.

    ReplyDelete
  3. It looks disgusting kwa sababu ya mazoea tu. Tofauti ya mbwa na nyama za porini tunazokula ni nini?

    Mbwa, mbuzi, nyati, biologically ni wale wale.

    Labla kiti moto ndio tofauti na wenzake. Biologically (scientifically, sio kidini) nguruwe ni mchafu na tunamla. Itakuwa mbwa?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2009

    Kwani mishikaki mingi sehemu za mijini alikuambia nani kwamba ni za nyama halal toka buchani wewe? Ulikuwepo? kwani wewe ni ndugu zao wakuonee huruma? nyingi infact ni nyamafu na ni za kila aina ya mnyama.
    wapenda mishikaki mjionee we!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2009

    NCHI IMELIWA YOTE NA MAFISADI, WALISEMA TUTAKULA HATA MAJINA, NA BADO. TUMEANZA NA KULA MBWA TUTAMALIZIA NA MAJANI

    ReplyDelete
  6. MnyarukoroJune 05, 2009

    Ni utamaduni wetu kula Mbwa huku Iringa... Hii ni asili tuliyoirithi toka kwa Mababu zetu.
    Japo kuwa siku hizi vijana wengi hufanya kwa siri siri kutokana na "Uzungu" wanaojifanya..

    lakini hata wewe mdau yawezekana ulisha kula Mbwa ukiwa Iringa bila ya wewe mwenyewe kujua...

    Karibuni sana Iringa

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2009

    Huyu hali wala nini. Anaenda kuichoma na kuiuza kama mishkaki kwenye baa au kwa wasafiri wanaotaka kujipoza. Lakini cha kushangaa ni nini? Mbona ng'ombe mnakula, nguruwe mnakula? Wana uzuri gani hao kuliko mbwa? Ni swala tu la kisaikolojia. Binadamu anaweza kufanywa aamini hiki ni X na kile ni Y ilimradi tu aweke akilini mwake. Hapa nilipo mimi wanakula vyura, kobe nk. na bado akili yao haijaenda hawajadata. Tatizo ni nini?

    ReplyDelete
  8. Semsola wa IlulaJune 05, 2009

    "Kaumbwa kenyewe kalikuwa kadogoo na kaligongwa na gari hapo kihesa."
    Wahehe wakiona mbwa mate yanawajaa midomoni maana kwao ndio kitoweo cha heshima. Teh Teh Teh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2009

    Kama Iringa ni hivi kuna watu wajinga na washenzi kama huyu hata siendi kutembea, Huyu ni wa kupata kibano kikubwa iwe mfano kwa wengine atafanya vipi kitu kama hichi hadharani bora nile majani kuliko mzoga wa mbwa, Kama anakula achukue mzoga nyumbani kwake akale si mbele ya watu, watu kama hawa ndio wanatuletea kila aina ya magonjwa mabaya mtasikia karibuni mafua ya mbwa tayari, naomba mungu yampate hilo lizee jinga life njiani kama mbwa liwe mzoga na lenyewe, wanaharibu sifa ya nchi watanzania tutadharauliwa halafu, hata kama wachina wanakula mbwa sila kila wanachofanya wachina na sisi tufate, basi wakifirwa na sisi tufirwe pumbavu sana hili lizee.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2009

    mmedata tu nyie, magonjwa hayo yote yanaletwa na nyama za ajabu ajabu bado hamsikii na hamuachi kula tunyama twa ajabu ajabu. Nyama zote hizo nzuri zilizojaa nchi kavu na baharini, kwa nini basi niikwaze afya yangu kwa kula mbwa?
    Lakini kupenda ni kuchagua...haya kuleni hata mizoga!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 05, 2009

    nitafurahi akienda kuiroast na kuiuza kwenye bar. mafisadi usiku wakija kujipumzisha waifakamie tu hii nyama...delicacy meat ....exotic meat....yummy yummy.....daaah

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2009

    kama wengine walivyo na haki ya kula kiti moto huyu naye anahaki ya kula kiti baridi hiki.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2009

    Tu mbwa twenyewe Baba tulikuwa tudogotudogo hahah Iringa ni asili yao kula mbwa kila mtz anajua hili sio jipya ila ni ushahidi tu wa maneno ya miaka kazaaa

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 05, 2009

    mwitiga kiki nyee???

    mtukome watu wa iringa,nyie haramu mwala ngapi?

