Shoto ni Falijala Mbutu mpiga gitaa mahiri pamoja na kiongozi wa The Kilimanjaro Connection Band Kanku Kelly wakiwajibika jukwaani wakati wa shoo yao ya mwisho jijini Kuala Lumpur jumamosi ilopita.

Kundi hili linatarajia kuwasili Dar leo kwa mapumziko likitokea Malaysia baada ya kumaliza mkataba wao wa awali. Kundi hilo hiyo Jumamosi lilifanya shoo yao ya mwisho kuwaaga mashabiki wao wa Malaysia, shoo ambayo ilikuwa ya kufa mtu na kuhudhuriwa na mamia kwa mamia ya mashabiki na kufanya ukumbi wa Rum Jungle kuwa mdogo.
Kundi hili ambalo lilikuwa nchini Malaysia kwa takribani miezi sita limejizolea umaarufu na kuitangaza Tanzania kwa kiasi kikubwa baada ya kuwa gumzo na story na picha zao kutawala kurasa za burudani kwenye magazeti yote ya Malaysia. Kwa habari na picha zaidi
http://spotistarehe.wordpress.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2009

    Bendi ni nzuri sana kwa hilo naipongeza. ila katika kuitangaza Tanzania haikuwa kihivyo coz mabango ya matangazo niliyoyaona mie yalikuwa yameandikwa "BAND FROM AFRICA" ingekuwa vizuri zaidi kama ni TANZANIA, AFRICA alteast.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2009

    Naungana na Anony 12:47:00PM
    Unajua Tanzania bado tumelewa ulevi wa Ujamaa! Hili ni kosa kubwa kwa wanamziki au bendi kujitangaza heti bendi kutoka Afrika!!! Jamani afrika ni kubwa ba kila nchi ina utamaduni na mziki wake,kwa nini wanamziki msitangazae moja kwa moja kuwa bendi kutoka Tanzania? hili swala la kujifanya Afrika moja ni siasa tu,wenzenu wanamziki kutoka Afrika magharibi katika matangazo yao wanataja kabisa mfano:bendi kutoka Ghana+West Africa,sasa na nyinyi kwa nini? msitangaze jina la Tanzania what's wrong?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2009

    Bwana nyie mnasema kila siku jamaa walikuwa wakinadiwa kuwa Band toka Tanzania na jamaa alikuwa anasema .... from Tanzania - africa, sio hiyo tuu hata Menu za Rum Jungle zimebadilika na kuwa Tanzania Roast Kuku na kadhalika hata menu za Pombe kali za kuchanganya pia kuna Tanzania Kick sasa mnatakaje?
    Pia kwenye Article iliyotoka The Star mwezi April na Malay Mail February iliandika Tanzania na wanyama kuwekwa mbali na picha za Band niambieni nyie mliposikia Africa pekee ni wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...