Dk. Licky Abdallah azungumzia fainali za confederation cup huko sauzi baina ya Brazil na Marekani ambapo Brazil walishinda 3-2 na kunyakua kombe kwa mbinde...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2009

    Hahahah. lmfao... DR Liky U have just made my day, Wallah ntaingalia hii tena na tena... hahahahahahahhaha.
    Yaani huyu jamaa ana poin sio masikhara jamani... Amenimaliza sana aliposema mnakula ubwabwa na nyama mnategemea kushinda fainali...Wenzenu wanakula fibre!!!!....Mnadhani sayansi na teknolojia ni macomputer na simu za mkononi?? ni mambo mengi kwa pamoja (so true)
    Mkuu wa nanihii hii ni burudani tosha, Shukran sana..

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2009

    One word you are funny man.. Chakula cha fibre ni kweli na vinywaji kama gatrode ni kweli, lakini kumbuka these kids are told for young age nothing is impossible. Determination to make it happen is an American attitude taught from a tender age. Nidhamu na discipline ya mchezo ipo. We angalia Kabumbu Marekani itakuwa ni gumzo miaka michache ijayo. Asante Dokta Ricky kwa vichekesho vyako.Kama ulivyosema ni matumaini sis pia tumejifunza kitu. The American team showed great team spirit and Patriotism.
    Asante

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2009

    Bongo chakula chenye fibre chaliwa vijijini au na walala hoi. Mastaa wanakula chips na mafuta mafuta na bia

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2009

    Ni kweli kabisa sayansi na teknolojia si makompyuta na simu za mikononi, bali hata mipango na mikakati inatengenezwa baada ya kufanyiwa tafiti nyingi na za kutosha. Waamerika wanaamini katika utafiti kwa kila jambo wanalolifanya. Kwa mfano utekelezaji wa mpango wa kukuza kandanda umeandaliwa kisayansi baada ya kufanyika tafiti nyingi kadhaa. Sasa hivi Amerika ina programu nyingi sana za soka katika level tofauti na wanafanya vizuri sana. Wanafahamu vizuri sana kuwa maendeleo ya michezo yanategemeana na taaluma kwa wanamichezo kwa hiyo basi mashuleni na vyuoni ndiyo maeneo mahususi ya kuwaanda vijana kuanza kutumikia michezo kwa kiwango cha juu zaidi, angalia Hasheem Thabeet amekuza kipaji chake UCONN.
    Americans are serious!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2009

    Hongera bwana michuzi kutuletea huyu bwana,kweli Tanzania tuwe tunajivunia lugha yetu ya taifa ya kiswahili.Kwani jamaa anapoongea hapa ananikumbusha kwetu kabisaa.Uwe unatutafutia huyu bwana kwa kutufurahisha pia kututaarif habali mbalimbali za mpila,,lakini misupu kwanini msiwe mnaongelea hata habali zingine kama zawachezaji mbalimbali? na ichukue hata 15 minite? nashulu misupu endelea kutupasha, mdau wa Japani

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 30, 2009

    Huyu Rick angekuwa anaishi Ulaya/USA angekuwa ni mmoja wa watu wenye mabilion kwa kuwa analyst mzuri mno wa soka
    Kaka Michuzi please kama kuna hata mechi za kitz hasa Taifa stars inacheza tunamtaka huyu jamaa awe anahojiwa,leo kanikumbusha home kabisa na kwa kweli hii crips nitaifanya kama home-page yangu!
    Alichosema kuhusu sayansi na soka ni kweli kabisa na timu za afrika haziwezi kufika mbali maana wanaitenga sayansi na soka
    udumu Rick,na tunakuomba uwe unatuletea mambo haya mara kwa mara

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 30, 2009

    Kaka, kwanza nashukuru kwa kusikiliza na kujibu maombi yetu kuwa utuletee tena huyu jamaa. Yaani Dr huyu ni burudani pekee. Mi nimeanza kucheka nilivyomuona tu, ana maneno ya ukweli yanayotolewa kwa burudani, ndo hivyo bro sayansi na teknolojia ni mpk vyakula, teh teh teh...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 30, 2009

    ni kweli mambo yanaitaji sayansi na techn hili ni kubwa kwetu sababu bongo tunakosa hasa common sense tazama leo hii viwanja vya mashuleni tumejenga madarasa sasa vijana watajifunza michezo wapi.mkoloni aliacha play ground sisi tumejenga madarasa.sijaona bado shule huku ughaibuni iliyojengwa bila viwanja.mipango ilishafanywa muda mrefu na mashuleni ndo kumeonekana ndo sahemu muhimu kukuza vipaji.

    labda tuanze upya kubomoa midarasa,eg kindondoni primary school,tandale,mwananyamala kisiwani n.k

