Ndugu yangu nina masikitiko makubwa sana kukufahamisha kwamba sisi wadau wako wa huku UCHINA hatukupati tena.
Inaonekana wamezuia blogs kwa hiyo inakuwa ngumu kidogo kukusoma. Sijui unashauri nini? Je unaweza kuwa unatutumia bahari mbalimbali kwa email. Tutashukuru sana ukinijibu.
Uwe na siku njema
We really appreciate your great contribution on our country development in Media.Keep it up!!!
Mdau China


china yasemekana ndio nchi inayoongoza kwa ukiukwaji wa haki za binadamu duniani, juzi kati walifunga you tube kisa sijui wanajeshi waliwadhalilisha watu na video ikawekwa you tube,porn sites walifunga miaka mingi iliyopita.
ReplyDeleteiran, indonesia na nchi nyingi za kiarabu/kiislam mda mfupi facebook itakuwa haipatikani tena.kutokana na mmomonyoko wa maadili,
tatizo la blog ni ngumu kumtambua mmiliki,its not official site.
jirani na china
unaweza kumpata kwa kusearch kwa yahoo au google kwakutumia search
ReplyDeleteUmewezaje kuandika huu ujumbe kama huwezi kuiona glob jii???
ReplyDeleteKijana Tumia hii proxyserver, www.freeproxyserver.ca, Walipoandika browse au walipoandika www.myspace.com futa andika www.issamichuzi.blogspot.com then click waliposema browse utamsoma mheshimiwa wa libeneke kama kawaida.
ReplyDeleteKazi njema pia Piga msuli kijana.
Asa hapa imefikaje?
ReplyDeleteTusipoteze mda kutoa maoni ya ushauri kwa huyu mdau maana hawezi kuupata ushauri weu.
ReplyDeletembali ya mchangiaji wa kwanza wote mlochangia mumeniskitisha sana na comments zenu za kijinga na kitoto. laiti mkingelikuwa na muda na akili za kukaa na kutafakari kabla ya kuruka tu na kujibu kila kinachoandikwa hapa mngelijua vizuri namna china inavyo control internet access kwa wananchi wake na wanaoishi china kwa ujumla. msione tu kwa kuwa huko mliko mnachotaka kuona au kusoma kwenye internet unaweza pata ukadhani ni kwa kila nchi. fumbueni macho, toweni taka taka masikioni msome na kusikiliza news za nchi za nje mtajifunza mengi na kushangazwa na mengi LAKINI la muhimu mtaacha kuandika porojo hapa.
ReplyDeleteNi kweli sisi wa Uchina tulikuwa tunaikosa Blog ya jamii,lkn tulikuwa tunatumia www.freeproxyserver.ca,baadae nayo ikawa na matatizo kidogo.Waweza kutumia Freegate http://127.0.0.1:8580/loc/phome.php?v=6.82&l=409
ReplyDeleteNb:Huenda na hii website wameshai-block so hutaweza kudownload hiyo software,so jaribu ukishindwa mwambie mtu aliye nje ya China a-download then akutumie(423KB) au wasiliana nami afkombo@hotmail.com.
Hii software inasaidia pia katika youtube,hi5 na mitandao yote iliyokuwa blocked na Wachina.
machkini weee, china mchakosa mdau wa milioni chita. Mi naichubiria hiyo nambari kwa hamu hapa, wachije wakatunyofoa na chichi huku.
ReplyDeletehuwenda alisave email ya mich au ipo kichwani
ReplyDeleteJune 02, 2009 5:13 PM unaakili sana unaona wabongo wananavyotwanga maji kwenye kinu?
michu amtumie comment za wadau kwa email asipoweza wadau wajajidili ni kwanini iwe hivyo kama anon wa kwanza
yeah kuna trick ukitumia unaweza kuendelea kupata service ya web iliyofungiwa katika nchi fulani tu, ila sio vyema kuwafundisha watu inabaki private, ila don't try kumtumia kama unapenda rafiki yako asiingie matatizoni, kwani nchi yenyewe unaijua, wakikukamata hawakuachii.
ReplyDeletefrom kiwavi wa net.
JAMAA WANAJARIBU KUWAFUMBA MACHO WATUWAOBIG TIME,HAYOMAMBO YALONG TIME YAANI,UCOMMUNIST HUO UNAENDELEA!!
ReplyDeleteNdiyo maana kasi ya maendeleo China ni kubwa mno. China wanawakopa hela wamarekani acheni hiyo. Hata sisi jamboforums ikifungiwa maendeleo yataongezeka maradufu.
ReplyDeleteNashangaa baadhi ya wadau wanakaa katika dunia gani. Yaani hawasomi kuwa serikali ya China ina wasomi wakali wa Komyuta na wananunua vifaa vya kuzuia website yoyote isionekane, ili kulinda ukomunisti. Sasa hivi huko Juni ni mwaka wa 20 tangu waue wanafunzi hapo Tianamen Square na hawataki watu waandamane kwa kutumia internet. Kwa sasa serikali yao ina nguvu sana mpaka serikali ya Marekani ikasema kuwa wanataka uhusiano wa biashara zaidi kuliko haki za binadamu, hawatapiga kelele sana kwa kuwa China inanunua madeni ya Marekani (U.S Treasury Bonds)na ina dola trilioni moja na upuuzi cash katika benki yao. Ikiamua kuuza basi dola itakufa thamani. Yote haya yapo kwenye magazeti, wadau someni sio tu kuangalia nanihii.
ReplyDelete