    kongolo wazee nyie

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2009

    Jamani kwa watu wa Iringa kula mbwa ni asili yao ndio tamaduni zao muacheni mbona wengine wanakula panya???..Ila ubaya ni pale tu kula mbwa ambaye ni kibudu (Aliyekwishakufa) Si vyema kula kitu kilichokufa bora angemchina akiwa hai. Chakusikitisha nikuwa inawezekana huyu anakwenda kumuuza kama nyama kwa wengine.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2009

    ni ufahamu mdogo wa mnaosupport hii issue, mbwa wanamagonjwa hatari sana na ambayo hayatibiki,na pia anabeba magonjwa ya ngono yanayompata binadamu kama gono,kaswende,anakifua kinachofanana na tb.

    sasa kama alikuwa anakichaa mlaji akianza kubweka mtaanza ooh mkono wa mtu huo,nk

    tofautisha mbwa wa mzungu anayeishi maisha bora nakupata matibabu na kufanyiwa medical checkup hata kama haumwi na mbwa wa mitaani bongo.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2009

    Anonymous June 05, 2009 6:50 AM katuchafulia hali ya hewa. Mzee wa nanihii vp? Umelemewa na uwingi wa comments? comments kama zake uwe unaziweka kapuni tu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 05, 2009

    kiingiacho si haramu ..
    haramu ni kitokacho kinywani!!

    jiulize umeongea mangapi mabaya siku ya leo??

    kama unaona kichefuchefu cha mbwa ona zaidi na zaidi kwa kuchafua hewa!!

    tukifanya hivyo amani itatawala!!

    ReplyDelete
  19. Du,i cant imagine!!!!!wanasheria mtusaidie.Huu ni uhuru wa binadamu ndani ya haki za binadamu au uvunjaji wa sheria? Binafsi sina jibu ila nashangaa tu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 05, 2009

    Men... this guy must be out if his mind.. huyu mtu sio mzima

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 05, 2009

    daaah! jamaa nahisi alikuwa amelewa huyo maana jirani na alipo kuna bar ya pombe aina ya ulanzi ni jirani sana kaka niniii na gest moja inaitwa....mjengwa anaweza kunipiga akiisikia.ila wazee wa kihehe kaka naniii wanakutafuta

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 05, 2009

    Huyu nilisikia ng'ombe wake hawajarudi zizini!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 05, 2009

    Usee TUIBANYEE!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 05, 2009

    Hivi T.S.P.C.A ilikufaga?Hii imenikumbusha mengi sana.Nimeshuhudia sehemu nyingi sana vijijini jinsi wanyama kama Punda ,Ng'ombe ,Paka na Mbwa jinsi wasivyo thaminiwa na wamiliki wao!Utakuta Punda ngozi ya shingo imechunika na inavuja damu kwa kubebeshwa mizigo kupita uwezo wake,LAKINI BADO,hakuna atakaye ona huruma,bado Punda yule atabebeshwa Mzigo mkubwa mno kupita uwezo wake na kipigo kwa juu!Mabwana Mifugo Vijijini wamefia wapi?Serikali za Vijiji zinafanya kazi gani?Lakini mahodari sana kukusanya ushuru na michango ya mbio za mwenge!Hii imekaaje?Paka wanauawa ovyo kwa imani za kishirikina.Mbwa akikatiza basi atafukuzwa kwa mvua ya mawe,utadhani Ibilisi kapita!Zamani kidogo sisi tukingali vijana wa shule za msingi kilikuwepo chama rasmi cha kuzuia ukatili kwa wanyama na sheria zilikuwepo za kuwaadhibu wale wote waliotenda ukatili kwa wanayama hai ambao Mwenyezi Mungu katukabidhi sisi Binadamu tuwalinde,tuwapende na kuishi nao!Lakini hivi sasa hakuna anayejali,si Viongozi,si Serikali yenyewe na si watanzania wenyewe!Kilikuwepo chama kilichojulikana kama R.S.P.C.A. kirefu chake Royal Society for the Prevention of Cruelty to Animals.Baada ya Tanganyika kupata uhuru chama hicho kikabadilishwa jina na kuitwa T.S.P.C.A. kirefu chake Tanzania Society for the Prevention of Cruelty to Animals!Na kilikuwa kinatengewa Ruzuku na Serikali ili kuendesha shughuli zake ikiwemo misaada lukuki kutoka nchi zilizoendelea.Na kilipigiwa upatu sana katika makuzi ya vijana katika shule za msingi hata wakathamini na kuwajali wanyama tunaoishi nao majumbani.Siku hizi tumekumbwa na Ibilisi gani Watanzania wenzangu?Usipo mjali Mbwa au Paka au Punda au Ng'ombe anayekusaidia kila siku na halalamiki ,utawezaje kumthamini Mtanzania au Binadamu mwenzako?Jamani tuishi tukimwogopa Mwenyezi Mungu!Wanyama ni kipimo cha Ubinadamu wetu!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 05, 2009