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 30, 2009

    Pure genious....mdau nimemkubali anaujua mpira.
    TATIZO LA BONGO: watu kama hawa wenye uelewa wa juu wa mambo kama soka wanapigwa majungu mpaka basi..hawapewi nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.Dr. you make my day unauelewa mpira ndani nje.
    Keep it up DR.ungekuwa huku ughaibuni kila siku ungekuwa unakula mabilion ya pounds.
    Cha chandu - UK

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 30, 2009

    kaka, Dr Liky, kweli hapo umesema..USA wako juu kimtindo!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 30, 2009

    http://majimbokenya.com/home/2009/06/29/ugandan-born-ms-grace-rwaramba-michael-jacksons-nanny-could-get-custody-of-the-children/

    ReplyDelete
  12. ndugu yangu Michuzi leo mchana aliniambia nichungulie nipate kusoma maoni ya wapenzi wa kabumbu wa nyumbani na wale wa ughaibuni, shukrani za dhati kwa wasomaji wote na kweli kabisa nimefarijika kuelewa kuwa nawafurahisha ndugu zanguni na kumbe wapo wengine nawakumbusha home, Bongo....bila shaka nikipata time nitakuwa najumuika nanyi kuwapa mpya mpya(mnakumbuka 'mambo mpwito mpwito' ya Charles Hilary) na pengine kuwapatia majibu ya maswali yenu....labda leo nianze na lile ni vipi tena mpaka nikawa najulikana kama Dr. Licky....hakika mimi si daktari wa kusomea wa fani yoyote(FYI hii imekuwa changamoto maana nitaanza kusomea sheria hivi punde tu), bali ni jina nililopewa na wapenzi wa kandanda waliokuwa wakinifuatilia nilipokuwa na Michuzi tukichambua ile michuano ya Euro 96 ilipokuwa inafanyika England na labda kwa mara ya kwanza wapenzi wa TV walipata uchambuzi uliokuwa wa aina yake kabisa kwa kwetu Bongo. Ingawa wakati wa michuano hiyo nilikuwa kila mara nikiwajulisha watazamaji wetu wa DTV(enzi zile kabla ya CH ten) kuwa mimi si Dr bado niliombwa nilikubali jina hilo, na hata siku moja tukiwa LIVE na Michuzi, alipiga simu Profesa mmoja kutoka Chuo Kikuu DSM akinitaka nikumbuke kwamba unaweza kupewa udaktari kama kuonyesha heshima tu kutokana na jambo fulani unalofanya, bila shaka kwangu alikuwa na maana ya kwamba heshima hiyo ilitokana na huo uchambuzi wangu wa kandanda, basi tena yaliyobaki ni historia maana tangu miaka hiyo hadi leo nimeendelea kuitwa Dr.......

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 01, 2009

    Dr. Licky,

    Uchambuzi wako umetulia sana.

    Unanifurahisha sana na lugha yako ya 'Uswahilini' katika kuleta mchanganuo wa soka.

    Michuzi; mtaalam Dr. Licky tunahitaji kumsikia sana wakati wa Kombe la Dunia.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 01, 2009

    Dr. usijali tunakuaminia na UDr. unajionesha wazi wazi kuna Ma Dr. wamgapi wamesomea lakini bado ni watupu kwenye fani yao??
    Tunamuomba Michuzi azidi kukupa nafasi ili na sisi tulioko ughaibuni tukupate live.
    Wewe ni hazina kubwa sana kwa taifa la bongo LAKINI ndo hivyo tena hawakutumii ipasavyo kuwasaidia.
    KEEP IT UP DR.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 01, 2009

    HUYU JAMAA ACHA TU NI BURUDANI YA KUTOSHA.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 01, 2009

    Dr.Licky huwa kweli unaangalia na kutathimini.Kwani hakuna hata siku moja ukatoamchango wako nisikubaliane na wewe.
    Muhimu ambalo ni funga kazi ulilozungumza ni kwamba Brazil walishinda kwa uzoefu.Nilikuwa nikilisubiri sana.
    Lakini pia mimi bado sikuwakubali waMarekani kuwa wanakiwango kizuri.Ila tu wakipata nafasi wanaitumia vizuri sana.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 01, 2009

    Habali; mpila; nashukulu - phew! Ndiyo nini? Mdomo haukazi? umelegea? Haipendezi kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 01, 2009

    michuzi tunashukuru sana kwa clip ta Dr... Najua science and technology bado bongo lkn wewe ni mfano wa kuelewa maana yake kwa kutuletea glob tuelimishane na kupenda nchi yetu ndiyo siri ya mafanikio ya USA.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 02, 2009

    Du jamaa poa anachambua vizuri na kwa kifupi, ni kweli wakati ni huu wa science na technolojia kwenye michezo..hapa Australia mpira wa miguu sio mchezo maarufu ila wameshafaulu kucheza kombe la dunia mwakani, wana colleges za michezo ambazo zinafundisha mwongozo wa michezo, nidhamu na teknolojia pia michezo inapewa kipaumbele mashuleni nk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...