JK na Rais wa Zanzibar Amani Karume wakipata maelezo kuhusu utafiti zao la Muhogo kutoka kwa Mtaalamu wa kilimo Kutoka kurugenzi ya utafiti na maendelo kwenye Wizara ya kilimo na Maendeleo ya chakula,Dr.Geoffey Mkamilo(kushoto)baada ya kufungua Mkutano wa Kilimo KWANZA kwenye hoteli ya kitalii ya Kunduchi Beach jijini Dar leo
JK akifungua mkutano wa kilimo Katika hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wengine katika picha waliokaa meza kuu ni Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karime, Waziri mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu kiongozi Philemon Luhanjo.

JK na Rais wa Zanzibar Amani abeid Karume wakiangalia mbegu katika maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Hoteli ya Kunduchi Beach muda mfupi baada ya kufungua mkutano wa kilimo jijini Dar leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2009

    ingekuwa vizuri zaidi ufanyike rukwa au mbeya kupata feedback kutoka kwa wakulima wenyewe

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2009

    Nakaaya ameimba mr. politician, utashi wa kuendeleza kilimo haupo nchini. kalagabaho...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2009

    This is absolutely the Wastage of time and resources...

    JK et al, kuna vitu vingine wa-TZ hatuhitaji kwenda shule ili kuvifahamu. Viko straight-forward mno ndugu zangu. Pesa iliyotumika kuandaa shughuli hii pamoja na kuwalipa allowance wahudhuriaji ingesaidia kuwapa mifuko ya bure ya mbolea wakulima zaidi ya 500 ili kuwaongezea ufanisi.

    Inaumiza sana mtu kuona vitu vya dizaini hii vikiendelezwa.

    We need to change the way we think. This might be one of the reasons why Tanzania ni masikini miaka zaidi ya 40 baada ya uhuru.

    ReplyDelete
  4. JAmani wafanyibiashara na wakulima wa mwanza na tanzania mnaotaka kuuza bidhaa zenu nje mtafuteni mtanzania mwenzenu Dr. Shayo analink ya wanunuzi wa bidhaa zenu huko ugaibuni.
    si mlifuatilia ile report yake ya opportunities za masoko nje ya nchi iliyotolewa katika hii website ya jamii.

    nakuombeni mtu mwenye e mail yake au simu yake aiweke hapa ili wakulima na wafanyibiashara wengi wa kitanzania waweze kunufaika na nafasi hii

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 03, 2009

    Hivi kwani sisi tumerogwa? Shame on us kwa kweli. So tukifanya hilo lisemina huko dar then tukaacha mazingira kama yalivyo huko vijijini what are we doing? Mkulima ambaye ndiye mzalishaji ameachwa kama yatima, hakuna mbolea na pembejeo zingine. Then kwa taabu akivuna, mchuuzi atakuja na mzani wake fake amwibie kwa bei aitakayo yeye mchuuzi. Oh my God when will be serious on serious issues?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...