    Sasa najuwa kwa nini wale mbwa wa waziri Mungai walikuwa wanapotea potea kila wakati.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 05, 2009

    Mkuu huyu jamaa ametutia soni sana sisi Watu wa Iringa, kwa nini hasinge mmbeba na kuzama nae msutu kidogo. kweli bongo mambo yapo ndo maisha bora hayo watu hawawezi kununua hata kilo ya nyama ya ng'ombe, ndo mapato ndo hayo.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 05, 2009

    Huyo angelikuwa Marekani nadhani angepewa kifungo cha maisha jela kwa kuamua kumla mume wa mtu. Huko USA Michael Vicky alikuwa akigombanisha mbwa kaenda jela, itakuwa kumchuna umle.

    ReplyDelete
  28. MMMH YA LEO KALI SASA KUNA LA KUJITETEA KWELI KWA WALE NDUGU ZETU WANYALUKOLO MAANA USHAHIDI UPO WAZI NA PICHA HII NAI SAVE KUWATUMIA WAHEHE WOOOOOTE HAHAHAHA.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 05, 2009

    Nyela wayawe umuyenu Mwagito uyoo siilya inyama iyo pe na kukae siifika. Isaka agusage mung'asi pa kilo.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 06, 2009

    Do!..huyu jamaa anatokea iringa? chansi ni kubwa sana kuwa ni mhehe...hizi story tulikuwa tunasikia long time sana na tulizani ni utani tu. Kama ni kweli, mbona wahehe ukiwaambia wanakula mmbwa wanakuwa wakali hivyo?...do kweli wahehe ndiyo wachina weusi!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 06, 2009

    Iringa hii mbona kawaida tu. Mie nilienda kutembea nikaletewa msosi umeungwa fresh nyama kibao wacha nile. Nikamaliza nyama yote na kutaka kuongezewa, nikaambiwa kuwa "Ka mbwa kenyewe kalikuwa kadogo" yaani kichefuchefu ila msosi ndio umeshakula na mtamu. Basi nikienda Iringa mie ni Vegiterian, kama Bob Marley vile sili Nyama Iringa

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 06, 2009

    ...mlaji mla leo ..mla jana kala nini? Kula upendacho ili mradi roho yako iridhike...huyu jama inaelekea hii siku ukimuuliza anakuambia mambo swafi sana leo...halafu mbwa mwenyewe pozi lake kama la mbuzi wanavyo chinjwa kule Vingunguti...

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 06, 2009

    Nakumbuka nilipokuwa Bongo ilitokea mkasa wa namna hii.Kuna jamaa kule Tandale aliogota mbwa barabarani akajificha , kamchuna na kisha akapita mitaani akinadi anauza Nyama pori...wengi walinunua...wengi walikula ''nyama pori huyo''Huyu ni mchoma mishikaki , na ni mshenzi inabidi apigwe..Anayo haki ya kula atakacho ila bwana mifugo wako wapi kuthibitisha uhalali wa mbwa huyo..Ng'ombe na Mbuzi tulazo hupigwa mihuri huko machinjioni...sasa huyu mwehu inabidi atafutwe na ajuzwe..asisingizie Wahehe kuwa wanakula Mbwa...Ni chizi maarifa huyu

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 06, 2009

    Duh kazi kweli kweli hakuna chochote ni ulafi tu na roho ngumu!

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 07, 2009

    THIS IS A VERY LOW STANDARD FOR US. WE DO NOT NEED TO SEE THESE KINDS OF PHOTOS, INCLUDING DEAD BODIES. PLEASE BE CREATIVE AND WRITE A DETAIL DESCRIPTION OF WHAT HAPPENED NOT POST DISGUSTING AND HUMULIATING PHOTOS...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...